Exodus 29
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Now this is what you are to do to consecrate Aaron and his sons to serve Me as priests: Take a young bull and two rams without blemish, | SWKCV 1 “Hili ndilo utakalofanya ili kuwaweka wakfu makuhani ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani: Chukua fahali mchanga mmoja na kondoo dume wawili wasio na dosari. |
| BSB 2 along with unleavened bread, unleavened cakes mixed with oil, and unleavened wafers anointed with oil. Make them out of fine wheat flour, | SWKCV 2 Kutokana na unga laini wa ngano usiotiwa chachu, tengeneza mikate na maandazi yaliyokandwa kwa mafuta, pamoja na mikate midogo myembamba. |
| BSB 3 put them in a basket, and present them in the basket, along with the bull and the two rams. | SWKCV 3 Viwekwe vyote ndani ya kikapu na kuvitoa pamoja na yule fahali na wale kondoo dume wawili. |
| BSB 4 Then present Aaron and his sons at the entrance to the Tent of Meeting and wash them with water. | SWKCV 4 Kisha mlete Aroni na wanawe kwenye lango la Hema la Kukutania na uwaoshe kwa maji. |
| BSB 5 Take the garments and clothe Aaron with the tunic, the robe of the ephod, the ephod itself, and the breastplate. Fasten the ephod on him with its woven waistband. | SWKCV 5 Chukua yale mavazi na umvike Aroni koti, joho la kisibau na kisibau chenyewe pamoja na kile kifuko cha kifuani. Mfungie hicho kisibau kwa ule mshipi wa kiunoni uliosukwa kwa ustadi. |
| BSB 6 Put the turban on his head and attach the holy diadem to the turban. | SWKCV 6 Weka kilemba kichwani mwake na kuweka taji takatifu ishikamane na hicho kilemba. |
| BSB 7 Then take the anointing oil and anoint him by pouring it on his head. | SWKCV 7 Chukua yale mafuta ya upako umimine juu ya kichwa chake. |
| BSB 8 Present his sons as well and clothe them with tunics. | SWKCV 8 Walete wanawe na uwavike makoti, |
| BSB 9 Wrap the sashes around Aaron and his sons and tie headbands on them. The priesthood shall be theirs by a permanent statute. In this way you are to ordain Aaron and his sons. | SWKCV 9 pia uwavike zile tepe za kichwani. Ndipo uwafunge Aroni na wanawe mishipi. Ukuhani ni wao kwa agizo la kudumu. Kwa njia hii utamweka wakfu Aroni na wanawe. |
| BSB 10 You are to present the bull at the front of the Tent of Meeting, and Aaron and his sons are to lay their hands on its head. | SWKCV 10 “Mlete yule fahali mbele ya Hema la Kukutania, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. |
| BSB 11 And you shall slaughter the bull before the LORD at the entrance to the Tent of Meeting. | SWKCV 11 Mchinje huyo fahali mbele za Bwana kwenye mlango wa Hema la Kukutania. |
| BSB 12 Take some of the blood of the bull and put it on the horns of the altar with your finger; then pour out the rest of the blood at the base of the altar. | SWKCV 12 Chukua sehemu ya damu ya huyo fahali na kuipaka kwenye pembe za hayo madhabahu kwa kidole chako, na damu iliyobaki uimwage sehemu ya chini ya madhabahu. |
| BSB 13 Take all the fat that covers the entrails and the lobe of the liver, and both kidneys with the fat on them, and burn them on the altar. | SWKCV 13 Kisha chukua mafuta yote ya huyo mnyama ya sehemu za ndani, yale yanayofunika ini, figo zote mbili pamoja na mafuta yake, uviteketeze juu ya madhabahu. |
| BSB 14 But burn the flesh of the bull and its hide and dung outside the camp; it is a sin offering. | SWKCV 14 Lakini nyama ya huyo fahali na ngozi yake na matumbo yake utavichoma nje ya kambi. Hii ni sadaka ya dhambi. |
| BSB 15 Take one of the rams, and Aaron and his sons shall lay their hands on its head. | SWKCV 15 “Chukua mmoja wa wale kondoo dume, naye Aroni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake. |
| BSB 16 You are to slaughter the ram, take its blood, and splatter it on all sides of the altar. | SWKCV 16 Mchinje huyo kondoo dume, chukua damu yake na uinyunyize pande zote za hayo madhabahu. |
| BSB 17 Cut the ram into pieces, wash the entrails and legs, and place them with its head and other pieces. | SWKCV 17 Mkate huyo kondoo dume vipande vipande na usafishe sehemu za ndani pamoja na miguu, ukiviweka pamoja na kichwa na vipande vingine. |
| BSB 18 Then burn the entire ram on the altar; it is a burnt offering to the LORD, a pleasing aroma, a food offering to the LORD. | SWKCV 18 Kisha mteketeze huyo kondoo dume mzima juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. |
| BSB 19 Take the second ram, and Aaron and his sons are to lay their hands on its head. | SWKCV 19 “Mchukue yule kondoo dume mwingine, naye Aroni na wanawe waweke mikono yao juu ya kichwa chake. |
| BSB 20 Slaughter the ram, take some of its blood, and put it on the right earlobes of Aaron and his sons, on the thumbs of their right hands, and on the big toes of their right feet. Splatter the remaining blood on all sides of the altar. | SWKCV 20 Mchinje, uchukue sehemu ya damu yake na kuipaka kwenye masikio ya Aroni na wanawe, kwenye vidole gumba vya mikono yao ya kuume, pia kwenye vidole gumba vya miguu yao ya kuume. Kisha nyunyiza hiyo damu pande zote za madhabahu. |
| BSB 21 And take some of the blood on the altar and some of the anointing oil and sprinkle it on Aaron and his garments, as well as on his sons and their garments. Then he and his garments will be consecrated, as well as his sons and their garments. | SWKCV 21 Pia chukua sehemu ya damu iliyo juu ya madhabahu na sehemu ya mafuta ya upako, umnyunyizie Aroni na mavazi yake, pia wanawe na mavazi yao. Ndipo Aroni na wanawe pamoja na mavazi yao watakuwa wamewekwa wakfu. |
| BSB 22 Take the fat from the ram, the fat tail, the fat covering the entrails, the lobe of the liver, both kidneys with the fat on them, and the right thigh (since this is a ram for ordination), | SWKCV 22 “Chukua mafuta ya huyu kondoo dume, mafuta ya mkia, mafuta ya sehemu za ndani yale yanayofunika ini, figo zote mbili na mafuta yake, pamoja na paja la kulia. (Huyo ndiye kondoo dume kwa ajili ya kuwaweka wakfu.) |
| BSB 23 along with one loaf of bread, one cake of bread made with oil, and one wafer from the basket of unleavened bread that is before the LORD. | SWKCV 23 Kutoka kwenye kile kikapu chenye mikate iliyotengenezwa bila chachu, kilichoko mbele za Bwana, chukua mkate, andazi lililokandwa kwa mafuta na mkate mdogo mwembamba. |
| BSB 24 Put all these in the hands of Aaron and his sons and wave them before the LORD as a wave offering. | SWKCV 24 Viweke vitu hivi vyote mikononi mwa Aroni na wanawe na uviinue mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa. |
| BSB 25 Then take them from their hands and burn them on the altar atop the burnt offering as a pleasing aroma before the LORD; it is a food offering to the LORD. | SWKCV 25 Kisha vichukue vitu hivyo kutoka mikononi mwao, uviteketeze juu ya madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa kuwa harufu nzuri ya kupendeza kwa Bwana, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. |
| BSB 26 Take the breast of the ram of Aaron’s ordination and wave it before the LORD as a wave offering, and it will be your portion. | SWKCV 26 Baada ya kuchukua kidari cha huyo kondoo dume wa kuwekwa wakfu kwa Aroni, kiinue mbele za Bwana kuwa sadaka ya kuinuliwa, nayo itakuwa fungu lako. |
| BSB 27 Consecrate for Aaron and his sons the breast of the wave offering that is waved and the thigh of the heave offering that is lifted up from the ram of ordination. | SWKCV 27 “Weka wakfu zile sehemu za kondoo dume aliyetumika kwa kumweka wakfu Aroni na wanawe: kidari kile kilichoinuliwa na lile paja lililotolewa. |
| BSB 28 This will belong to Aaron and his sons as a regular portion from the Israelites, for it is the heave offering the Israelites will make to the LORD from their peace offerings. | SWKCV 28 Siku zote hili litakuwa fungu la kawaida kutoka kwa Waisraeli kwa ajili ya Aroni na wanawe. Hili ni toleo la Waisraeli watakalotoa kwa Bwana kutoka sadaka zao za amani. |
| BSB 29 The holy garments that belong to Aaron will belong to his sons after him, so they can be anointed and ordained in them. | SWKCV 29 “Mavazi matakatifu ya Aroni yatakuwa ya wazao wake ili kwamba waweze kutiwa mafuta na kuwekwa wakfu wakiwa wameyavaa. |
| BSB 30 The son who succeeds him as priest and enters the Tent of Meeting to minister in the Holy Place must wear them for seven days. | SWKCV 30 Mwana atakayeingia mahali pake kuwa kuhani na kuja kwenye Hema la Kukutania kuhudumu katika Mahali Patakatifu atayavaa kwa siku saba. |
| BSB 31 You are to take the ram of ordination and boil its flesh in a holy place. | SWKCV 31 “Chukua nyama ya huyo kondoo dume wa kuwaweka wakfu uipike katika Mahali Patakatifu. |
| BSB 32 At the entrance to the Tent of Meeting, Aaron and his sons are to eat the meat of the ram and the bread that is in the basket. | SWKCV 32 Aroni na wanawe wataila ile nyama ya huyo kondoo dume pamoja na ile mikate iliyo kwenye hicho kikapu wakiwa hapo ingilio la Hema la Kukutania. |
| BSB 33 They must eat those things by which atonement was made for their ordination and consecration. But no outsider may eat them, because these things are sacred. | SWKCV 33 Watakula sadaka hizi ambazo upatanisho ulifanywa kwazo kwa ajili ya kuwaweka wakfu na kuwatakasa. Lakini hakuna mtu mwingine yeyote anayeruhusiwa kuvila, kwa sababu ni vitakatifu. |
| BSB 34 And if any of the meat of ordination or any bread is left until the morning, you are to burn up the remainder. It must not be eaten, because it is sacred. | SWKCV 34 Ikiwa nyama yoyote ya huyo kondoo dume iliyotumika kwa kuwaweka wakfu au mkate wowote umebaki mpaka asubuhi, vichomwe. Kamwe visiliwe, kwa sababu ni vitakatifu. |
| BSB 35 This is what you are to do for Aaron and his sons based on all that I have commanded you, taking seven days to ordain them. | SWKCV 35 “Hivyo utamfanyia Aroni na wanawe kila kitu kama vile nilivyokuamuru: Utachukua muda wa siku saba kuwaweka wakfu. |
| BSB 36 Sacrifice a bull as a sin offering each day for atonement. Purify the altar by making atonement for it, and anoint it to consecrate it. | SWKCV 36 Utatoa dhabihu ya fahali kila siku kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho. Takasa madhabahu kwa kufanya upatanisho kwa ajili yake, nayo uitie mafuta na kuiweka wakfu. |
| BSB 37 For seven days you shall make atonement for the altar and consecrate it. Then the altar will become most holy; whatever touches the altar will be holy. | SWKCV 37 Kwa muda wa siku saba fanya upatanisho kwa ajili ya madhabahu na kuiweka wakfu. Ndipo madhabahu itakuwa takatifu sana na chochote kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu. |
| BSB 38 This is what you are to offer regularly on the altar, each day: two lambs that are a year old. | SWKCV 38 “Kwa kawaida hiki ndicho utakachotoa juu ya madhabahu kila siku: wana-kondoo wawili wenye umri wa mwaka mmoja. |
| BSB 39 Offer one lamb in the morning and the other at twilight. | SWKCV 39 Utamtoa mmoja asubuhi na huyo mwingine jioni. |
| BSB 40 With the first lamb offer a tenth of an ephah of fine flour, mixed with a quarter hin of oil from pressed olives, and a drink offering of a quarter hin of wine. | SWKCV 40 Pamoja na mwana-kondoo wa kwanza utatoa efa moja ya unga wa ngano laini uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta yaliyokamuliwa, pamoja na robo ya hini ya divai kuwa sadaka ya kinywaji. |
| BSB 41 And offer the second lamb at twilight with the same grain offering and drink offering as in the morning, as a pleasing aroma, a food offering to the LORD. | SWKCV 41 Huyo mwana-kondoo mwingine mtoe dhabihu wakati wa machweo pamoja na sadaka za unga na za kinywaji kama vile ulivyofanya asubuhi, kuwa harufu ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto. |
| BSB 42 For the generations to come, this burnt offering shall be made regularly at the entrance to the Tent of Meeting before the LORD, where I will meet you to speak with you. | SWKCV 42 “Kwa vizazi vijavyo itakuwa kawaida kutoa sadaka hii ya kuteketezwa kila mara kwenye ingilio la Hema la Kukutania mbele za Bwana. Hapo ndipo nitakapokutana na ninyi na kusema nanyi, |
| BSB 43 I will also meet with the Israelites there, and that place will be consecrated by My glory. | SWKCV 43 Huko ndipo nitakapokutana na Waisraeli, nalo Hema la Kukutania litatakaswa na utukufu wangu. |
| BSB 44 So I will consecrate the Tent of Meeting and the altar, and I will consecrate Aaron and his sons to serve Me as priests. | SWKCV 44 “Kwa hiyo nitaliweka wakfu Hema la Kukutania pamoja na madhabahu, nami nitamweka wakfu Aroni na wanawe ili wanitumikie mimi katika kazi ya ukuhani. |
| BSB 45 Then I will dwell among the Israelites and be their God. | SWKCV 45 Ndipo nitakapofanya makao miongoni mwa Waisraeli na kuwa Mungu wao. |
| BSB 46 And they will know that I am the LORD their God, who brought them out of the land of Egypt so that I might dwell among them. I am the LORD their God. | SWKCV 46 Nao watajua kuwa Mimi Ndimi Bwana Mungu wao, aliyewatoa Misri ili nipate kufanya makao miongoni mwao. Mimi Ndimi Bwana Mungu wao. |
Questions about Exodus 29? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.