1 Kings 6
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 In the four hundred and eightieth year after the Israelites had come out of the land of Egypt, in the fourth year of Solomon’s reign over Israel, in the month of Ziv, the second month, he began to build the house of the LORD. | SWKCV 1 Katika mwaka wa 480 baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Solomoni katika Israeli, katika mwezi wa Zivu, ambao ndio mwezi wa pili, alianza kujenga Hekalu la Bwana. |
| BSB 2 The house that King Solomon built for the LORD was sixty cubits long, twenty cubits wide, and thirty cubits high. | SWKCV 2 Hekalu hilo Mfalme Solomoni alilojenga kwa ajili ya Bwana lilikuwa na urefu wa dhiraa sitini, upana wa dhiraa ishirini na kimo cha dhiraa thelathini kwenda juu. |
| BSB 3 The portico at the front of the main hall of the temple was twenty cubits long, extending across the width of the temple and projecting out ten cubits in front of the temple. | SWKCV 3 Baraza ya mbele ya Hekalu ilienea dhiraa ishirini kulingana na upana wa Hekalu na kujitokeza dhiraa kumi mbele ya Hekalu. |
| BSB 4 He also had narrow windows framed high in the temple. | SWKCV 4 Akatengeneza madirisha membamba yenye vidirisha vidogo vya juu katika Hekalu. |
| BSB 5 Against the walls of the temple and the inner sanctuary, Solomon built a chambered structure around the temple, in which he constructed the side rooms. | SWKCV 5 Akafanyiza vyumba vya pembeni kulizunguka Hekalu lote vikishikamana na kuta za Hekalu na za Patakatifu pa Patakatifu. |
| BSB 6 The bottom floor was five cubits wide, the middle floor six cubits, and the third floor seven cubits. He also placed offset ledges around the outside of the temple, so that nothing would be inserted into its walls. | SWKCV 6 Ghorofa ya chini kabisa ilikuwa na upana wa dhiraa tano, ya kati ilikuwa dhiraa sita na ya tatu ilikuwa dhiraa saba. Kuzunguka ukuta wa nje wa Hekalu akapunguza ukuta pande zote ili boriti zisishikane kwenye kuta za Hekalu. |
| BSB 7 The temple was constructed using finished stones cut at the quarry, so that no hammer or chisel or any other iron tool was heard in the temple while it was being built. | SWKCV 7 Katika kujenga Hekalu, yalitumika tu mawe yaliyochongwa huko machimboni, wala hakuna nyundo, patasi au chombo kingine chochote cha chuma kilichosikika sauti yake katika eneo la ujenzi wa Hekalu wakati lilipokuwa likijengwa. |
| BSB 8 The entrance to the bottom floor was on the south side of the temple. A stairway led up to the middle level, and from there to the third floor. | SWKCV 8 Ingilio la ghorofa ya chini kabisa lilikuwa upande wa kusini wa Hekalu, ngazi ilielekea ghorofa ya kati na kutokea hapo ilielekea hadi ghorofa ya tatu. |
| BSB 9 So Solomon built the temple and finished it, roofing it with beams and planks of cedar. | SWKCV 9 Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha, akiliweka paa za boriti na mbao za mierezi. |
| BSB 10 He built chambers all along the temple, each five cubits high and attached to the temple with beams of cedar. | SWKCV 10 Mfalme Solomoni akajenga vyumba vya pembeni kuzunguka Hekalu lote. Kimo cha kila kimoja kilikuwa dhiraa tano. Navyo vilikuwa vimeunganishwa na Hekalu kwa boriti za mierezi. |
| BSB 11 Then the word of the LORD came to Solomon, saying: | SWKCV 11 Neno la Bwana likamjia Solomoni kusema: |
| BSB 12 “As for this temple you are building, if you walk in My statutes, carry out My ordinances, and keep all My commandments by walking in them, I will fulfill through you the promise I made to your father David. | SWKCV 12 “Kwa habari ya Hekalu hili unalojenga, kama ukifuata amri zangu, ukatunza masharti yangu na kushika maagizo yangu yote na kuyatii, kwa kupitia wewe nitatimiza ahadi niliyomwahidi Daudi baba yako. |
| BSB 13 And I will dwell among the Israelites and will not abandon My people Israel.” | SWKCV 13 Nami nitakaa miongoni mwa Waisraeli, nami sitawaacha watu wangu Israeli.” |
| BSB 14 So Solomon built the temple and finished it. | SWKCV 14 Basi Solomoni akajenga Hekalu na kulikamilisha. |
| BSB 15 He lined the interior walls with cedar paneling from the floor of the temple to the ceiling, and he covered the floor with cypress boards. | SWKCV 15 Akazifunika kuta zake za ndani kwa mbao za mierezi, akizipigilia ukutani kuanzia sakafuni mwa Hekalu hadi kwenye dari na kufunika sakafu ya Hekalu kwa mbao za misunobari. |
| BSB 16 He partitioned off the twenty cubits at the rear of the temple with cedar boards from floor to ceiling to form within the temple an inner sanctuary, the Most Holy Place. | SWKCV 16 Akagawa dhiraa ishirini sehemu ya nyuma ya Hekalu kwa mbao za mierezi kuanzia kwenye sakafu hadi darini ili kufanya sehemu takatifu ya ndani, yaani Patakatifu pa Patakatifu. |
| BSB 17 And the main hall in front of this room was forty cubits long. | SWKCV 17 Ukumbi mkubwa uliokuwa mbele ya chumba hiki ndio ulikuwa na urefu wa dhiraa arobaini. |
| BSB 18 The cedar paneling inside the temple was carved with gourds and open flowers. Everything was cedar; not a stone could be seen. | SWKCV 18 Hekalu ndani ilikuwa ya mierezi iliyonakshiwa mifano ya maboga na maua yaliyochanua. Kila kitu kilikuwa cha mwerezi, hakuna jiwe ambalo lilionekana. |
| BSB 19 Solomon also prepared the inner sanctuary within the temple to set the ark of the covenant of the LORD there. | SWKCV 19 Ndani ya Hekalu akatengeneza sehemu takatifu ya ndani, kwa ajili ya kuweka Sanduku la Agano la Bwana. |
| BSB 20 The inner sanctuary was twenty cubits long, twenty cubits wide, and twenty cubits high. He overlaid the inside with pure gold, and he also overlaid the altar of cedar. | SWKCV 20 Sehemu takatifu ya ndani ilikuwa na upana, urefu na kimo cha dhiraa ishirini ndani kwa ndani. Akaifunika ndani kwa dhahabu safi, pia akaifunika madhabahu ya mierezi vivyo hivyo. |
| BSB 21 So Solomon overlaid the inside of the temple with pure gold, and he extended gold chains across the front of the inner sanctuary, which was overlaid with gold. | SWKCV 21 Solomoni akaifunika sehemu ya ndani ya Hekalu kwa dhahabu safi, naye akaitandaza mikufu ya dhahabu kutoka upande moja hadi ule mwingine mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, ambako palifunikwa kwa dhahabu. |
| BSB 22 So he overlaid with gold the whole interior of the temple, until everything was completely finished. He also overlaid with gold the entire altar that belonged to the inner sanctuary. | SWKCV 22 Basi akafunika sehemu yote ya ndani kwa dhahabu. Pia akafunika madhabahu yale yaliyokuwa ndani ya Patakatifu pa Patakatifu kwa dhahabu. |
| BSB 23 In the inner sanctuary he made two cherubim, each ten cubits high, out of olive wood. | SWKCV 23 Katika Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza makerubi wawili kwa mzeituni, kila moja likiwa na dhiraa kumi kwenda juu. |
| BSB 24 One wing of the first cherub was five cubits long, and the other wing was five cubits long as well. So the full wingspan was ten cubits. | SWKCV 24 Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa dhiraa tano na bawa jingine dhiraa tano, hivyo urefu kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa jingine ulikuwa dhiraa kumi. |
| BSB 25 The second cherub also measured ten cubits; both cherubim had the same size and shape, | SWKCV 25 Kerubi wa pili alikuwa na urefu wa dhiraa kumi pia, hivyo makerubi hao wawili walifanana kwa vipimo na kwa umbo. |
| BSB 26 and the height of each cherub was ten cubits. | SWKCV 26 Kimo cha kila kerubi kilikuwa dhiraa kumi. |
| BSB 27 And he placed the cherubim inside the innermost room of the temple. Since their wings were spread out, the wing of the first cherub touched one wall, while the wing of the second cherub touched the other wall, and in the middle of the room their wingtips touched. | SWKCV 27 Aliwaweka makerubi hao ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pa Hekalu, mabawa yake yakiwa yamekunjuliwa. Bawa la kerubi mmoja liligusa ukuta mmoja, wakati bawa la yule mwingine liligusa ukuta mwingine, nayo mabawa yao mengine yaligusana katikati ya chumba. |
| BSB 28 He also overlaid the cherubim with gold. | SWKCV 28 Akafunika wale makerubi kwa dhahabu. |
| BSB 29 Then he carved the walls all around the temple, in both the inner and outer sanctuaries, with carved engravings of cherubim, palm trees, and open flowers. | SWKCV 29 Juu ya kuta zote zilizozunguka Hekalu, za vyumba vya ndani na vya nje, zilipambwa kwa nakshi zilizokatwa za makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua. |
| BSB 30 And he overlaid the temple floor with gold in both the inner and outer sanctuaries. | SWKCV 30 Pia alifunika sakafu zote za vyumba vya ndani na vya nje vya Hekalu kwa dhahabu. |
| BSB 31 For the entrance to the inner sanctuary, Solomon constructed doors of olive wood with five-sided doorposts. | SWKCV 31 Kwa ingilio la Patakatifu pa Patakatifu akatengeneza milango ya mbao za mzeituni, zikiwa na miimo na vizingiti vyenye umbo la pembe tano. |
| BSB 32 The double doors were made of olive wood, and he carved into them cherubim, palm trees, and open flowers and overlaid the cherubim and palm trees with hammered gold. | SWKCV 32 Juu ya milango miwili ya mbao za mzeituni alinakshi makerubi, miti ya mitende pamoja na maua yaliyochanua na kufunika makerubi na miti ya mitende kwa dhahabu iliyofuliwa. |
| BSB 33 In the same way he made four-sided doorposts of olive wood for the sanctuary entrance. | SWKCV 33 Kwa njia iyo hiyo akatengeneza miimo yenye pande nne ya miti ya mizeituni, kwa ajili ya ingilio la ukumbi mkubwa. |
| BSB 34 The two doors were made of cypress wood, and each had two folding panels. | SWKCV 34 Kulikuwa na milango miwili iliyoweza kukunjuka iliyotengenezwa kwa mbao za msunobari na kila mmoja ulikuwa na bawaba ambazo zingeuwezesha kujikunja kila kipande juu ya kingine. |
| BSB 35 He carved into them cherubim, palm trees, and open flowers, and he overlaid them with gold hammered evenly over the carvings. | SWKCV 35 Akanakshi makerubi, miti ya mitende na maua yaliyochanua juu yake na kufunika kwa dhahabu iliyonyooshwa vizuri juu ya michoro. |
| BSB 36 Solomon built the inner courtyard with three rows of dressed stone and one row of trimmed cedar beams. | SWKCV 36 Tena akajenga ua wa ndani safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa. |
| BSB 37 The foundation of the house of the LORD was laid in the fourth year of Solomon’s reign, in the month of Ziv. | SWKCV 37 Msingi wa Hekalu la Bwana uliwekwa katika mwaka wa nne, katika mwezi wa Zivu, ndio mwezi wa tano. |
| BSB 38 In the eleventh year, in the month of Bul, the eighth month, the temple was finished in every detail and according to every specification. So he built the temple in seven years. | SWKCV 38 Katika mwaka wa kumi na moja, mwezi wa Buli, ndio mwezi wa nane, Hekalu lilikamilika katika hatua zake zote kwa kufuatana na maelekezo yake Solomoni. Alilijenga kwa miaka saba. |
Questions about 1 Kings 6? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.