Isaiah 10
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Woe to those who enact unjust statutes and issue oppressive decrees, | SWKCV 1 Ole wao wawekao sheria zisizo za haki, kwa wale watoao amri za kuonea, |
| BSB 2 to deprive the poor of fair treatment and withhold justice from the oppressed of My people, to make widows their prey and orphans their plunder. | SWKCV 2 kuwanyima maskini haki zao na kuzuilia haki za watu wangu walioonewa, kuwafanya wajane mawindo yao na kuwanyangʼanya yatima. |
| BSB 3 What will you do on the day of reckoning when devastation comes from afar? To whom will you flee for help? Where will you leave your wealth? | SWKCV 3 Mtafanya nini siku ya kutoa hesabu, wakati maafa yatakapokuja kutoka mbali? Mtamkimbilia nani awape msaada? Mtaacha wapi mali zenu? |
| BSB 4 Nothing will remain but to crouch among the captives or fall among the slain. Despite all this, His anger is not turned away; His hand is still upraised. | SWKCV 4 Hakutasalia kitu chochote, isipokuwa kujikunyata miongoni mwa mateka, au kuanguka miongoni mwa waliouawa. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu. |
| BSB 5 Woe to Assyria, the rod of My anger; the staff in their hands is My wrath. | SWKCV 5 “Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu, ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu! |
| BSB 6 I will send him against a godless nation; I will dispatch him against a people destined for My rage, to take spoils and seize plunder, and to trample them down like clay in the streets. | SWKCV 6 Ninamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu, ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha, kukamata mateka na kunyakua nyara, pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani. |
| BSB 7 But this is not his intention; this is not his plan. For it is in his heart to destroy and cut off many nations. | SWKCV 7 Lakini hili silo analokusudia, hili silo alilo nalo akilini; kusudi lake ni kuangamiza, kuyakomesha mataifa mengi. |
| BSB 8 “Are not all my commanders kings?” he says. | SWKCV 8 Maana asema, ‘Je, wafalme wote si majemadari wangu? |
| BSB 9 “Is not Calno like Carchemish? Is not Hamath like Arpad? Is not Samaria like Damascus? | SWKCV 9 Je, Kalno hakutendwa kama Karkemishi? Hamathi si kama Arpadi, nayo Samaria si kama Dameski? |
| BSB 10 As my hand seized the idolatrous kingdoms whose images surpassed those of Jerusalem and Samaria, | SWKCV 10 Kama vile mkono wangu ulivyotwaa falme za sanamu, falme ambazo vinyago vyao vilizidi vile vya Yerusalemu na Samaria: |
| BSB 11 and as I have done to Samaria and its idols, will I not also do to Jerusalem and her idols?” | SWKCV 11 je, nisiishughulikie Yerusalemu na sanamu zake kama nilivyoshughulikia Samaria na vinyago vyake?’” |
| BSB 12 So when the Lord has completed all His work against Mount Zion and Jerusalem, He will say, “I will punish the king of Assyria for the fruit of his arrogant heart and the proud look in his eyes. | SWKCV 12 Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.” |
| BSB 13 For he says: ‘By the strength of my hand I have done this, and by my wisdom, for I am clever. I have removed the boundaries of nations and plundered their treasures; like a mighty one I subdued their rulers. | SWKCV 13 Kwa kuwa anasema: “ ‘Kwa nguvu za mkono wangu nimefanya hili, kwa hekima yangu, kwa sababu nina ufahamu. Niliondoa mipaka ya mataifa, niliteka nyara hazina zao, kama yeye aliye shujaa niliwatiisha wafalme wao. |
| BSB 14 My hand reached as into a nest to seize the wealth of the nations. Like one gathering abandoned eggs, I gathered all the earth. No wing fluttered, no beak opened or chirped.’” | SWKCV 14 Kama mtu atiavyo mkono kwenye kiota, ndivyo mkono wangu ulivyochukua utajiri wa mataifa; kama watu wakusanyavyo mayai yaliyoachwa, ndivyo nilivyokusanya nchi zote; wala hakuna hata mmoja aliyepiga bawa au kufungua kinywa chake kutoa mlio.’” |
| BSB 15 Does an axe raise itself above the one who swings it? Does a saw boast over him who saws with it? It would be like a rod waving the one who lifts it, or a staff lifting him who is not wood! | SWKCV 15 Je, shoka laweza kujigamba kuwa na nguvu zaidi kuliko yule anayelitumia, au msumeno kujisifu dhidi ya yule anayeutumia? Ni kana kwamba fimbo ingeweza kumwinua yeye aichukuaye, au mkongojo ungemwinua mwenye kuutumia! |
| BSB 16 Therefore the Lord GOD of Hosts will send a wasting disease among Assyria’s stout warriors, and under his pomp will be kindled a fire like a burning flame. | SWKCV 16 Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatuma ugonjwa wa kudhoofisha kwa askari wake walio hodari, katika fahari yake moto utawaka kama mwali wa moto. |
| BSB 17 And the Light of Israel will become a fire, and its Holy One a flame. In a single day it will burn and devour Assyria’s thorns and thistles. | SWKCV 17 Nuru ya Israeli itakuwa moto, Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto; katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba na michongoma yake. |
| BSB 18 The splendor of its forests and orchards, both soul and body, it will completely destroy, as a sickness consumes a man. | SWKCV 18 Fahari ya misitu yake na mashamba yenye rutuba utateketeza kabisa, kama vile mtu mgonjwa adhoofikavyo. |
| BSB 19 The remaining trees of its forests will be so few that a child could count them. | SWKCV 19 Nayo miti inayobaki katika misitu yake itakuwa michache sana hata mtoto mdogo angeweza kuihesabu. |
| BSB 20 On that day the remnant of Israel and the survivors of the house of Jacob will no longer depend on him who struck them, but they will truly rely on the LORD, the Holy One of Israel. | SWKCV 20 Katika siku ile, mabaki ya Israeli, walionusurika wa nyumba ya Yakobo, hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga, lakini watamtegemea kwa kweli Bwana Aliye Mtakatifu wa Israeli. |
| BSB 21 A remnant will return—a remnant of Jacob—to the Mighty God. | SWKCV 21 Mabaki watarudi, mabaki wa Yakobo watamrudia Mungu Mwenye Nguvu. |
| BSB 22 Though your people, O Israel, be like the sand of the sea, only a remnant will return. Destruction has been decreed, overflowing with righteousness. | SWKCV 22 Ingawa watu wako, ee Israeli, ni wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki yao tu watakaorudi. Maangamizi yamekwisha amriwa, ni mengi tena ni haki. |
| BSB 23 For the Lord GOD of Hosts will carry out the destruction decreed upon the whole land. | SWKCV 23 Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atatekeleza maangamizi yaliyoamriwa juu ya nchi yote. |
| BSB 24 Therefore this is what the Lord GOD of Hosts says: “O My people who dwell in Zion, do not fear Assyria, who strikes you with a rod and lifts his staff against you as the Egyptians did. | SWKCV 24 Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Enyi watu wangu mkaao Sayuni, msiwaogope Waashuru, wanaowapiga ninyi kwa fimbo na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya. |
| BSB 25 For in just a little while My fury against you will subside, and My anger will turn to their destruction.” | SWKCV 25 Bado kitambo kidogo sana hasira yangu dhidi yenu itakoma, na ghadhabu yangu itaelekezwa kwenye maangamizi yao.” |
| BSB 26 And the LORD of Hosts will brandish a whip against them, as when He struck Midian at the rock of Oreb. He will raise His staff over the sea, as He did in Egypt. | SWKCV 26 Bwana Mwenye Nguvu Zote atawachapa kwa mjeledi, kama alivyowapiga Wamidiani katika mwamba wa Orebu, naye atainua fimbo yake juu ya maji, kama alivyofanya huko Misri. |
| BSB 27 On that day the burden will be lifted from your shoulders, and the yoke from your neck. The yoke will be broken because your neck will be too large. | SWKCV 27 Katika siku hiyo mzigo wao utainuliwa kutoka mabegani mwenu, na nira yao kutoka shingoni mwenu; nira itavunjwa kwa sababu ya kutiwa mafuta. |
| BSB 28 Assyria has entered Aiath and passed through Migron, storing their supplies at Michmash. | SWKCV 28 Wanaingia Ayathi, wanapita katikati ya Migroni, wanahifadhi mahitaji huko Mikmashi. |
| BSB 29 They have crossed at the ford: “We will spend the night at Geba.” Ramah trembles; Gibeah of Saul flees. | SWKCV 29 Wanavuka kivukoni, nao wanasema, “Tutapiga kambi huko Geba usiku kucha.” Rama inatetemeka; Gibea ya Sauli inakimbia. |
| BSB 30 Cry aloud, O Daughter of Gallim! Listen, O Laishah! O wretched Anathoth! | SWKCV 30 Piga kelele, ee Binti Galimu! Sikiliza, ee Laisha! Maskini Anathothi! |
| BSB 31 Madmenah flees; the people of Gebim take refuge. | SWKCV 31 Madmena inakimbia; watu wa Gebimu wanajificha. |
| BSB 32 Yet today they will halt at Nob, shaking a fist at the mount of Daughter Zion, at the hill of Jerusalem. | SWKCV 32 Siku hii ya leo watasimama Nobu; watatikisa ngumi zao kwa mlima wa Binti Sayuni, kwa kilima cha Yerusalemu. |
| BSB 33 Behold, the Lord GOD of Hosts will lop off the branches with terrifying power. The tall trees will be cut down, the lofty ones will be felled. | SWKCV 33 Tazama, Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, atayakata matawi kwa nguvu kuu. Miti mirefu sana itaangushwa, ile mirefu itashushwa chini. |
| BSB 34 He will clear the forest thickets with an axe, and Lebanon will fall before the Mighty One. | SWKCV 34 Atakata vichaka vya msitu kwa shoka; Lebanoni itaanguka mbele zake yeye Mwenye Nguvu. |
Questions about Isaiah 10? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.