Genesis 4
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 And Adam had relations with his wife Eve, and she conceived and gave birth to Cain. “With the help of the LORD I have brought forth a man,” she said. | SWKCV 1 Adamu akakutana kimwili na mkewe Eva, naye akapata mimba, akamzaa Kaini. Eva akasema, “Kwa msaada wa Bwana nimemzaa mwanaume.” |
| BSB 2 Later she gave birth to Cain’s brother Abel. Now Abel was a keeper of sheep, while Cain was a tiller of the soil. | SWKCV 2 Baadaye akamzaa Abeli ndugu yake. Basi Abeli akawa mfugaji, na Kaini akawa mkulima. |
| BSB 3 So in the course of time, Cain brought some of the fruit of the soil as an offering to the LORD, | SWKCV 3 Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana. |
| BSB 4 while Abel brought the best portions of the firstborn of his flock. And the LORD looked with favor on Abel and his offering, | SWKCV 4 Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Bwana akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake, |
| BSB 5 but He had no regard for Cain and his offering. So Cain became very angry, and his countenance fell. | SWKCV 5 lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni. |
| BSB 6 “Why are you angry,” said the LORD to Cain, “and why has your countenance fallen? | SWKCV 6 Kisha Bwana akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? |
| BSB 7 If you do what is right, will you not be accepted? But if you refuse to do what is right, sin is crouching at your door; it desires you, but you must master it.” | SWKCV 7 Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde.” |
| BSB 8 Then Cain said to his brother Abel, “Let us go out to the field.” And while they were in the field, Cain rose up against his brother Abel and killed him. | SWKCV 8 Basi Kaini akamwambia ndugu yake Abeli, “Twende shambani.” Walipokuwa shambani, Kaini akamshambulia Abeli ndugu yake, akamuua. |
| BSB 9 And the LORD said to Cain, “Where is your brother Abel?” “I do not know!” he answered. “Am I my brother’s keeper?” | SWKCV 9 Kisha Bwana akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Abeli yuko wapi?” Akamjibu, “Sijui, je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?” |
| BSB 10 “What have you done?” replied the LORD. “The voice of your brother’s blood cries out to Me from the ground. | SWKCV 10 Bwana akasema, “Umefanya nini? Sikiliza! Damu ya ndugu yako inanililia mimi kutoka ardhini. |
| BSB 11 Now you are cursed and banished from the ground, which has opened its mouth to receive your brother’s blood from your hand. | SWKCV 11 Sasa umelaaniwa na umehamishwa kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake na kupokea damu ya ndugu yako kutoka mkononi mwako. |
| BSB 12 When you till the ground, it will no longer yield its produce to you. You will be a fugitive and a wanderer on the earth.” | SWKCV 12 Utakapoilima ardhi, haitakupa tena mazao yake. Utakuwa mtu wa kutangatanga duniani asiye na utulivu.” |
| BSB 13 But Cain said to the LORD, “My punishment is greater than I can bear. | SWKCV 13 Kaini akamwambia Bwana, “Adhabu yangu ni zaidi ya niwezavyo kustahimili. |
| BSB 14 Behold, this day You have driven me from the face of the earth, and from Your face I will be hidden; I will be a fugitive and a wanderer on the earth, and whoever finds me will kill me.” | SWKCV 14 Leo unanifukuza kutoka nchi, nami nitafichwa mbali na uwepo wako. Nitakuwa mtu wa kutangatanga asiyetulia duniani na yeyote anionaye ataniua.” |
| BSB 15 “Not so!” replied the LORD. “If anyone slays Cain, then Cain will be avenged sevenfold.” And the LORD placed a mark on Cain, so that no one who found him would kill him. | SWKCV 15 Lakini Bwana akamwambia, “La sivyo, ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba zaidi.” Kisha Bwana akamwekea Kaini alama ili mtu yeyote ambaye angemwona asimuue. |
| BSB 16 So Cain went out from the presence of the LORD and settled in the land of Nod, east of Eden. | SWKCV 16 Kwa hiyo Kaini akaondoka mbele za Bwana akaenda kuishi katika nchi ya Nodi, iliyoko mashariki ya Edeni. |
| BSB 17 And Cain had relations with his wife, and she conceived and gave birth to Enoch. Then Cain built a city and named it after his son Enoch. | SWKCV 17 Kaini akakutana kimwili na mkewe, naye akapata mimba na akamzaa Enoki. Wakati huo Kaini alikuwa anajenga mji, akauita Enoki jina la mtoto wake. |
| BSB 18 Now to Enoch was born Irad, and Irad was the father of Mehujael, and Mehujael was the father of Methusael, and Methusael was the father of Lamech. | SWKCV 18 Enoki akamzaa Iradi, Iradi akamzaa Mehuyaeli, Mehuyaeli akamzaa Methushaeli, na Methushaeli akamzaa Lameki. |
| BSB 19 And Lamech married two women, one named Adah and the other Zillah. | SWKCV 19 Lameki alioa wanawake wawili, mmoja aliitwa Ada, na mwingine Sila. |
| BSB 20 Adah gave birth to Jabal; he was the father of those who dwell in tents and raise livestock. | SWKCV 20 Ada akamzaa Yabali ambaye ni baba wa wale walioishi katika mahema na kufuga wanyama. |
| BSB 21 And his brother’s name was Jubal; he was the father of all who play the harp and flute. | SWKCV 21 Kaka yake aliitwa Yubali, aliyekuwa baba wa wote wapigao zeze na filimbi. |
| BSB 22 And Zillah gave birth to Tubal-cain, a forger of every implement of bronze and iron. And the sister of Tubal-cain was Naamah. | SWKCV 22 Pia Sila alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Tubali-Kaini ambaye alifua vifaa vya aina mbalimbali vya shaba na chuma. Naama alikuwa dada wa Tubali-Kaini. |
| BSB 23 Then Lamech said to his wives: “Adah and Zillah, hear my voice; wives of Lamech, listen to my speech. For I have slain a man for wounding me, a young man for striking me. | SWKCV 23 Lameki akawaambia wake zake, “Ada na Sila nisikilizeni mimi; wake wa Lameki sikieni maneno yangu. Nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana mdogo kwa kuniumiza. |
| BSB 24 If Cain is avenged sevenfold, then Lamech seventy-sevenfold.” | SWKCV 24 Kama Kaini atalipizwa kisasi mara saba, basi Lameki itakuwa mara sabini na saba.” |
| BSB 25 And Adam again had relations with his wife, and she gave birth to a son and named him Seth, saying, “God has granted me another seed in place of Abel, since Cain killed him.” | SWKCV 25 Adamu akakutana kimwili na mke wake tena, akamzaa mwana, akamwita Sethi, akisema, “Mungu amenijalia mwana mwingine badala ya Abeli, kwa kuwa Kaini alimuua.” |
| BSB 26 And to Seth also a son was born, and he called him Enosh. At that time men began to call upon the name of the LORD. | SWKCV 26 Naye Sethi akamzaa mwana, akamwita Enoshi. Wakati huo watu wakaanza kuliitia jina la Bwana. |
Questions about Genesis 4? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.