Hebrews 11
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now faith is the assurance of what we hope for and the certainty of what we do not see. | SWKCV 1 Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, na udhahiri wa mambo yasiyoonekana. |
| BSB 2 This is why the ancients were commended. | SWKCV 2 Maana baba zetu wa kale walipongezwa kwa haya. |
| BSB 3 By faith we understand that the universe was formed at God’s command, so that what is seen was not made out of what was visible. | SWKCV 3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vyote vinavyoonekana havikuumbwa kutoka kwa vitu vinavyoonekana. |
| BSB 4 By faith Abel offered God a better sacrifice than Cain did. By faith he was commended as righteous when God gave approval to his gifts. And by faith he still speaks, even though he is dead. | SWKCV 4 Kwa imani Abeli alimtolea Mungu dhabihu bora zaidi kuliko Kaini. Kwa imani alishuhudiwa kuwa mwenye haki, Mungu mwenyewe akazishuhudia sadaka zake. Kwa imani bado ananena ingawa amekufa. |
| BSB 5 By faith Enoch was taken up so that he did not see death: “He could not be found, because God had taken him away.” For before he was taken, he was commended as one who pleased God. | SWKCV 5 Kwa imani Enoki alitwaliwa kutoka maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti. Hakuonekana, kwa sababu Mungu alikuwa amemchukua. Kwa kuwa kabla hajatwaliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza Mungu. |
| BSB 6 And without faith it is impossible to please God. For anyone who approaches Him must believe that He exists and that He rewards those who earnestly seek Him. | SWKCV 6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii. |
| BSB 7 By faith Noah, when warned about things not yet seen, in godly fear built an ark to save his family. By faith he condemned the world and became heir of the righteousness that comes by faith. | SWKCV 7 Kwa imani, Noa alipoonywa na Mungu kuhusu mambo ambayo hayajaonekana bado, kwa kumcha Mungu alitengeneza safina ili kuokoa jamaa yake. Kwa imani yake aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani. |
| BSB 8 By faith Abraham, when called to go to a place he would later receive as his inheritance, obeyed and went, without knowing where he was going. | SWKCV 8 Kwa imani Abrahamu, alipoitwa aende mahali ambapo Mungu angempa baadaye kuwa urithi, alitii na akaenda, ingawa hakujua anakokwenda. |
| BSB 9 By faith he dwelt in the promised land as a stranger in a foreign country. He lived in tents, as did Isaac and Jacob, who were heirs with him of the same promise. | SWKCV 9 Kwa imani alifanya maskani yake katika nchi ya ahadi kama mgeni katika nchi ya kigeni; aliishi katika mahema, kama Isaki na Yakobo walivyofanya, waliokuwa pia warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. |
| BSB 10 For he was looking forward to the city with foundations, whose architect and builder is God. | SWKCV 10 Kwa maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi ya kudumu ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. |
| BSB 11 By faith Sarah, even though she was barren and beyond the proper age, was enabled to conceive a child, because she considered Him faithful who had promised. | SWKCV 11 Kwa imani Abrahamu, ingawa alikuwa mzee wa umri, naye Sara mwenyewe aliyekuwa tasa, alipokea uwezo wa kuwa baba kwa sababu alimhesabu Mungu aliyemwahidi kuwa mwaminifu na kwamba angetimiza ahadi yake. |
| BSB 12 And so from one man, and he as good as dead, came descendants as numerous as the stars in the sky and as countless as the sand on the seashore. | SWKCV 12 Hivyo kutokana na huyu huyu ambaye alikuwa sawa na mfu, wakazaliwa wazao wengi kama nyota za mbinguni na kama mchanga wa pwani usiohesabika. |
| BSB 13 All these people died in faith, without having received the things they were promised. However, they saw them and welcomed them from afar. And they acknowledged that they were strangers and exiles on the earth. | SWKCV 13 Watu hawa wote wakafa katika imani bila kuzipokea zile ahadi, lakini waliziona kwa mbali na kuzishangilia. Nao walikubali kwamba walikuwa wageni na wasiokuwa na maskani hapa duniani. |
| BSB 14 Now those who say such things show that they are seeking a country of their own. | SWKCV 14 Watu wasemao mambo kama haya, wanaonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. |
| BSB 15 If they had been thinking of the country they had left, they would have had opportunity to return. | SWKCV 15 Kwa kweli kama wangekuwa wanafikiri kuhusu nchi waliyoiacha, wangalipata nafasi ya kurudi huko. |
| BSB 16 Instead, they were longing for a better country, a heavenly one. Therefore God is not ashamed to be called their God, for He has prepared a city for them. | SWKCV 16 Lakini badala yake walitamani nchi iliyo bora zaidi, yaani nchi ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa amekwisha kuandaa mji kwa ajili yao. |
| BSB 17 By faith Abraham, when he was tested, offered up Isaac on the altar. He who had received the promises was ready to offer his one and only son, | SWKCV 17 Kwa imani Abrahamu, alipojaribiwa na Mungu, alimtoa Isaki kuwa dhabihu. Yeye aliyekuwa amezipokea ahadi za Mungu alikuwa tayari kumtoa mwanawe, aliyekuwa mwanawe pekee awe dhabihu. |
| BSB 18 even though God had said to him, “Through Isaac your offspring will be reckoned.” | SWKCV 18 Ingawa Mungu alikuwa amemwambia Abrahamu, “Uzao wako utahesabiwa kupitia kwa Isaki,” |
| BSB 19 Abraham reasoned that God could raise the dead, and in a sense, he did receive Isaac back from death. | SWKCV 19 Abrahamu alihesabu kuwa Mungu angaliweza kumfufua Isaki kutoka kwa wafu. Na kwa kusema kwa mfano, alimpata tena Isaki kutoka kwa wafu. |
| BSB 20 By faith Isaac blessed Jacob and Esau concerning the future. | SWKCV 20 Kwa imani Isaki alimbariki Yakobo na Esau kuhusu maisha yao ya baadaye. |
| BSB 21 By faith Jacob, when he was dying, blessed each of Joseph’s sons and worshiped as he leaned on the top of his staff. | SWKCV 21 Kwa imani Yakobo alipokuwa anakufa, alimbariki kila mmoja wa mtoto wa Yosefu, akamwabudu Mungu akiwa ameegemea juu ya kichwa cha fimbo yake. |
| BSB 22 By faith Joseph, when his end was near, spoke about the exodus of the Israelites and gave instructions about his bones. | SWKCV 22 Kwa imani, Yosefu alipokaribia mwisho wa maisha yake, alinena habari za kutoka kwa wana wa Israeli huko Misri na akatoa maagizo kuhusu mifupa yake. |
| BSB 23 By faith Moses’ parents hid him for three months after his birth, because they saw that he was a beautiful child, and they were unafraid of the king’s edict. | SWKCV 23 Kwa imani, wazazi wa Mose walimficha kwa miezi mitatu baada ya kuzaliwa, kwa sababu waliona kuwa si mtoto wa kawaida, wala hawakuiogopa amri ya mfalme. |
| BSB 24 By faith Moses, when he was grown, refused to be called the son of Pharaoh’s daughter. | SWKCV 24 Kwa imani, Mose alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mwana wa binti Farao. |
| BSB 25 He chose to suffer oppression with God’s people rather than to experience the fleeting enjoyment of sin. | SWKCV 25 Akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa anasa za dhambi kwa kitambo kidogo tu. |
| BSB 26 He valued disgrace for Christ above the treasures of Egypt, for he was looking ahead to his reward. | SWKCV 26 Aliona kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni utajiri mkubwa zaidi kuliko hazina za Misri, maana alikuwa anatazamia kupata thawabu baadaye. |
| BSB 27 By faith Moses left Egypt, not fearing the king’s anger; he persevered because he saw Him who is invisible. | SWKCV 27 Kwa imani Mose aliondoka Misri bila kuogopa ghadhabu ya mfalme. Alivumilia kwa sababu alimwona yeye asiyeonekana kwa macho. |
| BSB 28 By faith he kept the Passover and the sprinkling of blood, so that the destroyer of the firstborn would not touch Israel’s own firstborn. | SWKCV 28 Kwa imani akaadhimisha Pasaka na kunyunyiza damu, ili yule mwenye kuwaangamiza wazaliwa wa kwanza asiwaguse wazaliwa wa Israeli. |
| BSB 29 By faith the people passed through the Red Sea as on dry land; but when the Egyptians tried to follow, they were drowned. | SWKCV 29 Kwa imani, watu walivuka Bahari ya Shamu kama vile juu ya nchi kavu; lakini Wamisri walipojaribu kufanya hivyo, walitoswa ndani ya maji. |
| BSB 30 By faith the walls of Jericho fell, after the people had marched around them for seven days. | SWKCV 30 Kwa imani kuta za Yeriko zilianguka, baada ya watu kuzizunguka kwa siku saba. |
| BSB 31 By faith the prostitute Rahab, because she welcomed the spies in peace, did not perish with those who were disobedient. | SWKCV 31 Kwa imani, Rahabu, yule kahaba, hakuangamizwa pamoja na wale waliomwasi Mungu, kwa kuwa aliwakaribisha wale wapelelezi. |
| BSB 32 And what more shall I say? Time will not allow me to tell of Gideon, Barak, Samson, Jephthah, David, Samuel, and the prophets, | SWKCV 32 Basi niseme nini zaidi? Sina wakati wa kusema habari za Gideoni, Baraka, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii, |
| BSB 33 who through faith conquered kingdoms, administered justice, and gained what was promised; who shut the mouths of lions, | SWKCV 33 ambao kwa imani walishinda milki za wafalme, walitekeleza haki, na wakapokea ahadi za Mungu; walifunga vinywa vya simba, |
| BSB 34 quenched the raging fire, and escaped the edge of the sword; who gained strength from weakness, became mighty in battle, and put foreign armies to flight. | SWKCV 34 wakazima makali ya miali ya moto, na wakaepuka kuuawa kwa upanga; udhaifu wao uligeuka kuwa nguvu; pia walikuwa hodari vitani na kuyafukuza majeshi ya wageni. |
| BSB 35 Women received back their dead, raised to life again. Others were tortured and refused their release, so that they might gain a better resurrection. | SWKCV 35 Wanawake walipokea watu wao waliokuwa wamekufa, wakafufuliwa. Lakini wengine waliteswa, nao wakakataa kufunguliwa, ili wapate ufufuo ulio bora zaidi. |
| BSB 36 Still others endured mocking and flogging, and even chains and imprisonment. | SWKCV 36 Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyororo na kutiwa gerezani. |
| BSB 37 They were stoned, they were sawed in two, they were put to death by the sword. They went around in sheepskins and goatskins, destitute, oppressed, and mistreated. | SWKCV 37 Walipigwa kwa mawe; walipasuliwa vipande viwili kwa msumeno; waliuawa kwa upanga. Walizungukazunguka wakiwa wamevaa ngozi za kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, wakiteswa na kutendwa mabaya, |
| BSB 38 The world was not worthy of them. They wandered in deserts and mountains, and hid in caves and holes in the ground. | SWKCV 38 watu ambao ulimwengu haukustahili kuwa nao. Walizunguka majangwani na milimani, katika mapango na katika mahandaki ardhini. |
| BSB 39 These were all commended for their faith, yet they did not receive what was promised. | SWKCV 39 Hawa wote walishuhudiwa vyema kwa sababu ya imani yao, lakini hakuna hata mmoja wao aliyepokea yale yaliyoahidiwa. |
| BSB 40 God had planned something better for us, so that together with us they would be made perfect. | SWKCV 40 Kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea kitu kilicho bora zaidi ili wao wasikamilishwe pasipo sisi. |
Questions about Hebrews 11? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.