Genesis 43
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now the famine was still severe in the land. | SWKCV 1 Wakati huu njaa ilikuwa bado ni kali mno katika nchi. |
| BSB 2 So when Jacob’s sons had eaten all the grain they had brought from Egypt, their father said to them, “Go back and buy us a little more food.” | SWKCV 2 Hivyo wakati walikuwa wamemaliza kula nafaka yote waliyoileta kutoka Misri, Yakobo baba yao akawaambia, “Rudini Misri mkatununulie chakula kingine zaidi.” |
| BSB 3 But Judah replied, “The man solemnly warned us, ‘You will not see my face again unless your brother is with you.’ | SWKCV 3 Lakini Yuda akamwambia, “Mtu yule alituonya kwa msisitizo, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje na ndugu yenu.’ |
| BSB 4 If you will send our brother with us, we will go down and buy food for you. | SWKCV 4 Kama utakubali ndugu yetu aende pamoja nasi, tutakwenda kuwanunulia chakula. |
| BSB 5 But if you will not send him, we will not go; for the man told us, ‘You will not see my face again unless your brother is with you.’” | SWKCV 5 Lakini ikiwa hutamruhusu aende, hatutakwenda, kwa sababu mtu yule alituambia, ‘Hamtauona uso wangu tena mpaka mje pamoja na ndugu yenu.’” |
| BSB 6 “Why did you bring this trouble upon me?” Israel asked. “Why did you tell the man you had another brother?” | SWKCV 6 Israeli akauliza, “Kwa nini mkaniletea taabu hii kwa kumwambia yule mtu mlikuwa na ndugu mwingine?” |
| BSB 7 They replied, “The man questioned us in detail about ourselves and our family: ‘Is your father still alive? Do you have another brother?’ And we answered him accordingly. How could we possibly know that he would say, ‘Bring your brother here’?” | SWKCV 7 Wakamjibu, “Yule mtu alituhoji kwa undani sana habari zetu na za jamaa yetu. Alituuliza, ‘Je, baba yenu bado yungali hai? Je mnaye ndugu mwingine?’ Sisi tulimjibu maswali yake tu. Tungewezaje kujua kwamba angesema, ‘Mleteni mdogo wenu hapa’?” |
| BSB 8 And Judah said to his father Israel, “Send the boy with me, and we will go at once, so that we may live and not die—neither we, nor you, nor our children. | SWKCV 8 Ndipo Yuda akamwambia baba yake Israeli, “Mtume kijana pamoja nami, nasi tutaondoka mara, ili sisi na wewe pamoja na watoto wetu tuweze kuishi, wala tusife. |
| BSB 9 I will guarantee his safety. You may hold me personally responsible. If I do not bring him back and set him before you, then may I bear the guilt before you all my life. | SWKCV 9 Mimi mwenyewe nitakuhakikishia usalama wake, mimi mwenyewe nitawajibika kumrudisha. Ikiwa sitamrudisha kwako na kumweka mbele yako, nitakuwa mwenye lawama mbele yako maisha yangu yote. |
| BSB 10 If we had not delayed, we could have come and gone twice by now.” | SWKCV 10 Hakika, kama hatukuchelewa kuondoka, tungekuwa tumekwenda na kurudi mara mbili.” |
| BSB 11 Then their father Israel said to them, “If it must be so, then do this: Put some of the best products of the land in your packs and carry them down as a gift for the man—a little balm and a little honey, spices and myrrh, pistachios and almonds. | SWKCV 11 Basi baba yao Israeli akawaambia, “Kama ni lazima iwe hivyo, basi fanyeni hivi: Wekeni baadhi ya mazao bora ya nchi katika mifuko yenu na mpelekeeni yule mtu kama zawadi, zeri kidogo, asali kidogo, vikolezo, manemane, kungu na lozi. |
| BSB 12 Take double the silver with you so that you may return the silver that was put back into the mouths of your sacks. Perhaps it was a mistake. | SWKCV 12 Chukueni fedha mara mbili, kwa kuwa mtazirudisha zile fedha zilizowekwa midomoni mwa magunia yenu. Labda ziliwekwa kwa makosa. |
| BSB 13 Take your brother as well, and return to the man at once. | SWKCV 13 Mchukueni ndugu yenu pia mrudi kwa huyo mtu mara moja. |
| BSB 14 May God Almighty grant you mercy before the man, that he may release your other brother along with Benjamin. As for me, if I am bereaved, I am bereaved.” | SWKCV 14 Naye Mungu Mwenyezi awajalieni rehema mbele ya huyo mtu ili apate kumwachia yule ndugu yenu na Benyamini mweze kurudi pamoja. Kwangu mimi kama nikufiwa nimefiwa.” |
| BSB 15 So the men took these gifts, along with double the amount of silver, and Benjamin as well. Then they hurried down to Egypt and stood before Joseph. | SWKCV 15 Basi hao watu wakazichukua zile zawadi na zile fedha mara mbili pamoja na Benyamini. Wakafanya haraka kwenda Misri na walipofika wakajionyesha kwa Yosefu. |
| BSB 16 When Joseph saw Benjamin with his brothers, he said to the steward of his house, “Take these men to my house. Slaughter an animal and prepare it, for they shall dine with me at noon.” | SWKCV 16 Yosefu alipomwona Benyamini pamoja nao, akamwambia msimamizi wa nyumba yake, “Wachukue watu hawa nyumbani kwangu, mchinje mnyama na kuandalia chakula kwa kuwa watakula chakula cha mchana pamoja nami.” |
| BSB 17 The man did as Joseph had commanded and took the brothers to Joseph’s house. | SWKCV 17 Yule Msimamizi akafanya kama Yosefu alivyomwambia na akawachukua wale watu nyumbani kwa Yosefu. |
| BSB 18 But the brothers were frightened that they had been taken to Joseph’s house. “We have been brought here because of the silver that was returned in our bags the first time,” they said. “They intend to overpower us and take us as slaves, along with our donkeys.” | SWKCV 18 Basi watu hao wakaogopa walipopelekwa nyumbani kwa Yosefu. Wakafikiri, “Tumeletwa hapa kwa ajili ya zile fedha zilizorudishwa katika magunia yetu mara ile ya kwanza. Anataka kutushambulia na kutushinda, atuchukue sisi kama watumwa, na atwae hawa punda zetu.” |
| BSB 19 So they approached Joseph’s steward and spoke to him at the entrance to the house. | SWKCV 19 Hivyo wakamwendea msimamizi wa nyumba wa Yosefu na kuzungumza naye kwenye ingilio la nyumbani. |
| BSB 20 “Please, sir,” they said, “we really did come down here the first time to buy food. | SWKCV 20 Wakasema, “Tafadhali bwana, tulikuja hapa mara ya kwanza kununua chakula. |
| BSB 21 But when we came to the place we lodged for the night, we opened our sacks and, behold, each of us found his silver in the mouth of his sack! It was the full amount of our silver, and we have brought it back with us. | SWKCV 21 Lakini mahali pale tulipotua wakati wa jioni tulifungua magunia yetu, na kila mmoja wetu akakuta fedha zake, kwenye mdomo wa gunia lake kiasi kile kile tulicholeta. Kwa hiyo tumezirudisha. |
| BSB 22 We have brought additional silver with us to buy food. We do not know who put our silver in our sacks.” | SWKCV 22 Pia tumeleta fedha nyingine kwa ajili ya kununulia chakula. Hatujui ni nani aliziweka fedha hizo katika magunia yetu.” |
| BSB 23 “It is fine,” said the steward. “Do not be afraid. Your God, the God of your father, gave you the treasure that was in your sacks. I received your silver.” Then he brought Simeon out to them. | SWKCV 23 Akawaambia, “Vema, msiogope. Mungu wenu, Mungu wa baba yenu, amewapa ninyi hazina katika magunia yenu; mimi nilipokea fedha yenu.” Ndipo akawaletea Simeoni. |
| BSB 24 And the steward took the men into Joseph’s house, gave them water to wash their feet, and provided food for their donkeys. | SWKCV 24 Msimamizi akawapeleka wale watu katika nyumba ya Yosefu, akawapa maji ya kunawa miguu na kuwapa punda wao majani. |
| BSB 25 Since the brothers had been told that they were going to eat a meal there, they prepared their gift for Joseph’s arrival at noon. | SWKCV 25 Wakaandaa zawadi zao ili wampe Yosefu wakati atakapofika adhuhuri, kwa kuwa walikuwa wamesikia kwamba watakula chakula huko. |
| BSB 26 When Joseph came home, they presented him with the gifts they had brought, and they bowed to the ground before him. | SWKCV 26 Yosefu alipokuja nyumbani, walimkabidhi zile zawadi walizokuwa nazo, ambazo walikuwa wamezileta mle nyumbani, nao wakamsujudia hadi nchi. |
| BSB 27 He asked if they were well, and then he asked, “How is your elderly father you told me about? Is he still alive?” | SWKCV 27 Akawauliza kuhusu hali yao, kisha akawaambia, “Yule baba yenu mzee mliyeniambia habari zake, yu hali gani? Je, bado yu hai?” |
| BSB 28 “Your servant our father is well,” they answered. “He is still alive.” And they bowed down to honor him. | SWKCV 28 Wakamjibu, “Mtumishi wako baba yetu bado anaishi na ni mzima.” Kisha wakainama chini kumpa heshima. |
| BSB 29 When Joseph looked up and saw his brother Benjamin, his own mother’s son, he asked, “Is this your youngest brother, the one you told me about?” Then he declared, “May God be gracious to you, my son.” | SWKCV 29 Alipotazama na kumwona Benyamini ndugu yake, mwana wa mama yake hasa, akauliza, “Je, huyu ndiye ndugu yenu wa mwisho, ambaye mlinieleza habari zake?” Ndipo akasema, “Mungu na akufadhili, mwanangu.” |
| BSB 30 Joseph hurried out because he was moved to tears for his brother, and he went to a private room to weep. | SWKCV 30 Akiwa ameguswa sana kwa kumwona ndugu yake, Yosefu akatoka nje kwa haraka na kutafuta mahali pa kulilia. Akaingia kwenye chumba chake cha pekee na kulilia humo. |
| BSB 31 Then he washed his face and came back out. Regaining his composure, he said, “Serve the meal.” | SWKCV 31 Baada ya kunawa uso wake, akatoka nje na huku akijizuia akasema, “Pakueni chakula.” |
| BSB 32 They separately served Joseph, his brothers, and the Egyptians. They ate separately because the Egyptians would not eat with the Hebrews, since that was detestable to them. | SWKCV 32 Wakampakulia Yosefu peke yake, ndugu zake peke yao na Wamisri waliokula pamoja naye peke yao, kwa sababu Wamisri wasingeweza kula pamoja na Waebrania, kwa maana ilikuwa ni chukizo kwa Wamisri. |
| BSB 33 They were seated before Joseph in order by age, from the firstborn to the youngest, and the men looked at one another in astonishment. | SWKCV 33 Watu hao walikuwa wameketi mbele yake kwa mfuatano wa umri wao, kuanzia mzaliwa wa kwanza hadi mzaliwa wa mwisho, wakatazamana wao kwa wao kwa mshangao. |
| BSB 34 When the portions were served to them from Joseph’s table, Benjamin’s portion was five times larger than any of the others. So they feasted and drank freely with Joseph. | SWKCV 34 Wakati walipelekewa sehemu ya chakula kutoka mezani mwa Yosefu, sehemu ya Benyamini ilikuwa mara tano zaidi ya sehemu ya wale wengine. Kwa hiyo wakanywa na kufurahi pamoja naye. |
Questions about Genesis 43? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.