1 Kings 17
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now Elijah the Tishbite, who was among the settlers of Gilead, said to Ahab, “As surely as the LORD, the God of Israel, lives, before whom I stand, there will be neither dew nor rain in these years except at my word!” | SWKCV 1 Basi Eliya, Mtishbi kutoka Tishbi katika Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninamtumikia, hapatakuwa na umande wala mvua katika miaka hii, isipokuwa kwa neno langu.” |
| BSB 2 Then a revelation from the LORD came to Elijah: | SWKCV 2 Kisha neno la Bwana likamjia Eliya, kusema, |
| BSB 3 “Leave here, turn eastward, and hide yourself by the Brook of Cherith, east of the Jordan. | SWKCV 3 “Ondoka hapa, elekea upande wa mashariki ukajifiche katika Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani. |
| BSB 4 And you are to drink from the brook, and I have commanded the ravens to feed you there.” | SWKCV 4 Utakunywa maji kutoka kile kijito, nami nimeagiza kunguru wakulishe huko.” |
| BSB 5 So Elijah did what the LORD had told him, and he went and lived by the Brook of Cherith, east of the Jordan. | SWKCV 5 Hivyo akafanya kile alichoambiwa na Bwana. Akaenda katika Kijito cha Kerithi, mashariki ya Yordani na akakaa huko. |
| BSB 6 The ravens would bring him bread and meat in the morning and evening, and he would drink from the brook. | SWKCV 6 Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji kutoka kile kijito. |
| BSB 7 Some time later, however, the brook dried up because there had been no rain in the land. | SWKCV 7 Baada ya muda, kile kijito kikakauka kwa sababu mvua haikuwa imenyesha katika nchi. |
| BSB 8 Then the word of the LORD came to Elijah: | SWKCV 8 Kisha neno la Bwana likamjia, kusema, |
| BSB 9 “Get up and go to Zarephath of Sidon, and stay there. Behold, I have commanded a widow there to provide for you.” | SWKCV 9 “Ondoka, uende Sarepta ya Sidoni na ukae huko. Nimemwagiza mjane katika sehemu ile akupatie chakula.” |
| BSB 10 So Elijah got up and went to Zarephath. When he arrived at the city gate, there was a widow gathering sticks. Elijah called to her and said, “Please bring me a little water in a cup, so that I may drink.” | SWKCV 10 Hivyo akaenda Sarepta. Alipofika kwenye lango la mji, mjane alikuwa huko akiokota kuni. Akamwita na kumwambia, “Naomba uniletee maji kidogo kwenye gudulia ili niweze kunywa.” |
| BSB 11 And as she was going to get it, he called to her and said, “Please bring me a piece of bread.” | SWKCV 11 Alipokuwa anakwenda kumletea, akamwita akasema, “Tafadhali niletee pia kipande cha mkate.” |
| BSB 12 But she replied, “As surely as the LORD your God lives, I have no bread—only a handful of flour in a jar and a little oil in a jug. Look, I am gathering a couple of sticks to take home and prepare a meal for myself and my son, so that we may eat it and die.” | SWKCV 12 Akamjibu, “Hakika kama Bwana Mungu wako aishivyo, sina mkate wowote, isipokuwa konzi ya unga kwenye gudulia na mafuta kidogo kwenye chupa. Ninakusanya kuni chache nipeleke nyumbani na nikapike chakula kwa ajili yangu na mwanangu, ili kwamba tule, kiishe, tukafe.” |
| BSB 13 “Do not be afraid,” Elijah said to her. “Go and do as you have said. But first make me a small cake of bread from what you have, and bring it out to me. Afterward, make some for yourself and your son, | SWKCV 13 Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda nyumbani ukafanye kama ulivyosema. Lakini kwanza unitengenezee mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyo navyo kisha uniletee na ndipo utayarishe chochote kwa ajili yako na mwanao. |
| BSB 14 for this is what the LORD, the God of Israel, says: ‘The jar of flour will not be exhausted and the jug of oil will not run dry until the day the LORD sends rain upon the face of the earth.’” | SWKCV 14 Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Lile gudulia la unga halitakwisha wala ile chupa ya mafuta haitakauka hadi siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.’” |
| BSB 15 So she went and did according to the word of Elijah, and there was food every day for Elijah and the woman and her household. | SWKCV 15 Akaondoka na kufanya kama Eliya alivyomwambia. Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Eliya, yule mwanamke na jamaa yake. |
| BSB 16 The jar of flour was not exhausted and the jug of oil did not run dry, according to the word that the LORD had spoken through Elijah. | SWKCV 16 Kwa kuwa lile gudulia la unga halikwisha na ile chupa ya mafuta haikukauka, sawasawa na lile neno la Bwana alilosema Eliya. |
| BSB 17 Later, the son of the woman who owned the house became ill, and his sickness grew worse and worse, until no breath remained in him. | SWKCV 17 Baada ya muda, mwana wa yule mwanamke mwenye nyumba akaugua. Hali yake ikaendelea kuwa mbaya sana, na hatimaye akaacha kupumua. |
| BSB 18 “O man of God,” said the woman to Elijah, “what have you done to me? Have you come to remind me of my iniquity and cause the death of my son?” | SWKCV 18 Akamwambia Eliya, “Una nini dhidi yangu, ewe mtu wa Mungu? Umekuja ili kukumbushia dhambi yangu na kusababisha kifo cha mwanangu?” |
| BSB 19 But Elijah said to her, “Give me your son.” So he took him from her arms, carried him to the upper room where he was staying, and laid him on his own bed. | SWKCV 19 Eliya akamjibu, “Nipe mwanao.” Eliya akampokea kutoka kifuani mwake, akambeba mpaka chumba cha juu alipokuwa anaishi, akamlaza kitandani mwake. |
| BSB 20 Then he cried out to the LORD, “O LORD my God, have You also brought tragedy on this widow who has opened her home to me, by causing her son to die?” | SWKCV 20 Kisha akamlilia Bwana, akasema “Ee Bwana Mungu wangu, je, pia umeleta msiba juu ya mjane huyu ninayeishi pamoja naye, kwa kusababisha mwanawe kufa?” |
| BSB 21 Then he stretched himself out over the child three times and cried out to the LORD, “O LORD my God, please let this boy’s life return to him!” | SWKCV 21 Kisha akajinyoosha juu ya kijana mara tatu na kumlilia Bwana, akisema, “Ee Bwana Mungu wangu, nakuomba roho ya huyu kijana imrudie!” |
| BSB 22 And the LORD listened to the voice of Elijah, and the child’s life returned to him, and he lived. | SWKCV 22 Bwana akasikia kilio cha Eliya, na roho ya kijana ikamrudia, naye akafufuka. |
| BSB 23 Then Elijah took the child, brought him down from the upper room into the house, and gave him to his mother. “Look, your son is alive,” Elijah declared. | SWKCV 23 Eliya akamtwaa kijana na kumbeba kutoka chumbani mwake akamshusha kumpeleka kwenye nyumba. Akampa mama yake na kusema, “Tazama, mwanao yu hai!” |
| BSB 24 Then the woman said to Elijah, “Now I know that you are a man of God and that the word of the LORD from your mouth is truth.” | SWKCV 24 Ndipo yule mwanamke akamwambia Eliya, “Sasa ninajua kwamba wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno la Bwana kutoka kinywani mwako ni kweli.” |
Questions about 1 Kings 17? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.