Genesis 37
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now Jacob lived in the land where his father had resided, the land of Canaan. | SWKCV 1 Yakobo akaishi Kanaani katika nchi ambayo baba yake alikuwa ameishi. |
| BSB 2 This is the account of Jacob. When Joseph was seventeen years old, he was tending the flock with his brothers, the sons of his father’s wives Bilhah and Zilpah, and he brought their father a bad report about them. | SWKCV 2 Zifuatazo ni habari za Yakobo. Yosefu, kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akichunga makundi ya kondoo na mbuzi pamoja na ndugu zake wa mama wengine, yaani wana wa Bilha na wana wa Zilpa wake za baba yake, naye akawa akimletea baba yake taarifa mbaya kuhusu hao ndugu zake. |
| BSB 3 Now Israel loved Joseph more than his other sons, because Joseph had been born to him in his old age; so he made him a robe of many colors. | SWKCV 3 Basi, Israeli akampenda Yosefu kuliko yeyote miongoni mwa kaka zake, kwani ni mwanawe wa uzeeni, akamshonea joho lililorembwa vizuri sana. |
| BSB 4 When Joseph’s brothers saw that their father loved him more than any of them, they hated him and could not speak a kind word to him. | SWKCV 4 Ndugu zake walipoona kwamba baba yao anampenda Yosefu kuliko yeyote mwingine miongoni mwao, walimchukia na hawakusema naye neno lolote jema. |
| BSB 5 Then Joseph had a dream, and when he told it to his brothers, they hated him even more. | SWKCV 5 Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. |
| BSB 6 He said to them, “Listen to this dream I had: | SWKCV 6 Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: |
| BSB 7 We were binding sheaves of grain in the field, and suddenly my sheaf rose and stood upright, while your sheaves gathered around and bowed down to mine.” | SWKCV 7 Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.” |
| BSB 8 “Do you intend to reign over us?” his brothers asked. “Will you actually rule us?” So they hated him even more because of his dream and his statements. | SWKCV 8 Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia. |
| BSB 9 Then Joseph had another dream and told it to his brothers. “Look,” he said, “I had another dream, and this time the sun and moon and eleven stars were bowing down to me.” | SWKCV 9 Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.” |
| BSB 10 He told his father and brothers, but his father rebuked him and said, “What is this dream that you have had? Will your mother and brothers and I actually come and bow down to the ground before you?” | SWKCV 10 Alipomwambia baba yake pamoja na ndugu zake, baba yake akamkemea akisema, “Ni ndoto gani hii uliyoota? Hivi kweli mama yako na mimi na ndugu zako tutakuja kukusujudia wewe hadi nchi?” |
| BSB 11 And his brothers were jealous of him, but his father kept in mind what he had said. | SWKCV 11 Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni. |
| BSB 12 Some time later, Joseph’s brothers had gone to pasture their father’s flocks near Shechem. | SWKCV 12 Basi, ndugu zake walikuwa wamekwenda kuchunga makundi ya baba yao karibu na Shekemu, |
| BSB 13 Israel said to him, “Are not your brothers pasturing the flocks at Shechem? Get ready; I am sending you to them.” “I am ready,” Joseph replied. | SWKCV 13 naye Israeli akamwambia Yosefu, “Kama ujuavyo, ndugu zako wanachunga makundi huko karibu na Shekemu. Njoo, nitakutuma kwao.” Yosefu akajibu, “Vema sana, niko tayari.” |
| BSB 14 Then Israel told him, “Go now and see how your brothers and the flocks are faring, and bring word back to me.” So he sent him off from the Valley of Hebron. And when Joseph arrived in Shechem, | SWKCV 14 Kwa hiyo akamwambia, “Nenda uone kama mambo yote ni salama kwa ndugu zako na makundi, kisha uniletee habari.” Ndipo akamtuma Yosefu kutoka Bonde la Hebroni. Yosefu alipofika Shekemu, |
| BSB 15 a man found him wandering in the field and asked, “What are you looking for?” | SWKCV 15 mtu mmoja akamkuta akizungukazunguka mashambani na akamuuliza, “Unatafuta nini?” |
| BSB 16 “I am looking for my brothers,” Joseph replied. “Can you please tell me where they are pasturing their flocks?” | SWKCV 16 Akajibu, “Ninawatafuta ndugu zangu. Unaweza kuniambia wanachunga wapi makundi yao?” |
| BSB 17 “They have moved on from here,” the man answered. “I heard them say, ‘Let us go to Dothan.’” So Joseph set out after his brothers and found them at Dothan. | SWKCV 17 Yule mtu akajibu, “Wamehama hapa. Nilisikia wakisema, ‘Twende Dothani.’” Kwa hiyo Yosefu akawafuatilia ndugu zake na kuwakuta karibu na Dothani. |
| BSB 18 Now Joseph’s brothers saw him in the distance, and before he arrived, they plotted to kill him. | SWKCV 18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga shauri baya la kumuua. |
| BSB 19 “Here comes that dreamer!” they said to one another. | SWKCV 19 Wakaambiana, “Yule mwota ndoto anakuja! |
| BSB 20 “Come now, let us kill him and throw him into one of the pits. We can say that a vicious animal has devoured him. Then we shall see what becomes of his dreams!” | SWKCV 20 Njooni sasa, tumuue na kumtupa katika shimo mojawapo na tuseme kwamba mnyama mkali amemrarua. Kisha tutaona matokeo ya ndoto zake.” |
| BSB 21 When Reuben heard this, he tried to rescue Joseph from their hands. “Let us not take his life,” he said. | SWKCV 21 Reubeni aliposikia jambo hili, akajaribu kumwokoa kutoka mikononi mwao akasema, “Tusiutoe uhai wake. |
| BSB 22 “Do not shed his blood. Throw him into this pit in the wilderness, but do not lay a hand on him.” Reuben said this so that he could rescue Joseph from their hands and return him to his father. | SWKCV 22 Tusimwage damu yoyote. Mtupeni katika shimo lililoko hapa jangwani, lakini msimguse.” Reubeni alisema hivyo ili amwokoe kutoka mikononi mwao, kisha amrudishe nyumbani kwa baba yake. |
| BSB 23 So when Joseph came to his brothers, they stripped him of his robe—the robe of many colors he was wearing— | SWKCV 23 Kwa hiyo Yosefu alipowafikia ndugu zake, walimvua lile joho lake, lile joho lililorembwa vizuri alilokuwa amevaa. |
| BSB 24 and they took him and threw him into the pit. Now the pit was empty, with no water in it. | SWKCV 24 Kisha wakamchukua wakamtupa katika shimo. Wakati huo shimo lilikuwa tupu, halikuwa na maji ndani yake. |
| BSB 25 And as they sat down to eat a meal, they looked up and saw a caravan of Ishmaelites coming from Gilead. Their camels were carrying spices, balm, and myrrh on their way down to Egypt. | SWKCV 25 Walipokaa ili wale chakula chao, wakainua macho wakaona msafara wa Waishmaeli ukija kutoka Gileadi. Ngamia wao walikuwa wamepakizwa mizigo ya vikolezo, uvumba na manemane, nao walikuwa njiani kuvipeleka Misri. |
| BSB 26 Then Judah said to his brothers, “What profit will we gain if we kill our brother and cover up his blood? | SWKCV 26 Yuda akawaambia ndugu zake, “Tutafaidi nini ikiwa tutamuua ndugu yetu na kuificha damu yake? |
| BSB 27 Come, let us sell him to the Ishmaelites and not lay a hand on him; for he is our brother, our own flesh.” And they agreed. | SWKCV 27 Njooni, tumuuze kwa hawa Waishmaeli. Tusimguse, kwa kuwa hata hivyo yeye ni ndugu yetu, nyama yetu na damu yetu wenyewe.” Ndugu zake wakakubali. |
| BSB 28 So when the Midianite traders passed by, his brothers pulled Joseph out of the pit and sold him for twenty shekels of silver to the Ishmaelites, who took him to Egypt. | SWKCV 28 Kwa hiyo wale wafanyabiashara Wamidiani walipofika pale, ndugu zake wakamtoa Yosefu kutoka kwenye lile shimo, na kumuuza kwa shekeli ishirini za fedha kwa wale Waishmaeli, ambao walimpeleka Misri. |
| BSB 29 When Reuben returned to the pit and saw that Joseph was not there, he tore his clothes, | SWKCV 29 Reubeni aliporudi kutazama kwenye lile shimo na kuona kwamba Yosefu hayupo, alirarua nguo zake. |
| BSB 30 returned to his brothers, and said, “The boy is gone! What am I going to do?” | SWKCV 30 Akawarudia ndugu zake na kusema, “Kijana hayuko mle! Nielekee wapi sasa?” |
| BSB 31 Then they took Joseph’s robe, slaughtered a young goat, and dipped the robe in its blood. | SWKCV 31 Kisha wakalichukua lile joho la Yosefu, wakachinja mbuzi na kulichovya katika damu. |
| BSB 32 They sent the robe of many colors to their father and said, “We found this. Examine it to see whether it is your son’s robe or not.” | SWKCV 32 Wakalichukua lile joho lililorembwa vizuri na kulipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeliokota hili joho. Uchunguze uone kama ni la mwanao.” |
| BSB 33 His father recognized it and said, “It is my son’s robe! A vicious animal has devoured him. Joseph has surely been torn to pieces!” | SWKCV 33 Baba yao akalitambua akasema, “Hili ni joho la mwanangu! Mnyama mkali amemrarua. Hakika Yosefu ameraruliwa vipande vipande.” |
| BSB 34 Then Jacob tore his clothes, put sackcloth around his waist, and mourned for his son many days. | SWKCV 34 Kisha Yakobo akararua nguo zake, akavaa nguo ya gunia na kumwombolezea mwanawe kwa siku nyingi. |
| BSB 35 All his sons and daughters tried to comfort him, but he refused to be comforted. “No,” he said. “I will go down to Sheol mourning for my son.” So his father wept for him. | SWKCV 35 Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia. |
| BSB 36 Meanwhile, the Midianites sold Joseph in Egypt to Potiphar, an officer of Pharaoh and captain of the guard. | SWKCV 36 Wakati ule ule, Wamidiani wakamuuza Yosefu huko Misri kwa Potifa, mmojawapo wa maafisa wa Farao, aliyekuwa mkuu wa ulinzi. |
Questions about Genesis 37? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.