Judges 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 On that day Deborah and Barak son of Abinoam sang this song: | SWKCV 1 Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu: |
| BSB 2 “When the princes take the lead in Israel, when the people volunteer, bless the LORD. | SWKCV 2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza, wakati watu wanapojitoa kwa hiari yao wenyewe: mhimidini Bwana! |
| BSB 3 Listen, O kings! Give ear, O princes! I will sing to the LORD; I will sing praise to the LORD, the God of Israel. | SWKCV 3 “Sikieni hili, enyi wafalme! Sikilizeni, enyi watawala! Nitamwimbia Bwana, nitaimba; kwa wimbo nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli. |
| BSB 4 O LORD, when You went out from Seir, when You marched from the land of Edom, the earth trembled, the heavens poured out rain, and the clouds poured down water. | SWKCV 4 “Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, naam, mawingu yakamwaga maji. |
| BSB 5 The mountains quaked before the LORD, the One of Sinai, before the LORD, the God of Israel. | SWKCV 5 Milima ilitetemeka mbele za Bwana, hata ule wa Sinai, mbele za Bwana, Mungu wa Israeli. |
| BSB 6 In the days of Shamgar son of Anath, in the days of Jael, the highways were deserted and the travelers took the byways. | SWKCV 6 “Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, katika siku za Yaeli, barabara kuu hazikuwa na watu; wasafiri walipita njia za kando. |
| BSB 7 Life in the villages ceased; it ended in Israel, until I, Deborah, arose, a mother in Israel. | SWKCV 7 Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli. |
| BSB 8 When they chose new gods, then war came to their gates. Not a shield or spear was found among forty thousand in Israel. | SWKCV 8 Walipochagua miungu migeni, vita vilikuja katika malango ya mji, hapakuonekana ngao wala mkuki miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli. |
| BSB 9 My heart is with the princes of Israel, with the volunteers among the people. Bless the LORD! | SWKCV 9 Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, pamoja na wale wanaojitoa wenyewe kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini Bwana! |
| BSB 10 You who ride white donkeys, who sit on saddle blankets, and you who travel the road, ponder | SWKCV 10 “Nanyi mpandao punda weupe, mkiketi juu ya matandiko ya thamani, nanyi mtembeao barabarani, fikirini |
| BSB 11 the voices of the singers at the watering places. There they shall recount the righteous acts of the LORD, the righteous deeds of His villagers in Israel. Then the people of the LORD went down to the gates: | SWKCV 11 juu ya sauti za waimbaji mahali pa kunyweshea maji. Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana, matendo ya haki ya mashujaa wake katika Israeli. “Ndipo watu wa Bwana walipoteremka malangoni pa mji. |
| BSB 12 ‘Awake, awake, O Deborah! Awake, awake, sing a song! Arise, O Barak, and take hold of your captives, O son of Abinoam!’ | SWKCV 12 ‘Amka, amka! Debora! Amka, amka, uimbe! Ee Baraka! Inuka, chukua mateka wako uliowateka, ee mwana wa Abinoamu.’ |
| BSB 13 Then the survivors came down to the nobles; the people of the LORD came down to me against the mighty. | SWKCV 13 “Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wenye nguvu, watu wa Bwana, wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu. |
| BSB 14 Some came from Ephraim, with their roots in Amalek; Benjamin came with your people after you. The commanders came down from Machir, the bearers of the marshal’s staff from Zebulun. | SWKCV 14 Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki; Benyamini akiwa miongoni mwa watu waliokufuata. Kutoka Makiri wakashuka viongozi, na kutoka Zabuloni wale washikao fimbo ya jemadari. |
| BSB 15 The princes of Issachar were with Deborah, and Issachar was with Barak, rushing into the valley at his heels. In the clans of Reuben there was great indecision. | SWKCV 15 Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora; naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka, wakija nyuma yake kwa mbio wakielekea bondeni. Katika jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. |
| BSB 16 Why did you sit among the sheepfolds to hear the whistling for the flocks? In the clans of Reuben there was great indecision. | SWKCV 16 Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi? Kwa jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni. |
| BSB 17 Gilead remained beyond the Jordan. Dan, why did you linger by the ships? Asher stayed at the coast and remained in his harbors. | SWKCV 17 Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani. Naye Dani, kwa nini alikaa kwenye merikebu siku nyingi? Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari, akikaa kwenye ghuba zake ndogo. |
| BSB 18 Zebulun was a people who risked their lives; Naphtali, too, on the heights of the battlefield. | SWKCV 18 Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao, vilevile nao watu wa Naftali. |
| BSB 19 Kings came and fought; then the kings of Canaan fought at Taanach by the waters of Megiddo, but they took no plunder of silver. | SWKCV 19 “Wafalme walikuja na kufanya vita; wafalme wa Kanaani walipigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido, lakini hawakuchukua fedha wala nyara. |
| BSB 20 From the heavens the stars fought; from their courses they fought against Sisera. | SWKCV 20 Kutoka mbinguni nyota zilipigana, nyota kutoka njia zake zilipigana na Sisera. |
| BSB 21 The River Kishon swept them away, the ancient river, the River Kishon. March on, O my soul, in strength! | SWKCV 21 Mto wa Kishoni uliwasomba, ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Songa mbele, ee nafsi yangu, kwa ujasiri! |
| BSB 22 Then the hooves of horses thundered—the mad galloping of his stallions. | SWKCV 22 Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo: farasi wake wenye nguvu huenda mbio kwa kurukaruka. |
| BSB 23 ‘Curse Meroz,’ says the angel of the LORD. ‘Bitterly curse her inhabitants; for they did not come to help the LORD, to help the LORD against the mighty.’ | SWKCV 23 Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe. Walaaniwe watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’ |
| BSB 24 Most blessed among women is Jael, the wife of Heber the Kenite, most blessed of tent-dwelling women. | SWKCV 24 “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, mkewe Heberi, Mkeni, abarikiwe kuliko wanawake wote waishio kwenye mahema. |
| BSB 25 He asked for water, and she gave him milk. In a magnificent bowl she brought him curds. | SWKCV 25 Aliomba maji, naye akampa maziwa; kwenye bakuli la heshima akamletea maziwa mgando. |
| BSB 26 She reached for the tent peg, her right hand for the workman’s hammer. She struck Sisera and crushed his skull; she shattered and pierced his temple. | SWKCV 26 Akanyoosha mkono wake akashika kigingi cha hema, mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi. Akampiga Sisera kwa nyundo, akamponda kichwa chake, akamvunjavunja na kumtoboa paji lake la uso. |
| BSB 27 At her feet he collapsed, he fell, there he lay still; at her feet he collapsed, he fell; where he collapsed, there he fell dead. | SWKCV 27 Aliinama miguuni pa Yaeli, akaanguka; akalala hapo. Pale alipoinama miguuni pake, alianguka; pale alipoinamia, ndipo alipoanguka, akiwa amekufa. |
| BSB 28 Sisera’s mother looked through the window; she peered through the lattice and lamented: ‘Why is his chariot so long in coming? What has delayed the clatter of his chariots?’ | SWKCV 28 “Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia; nyuma ya dirisha alilia, akasema, ‘Mbona gari lake linachelewa kufika? Mbona vishindo vya magari yake vimechelewa?’ |
| BSB 29 Her wisest ladies answer; indeed she keeps telling herself, | SWKCV 29 Wanawake wenye busara kuliko wengine wote wakamjibu; naam, husema moyoni mwake, |
| BSB 30 ‘Are they not finding and dividing the spoil—a girl or two for each warrior, a plunder of dyed garments for Sisera, the spoil of embroidered garments for the neck of the looter?’ | SWKCV 30 ‘Je, hawapati na kugawanya nyara: msichana mmoja au wawili kwa kila mtu, mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara, mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa, mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu: yote haya yakiwa nyara?’ |
| BSB 31 So may all Your enemies perish, O LORD! But may those who love You shine like the sun at its brightest.” And the land had rest for forty years. | SWKCV 31 “Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini. |
Questions about Judges 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.