1 Samuel 30
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 On the third day David and his men arrived in Ziklag, and the Amalekites had raided the Negev, attacked Ziklag, and burned it down. | SWKCV 1 Daudi na watu wake wakafika Siklagi siku ya tatu. Basi Waamaleki walikuwa wamevamia Negebu na Siklagi. Wakawa wameshambulia mji wa Siklagi na kuuteketeza kwa moto, |
| BSB 2 They had taken captive the women and all who were there, both young and old. They had not killed anyone, but had carried them off as they went on their way. | SWKCV 2 nao wakawa wamewachukua mateka wanawake pamoja na wote waliokuwamo humo, vijana na wazee. Hawakuua yeyote, bali waliwachukua wakaenda zao. |
| BSB 3 When David and his men came to the city, they found it burned down and their wives and sons and daughters taken captive. | SWKCV 3 Daudi na watu wake walipofika Siklagi, wakakuta mji umeangamizwa kwa moto na wake zao pamoja na wana wao na binti zao wamechukuliwa mateka. |
| BSB 4 So David and the troops with him lifted up their voices and wept until they had no strength left to weep. | SWKCV 4 Hivyo Daudi na watu wake wakapiga yowe mpaka wakaishiwa na nguvu za kulia. |
| BSB 5 David’s two wives, Ahinoam of Jezreel and Abigail the widow of Nabal of Carmel, had been taken captive. | SWKCV 5 Wake wawili wa Daudi walikuwa wametekwa: yaani Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. |
| BSB 6 And David was greatly distressed because the people spoke of stoning him, because the soul of every man grieved for his sons and daughters. But David found strength in the LORD his God. | SWKCV 6 Daudi alihuzunika sana kwa sababu watu walikuwa wakisemezana juu ya kumpiga kwa mawe. Kila mmoja alikuwa na uchungu rohoni kwa sababu ya wanawe na binti zake. Lakini Daudi akajitia nguvu katika Bwana, Mungu wake. |
| BSB 7 Then David said to Abiathar the priest, the son of Ahimelech, “Bring me the ephod.” So Abiathar brought it to him, | SWKCV 7 Kisha Daudi akamwambia kuhani Abiathari mwana wa Ahimeleki, “Niletee kisibau.” Abiathari akamletea, |
| BSB 8 and David inquired of the LORD: “Should I pursue these raiders? Will I overtake them?” “Pursue them,” the LORD replied, “for you will surely overtake them and rescue the captives.” | SWKCV 8 naye Daudi akamuuliza Bwana, “Je, nifuatie kundi hili la wavamizi? Je, nitawapata?” Bwana akajibu, “Wafuatie. Hakika utawapata na utafanikiwa kuwaokoa.” |
| BSB 9 So David and his six hundred men went to the Brook of Besor, where some stayed behind | SWKCV 9 Daudi pamoja na watu wake 600 wakafika kwenye Bonde la Besori, mahali ambapo wengine waliachwa nyuma, |
| BSB 10 because two hundred men were too exhausted to cross the brook. But David and four hundred men continued in pursuit. | SWKCV 10 kwa kuwa watu 200 walikuwa wamechoka sana kuweza kuvuka hilo bonde. Lakini Daudi pamoja na watu 400 wakaendelea kufuatia. |
| BSB 11 Now his men found an Egyptian in the field and brought him to David. They gave the man water to drink and food to eat— | SWKCV 11 Wakamkuta Mmisri katika shamba fulani, nao wakamleta kwa Daudi. Wakampa huyo Mmisri maji ya kunywa na chakula; |
| BSB 12 a piece of a fig cake and two clusters of raisins. So he ate and was revived, for he had not had any food or water for three days and three nights. | SWKCV 12 kipande cha andazi la tini na andazi la zabibu zilizokaushwa. Akala naye akapata nguvu, kwa kuwa hakuwa amekula chakula chochote wala kunywa maji kwa siku tatu usiku na mchana. |
| BSB 13 Then David asked him, “To whom do you belong, and where are you from?” “I am an Egyptian,” he replied, “the slave of an Amalekite. My master abandoned me three days ago when I fell ill. | SWKCV 13 Daudi akamuuliza, “Wewe ni wa nani, na umetoka wapi?” Akajibu, “Mimi ni Mmisri, mtumwa wa Mwamaleki. Bwana wangu alinitelekeza nilipougua siku tatu zilizopita. |
| BSB 14 We raided the Negev of the Cherethites, the territory of Judah, and the Negev of Caleb, and we burned down Ziklag.” | SWKCV 14 Tulivamia Negebu ya Wakerethi, na nchi ya Yuda, na Negebu ya Kalebu. Nasi tulichoma moto Siklagi.” |
| BSB 15 “Will you lead me to these raiders?” David asked. And the man replied, “Swear to me by God that you will not kill me or deliver me into the hand of my master, and I will lead you to them.” | SWKCV 15 Daudi akamuuliza, “Je, unaweza kuniongoza kufikia kundi hili la uvamizi?” Akajibu, “Niapie mbele ya Mungu kwamba hutaniua wala kunikabidhi mikononi mwa bwana wangu, nami nitakupeleka hadi waliko.” |
| BSB 16 So he led David down, and there were the Amalekites spread out over all the land, eating, drinking, and celebrating the great amount of plunder they had taken from the land of the Philistines and the land of Judah. | SWKCV 16 Akamwongoza Daudi mpaka mahali walipokuwa, nao walikuwa wametawanyika eneo lote, wakila, wakinywa na wakifanya karamu kwa sababu ya nyara nyingi walizochukua kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka Yuda. |
| BSB 17 And David struck them down from twilight until the evening of the next day. Not a man escaped, except four hundred young men who fled, riding off on camels. | SWKCV 17 Daudi akapigana nao kuanzia machweo ya jua hadi kesho yake jioni, na hakuna yeyote miongoni mwao aliyetoroka, isipokuwa vijana wanaume 400 waliopanda ngamia na kutoroka. |
| BSB 18 So David recovered everything the Amalekites had taken, including his two wives. | SWKCV 18 Daudi akarudisha kila kitu Waamaleki walikuwa wamechukua, pamoja na wake zake wawili. |
| BSB 19 Nothing was missing, young or old, son or daughter, or any of the plunder the Amalekites had taken. David brought everything back. | SWKCV 19 Hakuna chochote kilichopotea: kijana au mzee, mvulana au msichana, nyara au kitu kingine chochote walichokuwa wamechukua. Daudi akarudisha kila kitu. |
| BSB 20 And he took all the flocks and herds, which his men drove ahead of the other livestock, calling out, “This is David’s plunder!” | SWKCV 20 Akachukua makundi yote ya kondoo, mbuzi na ngʼombe, nao watu wake wakawaswaga wanyama hao mbele ya wanyama wengine wa kufugwa, wakisema, “Hizi ni nyara za Daudi.” |
| BSB 21 When David came to the two hundred men who had been too exhausted to follow him and who were left behind at the Brook of Besor, they came out to meet him and the troops with him. As David approached the men, he greeted them, | SWKCV 21 Kisha Daudi akafika kwa wale watu 200 waliokuwa wamechoka sana kumfuata na ambao waliachwa nyuma kwenye Bonde la Besori. Wakatoka kwenda kumlaki Daudi na wale watu aliokuwa nao. Daudi na watu wake walipowakaribia, akawasalimu. |
| BSB 22 but all the wicked and worthless men among those who had gone with David said, “Because they did not go with us, we will not share with them the plunder we recovered, except for each man’s wife and children. They may take them and go.” | SWKCV 22 Lakini watu wote waovu na wakorofi miongoni mwa wafuasi wa Daudi wakasema, “Kwa sababu hawakwenda pamoja nasi, hatutagawana nao nyara tulizorudisha. Lakini, kila mtu aweza kuchukua mkewe na watoto wake na kuondoka.” |
| BSB 23 But David said, “My brothers, you must not do this with what the LORD has given us. He has protected us and delivered into our hands the raiders who came against us. | SWKCV 23 Daudi akajibu, “La hasha, ndugu zangu, kamwe hamwezi kufanya hivyo kwa kile ambacho Bwana ametupatia. Yeye ametulinda na kuweka mikononi mwetu majeshi yale yaliyokuja kupigana dhidi yetu. |
| BSB 24 Who will listen to your proposal? The share of the one who went to battle will match the share of the one who stayed with the supplies. They will share alike.” | SWKCV 24 Ni nani atasikiliza yale mnayosema? Fungu la mtu aliyekaa na vyombo litakuwa sawa na la yule aliyekwenda vitani. Wote watashiriki sawa.” |
| BSB 25 And so it has been from that day forward. David established this statute and ordinance for Israel to this very day. | SWKCV 25 Daudi akafanya hili liwe amri na agizo kwa Israeli kutoka siku ile hata leo. |
| BSB 26 When David arrived in Ziklag, he sent some of the plunder to his friends, the elders of Judah, saying, “Here is a gift for you from the plunder of the LORD’s enemies.” | SWKCV 26 Daudi alipofika Siklagi, akatuma baadhi ya nyara kwa wazee wa Yuda, waliokuwa rafiki zake, akasema, “Tazama, hapa kuna zawadi kwa ajili yenu kutoka nyara za adui za Bwana.” |
| BSB 27 He sent gifts to those in Bethel, Ramoth Negev, and Jattir; | SWKCV 27 Akazituma kwa wale waliokuwa Betheli, Ramoth-Negebu na Yatiri; |
| BSB 28 to those in Aroer, Siphmoth, and Eshtemoa; | SWKCV 28 kwa wale walioko Aroeri, Sifmothi, Eshtemoa |
| BSB 29 to those in Racal and in the cities of the Jerahmeelites and Kenites; | SWKCV 29 na Rakali; kwa wale waliokuwa katika miji ya Wayerameeli na ya Wakeni; |
| BSB 30 to those in Hormah, Bor-ashan, and Athach; | SWKCV 30 na kwa wale walioko Horma, Bori-Ashani, Athaki, |
| BSB 31 and to those in Hebron and in all the places where David and his men had roamed. | SWKCV 31 na kwa wakazi wa Hebroni; na kwa wale waliokuwa mahali pengine pote ambako Daudi na watu wake walitembelea. |
Questions about 1 Samuel 30? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.