Genesis 26
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now there was another famine in the land, subsequent to the one that had occurred in Abraham’s time. And Isaac went to Abimelech king of the Philistines at Gerar. | SWKCV 1 Basi njaa kubwa ikawa katika nchi hiyo, kuliko ile njaa iliyotangulia iliyotokea wakati wa Abrahamu. Isaki akamwendea Abimeleki mfalme wa Wafilisti huko Gerari. |
| BSB 2 The LORD appeared to Isaac and said, “Do not go down to Egypt. Settle in the land where I tell you. | SWKCV 2 Bwana akamtokea Isaki, akamwambia, “Usiende Misri, bali ukae katika nchi nitakayokuambia. |
| BSB 3 Stay in this land as a foreigner, and I will be with you and bless you. For I will give all these lands to you and your offspring, and I will confirm the oath that I swore to your father Abraham. | SWKCV 3 Kaa katika nchi hii kwa kitambo, mimi nitakuwa pamoja na wewe na nitakubariki. Kwa maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote na nitatimiza kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako. |
| BSB 4 I will make your descendants as numerous as the stars in the sky, and I will give them all these lands, and through your offspring all nations of the earth will be blessed, | SWKCV 4 Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa, |
| BSB 5 because Abraham listened to My voice and kept My charge, My commandments, My statutes, and My laws.” | SWKCV 5 kwa sababu Abrahamu alinitii mimi akatunza kanuni zangu na maagizo yangu, amri zangu pamoja na sheria zangu.” |
| BSB 6 So Isaac settled in Gerar. | SWKCV 6 Hivyo Isaki akaishi huko Gerari. |
| BSB 7 But when the men of that place asked about his wife, he said, “She is my sister.” For he was afraid to say, “She is my wife,” since he thought to himself, “The men of this place will kill me on account of Rebekah, because she is so beautiful.” | SWKCV 7 Watu wa mahali pale walipomuuliza habari za mke wake, akasema, “Huyu ni dada yangu,” kwa sababu aliogopa kusema, “Huyu ni mke wangu.” Alifikiri, “Watu wa mahali pale wataweza kumuua kwa sababu ya Rebeka, kwa kuwa alikuwa mzuri wa sura.” |
| BSB 8 When Isaac had been there a long time, Abimelech king of the Philistines looked down from the window and was surprised to see Isaac caressing his wife Rebekah. | SWKCV 8 Wakati Isaki alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki mfalme wa Wafilisti akachungulia dirishani, akaona jinsi Isaki alivyomkumbatia Rebeka mke wake. |
| BSB 9 Abimelech sent for Isaac and said, “So she is really your wife! How could you say, ‘She is my sister’?” Isaac replied, “Because I thought I might die on account of her.” | SWKCV 9 Abimeleki akamwita Isaki akamwambia, “Hakika huyu ni mke wako! Mbona uliniambia, ‘Huyu ni dada yangu?’” Isaki akamjibu, “Kwa sababu nilifikiri ningeweza kuuawa kwa sababu yake.” |
| BSB 10 “What is this you have done to us?” asked Abimelech. “One of the people could easily have slept with your wife, and you would have brought guilt upon us.” | SWKCV 10 Ndipo Abimeleki akamjibu, “Ni nini hiki ulichotufanyia? Ingewezekana mtu yeyote akawa amekutana kimwili na mke wako, nawe ungeleta hatia juu yetu.” |
| BSB 11 So Abimelech warned all the people, saying, “Whoever harms this man or his wife will surely be put to death.” | SWKCV 11 Hivyo Abimeleki akatoa amri kwa watu wote, akisema, “Yeyote atakayemnyanyasa mtu huyu au mkewe hakika atauawa.” |
| BSB 12 Now Isaac sowed seed in the land, and that very year he reaped a hundredfold. And the LORD blessed him, | SWKCV 12 Isaki akapanda mazao katika nchi hiyo, kwa mwaka huo huo, akavuna mara mia, kwa sababu Bwana alimbariki. |
| BSB 13 and he became richer and richer, until he was exceedingly wealthy. | SWKCV 13 Isaki akawa tajiri, mali zake zikaendelea kuongezeka mpaka akawa tajiri sana. |
| BSB 14 He owned so many flocks and herds and servants that the Philistines envied him. | SWKCV 14 Akawa na mifugo ya kondoo na ngʼombe, na watumishi wengi sana, kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu. |
| BSB 15 So the Philistines took dirt and stopped up all the wells that his father’s servants had dug in the days of his father Abraham. | SWKCV 15 Kwa hiyo visima vyote vilivyochimbwa na watumishi wakati wa Abrahamu baba yake, Wafilisti wakavifukia, wakavijaza udongo. |
| BSB 16 Then Abimelech said to Isaac, “Depart from us, for you are much too powerful for us.” | SWKCV 16 Ndipo Abimeleki akamwambia Isaki, “Ondoka kwetu, kwa maana umetuzidi nguvu sana.” |
| BSB 17 So Isaac left that place and encamped in the Valley of Gerar and settled there. | SWKCV 17 Basi Isaki akatoka huko akajenga kambi katika Bonde la Gerari, akaishi huko. |
| BSB 18 Isaac reopened the wells that had been dug in the days of his father Abraham, which the Philistines had stopped up after Abraham died. And he gave these wells the same names his father had given them. | SWKCV 18 Ndipo Isaki akavichimbua tena vile visima vya maji ambavyo vilichimbwa siku zile za Abrahamu baba yake, ambavyo Wafilisti walivifukia baada ya kufa Abrahamu, akavipa majina yale yale ambayo baba yake alikuwa amevipa. |
| BSB 19 Then Isaac’s servants dug in the valley and found a well of fresh water there. | SWKCV 19 Watumishi wa Isaki wakachimba katika lile bonde wakagundua huko kisima chenye maji safi. |
| BSB 20 But the herdsmen of Gerar quarreled with Isaac’s herdsmen and said, “The water is ours!” So he named the well Esek, because they contended with him. | SWKCV 20 Lakini wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaki wakisema, “Maji haya ni yetu!” Ndipo akakiita kile kisima Eseki, kwa sababu waligombana naye. |
| BSB 21 Then they dug another well and quarreled over that one also; so he named it Sitnah. | SWKCV 21 Kisha wakachimba kisima kingine, lakini hata hicho pia wakakigombania, akakiita Sitna. |
| BSB 22 He moved on from there and dug another well, and they did not quarrel over it. He named it Rehoboth and said, “At last the LORD has made room for us, and we will be fruitful in the land.” | SWKCV 22 Akaondoka huko, akachimba kisima kingine, wala hakuna yeyote aliyekigombania. Akakiita Rehobothi, akisema, “Sasa Bwana ametufanyia nafasi, nasi tutastawi katika nchi.” |
| BSB 23 From there Isaac went up to Beersheba, | SWKCV 23 Kutoka pale akaenda Beer-Sheba. |
| BSB 24 and that night the LORD appeared to him and said, “I am the God of your father Abraham. Do not be afraid, for I am with you. I will bless you and multiply your descendants for the sake of My servant Abraham.” | SWKCV 24 Usiku ule Bwana akamtokea, akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa Abrahamu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi niko pamoja nawe, nitakubariki na kuongeza idadi ya wazao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.” |
| BSB 25 So Isaac built an altar there and called on the name of the LORD, and he pitched his tent there. His servants also dug a well there. | SWKCV 25 Isaki akajenga madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Akapiga hema lake huko, nao watumishi wake wakachimba kisima. |
| BSB 26 Later, Abimelech came to Isaac from Gerar, with Ahuzzath his adviser and Phicol the commander of his army. | SWKCV 26 Wakati huo, Abimeleki alikuwa amemjia kutoka Gerari, akifuatana na Ahuzathi mshauri wake, pamoja na Fikoli jemadari wa majeshi yake. |
| BSB 27 “Why have you come to me?” Isaac asked them. “You hated me and sent me away.” | SWKCV 27 Isaki akawauliza, “Mbona mmekuja kwangu na ninyi mlinichukia na kunifukuza?” |
| BSB 28 “We can plainly see that the LORD has been with you,” they replied. “We recommend that there should now be an oath between us and you. Let us make a covenant with you | SWKCV 28 Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwa Bwana alikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu, kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe |
| BSB 29 that you will not harm us, just as we have not harmed you but have done only good to you, sending you on your way in peace. And now you are blessed by the LORD.” | SWKCV 29 kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na Bwana.’” |
| BSB 30 So Isaac prepared a feast for them, and they ate and drank. | SWKCV 30 Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa. |
| BSB 31 And they got up early the next morning and swore an oath to each other. Then Isaac sent them on their way, and they left him in peace. | SWKCV 31 Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani. |
| BSB 32 On that same day, Isaac’s servants came and told him about the well they had dug. “We have found water!” they told him. | SWKCV 32 Siku hiyo watumishi wa Isaki wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!” |
| BSB 33 So he called it Shibah, and to this day the name of the city is Beersheba. | SWKCV 33 Naye akakiita Shiba, mpaka leo mji huo unaitwa Beer-Sheba. |
| BSB 34 When Esau was forty years old, he took as his wives Judith daughter of Beeri the Hittite and Basemath daughter of Elon the Hittite. | SWKCV 34 Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akamwoa Yudithi binti Beeri Mhiti, kisha akamwoa Basemathi binti Eloni Mhiti. |
| BSB 35 And they brought grief to Isaac and Rebekah. | SWKCV 35 Hawa walikuwa chanzo cha huzuni ya Isaki na Rebeka. |
Questions about Genesis 26? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.