Genesis 35
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then God said to Jacob, “Arise, go up to Bethel, and settle there. Build an altar there to the God who appeared to you when you fled from your brother Esau.” | SWKCV 1 Kisha Mungu akamwambia Yakobo, “Panda uende Betheli ukakae huko na ukamjengee Mungu madhabahu huko, Yeye aliyekutokea ulipokuwa unamkimbia Esau ndugu yako.” |
| BSB 2 So Jacob told his household and all who were with him, “Get rid of the foreign gods that are among you. Purify yourselves and change your garments. | SWKCV 2 Hivyo Yakobo akawaambia watu wa nyumbani mwake pamoja na wote waliokuwa naye, “Iondoeni miungu ya kigeni ile iliyoko katikati yenu, jitakaseni na mkabadilishe nguo zenu. |
| BSB 3 Then let us arise and go to Bethel. I will build an altar there to God, who answered me in my day of distress. He has been with me wherever I have gone.” | SWKCV 3 Kisha njooni, twende Betheli, mahali nitakapomjengea Mungu madhabahu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, ambaye amekuwa pamoja nami popote nilipokwenda.” |
| BSB 4 So they gave Jacob all their foreign gods and all their earrings, and Jacob buried them under the oak near Shechem. | SWKCV 4 Kwa hiyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni waliyokuwa nayo, pamoja na pete zilizokuwa masikioni mwao. Yakobo akavizika chini ya mti wa mwaloni huko Shekemu. |
| BSB 5 As they set out, a terror from God fell over the surrounding cities, so that they did not pursue Jacob’s sons. | SWKCV 5 Kisha wakaondoka, na hofu ya Mungu ikawapata miji yote iliyowazunguka. Kwa hiyo hakuna aliyewafuatia wana wa Yakobo. |
| BSB 6 So Jacob and everyone with him arrived in Luz (that is, Bethel) in the land of Canaan. | SWKCV 6 Yakobo na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafika Luzu (ndio Betheli), katika nchi ya Kanaani. |
| BSB 7 There Jacob built an altar, and he called that place El-bethel, because it was there that God had revealed Himself to Jacob as he fled from his brother. | SWKCV 7 Huko akajenga madhabahu na akapaita mahali pale El-Betheli, kwa sababu mahali pale ndipo Mungu alipojifunua kwake alipokuwa akimkimbia ndugu yake. |
| BSB 8 Now Deborah, Rebekah’s nurse, died and was buried under the oak below Bethel. So Jacob named it Allon-bacuth. | SWKCV 8 Wakati huu Debora, mlezi wa Rebeka, akafa na akazikwa chini ya mti wa mwaloni ulioko chini ya Betheli. Kwa hiyo pakaitwa Alon-Bakuthi. |
| BSB 9 After Jacob had returned from Paddan-aram, God appeared to him again and blessed him. | SWKCV 9 Baada ya Yakobo kurudi kutoka Padan-Aramu, Mungu alimtokea tena na kumbariki. |
| BSB 10 And God said to him, “Though your name is Jacob, you will no longer be called Jacob. Instead, your name will be Israel.” So God named him Israel. | SWKCV 10 Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini hutaitwa tena Yakobo, jina lako utakuwa Israeli.” Kwa hiyo akamwita Israeli. |
| BSB 11 And God told him, “I am God Almighty. Be fruitful and multiply. A nation—even a company of nations—shall come from you, and kings shall descend from you. | SWKCV 11 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu Mwenyezi, ukazae na kuongezeka. Taifa na jamii ya mataifa itatoka kwako, nao wafalme watatoka viunoni mwako. |
| BSB 12 The land that I gave to Abraham and Isaac I will give to you, and I will give this land to your descendants after you.” | SWKCV 12 Nchi niliyowapa Abrahamu na Isaki nakupa wewe pia, nami nitawapa wazao wako baada yako.” |
| BSB 13 Then God went up from the place where He had spoken with him. | SWKCV 13 Kisha Mungu akapanda juu kutoka kwake mahali pale alipozungumza naye. |
| BSB 14 So Jacob set up a pillar in the place where God had spoken with him—a stone marker—and he poured out a drink offering on it and anointed it with oil. | SWKCV 14 Yakobo akasimamisha nguzo ya jiwe mahali pale Mungu alipozungumza naye, akamimina sadaka ya kinywaji juu yake, pia akamimina mafuta juu yake. |
| BSB 15 Jacob called the place where God had spoken with him Bethel. | SWKCV 15 Yakobo akapaita mahali pale Mungu alipozungumza naye Betheli. |
| BSB 16 Later, they set out from Bethel, and while they were still some distance from Ephrath, Rachel began to give birth, and her labor was difficult. | SWKCV 16 Kisha wakaondoka Betheli. Walipokuwa umbali fulani kabla ya kufika Efrathi, Raheli akaanza kusikia uchungu na alipata shida kuu. |
| BSB 17 During her severe labor, the midwife said to her, “Do not be afraid, for you are having another son.” | SWKCV 17 Alipokuwa katika shida hii katika kujifungua, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwa sababu umempata mwana mwingine.” |
| BSB 18 And with her last breath—for she was dying—she named him Ben-oni. But his father called him Benjamin. | SWKCV 18 Hapo alipopumua pumzi yake ya mwisho, kwa maana alikuwa akifa, akamwita mwanawe Benoni. Lakini babaye akamwita Benyamini. |
| BSB 19 So Rachel died and was buried on the way to Ephrath (that is, Bethlehem). | SWKCV 19 Kwa hiyo Raheli akafa, akazikwa kando ya njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu). |
| BSB 20 Jacob set up a pillar on her grave; it marks Rachel’s tomb to this day. | SWKCV 20 Juu ya kaburi lake, Yakobo akasimamisha nguzo, ambayo mpaka leo inatambulisha kaburi la Raheli. |
| BSB 21 Israel again set out and pitched his tent beyond the Tower of Eder. | SWKCV 21 Israeli akaendelea tena na safari yake na kupiga hema mbele mnara wa Ederi. |
| BSB 22 While Israel was living in that region, Reuben went in and slept with his father’s concubine Bilhah, and Israel heard about it. Jacob had twelve sons: | SWKCV 22 Wakati Israeli alipokuwa akiishi katika nchi ile, Reubeni mwanawe alikutana kimwili na suria wa baba yake aitwaye Bilha, naye Israeli akasikia jambo hili. Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili: |
| BSB 23 The sons of Leah were Reuben the firstborn of Jacob, Simeon, Levi, Judah, Issachar, and Zebulun. | SWKCV 23 Wana wa Lea walikuwa: Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zabuloni. |
| BSB 24 The sons of Rachel were Joseph and Benjamin. | SWKCV 24 Wana wa Raheli walikuwa: Yosefu na Benyamini. |
| BSB 25 The sons of Rachel’s maidservant Bilhah were Dan and Naphtali. | SWKCV 25 Wana waliozaliwa na Bilha mtumishi wa kike wa Raheli walikuwa: Dani na Naftali. |
| BSB 26 And the sons of Leah’s maidservant Zilpah were Gad and Asher. These are the sons of Jacob, who were born to him in Paddan-aram. | SWKCV 26 Wana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa: Gadi na Asheri. Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu. |
| BSB 27 Jacob returned to his father Isaac at Mamre, near Kiriath-arba (that is, Hebron), where Abraham and Isaac had stayed. | SWKCV 27 Yakobo akarudi nyumbani kwa baba yake Isaki huko Mamre, karibu na Kiriath-Arba (yaani Hebroni), ambapo walikuwa wameishi Abrahamu na Isaki. |
| BSB 28 And Isaac lived 180 years. | SWKCV 28 Isaki aliishi miaka 180. |
| BSB 29 Then he breathed his last and died and was gathered to his people, old and full of years. And his sons Esau and Jacob buried him. | SWKCV 29 Kisha Isaki akapumua pumzi yake ya mwisho akafa, akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee wa miaka mingi. Nao wanawe Esau na Yakobo wakamzika. |
Questions about Genesis 35? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.