Exodus 28
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 “Next, have your brother Aaron brought to you from among the Israelites, along with his sons Nadab, Abihu, Eleazar, and Ithamar, to serve Me as priests. | SWKCV 1 “Mtwae Aroni ndugu yako aliyeletwa kwako kutoka miongoni mwa Waisraeli, pamoja na wanawe Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. |
| BSB 2 Make holy garments for your brother Aaron, to give him glory and splendor. | SWKCV 2 Mshonee Aroni ndugu yako mavazi matakatifu ili yampe ukuu na heshima. |
| BSB 3 You are to instruct all the skilled craftsmen, whom I have filled with a spirit of wisdom, to make garments for Aaron’s consecration, so that he may serve Me as priest. | SWKCV 3 Waambie mafundi stadi wote niliowapa hekima katika shughuli hiyo wamtengenezee Aroni mavazi hayo, ili awekwe wakfu, anitumikie katika kazi ya ukuhani. |
| BSB 4 These are the garments that they shall make: a breastpiece, an ephod, a robe, a woven tunic, a turban, and a sash. They are to make these holy garments for your brother Aaron and his sons, so that they may serve Me as priests. | SWKCV 4 Haya ndiyo mavazi watakayoshona: kifuko cha kifuani, kisibau, kanzu, joho lililorembwa, kilemba na mshipi. Mavazi haya yatashonwa kwa ajili ya ndugu yako Aroni na wanawe ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. |
| BSB 5 They shall use gold, along with blue, purple, and scarlet yarn, and fine linen. | SWKCV 5 Waambie watumie dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu pamoja na kitani safi. |
| BSB 6 They are to make the ephod of finely spun linen embroidered with gold, and with blue, purple, and scarlet yarn. | SWKCV 6 “Tengeneza kisibau cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, za rangi nyekundu na kitani safi iliyosokotwa, kazi ya fundi stadi. |
| BSB 7 It shall have two shoulder pieces attached at two of its corners, so it can be fastened. | SWKCV 7 Kitakuwa na vipande viwili vya mabegani vilivyoshikizwa kwenye pembe zake mbili ili kufungia kisibau. |
| BSB 8 And the skillfully woven waistband of the ephod must be of one piece, of the same workmanship—with gold, with blue, purple, and scarlet yarn, and with finely spun linen. | SWKCV 8 Mshipi wa kiunoni uliofumwa kwa ustadi utafanana nacho: utakuwa kitu kimoja na hicho kisibau, nao utengenezwe kwa dhahabu na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na nyekundu na kwa kitani iliyosokotwa vizuri. |
| BSB 9 Take two onyx stones and engrave on them the names of the sons of Israel: | SWKCV 9 “Chukua vito viwili vya shohamu, na uchore juu yake majina ya wana wa Israeli |
| BSB 10 six of their names on one stone and the remaining six on the other, in the order of their birth. | SWKCV 10 kufuatana na walivyozaliwa: majina sita katika kito kimoja, na mengine sita katika kito kingine. |
| BSB 11 Engrave the names of the sons of Israel on the two stones the way a gem cutter engraves a seal. Then mount the stones in gold filigree settings. | SWKCV 11 Yachore majina ya wana wa Israeli juu ya vito hivyo viwili kama vile sonara anavyochonga muhuri. Kisha uvitie vito hivyo katika vijalizo vya dhahabu, |
| BSB 12 Fasten both stones on the shoulder pieces of the ephod as memorial stones for the sons of Israel. Aaron is to bear their names on his two shoulders as a memorial before the LORD. | SWKCV 12 na uvifungie juu ya vipande vya mabega ya kisibau yawe kama vito vya ukumbusho kwa wana wa Israeli. Aroni atavaa majina hayo mabegani mwake kama kumbukumbu mbele za Bwana. |
| BSB 13 Fashion gold filigree settings | SWKCV 13 Tengeneza vijalizo vya dhahabu |
| BSB 14 and two chains of pure gold, made of braided cord work; and attach these chains to the settings. | SWKCV 14 na mikufu miwili ya dhahabu safi iliyosokotwa kama kamba, na uifunge mikufu hiyo kwenye vijalizo. |
| BSB 15 You are also to make a breastpiece of judgment with the same workmanship as the ephod. Construct it with gold, with blue, purple, and scarlet yarn, and with finely spun linen. | SWKCV 15 “Fanyiza kifuko cha kifuani kwa ajili ya kufanya maamuzi, kazi ya fundi stadi. Kitengeneze kama kile kisibau: cha dhahabu, na nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu, cha kitani safi iliyosokotwa. |
| BSB 16 It must be square when folded over double, a span long and a span wide. | SWKCV 16 Kitakuwa cha mraba, chenye urefu wa shibiri moja na upana wa shibiri moja, na kikunjwe mara mbili. |
| BSB 17 And mount on it a setting of gemstones, four rows of stones: In the first row there shall be a ruby, a topaz, and an emerald; | SWKCV 17 Kisha weka safu nne za vito vya thamani juu yake. Safu ya kwanza itakuwa na akiki, yakuti manjano na zabarajadi; |
| BSB 18 in the second row a turquoise, a sapphire, and a diamond; | SWKCV 18 katika safu ya pili itakuwa na almasi, yakuti samawi na zumaridi; |
| BSB 19 in the third row a jacinth, an agate, and an amethyst; | SWKCV 19 safu ya tatu itakuwa na hiakintho, akiki nyekundu na amethisto; |
| BSB 20 and in the fourth row a beryl, an onyx, and a jasper. Mount these stones in gold filigree settings. | SWKCV 20 na safu ya nne itakuwa na krisolitho, shohamu na yaspi. Yote yatiwe kwenye vijalizo vya dhahabu. |
| BSB 21 The twelve stones are to correspond to the names of the sons of Israel, each engraved like a seal with the name of one of the twelve tribes. | SWKCV 21 Patakuwa na vito kumi na viwili, kila kimoja kwa jina mojawapo la wana wa Israeli, kila kimoja kichorwe kama muhuri kikiwa na jina mojawapo la yale makabila kumi na mawili. |
| BSB 22 For the breastpiece, make braided chains like cords of pure gold. | SWKCV 22 “Kwa ajili ya kile kifuko cha kifuani, tengeneza mikufu ya dhahabu safi, iliyosokotwa kama kamba. |
| BSB 23 You are also to make two gold rings and fasten them to the two corners of the breastpiece. | SWKCV 23 Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili yake, uzifungie kwenye pembe mbili za hicho kifuko cha kifuani. |
| BSB 24 Then fasten the two gold chains to the two gold rings at the corners of the breastpiece, | SWKCV 24 Funga ile mikufu miwili ya dhahabu kwenye hizo pete zilizo katika pembe za hicho kifuko cha kifuani, |
| BSB 25 and fasten the other ends of the two chains to the two filigree settings, attaching them to the shoulder pieces of the ephod at the front. | SWKCV 25 nazo zile ncha nyingine za mkufu zifunge kwenye vile vijalizo viwili, na uzishikamanishe na vile vipande vya mabega vya kile kisibau upande wa mbele. |
| BSB 26 Make two more gold rings and attach them to the other two corners of the breastpiece, on the inside edge next to the ephod. | SWKCV 26 Tengeneza pete mbili za dhahabu, uzishikamanishe kwenye pembe mbili za chini, upande wa ndani wa kifuko cha kifuani karibu na kisibau. |
| BSB 27 Make two additional gold rings and attach them to the bottom of the two shoulder pieces of the ephod, on its front, near its seam just above its woven waistband. | SWKCV 27 Tengeneza pete nyingine mbili za dhahabu, na uzishikamanishe sehemu ya chini ya vipande vya mabega upande wa mbele wa kile kisibau, karibu na pindo juu kidogo ya mshipi wa kiunoni wa kisibau. |
| BSB 28 The rings of the breastpiece shall be tied to the rings of the ephod with a cord of blue yarn, so that the breastpiece is above the waistband of the ephod and does not swing out from the ephod. | SWKCV 28 Pete za kifuko cha kifuani zitafungwa kwenye pete zile za kisibau kwa kamba ya buluu, ziunganishwe na ule mshipi wa kiunoni, ili kifuko cha kifuani kisisogee kutoka kwenye kile kisibau. |
| BSB 29 Whenever Aaron enters the Holy Place, he shall bear the names of the sons of Israel over his heart on the breastpiece of judgment, as a continual reminder before the LORD. | SWKCV 29 “Wakati wowote Aroni aingiapo Mahali Patakatifu, atakuwa na yale majina ya wana wa Israeli moyoni mwake juu ya kile kifuko cha kifuani cha uamuzi kama kumbukumbu ya kudumu mbele za Bwana. |
| BSB 30 And place the Urim and Thummim in the breastpiece of judgment, so that they will also be over Aaron’s heart whenever he comes before the LORD. Aaron will continually carry the judgment of the sons of Israel over his heart before the LORD. | SWKCV 30 Pia weka Urimu na Thumimu ndani ya kifuko cha kifuani, yawe juu ya moyo wa Aroni kila mara aingiapo mbele za Bwana. Kwa hiyo siku zote Aroni atakuwa na uwezo kufanya maamuzi kwa ajili ya wana wa Israeli mbele za Bwana. |
| BSB 31 You are to make the robe of the ephod entirely of blue cloth, | SWKCV 31 “Shona joho la kisibau lote kwa kitambaa cha rangi ya buluu tupu, |
| BSB 32 with an opening at its top in the center. Around the opening shall be a woven collar with an opening like that of a garment, so that it will not tear. | SWKCV 32 na katikati uweke nafasi ya kuingizia kichwa. Kutakuwa na utepe uliofumwa, unaofanana na ukosi kuizunguka nafasi hiyo, ili isichanike. |
| BSB 33 Make pomegranates of blue, purple, and scarlet yarn all the way around the lower hem, with gold bells between them, | SWKCV 33 Tengeneza makomamanga ya nyuzi za rangi ya buluu, za zambarau, na za rangi nyekundu kuzunguka pindo la hilo joho, na uweke pia vikengele vya dhahabu kati ya hayo makomamanga. |
| BSB 34 alternating the gold bells and pomegranates around the lower hem of the robe. | SWKCV 34 Hivyo vikengele vya dhahabu na makomamanga vitapishana kuzunguka upindo wa joho lile. |
| BSB 35 Aaron must wear the robe whenever he ministers, and its sound will be heard when he enters or exits the sanctuary before the LORD, so that he will not die. | SWKCV 35 Ni lazima Aroni alivae anapofanya huduma. Sauti ya hivyo vikengele itasikika anapoingia na kutoka Mahali Patakatifu mbele za Bwana, ili asije akafa. |
| BSB 36 You are to make a plate of pure gold and engrave on it as on a seal: HOLY TO THE LORD. | SWKCV 36 “Tengeneza bamba la dhahabu safi na uchore juu yake maneno haya kama vile muhuri huchorwa: Mtakatifu kwa Bwana. |
| BSB 37 Fasten to it a blue cord to mount it on the turban; it shall be on the front of the turban. | SWKCV 37 Lifunge hilo bamba kwa kamba ya buluu kwenye kilemba, nalo ni lazima liwe mbele ya kilemba. |
| BSB 38 And it will be worn on Aaron’s forehead, so that he may bear the iniquity of the holy things that the sons of Israel consecrate with regard to all their holy gifts. It shall always be on his forehead, so that they may be acceptable before the LORD. | SWKCV 38 Aroni alivae bamba hilo kwenye paji la uso wake, naye atachukua hatia kuhusu sadaka takatifu za Waisraeli wanazoweka wakfu, sadaka za aina yoyote. Litakuwa kwenye paji la uso wa Aroni daima ili zikubalike kwa Bwana. |
| BSB 39 You are to weave the tunic with fine linen, make the turban of fine linen, and fashion an embroidered sash. | SWKCV 39 “Fuma koti la kitani safi na ufanye kilemba cha kitani safi. Mshipi uwe ni kazi ya mtarizi. |
| BSB 40 Make tunics, sashes, and headbands for Aaron’s sons, to give them glory and splendor. | SWKCV 40 Watengenezee wana wa Aroni makoti, mishipi na kofia, ili kuwapa ukuu na heshima. |
| BSB 41 After you put these garments on your brother Aaron and his sons, anoint them, ordain them, and consecrate them so that they may serve Me as priests. | SWKCV 41 Baada ya kumvika Aroni ndugu yako pamoja na wanawe nguo hizi, watie mafuta na kuwabariki. Waweke wakfu ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani. |
| BSB 42 Make linen undergarments to cover their bare flesh, extending from waist to thigh. | SWKCV 42 “Watengenezee nguo za ndani za kitani zitakazofunika mwili, kutoka kiunoni hadi mapajani. |
| BSB 43 Aaron and his sons must wear them whenever they enter the Tent of Meeting or approach the altar to minister in the Holy Place, so that they will not incur guilt and die. This is to be a permanent statute for Aaron and his descendants. | SWKCV 43 Aroni na wanawe ni lazima wavae haya kila wanapoingia katika Hema la Kukutania au wanaposogelea madhabahu wakati wa kutoa huduma katika Mahali Patakatifu, ili wasije wakafanya kosa wakafa. “Haya yawe maagizo ya kudumu kwa Aroni na vizazi vyake. |
Questions about Exodus 28? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.