Hosea 11
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 When Israel was a child, I loved him, and out of Egypt I called My son. | SWKCV 1 “Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda, nilimwita mwanangu kutoka Misri. |
| BSB 2 But the more I called Israel, the farther they departed from Me. They sacrificed to the Baals and burned incense to carved images. | SWKCV 2 Lakini kadiri nilivyomwita Israeli, ndivyo walivyokwenda mbali nami. Walitoa dhabihu kwa Mabaali na kufukiza uvumba kwa vinyago. |
| BSB 3 It was I who taught Ephraim to walk, taking them by the arms, but they never realized that it was I who healed them. | SWKCV 3 Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea, nikiwashika mikono; lakini hawakutambua kuwa ni mimi niliyewaponya. |
| BSB 4 I led them with cords of kindness, with ropes of love; I lifted the yoke from their necks and bent down to feed them. | SWKCV 4 Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu, kwa vifungo vya upendo; niliondoa nira shingoni mwao nami nikainama kuwalisha. |
| BSB 5 Will they not return to the land of Egypt and be ruled by Assyria because they refused to repent? | SWKCV 5 “Je, hawatarudi Misri, nayo Ashuru haitawatawala kwa sababu wamekataa kutubu? |
| BSB 6 A sword will flash through their cities; it will destroy the bars of their gates and consume them in their own plans. | SWKCV 6 Panga zitametameta katika miji yao, zitaharibu makomeo ya malango yao na kukomesha mipango yao. |
| BSB 7 My people are bent on turning from Me. Though they call to the Most High, He will by no means exalt them. | SWKCV 7 Watu wangu wamedhamiria kuniacha. Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana, kwa vyovyote hatawainua. |
| BSB 8 How could I give you up, O Ephraim? How could I surrender you, O Israel? How could I make you like Admah? How could I treat you like Zeboiim? My heart is turned within Me; My compassion is stirred! | SWKCV 8 “Efraimu, ninawezaje kukuacha? Ee Israeli, ninawezaje kukutoa? Nitawezaje kukutendea kama Adma? Nitawezaje kukufanya kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zote zimeamshwa. |
| BSB 9 I will not execute the full fury of My anger; I will not destroy Ephraim again. For I am God and not man—the Holy One among you—and I will not come in wrath. | SWKCV 9 Sitatimiza hasira yangu kali, wala sitageuka na kumharibu Efraimu. Kwa kuwa mimi ndimi Mungu, wala si mwanadamu, Aliye Mtakatifu miongoni mwenu. Sitakuja kwa ghadhabu. |
| BSB 10 They will walk after the LORD; He will roar like a lion. When He roars, His children will come trembling from the west. | SWKCV 10 Watamfuata Bwana; atanguruma kama simba. Wakati angurumapo, watoto wake watakuja wakitetemeka kutoka magharibi. |
| BSB 11 They will come trembling like birds from Egypt and like doves from the land of Assyria. Then I will settle them in their homes, declares the LORD. | SWKCV 11 Watakuja wakitetemeka kama ndege wakitoka Misri, kama hua wakitoka Ashuru. Nitawakalisha katika nyumba zao,” asema Bwana. |
| BSB 12 Ephraim surrounds Me with lies, the house of Israel with deceit; but Judah still walks with God and is faithful to the Holy One. | SWKCV 12 Efraimu amenizunguka kwa uongo, nyumba ya Israeli kwa udanganyifu. Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu, hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu. |
Questions about Hosea 11? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.