Genesis 31
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now Jacob heard that Laban’s sons were saying, “Jacob has taken away all that belonged to our father and built all this wealth at our father’s expense.” | SWKCV 1 Yakobo akawasikia wana wa Labani wakisema, “Yakobo amechukua kila kitu kilichokuwa cha baba yetu naye amepata utajiri huu wote kutokana na vile vilivyokuwa mali ya baba yetu.” |
| BSB 2 And Jacob saw from the countenance of Laban that his attitude toward him had changed. | SWKCV 2 Yakobo akatambua kwamba moyo wa Labani kwake haukuwa kama ulivyokuwa mwanzo. |
| BSB 3 Then the LORD said to Jacob, “Go back to the land of your fathers and to your kindred, and I will be with you.” | SWKCV 3 Ndipo Bwana akamwambia Yakobo, “Rudi katika nchi ya baba zako na kwa watu wako, nami nitakuwa pamoja nawe.” |
| BSB 4 So Jacob sent word and called Rachel and Leah to the field where his flocks were, | SWKCV 4 Hivyo Yakobo akatuma ujumbe kwa Raheli na Lea waje machungani yalikokuwa makundi yake. |
| BSB 5 and he told them, “I can see from your father’s countenance that his attitude toward me has changed; but the God of my father has been with me. | SWKCV 5 Akawaambia, “Naona moyo wa baba yenu kwangu sivyo kama ulivyokuwa mwanzoni, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami. |
| BSB 6 You know that I have served your father with all my strength. | SWKCV 6 Mnajua kwamba nimemtumikia baba yenu kwa nguvu zangu zote, |
| BSB 7 And although he has cheated me and changed my wages ten times, God has not allowed him to harm me. | SWKCV 7 hata hivyo baba yenu amenidanganya kwa kubadilisha ujira wangu mara kumi. Hata hivyo, Mungu hakumruhusu kunidhuru. |
| BSB 8 If he said, ‘The speckled will be your wages,’ then the whole flock bore speckled offspring. If he said, ‘The streaked will be your wages,’ then the whole flock bore streaked offspring. | SWKCV 8 Kama alisema, ‘Wenye madoadoa watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye madoadoa, kama alisema, ‘Wenye mistari watakuwa ujira wako,’ basi makundi yote yalizaa wenye mistari. |
| BSB 9 Thus God has taken away your father’s livestock and given them to me. | SWKCV 9 Hivyo Mungu amechukua mifugo ya baba yenu na amenipa mimi. |
| BSB 10 When the flocks were breeding, I saw in a dream that the streaked, spotted, and speckled males were mating with the females. | SWKCV 10 “Wakati fulani majira ya kuzaliana niliota ndoto ambayo niliinua macho na kuona kwamba wale mabeberu waliokuwa wakipanda kundi walikuwa wa mistari, madoadoa na mabakabaka. |
| BSB 11 In that dream the angel of God said to me, ‘Jacob!’ And I replied, ‘Here I am.’ | SWKCV 11 Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, ‘Yakobo.’ Nikamjibu, ‘Mimi hapa.’ |
| BSB 12 ‘Look up,’ he said, ‘and see that all the males that are mating with the flock are streaked, spotted, or speckled; for I have seen all that Laban has done to you. | SWKCV 12 Akasema, ‘Inua macho yako uone wale mabeberu wote wanaopanda kundi wana mistari, madoadoa au mabakabaka, kwa maana nimeona yale yote ambayo Labani amekuwa akikutendea. |
| BSB 13 I am the God of Bethel, where you anointed the pillar and made a solemn vow to Me. Now get up, leave this land at once, and return to your native land.’” | SWKCV 13 Mimi ndiye Mungu wa Betheli, ulikomiminia ile nguzo mafuta na pale mahali uliponiwekea nadhiri. Sasa ondoka katika nchi hii mara moja urudi katika nchi uliyozaliwa.’” |
| BSB 14 And Rachel and Leah replied, “Do we have any portion or inheritance left in our father’s house? | SWKCV 14 Ndipo Raheli na Lea wakajibu, “Je bado tu tunalo fungu lolote katika urithi wa nyumba ya baba yetu? |
| BSB 15 Are we not regarded by him as outsiders? Not only has he sold us, but he has certainly squandered what was paid for us. | SWKCV 15 Je, yeye hatuhesabu sisi kama wageni? Sio kwamba ametuuza tu, bali ametumia hata na vile vilivyolipwa kwa ajili yetu. |
| BSB 16 Surely all the wealth that God has taken away from our father belongs to us and to our children. So do whatever God has told you.” | SWKCV 16 Hakika utajiri wote ambao Mungu ameuchukua kutoka kwa baba yetu ni mali yetu na watoto wetu. Hivyo fanya lolote lile Mungu alilokuambia.” |
| BSB 17 Then Jacob got up and put his children and his wives on camels, | SWKCV 17 Ndipo Yakobo akawapandisha watoto wake na wake zake juu ya ngamia, |
| BSB 18 and he drove all his livestock before him, along with all the possessions he had acquired in Paddan-aram, to go to his father Isaac in the land in Canaan. | SWKCV 18 naye akawaswaga wanyama wote mbele yake pamoja na vitu vyote alivyokuwa amechuma huko Padan-Aramu kwenda kwa baba yake Isaki katika nchi ya Kanaani. |
| BSB 19 Now while Laban was out shearing his sheep, Rachel stole her father’s household idols. | SWKCV 19 Labani alipokuwa amekwenda kukata kondoo wake manyoya, Raheli aliiba miungu ya nyumba ya baba yake. |
| BSB 20 Moreover, Jacob deceived Laban the Aramean by not telling him that he was running away. | SWKCV 20 Zaidi ya hayo, Yakobo alimdanganya Labani Mwaramu kwa kutokumwambia kwamba anakimbia. |
| BSB 21 So he fled with all his possessions, crossed the Euphrates, and headed for the hill country of Gilead. | SWKCV 21 Hivyo akakimbia pamoja na vitu vyote alivyokuwa navyo na kuvuka Mto Frati akaelekea nchi ya vilima katika Gileadi. |
| BSB 22 On the third day Laban was informed that Jacob had fled. | SWKCV 22 Siku ya tatu Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia. |
| BSB 23 So he took his relatives with him, pursued Jacob for seven days, and overtook him in the hill country of Gilead. | SWKCV 23 Akiwachukua jamaa zake, akamfuatia Yakobo kwa siku saba na kumkuta kwenye nchi ya vilima katika Gileadi. |
| BSB 24 But that night God came to Laban the Aramean in a dream and warned him, “Be careful not to say anything to Jacob, either good or bad.” | SWKCV 24 Ndipo Mungu akamjia Labani Mwaramu katika ndoto usiku na kumwambia, “Jihadhari usiseme neno lolote kwa Yakobo, liwe zuri au baya.” |
| BSB 25 Now Jacob had pitched his tent in the hill country of Gilead when Laban overtook him, and Laban and his relatives camped there as well. | SWKCV 25 Yakobo alikuwa amepiga hema lake katika nchi ya vilima katika Gileadi wakati Labani alipomkuta, Labani na jamaa yake wakapiga kambi huko pia. |
| BSB 26 Then Laban said to Jacob, “What have you done? You have deceived me and carried off my daughters like captives of war! | SWKCV 26 Ndipo Labani akamwambia Yakobo, “Umefanya nini? Umenidanganya na umewachukua binti zangu kama mateka katika vita. |
| BSB 27 Why did you run away secretly and deceive me, without even telling me? I would have sent you away with joy and singing, with tambourines and harps. | SWKCV 27 Kwa nini ulikimbia kwa siri na kunidanganya? Kwa nini hukuniambia ili nikuage kwa furaha na nyimbo za matari na vinubi? |
| BSB 28 But you did not even let me kiss my grandchildren and my daughters goodbye. Now you have done a foolish thing. | SWKCV 28 Hata hukuniruhusu niwabusu wajukuu zangu na kuwaaga binti zangu. Umefanya kitu cha kipumbavu. |
| BSB 29 I have power to do you great harm, but last night the God of your father said to me, ‘Be careful not to say anything to Jacob, either good or bad.’ | SWKCV 29 Nina uwezo wa kukudhuru, lakini usiku uliopita Mungu wa baba yako alisema nami, akaniambia, ‘Jihadhari, usiseme neno lolote kwa Yakobo liwe zuri au baya.’ |
| BSB 30 Now you have gone off because you long for your father’s house. But why have you stolen my gods?” | SWKCV 30 Sasa umeondoka kwa sababu umetamani kurudi nyumbani kwa baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu?” |
| BSB 31 “I was afraid,” Jacob answered, “for I thought you would take your daughters from me by force. | SWKCV 31 Yakobo akamjibu Labani, “Niliogopa, kwa sababu nilifikiri ungeweza kuninyangʼanya binti zako kwa nguvu. |
| BSB 32 If you find your gods with anyone here, he shall not live! In the presence of our relatives, see for yourself if anything is yours, and take it back.” For Jacob did not know that Rachel had stolen the idols. | SWKCV 32 Lakini kama ukimkuta yeyote aliye na miungu yako, hataishi. Mbele ya jamaa yetu, angalia mwenyewe uone kama kuna chochote chako hapa nilicho nacho, kama kipo, kichukue.” Basi Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiba hiyo miungu. |
| BSB 33 So Laban went into Jacob’s tent, then Leah’s tent, and then the tents of the two maidservants, but he found nothing. Then he left Leah’s tent and entered Rachel’s tent. | SWKCV 33 Kwa hiyo Labani akaingia ndani ya hema la Yakobo na ndani ya hema la Lea na ndani ya hema la watumishi wawili wa kike, lakini hakukuta chochote. Baadaye alipotoka katika hema la Lea, akaingia hema la Raheli. |
| BSB 34 Now Rachel had taken Laban’s household idols, put them in the saddlebag of her camel, and was sitting on them. And Laban searched everything in the tent but found nothing. | SWKCV 34 Basi Raheli ndiye alikuwa amechukua ile miungu ya nyumbani kwao na kuiweka katika matandiko ya ngamia na kukalia. Labani akatafuta kila mahali kwenye hema lakini hakupata chochote. |
| BSB 35 Rachel said to her father, “Sir, do not be angry that I cannot stand up before you; for I am having my period.” So Laban searched but could not find the household idols. | SWKCV 35 Raheli akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu kwa kuwa siwezi kusimama ukiwepo, niko katika hedhi.” Labani akatafuta lakini hakuweza kuipata miungu ya nyumbani kwake. |
| BSB 36 Then Jacob became incensed and challenged Laban. “What is my crime?” he said. “For what sin of mine have you so hotly pursued me? | SWKCV 36 Yakobo akakasirika na kumshutumu Labani, akisema, “Uhalifu wangu ni nini?” Akamuuliza Labani, “Ni dhambi gani niliyofanya hata unaniwinda? |
| BSB 37 You have searched all my goods! Have you found anything that belongs to you? Put it here before my brothers and yours, that they may judge between the two of us. | SWKCV 37 Sasa kwa kuwa umepekua vitu vyangu vyote umepata nini kilicho cha nyumbani mwako? Kiweke hapa mbele ya jamaa yako na yangu, nao waamue kati yetu sisi wawili. |
| BSB 38 I have been with you for twenty years now. Your sheep and goats have not miscarried, nor have I eaten the rams of your flock. | SWKCV 38 “Mpaka sasa nimekuwa pamoja nawe miaka ishirini. Kondoo wako na mbuzi wako hawajaharibu mimba, wala sijala kondoo dume kutoka makundi yako. |
| BSB 39 I did not bring you anything torn by wild beasts; I bore the loss myself. And you demanded payment from me for what was stolen by day or night. | SWKCV 39 Sikukuletea mfugo aliyeraruliwa na wanyama pori, nilibeba hasara mimi mwenyewe. Tena ulinidai malipo kwa chochote kilichoibwa mchana au usiku. |
| BSB 40 As it was, the heat consumed me by day and the frost by night, and sleep fled from my eyes. | SWKCV 40 Hii ndiyo iliyokuwa hali yangu: Niliumia kwa joto la mchana na baridi usiku, pia usingizi ulinipa. |
| BSB 41 Thus for twenty years I have served in your household—fourteen years for your two daughters and six years for your flocks—and you have changed my wages ten times! | SWKCV 41 Ilikuwa hivi kwa miaka ile ishirini niliyokuwa nyumbani kwako. Nilikutumikia miaka ile kumi na minne kwa ajili ya binti zako wawili, miaka sita kwa ajili ya makundi yako, nawe ulibadilisha ujira wangu mara kumi. |
| BSB 42 If the God of my father, the God of Abraham and the Fear of Isaac, had not been with me, surely by now you would have sent me away empty-handed. But God has seen my affliction and the toil of my hands, and last night He rendered judgment.” | SWKCV 42 Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaki, hakuwa pamoja nami, hakika ungenifukuza mikono mitupu. Lakini Mungu ameona taabu yangu na kazi ngumu ya mikono yangu, naye usiku uliopita amekukemea.” |
| BSB 43 But Laban answered Jacob, “These daughters are my daughters, these sons are my sons, and these flocks are my flocks! Everything you see is mine! Yet what can I do today about these daughters of mine or the children they have borne? | SWKCV 43 Labani akamjibu Yakobo, “Wanawake hawa ni binti zangu, watoto hawa ni watoto wangu na makundi haya ni makundi yangu. Vyote unavyoviona ni vyangu. Lakini hata hivyo ninaweza kufanya nini kuhusu hawa binti zangu, au kuhusu watoto waliowazaa? |
| BSB 44 Come now, let us make a covenant, you and I, and let it serve as a witness between you and me.” | SWKCV 44 Njoo sasa na tufanye agano, wewe na mimi, na liwe kama shahidi kati yetu.” |
| BSB 45 So Jacob picked out a stone and set it up as a pillar, | SWKCV 45 Hivyo Yakobo akachukua jiwe, akalisimamisha kama nguzo. |
| BSB 46 and he said to his relatives, “Gather some stones.” So they took stones and made a mound, and there by the mound they ate. | SWKCV 46 Akawaambia jamaa yake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kuyakusanya yakawa lundo, wakala chakula hapo karibu na hilo lundo. |
| BSB 47 Laban called it Jegar-sahadutha, and Jacob called it Galeed. | SWKCV 47 Labani akaliita Yegar-Sahadutha na Yakobo akaliita Galeedi. |
| BSB 48 Then Laban declared, “This mound is a witness between you and me this day.” Therefore the place was called Galeed. | SWKCV 48 Labani akasema, “Lundo hili ni shahidi kati yako na mimi leo.” Ndiyo maana likaitwa Galeedi. |
| BSB 49 It was also called Mizpah, because Laban said, “May the LORD keep watch between you and me when we are absent from each other. | SWKCV 49 Pia liliitwa Mispa, kwa sababu alisema, “Bwana na aweke ulinzi kati yako na mimi wakati kila mmoja akiwa mbali na mwingine. |
| BSB 50 If you mistreat my daughters or take other wives, although no one is with us, remember that God is a witness between you and me.” | SWKCV 50 Kama ukiwatenda mabaya binti zangu au ukioa wake wengine zaidi ya binti zangu, hata ingawa hakuna hata mmoja aliye pamoja nasi, kumbuka kwamba Mungu ni shahidi kati yako na mimi.” |
| BSB 51 Laban also said to Jacob, “Here is the mound, and here is the pillar I have set up between you and me. | SWKCV 51 Pia Labani akamwambia Yakobo, “Hili ndilo lundo, na hii ndiyo nguzo niliyoisimamisha kati yako na mimi. |
| BSB 52 This mound is a witness, and this pillar is a witness, that I will not go past this mound to harm you, and you will not go past this mound and pillar to harm me. | SWKCV 52 Lundo hili ni shahidi na nguzo hii ni shahidi, kwamba sitavuka lundo hili kuja upande wako kukudhuru, nawe kwamba hutavuka lundo hili na nguzo hii kuja upande wangu kunidhuru. |
| BSB 53 May the God of Abraham and the God of Nahor, the God of their father, judge between us.” So Jacob swore by the Fear of his father Isaac. | SWKCV 53 Mungu wa Abrahamu na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba zao, aamue kati yetu.” Hivyo Yakobo akaapa kwa jina la Hofu ya baba yake Isaki. |
| BSB 54 Then Jacob offered a sacrifice on the mountain and invited his relatives to eat a meal. And after they had eaten, they spent the night on the mountain. | SWKCV 54 Yakobo akatoa dhabihu juu ya kilima na akawaalika jamaa zake kula chakula. Baada ya kula, wakalala huko. |
| BSB 55 Early the next morning, Laban got up and kissed his grandchildren and daughters and blessed them. Then he left to return home. | SWKCV 55 Kesho yake asubuhi na mapema, Labani akawabusu wajukuu zake, binti zake na kuwabariki. Kisha akaondoka, akarudi nyumbani. |
Questions about Genesis 31? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.