1 Corinthians 1
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Paul, called to be an apostle of Christ Jesus by the will of God, and our brother Sosthenes, | SWKCV 1 Paulo, niliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Kristo Yesu, na Sosthene ndugu yetu. |
| BSB 2 To the church of God in Corinth, to those sanctified in Christ Jesus and called to be holy, together with all those everywhere who call on the name of our Lord Jesus Christ, their Lord and ours: | SWKCV 2 Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale waliotakaswa katika Kristo Yesu na walioitwa kuwa watakatifu, pamoja na wale wote ambao kila mahali wanaliitia Jina la Kristo Yesu Bwana wetu, aliye Bwana wao na wetu pia: |
| BSB 3 Grace and peace to you from God our Father and the Lord Jesus Christ. | SWKCV 3 Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo iwe nanyi. |
| BSB 4 I always thank my God for you because of the grace He has given you in Christ Jesus. | SWKCV 4 Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Kristo Yesu. |
| BSB 5 For in Him you have been enriched in every way, in all speech and all knowledge, | SWKCV 5 Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kusema kwenu na katika maarifa yenu yote, |
| BSB 6 because our testimony about Christ was confirmed in you. | SWKCV 6 kwa sababu ushuhuda wetu kumhusu Kristo ulithibitishwa ndani yenu. |
| BSB 7 Therefore you do not lack any spiritual gift as you eagerly await the revelation of our Lord Jesus Christ. | SWKCV 7 Kwa hiyo hamkupungukiwa na karama yoyote ya kiroho wakati mnangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. |
| BSB 8 He will sustain you to the end, so that you will be blameless on the day of our Lord Jesus Christ. | SWKCV 8 Atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. |
| BSB 9 God, who has called you into fellowship with His Son Jesus Christ our Lord, is faithful. | SWKCV 9 Mungu ambaye mmeitwa naye ili mwe na ushirika na Mwanawe Yesu Kristo, Bwana wetu ni mwaminifu. |
| BSB 10 I appeal to you, brothers, in the name of our Lord Jesus Christ, that all of you agree together, so that there may be no divisions among you and that you may be united in mind and conviction. | SWKCV 10 Nawasihi ndugu zangu, katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi, ili pasiwepo na matengano katikati yenu na kwamba mwe na umoja kikamilifu katika nia na katika kusudi. |
| BSB 11 My brothers, some from Chloe’s household have informed me that there are quarrels among you. | SWKCV 11 Ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa baadhi ya watu wa nyumbani mwa Kloe kwamba kuna magomvi katikati yenu. |
| BSB 12 What I mean is this: Individuals among you are saying, “I follow Paul,” “I follow Apollos,” “I follow Cephas,” or “I follow Christ.” | SWKCV 12 Maana yangu ni kwamba: Mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo”; mwingine, “Mimi ni wa Apolo”; mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.” |
| BSB 13 Is Christ divided? Was Paul crucified for you? Were you baptized into the name of Paul? | SWKCV 13 Je, Kristo amegawanyika? Je, Paulo ndiye alisulubishwa kwa ajili yenu? Je, mlibatizwa kwa jina la Paulo? |
| BSB 14 I thank God that I did not baptize any of you except Crispus and Gaius, | SWKCV 14 Nashukuru kwamba sikumbatiza mtu yeyote isipokuwa Krispo na Gayo. |
| BSB 15 so no one can say that you were baptized into my name. | SWKCV 15 Kwa hiyo hakuna mtu yeyote anayeweza kusema kwamba alibatizwa kwa jina langu. |
| BSB 16 Yes, I also baptized the household of Stephanas; beyond that I do not remember if I baptized anyone else. | SWKCV 16 (Naam, niliwabatiza pia watu wa nyumbani mwa Stefana. Lakini zaidi ya hao sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote.) |
| BSB 17 For Christ did not send me to baptize, but to preach the gospel, not with words of wisdom, lest the cross of Christ be emptied of its power. | SWKCV 17 Kwa maana Kristo hakunituma ili kubatiza bali kuhubiri Injili; sio kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili msalaba wa Kristo usije ukakosa nguvu yake. |
| BSB 18 For the message of the cross is foolishness to those who are perishing, but to us who are being saved it is the power of God. | SWKCV 18 Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. |
| BSB 19 For it is written: “I will destroy the wisdom of the wise; the intelligence of the intelligent I will frustrate.” | SWKCV 19 Kwa maana imeandikwa: “Nitaiharibu hekima ya wenye hekima, na kubatilisha akili ya wenye akili.” |
| BSB 20 Where is the wise man? Where is the scribe? Where is the philosopher of this age? Has not God made foolish the wisdom of the world? | SWKCV 20 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? |
| BSB 21 For since in the wisdom of God the world through its wisdom did not know Him, God was pleased through the foolishness of what was preached to save those who believe. | SWKCV 21 Kwa kuwa katika hekima ya Mungu, ulimwengu kwa hekima yake haukumjua yeye, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wale walioamini kwa upuzi wa lile neno lililohubiriwa. |
| BSB 22 Jews demand signs and Greeks search for wisdom, | SWKCV 22 Wayahudi wanadai ishara za miujiza na Wayunani wanatafuta hekima. |
| BSB 23 but we preach Christ crucified, a stumbling block to Jews and foolishness to Gentiles, | SWKCV 23 Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa: yeye kwa Wayahudi ni kikwazo na kwa Wayunani ni upuzi. |
| BSB 24 but to those who are called, both Jews and Greeks, Christ the power of God and the wisdom of God. | SWKCV 24 Lakini kwa wale ambao Mungu amewaita, Wayahudi na pia Wayunani, Kristo ndiye nguvu ya Mungu na pia hekima ya Mungu. |
| BSB 25 For the foolishness of God is wiser than man’s wisdom, and the weakness of God is stronger than man’s strength. | SWKCV 25 Kwa maana upumbavu wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, nao udhaifu wa Mungu una nguvu kuliko nguvu ya wanadamu. |
| BSB 26 Brothers, consider the time of your calling: Not many of you were wise by human standards; not many were powerful; not many were of noble birth. | SWKCV 26 Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa mlipoitwa. Kwa kipimo cha kibinadamu, si wengi wenu mliokuwa na hekima. Si wengi mliokuwa na ushawishi, si wengi mliozaliwa katika jamaa zenye vyeo. |
| BSB 27 But God chose the foolish things of the world to shame the wise; God chose the weak things of the world to shame the strong. | SWKCV 27 Lakini Mungu alivichagua vitu vipumbavu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye hekima, Mungu alivichagua vitu dhaifu vya ulimwengu ili awaaibishe wenye nguvu. |
| BSB 28 He chose the lowly and despised things of the world, and the things that are not, to nullify the things that are, | SWKCV 28 Alivichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa vya dunia hii, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko, |
| BSB 29 so that no one may boast in His presence. | SWKCV 29 ili mtu yeyote asijisifu mbele zake. |
| BSB 30 It is because of Him that you are in Christ Jesus, who has become for us wisdom from God: our righteousness, holiness, and redemption. | SWKCV 30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu, yaani haki, na utakatifu na ukombozi. |
| BSB 31 Therefore, as it is written: “Let him who boasts boast in the Lord.” | SWKCV 31 Hivyo, kama ilivyoandikwa: “Yeye ajisifuye na ajisifu katika Bwana.” |
Questions about 1 Corinthians 1? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.