Exodus 18
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now Moses’ father-in-law Jethro, the priest of Midian, heard about all that God had done for Moses and His people Israel, and how the LORD had brought Israel out of Egypt. | SWKCV 1 Basi Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wa Mose, akawa amesikia kila kitu Mungu alichomfanyia Mose na watu wake wa Israeli, pia jinsi Bwana alivyowatoa Israeli Misri. |
| BSB 2 After Moses had sent back his wife Zipporah, his father-in-law Jethro had received her, | SWKCV 2 Baada ya Mose kumrudisha mkewe Sipora, Yethro baba mkwe wake alimpokea |
| BSB 3 along with her two sons. One son was named Gershom, for Moses had said, “I have been a foreigner in a foreign land.” | SWKCV 3 pamoja na wanawe wawili. Jina la mmoja aliitwa Gershomu, kwa kuwa Mose alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.” |
| BSB 4 The other son was named Eliezer, for Moses had said, “The God of my father was my helper and delivered me from the sword of Pharaoh.” | SWKCV 4 Mwingine aliitwa Eliezeri, kwa kuwa alisema, “Mungu wa baba yangu alikuwa msaada wangu, akaniokoa kutoka upanga wa Farao.” |
| BSB 5 Moses’ father-in-law Jethro, along with Moses’ wife and sons, came to him in the desert, where he was encamped at the mountain of God. | SWKCV 5 Yethro, baba mkwe wa Mose, pamoja na wana wawili wa Mose na mkewe, wakamjia Mose huko jangwani, mahali alipokuwa amepiga kambi karibu na mlima wa Mungu. |
| BSB 6 He sent word to Moses, “I, your father-in-law Jethro, am coming to you with your wife and her two sons.” | SWKCV 6 Yethro alikuwa ametuma ujumbe kwake Mose, kusema, “Mimi Yethro baba mkwe wako ninakuja kwako pamoja na mke wako na wanao wawili.” |
| BSB 7 So Moses went out to meet his father-in-law and bowed down and kissed him. They greeted each other and went into the tent. | SWKCV 7 Kwa hiyo Mose akatoka kumlaki baba mkwe wake, akainama na kumbusu. Wakasalimiana, kisha wakaingia hemani. |
| BSB 8 Then Moses recounted to his father-in-law all that the LORD had done to Pharaoh and the Egyptians for Israel’s sake, all the hardships they had encountered along the way, and how the LORD had delivered them. | SWKCV 8 Mose akamwambia baba mkwe wake kuhusu kila kitu Bwana alichomfanyia Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na pia kuhusu shida zote walizokutana nazo njiani na jinsi Bwana alivyowaokoa. |
| BSB 9 And Jethro rejoiced over all the good things the LORD had done for Israel, whom He had rescued from the hand of the Egyptians. | SWKCV 9 Yethro akafurahishwa sana kusikia juu ya mambo yote mazuri Bwana aliyowatendea Waisraeli kuwaokoa kutoka mkono wa Wamisri. |
| BSB 10 Jethro declared, “Blessed be the LORD, who has delivered you from the hand of the Egyptians and of Pharaoh, and who has delivered the people from the hand of the Egyptians. | SWKCV 10 Yethro akasema, “Sifa na ziwe kwa Bwana, aliyekuokoa wewe kutoka mikononi mwa Wamisri na Farao, na aliyewaokoa watu kutoka mikononi mwa Wamisri. |
| BSB 11 Now I know that the LORD is greater than all other gods, for He did this when they treated Israel with arrogance.” | SWKCV 11 Sasa najua ya kuwa Bwana ni mkuu kuliko miungu mingine yote, kwa kuwa amewatendea hivi wale waliowatenda Israeli kwa ujeuri.” |
| BSB 12 Then Moses’ father-in-law Jethro brought a burnt offering and sacrifices to God, and Aaron came with all the elders of Israel to eat bread with Moses’ father-in-law in the presence of God. | SWKCV 12 Kisha Yethro, baba mkwe wa Mose, akaleta sadaka ya kuteketezwa na dhabihu nyingine kwa Mungu, naye Aroni pamoja na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula pamoja na baba mkwe wa Mose mbele za Mungu. |
| BSB 13 The next day Moses took his seat to judge the people, and they stood around him from morning until evening. | SWKCV 13 Siku iliyofuata, Mose akachukua nafasi yake kama hakimu wa watu, nao wakasimama kumzunguka kuanzia asubuhi hadi jioni. |
| BSB 14 When his father-in-law saw all that Moses was doing for the people, he asked, “What is this that you are doing for the people? Why do you sit alone as judge, with all the people standing around you from morning till evening?” | SWKCV 14 Baba mkwe wake alipoona yote Mose anayowafanyia watu, akasema, “Ni nini hiki unachowafanyia watu? Kwa nini wewe unakuwa mwamuzi wa watu hawa peke yako, wakati watu hawa wamesimama wakikuzunguka tangu asubuhi mpaka jioni?” |
| BSB 15 “Because the people come to me to inquire of God,” Moses replied. | SWKCV 15 Mose akamjibu, “Kwa sababu watu wananijia kutaka mapenzi ya Mungu. |
| BSB 16 “Whenever they have a dispute, it is brought to me to judge between one man and another, and I make known to them the statutes and laws of God.” | SWKCV 16 Kila wakiwa na shauri huletwa kwangu, nami huamua kati ya mtu na mwenzake na kuwajulisha juu ya amri na sheria za Mungu.” |
| BSB 17 But Moses’ father-in-law said to him, “What you are doing is not good. | SWKCV 17 Baba mkwe wa Mose akamjibu, “Unachofanya sio kizuri. |
| BSB 18 Surely you and these people with you will wear yourselves out, because the task is too heavy for you. You cannot handle it alone. | SWKCV 18 Wewe pamoja na watu hawa wanaokujia mtajichosha bure. Kazi ni nzito sana kwako, huwezi kuibeba mwenyewe. |
| BSB 19 Now listen to me; I will give you some advice, and may God be with you. You must be the people’s representative before God and bring their causes to Him. | SWKCV 19 Sasa nisikilize mimi, nitakupa shauri, naye Mungu na awe pamoja nawe. Yapasa wewe uwe mwakilishi wa watu mbele za Mungu na ulete mashauri yao kwake. |
| BSB 20 Teach them the statutes and laws, and show them the way to live and the work they must do. | SWKCV 20 Uwafundishe amri na sheria, tena uwaonyeshe namna ya kuishi na kazi zinazowapasa wao kufanya. |
| BSB 21 Furthermore, select capable men from among the people—God-fearing, trustworthy men who are averse to dishonest gain. Appoint them over the people as leaders of thousands, of hundreds, of fifties, and of tens. | SWKCV 21 Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. |
| BSB 22 Have these men judge the people at all times. Then they can bring you any major issue, but all minor cases they can judge on their own, so that your load may be lightened as they share it with you. | SWKCV 22 Waweke wawe waamuzi wa watu kwa wakati wote, lakini waambie wakuletee kila shauri lililo gumu; yale yaliyo rahisi wayaamue wao wenyewe. Hii itafanya mzigo wako kuwa mwepesi, kwa sababu watashirikiana nawe. |
| BSB 23 If you follow this advice and God so directs you, then you will be able to endure, and all these people can go home in peace.” | SWKCV 23 Kama ukifanya hivi, na ikiwa Mungu ameagiza hivyo, utaweza kushinda uchovu, nao watu hawa wote watarudi nyumbani wameridhika.” |
| BSB 24 Moses listened to his father-in-law and did everything he said. | SWKCV 24 Mose akamsikiliza baba mkwe wake na kufanya kila kitu alichosema. |
| BSB 25 So Moses chose capable men from all Israel and made them heads over the people as leaders of thousands, of hundreds, of fifties, and of tens. | SWKCV 25 Mose akawachagua watu wenye uwezo kutoka Israeli yote, akawafanya kuwa viongozi wa watu, maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi. |
| BSB 26 And they judged the people at all times; they would bring the difficult cases to Moses, but any minor issue they would judge themselves. | SWKCV 26 Wakatumika kama waamuzi wa watu kwa wakati wote. Mashauri magumu wakayaleta kwa Mose, lakini yale yaliyo rahisi wakayaamua wenyewe. |
| BSB 27 Then Moses sent his father-in-law on his way, and Jethro returned to his own land. | SWKCV 27 Kisha Mose akaagana na Yethro baba mkwe wake, naye akarudi kwa nchi yake. |
Questions about Exodus 18? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.