1 Chronicles 16
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 So they brought the ark of God and placed it inside the tent that David had pitched for it. And they presented burnt offerings and peace offerings before God. | SWKCV 1 Wakaleta Sanduku la Mungu na kuliweka ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha kwa ajili yake, na wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Mungu. |
| BSB 2 When David had finished sacrificing the burnt offerings and peace offerings, he blessed the people in the name of the LORD. | SWKCV 2 Baada ya Daudi kumaliza kutoa hizo sadaka za kuteketezwa na hizo sadaka za amani, akawabariki watu katika jina la Bwana. |
| BSB 3 Then he distributed to every man and woman of Israel a loaf of bread, a date cake, and a raisin cake. | SWKCV 3 Kisha akamgawia kila Mwisraeli mwanaume na mwanamke mkate, andazi la tende na andazi la zabibu kavu. |
| BSB 4 David appointed some of the Levites to minister before the ark of the LORD, to celebrate, to give thanks, and to praise the LORD, the God of Israel. | SWKCV 4 Akawaweka pia baadhi ya Walawi ili wahudumu mbele ya Sanduku la Bwana kufanya maombi, kumshukuru na kumsifu Bwana, Mungu wa Israeli: |
| BSB 5 Asaph was the chief, Zechariah was second, then Jeiel, Shemiramoth, Jehiel, Mattithiah, Eliab, Benaiah, Obed-edom, and Jeiel. They were to play the harps and lyres, while Asaph sounded the cymbals | SWKCV 5 Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, |
| BSB 6 and the priests Benaiah and Jahaziel blew the trumpets regularly before the ark of the covenant of God. | SWKCV 6 nao Benaya na Yahazieli makuhani, ndio wangepiga tarumbeta mara kwa mara mbele ya Sanduku la Agano la Mungu. |
| BSB 7 On that day David first committed to Asaph and his associates this song of thanksgiving to the LORD: | SWKCV 7 Siku ile, kitu cha kwanza Daudi alichofanya ni kumkabidhi Asafu na wenzake zaburi hii ya shukrani kwa Bwana: |
| BSB 8 “Give thanks to the LORD; call upon His name; make known His deeds among the nations. | SWKCV 8 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. |
| BSB 9 Sing to Him, sing praises to Him; tell of all His wonders. | SWKCV 9 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa; waambieni matendo yake yote ya ajabu. |
| BSB 10 Glory in His holy name; let the hearts of those who seek the LORD rejoice. | SWKCV 10 Lishangilieni jina lake takatifu; mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi. |
| BSB 11 Seek out the LORD and His strength; seek His face always. | SWKCV 11 Mtafuteni Bwana na nguvu zake; utafuteni uso wake siku zote. |
| BSB 12 Remember the wonders He has done, His marvels, and the judgments He has pronounced, | SWKCV 12 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, |
| BSB 13 O offspring of His servant Israel, O sons of Jacob, His chosen ones. | SWKCV 13 enyi wazao wa Israeli mtumishi wake, enyi wana wa Yakobo, wateule wake. |
| BSB 14 He is the LORD our God; His judgments carry throughout the earth. | SWKCV 14 Yeye ndiye Bwana Mungu wetu; hukumu zake zimo duniani pote. |
| BSB 15 Remember His covenant forever, the word He ordained for a thousand generations— | SWKCV 15 Hulikumbuka agano lake milele, neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu, |
| BSB 16 the covenant He made with Abraham, and the oath He swore to Isaac. | SWKCV 16 agano alilolifanya na Abrahamu, kiapo alichomwapia Isaki. |
| BSB 17 He confirmed it to Jacob as a decree, to Israel as an everlasting covenant: | SWKCV 17 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri, kwa Israeli liwe agano la milele: |
| BSB 18 ‘I will give you the land of Canaan as the portion of your inheritance.’ | SWKCV 18 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani kuwa sehemu utakayoirithi.” |
| BSB 19 When they were few in number, few indeed, and strangers in the land, | SWKCV 19 Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana na wageni ndani yake, |
| BSB 20 they wandered from nation to nation, from one kingdom to another. | SWKCV 20 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine. |
| BSB 21 He let no man oppress them; He rebuked kings on their behalf: | SWKCV 21 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee; kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema: |
| BSB 22 ‘Do not touch My anointed ones! Do no harm to My prophets!’ | SWKCV 22 “Msiwaguse niliowatia mafuta; msiwadhuru manabii wangu.” |
| BSB 23 Sing to the LORD, all the earth. Proclaim His salvation day after day. | SWKCV 23 Mwimbieni Bwana dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku. |
| BSB 24 Declare His glory among the nations, His wonders among all peoples. | SWKCV 24 Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote. |
| BSB 25 For great is the LORD, and greatly to be praised; He is to be feared above all gods. | SWKCV 25 Kwa kuwa Bwana ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote. |
| BSB 26 For all the gods of the nations are idols, but it is the LORD who made the heavens. | SWKCV 26 Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu. |
| BSB 27 Splendor and majesty are before Him; strength and joy fill His dwelling. | SWKCV 27 Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake. |
| BSB 28 Ascribe to the LORD, O families of the nations, ascribe to the LORD glory and strength. | SWKCV 28 Mpeni Bwana, enyi jamaa za mataifa, mpeni Bwana utukufu na nguvu, |
| BSB 29 Ascribe to the LORD the glory due His name; bring an offering and come before Him. Worship the LORD in the splendor of His holiness; | SWKCV 29 mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake. Leteni sadaka na mje katika nyua zake; mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake. |
| BSB 30 tremble before Him, all the earth. The world is firmly established; it cannot be moved. | SWKCV 30 Dunia yote na itetemeke mbele zake! Ulimwengu ameuweka imara; hauwezi kusogezwa. |
| BSB 31 Let the heavens be glad, and the earth rejoice. Let them say among the nations, ‘The LORD reigns!’ | SWKCV 31 Mbingu na zishangilie, nchi na ifurahi; semeni katikati ya mataifa, “Bwana anatawala!” |
| BSB 32 Let the sea resound, and all that fills it; let the fields exult, and all that is in them. | SWKCV 32 Bahari na ivume, na vyote vilivyomo ndani yake; mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo ndani yake. |
| BSB 33 Then the trees of the forest will sing for joy before the LORD, for He is coming to judge the earth. | SWKCV 33 Kisha miti ya msituni itaimba, itaimba kwa furaha mbele za Bwana, kwa maana anakuja kuihukumu dunia. |
| BSB 34 Give thanks to the LORD, for He is good; His loving devotion endures forever. | SWKCV 34 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; upendo wake wadumu milele. |
| BSB 35 Then cry out: ‘Save us, O God of our salvation; gather and deliver us from the nations, that we may give thanks to Your holy name, that we may glory in Your praise.’ | SWKCV 35 Mlilieni, “Ee Mungu Mwokozi wetu, tuokoe. Tukusanye tena na utukomboe kutoka kwa mataifa, ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu, na kushangilia katika sifa zako.” |
| BSB 36 Blessed be the LORD, the God of Israel, from everlasting to everlasting.” Then all the people said, “Amen!” and “Praise the LORD!” | SWKCV 36 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, tangu milele na hata milele. Nao watu wote wakasema, “Amen,” na “Msifuni Bwana.” |
| BSB 37 So David left Asaph and his associates there before the ark of the covenant of the LORD, to minister there regularly according to the daily requirements, | SWKCV 37 Daudi akamwacha Asafu na wenzake mbele ya Sanduku la Agano la Bwana ili wahudumu humo mara kwa mara, kulingana na mahitaji ya kila siku. |
| BSB 38 along with Obed-edom and his sixty-eight relatives. Obed-edom son of Jeduthun, and also Hosah, were to be gatekeepers. | SWKCV 38 Pia akamwacha Obed-Edomu pamoja na wenzake sitini na wanane wahudumu pamoja nao. Obed-Edomu mwana wa Yeduthuni na pia Hosa walikuwa mabawabu wa lango. |
| BSB 39 And David left Zadok the priest and his fellow priests before the tabernacle of the LORD at the high place in Gibeon | SWKCV 39 Daudi akamwacha kuhani Sadoki pamoja na makuhani wenzake mbele ya hema ya ibada ya Bwana katika mahali pa juu pa kuabudia huko Gibeoni |
| BSB 40 to regularly present burnt offerings to the LORD on the altar of burnt offerings, morning and evening, according to all that was written in the Law of the LORD, which He had commanded Israel to keep. | SWKCV 40 ili kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Bwana kwenye madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mara kwa mara, asubuhi na jioni, sawasawa na kila kitu kilichoandikwa katika sheria ya Bwana ambayo alikuwa amempa Israeli. |
| BSB 41 With them were Heman, Jeduthun, and the rest of those chosen and designated by name to give thanks to the LORD, for “His loving devotion endures forever.” | SWKCV 41 Waliohudumu pamoja nao walikuwa Hemani, Yeduthuni na wale wote waliochaguliwa na kutajwa kwa jina kumpa Bwana shukrani, “Kwa maana fadhili zake zadumu milele.” |
| BSB 42 Heman and Jeduthun had with them trumpets and cymbals for the music and instruments for the songs of God. And the sons of Jeduthun were stationed at the gate. | SWKCV 42 Hemani na Yeduthuni walikuwa na wajibu wa kupiga tarumbeta, matoazi na kutumia vyombo vingine kwa ajili ya nyimbo za sifa kwa Mungu. Wana wa Yeduthuni waliwekwa langoni. |
| BSB 43 Then all the people departed for their homes, and David returned home to bless his household. | SWKCV 43 Kisha watu wote wakaondoka, kila mmoja akarudi nyumbani kwake, naye Daudi akarudi nyumbani kuibariki jamaa yake. |
Questions about 1 Chronicles 16? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.