Deuteronomy 6
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 These are the commandments and statutes and ordinances that the LORD your God has instructed me to teach you to follow in the land that you are about to enter and possess, | SWKCV 1 Haya ndiyo maagizo, amri na sheria ambazo Bwana Mungu wenu aliniagiza niwafundishe ninyi ili mpate kuyashika katika nchi ambayo ninyi mnavuka Yordani kuimiliki, |
| BSB 2 so that you and your children and grandchildren may fear the LORD your God all the days of your lives by keeping all His statutes and commandments that I give you, and so that your days may be prolonged. | SWKCV 2 ili kwamba ninyi, watoto wenu na watoto wao baada yao wamche Bwana Mungu wenu siku zote kwa kushika amri na maagizo yake yote ninayowapa, ili mweze kuyafurahia maisha marefu. |
| BSB 3 Hear, O Israel, and be careful to observe them, so that you may prosper and multiply greatly in a land flowing with milk and honey, just as the LORD, the God of your fathers, has promised you. | SWKCV 3 Sikia, ee Israeli, nawe uwe mwangalifu kutii ili upate kufanikiwa na kuongezeka sana katika nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Bwana, Mungu wa baba zenu, alivyowaahidi ninyi. |
| BSB 4 Hear, O Israel: The LORD our God, the LORD is One. | SWKCV 4 Sikia, ee Israeli: Bwana Mungu wako, Bwana ni mmoja. |
| BSB 5 And you shall love the LORD your God with all your heart and with all your soul and with all your strength. | SWKCV 5 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. |
| BSB 6 These words I am commanding you today are to be upon your hearts. | SWKCV 6 Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. |
| BSB 7 And you shall teach them diligently to your children and speak of them when you sit at home and when you walk along the road, when you lie down and when you get up. | SWKCV 7 Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. |
| BSB 8 Tie them as reminders on your hands and bind them on your foreheads. | SWKCV 8 Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. |
| BSB 9 Write them on the doorposts of your houses and on your gates. | SWKCV 9 Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako. |
| BSB 10 And when the LORD your God brings you into the land He swore to your fathers, to Abraham, Isaac, and Jacob, that He would give you—a land with great and splendid cities that you did not build, | SWKCV 10 Wakati Bwana Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Abrahamu, Isaki na Yakobo, kukupa wewe, nchi kubwa, ina miji inayopendeza ambayo hukuijenga, |
| BSB 11 with houses full of every good thing with which you did not fill them, with wells that you did not dig, and with vineyards and olive groves that you did not plant—and when you eat and are satisfied, | SWKCV 11 nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina nyingi ambavyo hukuvijaza, visima ambavyo hukuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hukupanda wewe, basi, utakapokula na kushiba, |
| BSB 12 be careful not to forget the LORD who brought you out of the land of Egypt, out of the house of slavery. | SWKCV 12 jihadhari usije ukamwacha Bwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. |
| BSB 13 Fear the LORD your God, serve Him only, and take your oaths in His name. | SWKCV 13 Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake. |
| BSB 14 Do not follow other gods, the gods of the peoples around you. | SWKCV 14 Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka; |
| BSB 15 For the LORD your God, who is among you, is a jealous God. Otherwise the anger of the LORD your God will be kindled against you, and He will wipe you off the face of the earth. | SWKCV 15 kwa kuwa Bwana Mungu wako, ambaye yuko katikati yako, ni Mungu mwenye wivu na hasira yake itawaka dhidi yako, naye atakuangamiza kutoka uso wa nchi. |
| BSB 16 Do not test the LORD your God as you tested Him at Massah. | SWKCV 16 Usimjaribu Bwana Mungu wako kama ulivyofanya huko Masa. |
| BSB 17 You are to diligently keep the commandments of the LORD your God and the testimonies and statutes He has given you. | SWKCV 17 Utayashika maagizo ya Bwana Mungu wako kwa bidii, na masharti na amri alizokupa. |
| BSB 18 Do what is right and good in the sight of the LORD, so that it may be well with you and that you may enter and possess the good land that the LORD your God swore to give your fathers, | SWKCV 18 Fanya lililo haki na jema mbele za Bwana, ili upate kufanikiwa, uweze kuingia na kuimiliki nchi nzuri ambayo Bwana aliahidi kwa kiapo kwa baba zako, |
| BSB 19 driving out all your enemies before you, as the LORD has said. | SWKCV 19 kuwafukuza kwa nguvu adui zako mbele yako kama Bwana alivyosema. |
| BSB 20 In the future, when your son asks, “What is the meaning of the decrees and statutes and ordinances that the LORD our God has commanded you?” | SWKCV 20 Siku zijazo, mtoto wako atakapokuuliza, “Ni nini maana ya masharti haya, amri na sheria hizi ambazo Bwana Mungu wako alikuagiza wewe?” |
| BSB 21 then you are to tell him, “We were slaves of Pharaoh in Egypt, but the LORD brought us out of Egypt with a mighty hand. | SWKCV 21 Mwambie: “Tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, lakini Bwana alitutoa sisi kutoka Misri kwa mkono wenye nguvu. |
| BSB 22 Before our eyes the LORD inflicted great and devastating signs and wonders on Egypt, on Pharaoh, and on all his household. | SWKCV 22 Bwana akapeleka mbele yetu ishara za miujiza na maajabu makubwa na ya kutisha mno juu ya Misri na Farao pamoja na nyumba yake yote. |
| BSB 23 But He brought us out from there to lead us in and give us the land that He had sworn to our fathers. | SWKCV 23 Lakini Mungu akatutoa huko, akatuleta na kutupa nchi hii ambayo aliwaahidi baba zetu kwa kiapo. |
| BSB 24 And the LORD commanded us to observe all these statutes and to fear the LORD our God, that we may always be prosperous and preserved, as we are to this day. | SWKCV 24 Bwana akatuagiza tutii amri hizi zote na kumcha Bwana Mungu wetu, ili tupate kustawi na kuendelea kuwa hai kama ilivyo leo. |
| BSB 25 And if we are careful to observe every one of these commandments before the LORD our God, as He has commanded us, then that will be our righteousness.” | SWKCV 25 Kama tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Bwana Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.” |
Questions about Deuteronomy 6? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.