2 Thessalonians 1
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Paul, Silvanus, and Timothy, To the church of the Thessalonians in God our Father and the Lord Jesus Christ: | SWKCV 1 Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kanisa la Wathesalonike mlio katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo: |
| BSB 2 Grace and peace to you from God our Father and the Lord Jesus Christ. | SWKCV 2 Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi. |
| BSB 3 We are obligated to thank God for you all the time, brothers, as is fitting, because your faith is growing more and more, and your love for one another is increasing. | SWKCV 3 Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka. |
| BSB 4 That is why we boast among God’s churches about your perseverance and faith in the face of all the persecution and affliction you are enduring. | SWKCV 4 Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili. |
| BSB 5 All this is clear evidence of God’s righteous judgment. And so you will be counted worthy of the kingdom of God, for which you are suffering. | SWKCV 5 Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake. |
| BSB 6 After all, it is only right for God to repay with affliction those who afflict you, | SWKCV 6 Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi |
| BSB 7 and to grant relief to you who are oppressed and to us as well. This will take place when the Lord Jesus is revealed from heaven with His mighty angels | SWKCV 7 na kuwapa ninyi mnaoteseka raha pamoja na sisi, wakati Bwana Yesu atakapodhihirishwa kutoka mbinguni katika mwali wa moto pamoja na malaika wake wenye nguvu. |
| BSB 8 in blazing fire, inflicting vengeance on those who do not know God and do not obey the gospel of our Lord Jesus. | SWKCV 8 Atawaadhibu wale wasiomjua Mungu na ambao hawakuitii Injili ya Bwana wetu Yesu. |
| BSB 9 They will suffer the penalty of eternal destruction, separated from the presence of the Lord and the glory of His might, | SWKCV 9 Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake, |
| BSB 10 on the day He comes to be glorified in His saints and regarded with wonder by all who have believed, including you who have believed our testimony. | SWKCV 10 siku hiyo atakapokuja kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini. Ninyi pia mtakuwa miongoni mwa hawa kwa sababu mliamini ushuhuda wetu kwenu. |
| BSB 11 To this end, we always pray for you, that our God will count you worthy of His calling, and that He will powerfully fulfill your every good desire and work of faith, | SWKCV 11 Kwa sababu hii, tunawaombea ninyi bila kukoma, ili Mungu apate kuwahesabu kuwa mnastahili wito wake na kwamba kwa uwezo wake apate kutimiza kila kusudi lenu jema na kila tendo linaloongozwa na imani yenu. |
| BSB 12 so that the name of our Lord Jesus will be glorified in you, and you in Him, according to the grace of our God and of the Lord Jesus Christ. | SWKCV 12 Tunaomba hivi ili Jina la Bwana wetu Yesu lipate kutukuzwa ndani yenu, nanyi ndani yake, kulingana na neema ya Mungu wetu na Bwana Yesu Kristo. |
Questions about 2 Thessalonians 1? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.