Ecclesiastes 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Guard your steps when you go to the house of God. Draw near to listen rather than to offer the sacrifice of fools, who do not know that they do wrong. | SWKCV 1 Linda hatua zako uendapo katika nyumba ya Mungu. Karibia usikilize kuliko kutoa dhabihu ya wapumbavu, ambao hawajui kuwa wanafanya kosa. |
| BSB 2 Do not be quick to speak, and do not be hasty in your heart to utter a word before God. For God is in heaven and you are on earth. So let your words be few. | SWKCV 2 Usiwe mwepesi kuzungumza, usiwe na haraka katika moyo wako kuzungumza lolote mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni nawe uko duniani, kwa hiyo maneno yako na yawe machache. |
| BSB 3 As a dream comes through many cares, so the speech of a fool comes with many words. | SWKCV 3 Kama vile ndoto huja wakati kuna shughuli nyingi, ndivyo yalivyo mazungumzo ya mpumbavu wakati kuna maneno mengi. |
| BSB 4 When you make a vow to God, do not delay in fulfilling it, because He takes no pleasure in fools. Fulfill your vow. | SWKCV 4 Wakati unapomwekea Mungu nadhiri, usikawie kuitimiza. Yeye hafurahii wapumbavu; timiza nadhiri yako. |
| BSB 5 It is better not to vow than to make a vow and not fulfill it. | SWKCV 5 Ni afadhali usiweke nadhiri kuliko kuiweka na usiitimize. |
| BSB 6 Do not let your mouth cause your flesh to sin, and do not tell the messenger that your vow was a mistake. Why should God be angry with your words and destroy the work of your hands? | SWKCV 6 Usiruhusu kinywa chako kukuingiza dhambini. Tena usijitetee mbele ya huyo mjumbe wa hekaluni, ukisema, “Niliweka nadhiri kwa makosa.” Kwa nini Mungu akasirike kwa ajili ya yale unayosema na kuiharibu kazi ya mikono yako? |
| BSB 7 For as many dreams bring futility, so do many words. Therefore, fear God. | SWKCV 7 Kuota ndoto kwingi na maneno mengi ni ubatili. Kwa hiyo simama katika kicho cha Mungu. |
| BSB 8 If you see the oppression of the poor and the denial of justice and righteousness in the province, do not be astonished at the matter; for one official is watched by a superior, and others higher still are over them. | SWKCV 8 Kama ukiona maskini wanaonewa katika nchi, hukumu na haki vikipotoshwa, usishangazwe na mambo hayo, kwa maana afisa mmoja anaangaliwa na aliye juu yake zaidi na juu ya hao wawili kuna wengine walio juu zaidi yao. |
| BSB 9 The produce of the earth is taken by all; the king himself profits from the fields. | SWKCV 9 Mafanikio ya nchi ni kwa ajili ya wote, hata mfalme mwenyewe hufaidi kutoka mashambani. |
| BSB 10 He who loves money is never satisfied by money, and he who loves wealth is never satisfied by income. This too is futile. | SWKCV 10 Yeyote apendaye fedha kamwe hatosheki na fedha; yeyote apendaye utajiri kamwe hatosheki na kipato chake. Hili nalo pia ni ubatili. |
| BSB 11 When good things increase, so do those who consume them; what then is the profit to the owner, except to behold them with his eyes? | SWKCV 11 Mali ikiongezeka, ndivyo walaji wanavyoongezeka. Hii nayo inamfaidia nini mwenye mali isipokuwa ni kushibisha macho yake? |
| BSB 12 The sleep of the worker is sweet, whether he eats little or much, but the abundance of the rich man permits him no sleep. | SWKCV 12 Usingizi wa kibarua ni mtamu, awe amekula kidogo au kingi, lakini wingi wa mali humnyima tajiri usingizi. |
| BSB 13 There is a grievous evil I have seen under the sun: wealth hoarded to the harm of its owner, | SWKCV 13 Nimeshaona uovu mzito chini ya jua: Utajiri uliolimbikizwa kwa kujinyima na kuleta madhara kwa mwenye mali, |
| BSB 14 or wealth lost in a failed venture, so when that man has a son there is nothing to pass on. | SWKCV 14 au utajiri uliopotea kwa bahati mbaya, hivyo kwamba wakati akiwa na mwana hakuna chochote kilichobaki kwa ajili yake. |
| BSB 15 As a man came from his mother’s womb, so he will depart again, naked as he arrived. He takes nothing for his labor to carry in his hands. | SWKCV 15 Mtu hutoka tumboni mwa mama yake uchi, naye jinsi alivyokuja vivyo hivyo huondoka. Hachukui chochote kutokana na kazi yake ambacho anaweza kukibeba mkononi mwake. |
| BSB 16 This too is a grievous affliction: Exactly as a man is born, so he will depart. What does he gain as he toils for the wind? | SWKCV 16 Hili nalo ni baya la kusikitisha: Kama vile mtu ajavyo, vivyo hivyo huondoka, naye anapata faida gani, maadamu hutaabika kwa ajili ya upepo? |
| BSB 17 Moreover, all his days he eats in darkness, with much sorrow, sickness, and anger. | SWKCV 17 Siku zake zote hula gizani, pamoja na fadhaa kubwa, mateso na hasira. |
| BSB 18 Here is what I have seen to be good and fitting: to eat and drink, and to find satisfaction in all the labor one does under the sun during the few days of life that God has given him—for this is his lot. | SWKCV 18 Ndipo nikatambua kwamba ni vyema na sahihi kwa mtu kula na kunywa na kutosheka katika kazi yake ngumu chini ya jua katika siku chache za maisha yake Mungu alizompa, kwa maana hili ndilo fungu lake. |
| BSB 19 Furthermore, God has given riches and wealth to every man, and He has enabled him to enjoy them, to accept his lot, and to rejoice in his labor. This is a gift from God. | SWKCV 19 Zaidi ya yote, Mungu anapompa mtu yeyote utajiri na milki, humwezesha kuvifurahia, kukubali fungu lake na kuwa na furaha katika kazi yake, hii ni karama ya Mungu. |
| BSB 20 For a man seldom considers the days of his life, because God keeps him occupied with the joy of his heart. | SWKCV 20 Mara chache mtu huzifikiri siku za maisha yake, kwa sababu Mungu humfanya ashikwe na furaha ya moyoni. |
Questions about Ecclesiastes 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.