1 Corinthians 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 It is actually reported that there is sexual immorality among you, and of a kind that is intolerable even among pagans: A man has his father’s wife. | SWKCV 1 Yamkini habari imeenea ya kuwa miongoni mwenu kuna uzinzi ambao haujatokea hata miongoni mwa watu wasiomjua Mungu: Kwamba mtu anaishi na mke wa baba yake. |
| BSB 2 And you are proud! Shouldn’t you rather have been stricken with grief and have removed from your fellowship the man who did this? | SWKCV 2 Nanyi mwajivuna! Je, haiwapasi kuhuzunika na kumtenga na ushirika wenu mtu huyo aliyefanya mambo hayo? |
| BSB 3 Although I am absent from you in body, I am present with you in spirit, and I have already pronounced judgment on the one who did this, just as if I were present. | SWKCV 3 Hata kama siko pamoja nanyi katika mwili, niko nanyi katika roho. Nami nimekwisha kumhukumu mtu huyo aliyetenda jambo hili, kama vile ningekuwepo. |
| BSB 4 When you are assembled in the name of our Lord Jesus and I am with you in spirit, along with the power of the Lord Jesus, | SWKCV 4 Mnapokutana katika Jina la Bwana wetu Yesu nami nikiwepo pamoja nanyi katika roho na uweza wa Bwana Yesu ukiwepo, |
| BSB 5 hand this man over to Satan for the destruction of the flesh, so that his spirit may be saved on the Day of the Lord. | SWKCV 5 mkabidhini mtu huyu kwa Shetani, ili mwili wake uharibiwe, ili roho yake iokolewe katika siku ya Bwana. |
| BSB 6 Your boasting is not good. Do you not know that a little leaven works through the whole batch of dough? | SWKCV 6 Majivuno yenu si mazuri. Je, hamjui ya kwamba chachu kidogo huchachusha donge zima la unga? |
| BSB 7 Get rid of the old leaven, that you may be a new unleavened batch, as you really are. For Christ, our Passover lamb, has been sacrificed. | SWKCV 7 Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu, kama vile mlivyo. Kwa maana Kristo, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kuwa dhabihu. |
| BSB 8 Therefore let us keep the feast, not with the old bread, leavened with malice and wickedness, but with the unleavened bread of sincerity and of truth. | SWKCV 8 Kwa hiyo, tusiiadhimishe sikukuu hii, kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu, bali kwa mkate usiotiwa chachu, ndio weupe wa moyo na kweli. |
| BSB 9 I wrote you in my letter not to associate with sexually immoral people. | SWKCV 9 Niliwaandikia katika waraka wangu kuwa msishirikiane na wazinzi. |
| BSB 10 I was not including the sexually immoral of this world, or the greedy and swindlers, or idolaters. In that case you would have to leave this world. | SWKCV 10 Sina maana kwamba msishirikiane na wazinzi wa ulimwengu huu, au wenye tamaa mbaya, wanyangʼanyi au waabudu sanamu. Kwa kufanya hivyo ingewalazimu mtoke ulimwenguni humu. |
| BSB 11 But now I am writing you not to associate with anyone who claims to be a brother but is sexually immoral or greedy, an idolater or a verbal abuser, a drunkard or a swindler. With such a man do not even eat. | SWKCV 11 Lakini sasa nawaandikia kwamba msishirikiane na mtu yeyote anayejiita ndugu, hali akiwa ni mzinzi, au mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu au msingiziaji, mlevi au mdhalimu. Mtu kama huyo hata msile naye. |
| BSB 12 What business of mine is it to judge those outside the church? Are you not to judge those inside? | SWKCV 12 Yanihusu nini kuwahukumu wale watu walio nje ya kanisa? Je, si mnapaswa kuwahukumu hao walio ndani? |
| BSB 13 God will judge those outside. “Expel the wicked man from among you.” | SWKCV 13 Mungu atawahukumu hao walio nje. “Ninyi mwondoeni huyo mtu mwovu miongoni mwenu.” |
Questions about 1 Corinthians 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.