Exodus 26
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “You are to construct the tabernacle itself with ten curtains of finely spun linen, each with blue, purple, and scarlet yarn, and cherubim skillfully worked into them. | SWKCV 1 “Tengeneza maskani kwa mapazia kumi ya kitani iliyosokotwa vizuri na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, naye fundi stadi atatarizi makerubi kwenye mapazia hayo. |
| BSB 2 Each curtain shall be twenty-eight cubits long and four cubits wide—all curtains the same size. | SWKCV 2 Mapazia yote yatatoshana kwa ukubwa: kila moja litakuwa na urefu wa dhiraa ishirini na nane, na upana wa dhiraa nne |
| BSB 3 Five of the curtains are to be joined together, and the other five joined as well. | SWKCV 3 Unganisha mapazia matano pamoja; fanya vivyo hivyo kwa hayo mengine matano. |
| BSB 4 Make loops of blue material on the edge of the end curtain in the first set, and do the same for the end curtain in the second set. | SWKCV 4 Tengeneza vitanzi vya kitambaa cha buluu kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu la kwanza, na ufanye vivyo hivyo na pazia la fungu la mwisho. |
| BSB 5 Make fifty loops on one curtain and fifty loops on the end curtain of the second set, so that the loops line up opposite one another. | SWKCV 5 Fanya vitanzi hamsini katika pazia mmoja, na vitanzi vingine hamsini kwenye pazia la mwisho la fungu hilo lingine, nazo vitanzi vyote vielekeane. |
| BSB 6 Make fifty gold clasps as well, and join the curtains together with the clasps, so that the tabernacle will be a unit. | SWKCV 6 Kisha tengeneza vifungo hamsini vya dhahabu ili vitumike kufunga na kuunganisha mapazia pamoja kufanya Hema liwe kitu kimoja. |
| BSB 7 You are to make curtains of goat hair for the tent over the tabernacle—eleven curtains in all. | SWKCV 7 “Tengeneza mapazia kumi na moja ya singa za mbuzi kwa ajili ya kufunika maskani. |
| BSB 8 Each of the eleven curtains is to be the same size—thirty cubits long and four cubits wide. | SWKCV 8 Mapazia hayo kumi na moja yatakuwa na kipimo kimoja, yaani urefu wa dhiraa thelathini, na upana wa dhiraa nne. |
| BSB 9 Join five of the curtains into one set and the other six into another. Then fold the sixth curtain over double at the front of the tent. | SWKCV 9 Unganisha hayo mapazia matano yawe fungu moja, na hayo mengine sita yawe fungu lingine. Kunja hilo pazia la sita mara mbili mbele ya maskani. |
| BSB 10 Make fifty loops along the edge of the end curtain in the first set, and fifty loops along the edge of the corresponding curtain in the second set. | SWKCV 10 Tengeneza vitanzi hamsini kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu moja, na vivyo hivyo kwenye upindo wa pazia la mwisho la fungu hilo lingine. |
| BSB 11 Make fifty bronze clasps and put them through the loops to join the tent together as a unit. | SWKCV 11 Kisha tengeneza vifungo hamsini vya shaba, uviingize katika vile vitanzi ili kukaza hema pamoja kuwa kitu kimoja. |
| BSB 12 As for the overlap that remains of the tent curtains, the half curtain that is left over shall hang down over the back of the tabernacle. | SWKCV 12 Kuhusu kile kipande cha ziada cha pazia la Hema, nusu ya hilo pazia lililobaki litaningʼinizwa upande wa nyuma wa Hema. |
| BSB 13 And the tent curtains will be a cubit longer on either side, and the excess will hang over the sides of the tabernacle to cover it. | SWKCV 13 Mapazia ya hema yatakuwa na urefu wa dhiraa moja zaidi pande zote, sehemu itakayobaki itaningʼinia pande zote za Hema ili kuifunika. |
| BSB 14 Also make a covering for the tent out of ram skins dyed red, and over that a covering of fine leather. | SWKCV 14 Tengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo. |
| BSB 15 You are to construct upright frames of acacia wood for the tabernacle. | SWKCV 15 “Tengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. |
| BSB 16 Each frame is to be ten cubits long and a cubit and a half wide. | SWKCV 16 Kila mhimili uwe na urefu wa dhiraa kumi na upana wa dhiraa moja na nusu, |
| BSB 17 Two tenons must be connected to each other for each frame. Make all the frames of the tabernacle in this way. | SWKCV 17 zikiwa na ndimi mbili zilizo sambamba kila mmoja na mwingine. Tengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. |
| BSB 18 Construct twenty frames for the south side of the tabernacle, | SWKCV 18 Tengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, |
| BSB 19 with forty silver bases under the twenty frames—two bases for each frame, one under each tenon. | SWKCV 19 kisha tengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. |
| BSB 20 For the second side of the tabernacle, the north side, make twenty frames | SWKCV 20 Kuhusu upande wa kaskazini wa maskani, tengeneza mihimili ishirini |
| BSB 21 and forty silver bases—two bases under each frame. | SWKCV 21 na vitako arobaini vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. |
| BSB 22 Make six frames for the rear of the tabernacle, the west side, | SWKCV 22 Kisha tengeneza mihimili sita kwa mwisho ulio mbali, yaani upande wa magharibi wa maskani, |
| BSB 23 and two frames for the two back corners of the tabernacle, | SWKCV 23 na pia utengeneze mihimili miwili ya pembe za upande ulio mbali. |
| BSB 24 coupled together from bottom to top and fitted into a single ring. These will serve as the two corners. | SWKCV 24 Katika pembe hizi mbili ni lazima mihimili yake iwe miwili kuanzia chini mpaka juu, na iingizwe kwenye pete moja; mihimili ya pembe hizi mbili itafanana. |
| BSB 25 So there are to be eight frames and sixteen silver bases—two under each frame. | SWKCV 25 Kwa hiyo itakuwepo mihimili minane, na vitako kumi na sita vya fedha, viwili chini ya kila mhimili. |
| BSB 26 You are also to make five crossbars of acacia wood for the frames on one side of the tabernacle, | SWKCV 26 “Pia tengeneza mataruma ya mti wa mshita: matano kwa ajili ya mihimili ya upande mmoja wa maskani, |
| BSB 27 five for those on the other side, and five for those on the rear side of the tabernacle, to the west. | SWKCV 27 matano kwa ajili ya mihimili ya upande mwingine, na matano kwa ajili ya mihimili ya upande wa magharibi, mwisho kabisa mwa maskani. |
| BSB 28 The central crossbar in the middle of the frames shall extend from one end to the other. | SWKCV 28 Taruma la katikati litapenya katikati ya mihimili kutoka mwisho mmoja hadi mwisho mwingine. |
| BSB 29 Overlay the frames with gold and make gold rings to hold the crossbars. Also overlay the crossbars with gold. | SWKCV 29 Funika hiyo mihimili kwa dhahabu, kisha tengeneza pete za dhahabu ambazo zitashikilia hayo mataruma. Pia funika hayo mataruma kwa dhahabu. |
| BSB 30 So you are to set up the tabernacle according to the pattern shown you on the mountain. | SWKCV 30 “Simamisha Hema sawasawa na mfano ulioonyeshwa kule mlimani. |
| BSB 31 Make a veil of blue, purple, and scarlet yarn, and finely spun linen, with cherubim skillfully worked into it. | SWKCV 31 “Tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, naye fundi stadi atirizi makerubi kwenye hilo pazia. |
| BSB 32 Hang it with gold hooks on four posts of acacia wood, overlaid with gold and standing on four silver bases. | SWKCV 32 Litundike kwa kulabu za dhahabu kwenye nguzo nne za mti wa mshita ambazo zimefunikwa kwa dhahabu, zikiwa zimesimamishwa kwenye vitako vinne vya fedha. |
| BSB 33 And hang the veil from the clasps and place the ark of the Testimony behind the veil. So the veil will separate the Holy Place from the Most Holy Place. | SWKCV 33 Ningʼiniza pazia hilo kwenye vifungo, kisha weka Sanduku la Ushuhuda nyuma ya pazia. Pazia litatenganisha Mahali Patakatifu kutoka Patakatifu pa Patakatifu. |
| BSB 34 Put the mercy seat on the ark of the Testimony in the Most Holy Place. | SWKCV 34 Weka kifuniko cha kiti cha rehema juu ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. |
| BSB 35 And place the table outside the veil on the north side of the tabernacle, and put the lampstand opposite the table, on the south side. | SWKCV 35 Weka meza nje ya pazia upande wa kaskazini wa Hema, kisha weka kinara cha taa upande wa kusini wa Hema. |
| BSB 36 For the entrance to the tent, you are to make a curtain embroidered with blue, purple, and scarlet yarn, and finely spun linen. | SWKCV 36 “Kwa ajili ya ingilio la hema, tengeneza pazia la nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa vizuri, kazi ya mtarizi. |
| BSB 37 Make five posts of acacia wood for the curtain, overlay them with gold, use hooks of gold, and cast five bronze bases for them. | SWKCV 37 Tengeneza kulabu za dhahabu kwa ajili ya hilo pazia, na nguzo tano za mshita zilizofunikwa kwa dhahabu. Kisha mimina vitako vitano vya shaba kwa ajili yake. |
Questions about Exodus 26? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.