Isaiah 22
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 This is the burden against the Valley of Vision: What ails you now, that you have all gone up to the rooftops, | SWKCV 1 Neno kuhusu Bonde la Maono: Nini kinachokutaabisha sasa, kwamba ninyi nyote mmepanda juu ya mapaa? |
| BSB 2 O city of commotion, O town of revelry? Your slain did not die by the sword, nor were they killed in battle. | SWKCV 2 Ewe mji uliojaa ghasia, ewe mji wa makelele na sherehe! Watu wenu waliokufa hawakuuawa kwa upanga, wala hawakufa vitani. |
| BSB 3 All your rulers have fled together, captured without a bow. All your fugitives were captured together, having fled to a distant place. | SWKCV 3 Viongozi wako wote wamekimbia pamoja, wamekamatwa bila kutumia upinde. Ninyi nyote mliokamatwa mlichukuliwa wafungwa pamoja, mlikimbia wakati adui alipokuwa bado mbali. |
| BSB 4 Therefore I said, “Turn away from me, let me weep bitterly! Do not try to console me over the destruction of the daughter of my people.” | SWKCV 4 Kwa hiyo nilisema, “Geukia mbali nami, niache nilie kwa uchungu. Usijaribu kunifariji juu ya maangamizi ya watu wangu.” |
| BSB 5 For the Lord GOD of Hosts has set a day of tumult and trampling and confusion in the Valley of Vision—of breaking down the walls and crying to the mountains. | SWKCV 5 Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayo siku ya ghasia, ya kukanyaga, na ya kuogofya katika Bonde la Maono, siku ya kuangusha kuta na ya kupiga kelele mpaka milimani. |
| BSB 6 Elam takes up a quiver, with chariots and horsemen, and Kir uncovers the shield. | SWKCV 6 Elamu analichukua podo, pamoja na waendesha magari ya vita na farasi. Kiri anaifungua ngao. |
| BSB 7 Your choicest valleys are full of chariots, and horsemen are posted at the gates. | SWKCV 7 Mabonde yako yaliyo mazuri sana yamejaa magari ya vita, nao wapanda farasi wamewekwa kwenye malango ya mji; |
| BSB 8 He has uncovered the defenses of Judah. On that day you looked to the weapons in the House of the Forest. | SWKCV 8 ulinzi wa Yuda umeondolewa. Nawe ulitazama siku ile silaha katika Jumba la Kifalme la Mwituni, |
| BSB 9 You saw that there were many breaches in the walls of the City of David. You collected water from the lower pool. | SWKCV 9 mkaona kuwa Mji wa Daudi una matundu mengi katika ulinzi wake, mkaweka akiba ya maji kwenye Bwawa la Chini. |
| BSB 10 You counted the houses of Jerusalem and tore them down to strengthen the wall. | SWKCV 10 Mlihesabu majengo katika Yerusalemu nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta. |
| BSB 11 You built a reservoir between the walls for the waters of the ancient pool, but you did not look to the One who made it, or consider Him who planned it long ago. | SWKCV 11 Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani, lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza, au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale. |
| BSB 12 On that day the Lord GOD of Hosts called for weeping and wailing, for shaven heads and the wearing of sackcloth. | SWKCV 12 Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, aliwaita siku ile ili kulia na kuomboleza, kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia. |
| BSB 13 But look, there is joy and gladness, butchering of cattle and slaughtering of sheep, eating of meat and drinking of wine: “Let us eat and drink, for tomorrow we die!” | SWKCV 13 Lakini tazama, kuna furaha na sherehe, kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo, kula nyama na kunywa mvinyo! Mnasema, “Tuleni na kunywa, kwa kuwa kesho tutakufa!” |
| BSB 14 The LORD of Hosts has revealed in my hearing: “Until your dying day, this sin of yours will never be atoned for,” says the Lord GOD of Hosts. | SWKCV 14 Bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.” |
| BSB 15 This is what the Lord GOD of Hosts says: “Go, say to Shebna, the steward in charge of the palace: | SWKCV 15 Hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Nenda ukamwambie huyu wakili Shebna, ambaye ni msimamizi wa jumba la kifalme: |
| BSB 16 What are you doing here, and who authorized you to carve out a tomb for yourself here—to chisel your tomb in the height and cut your resting place in the rock? | SWKCV 16 Unafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa kujikatia kaburi lako mwenyewe, ukichonga kaburi lako mahali palipo juu, na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba? |
| BSB 17 Look, O mighty man! The LORD is about to shake you violently. He will take hold of you, | SWKCV 17 “Jihadhari, Bwana yu karibu kukukamata thabiti, na kukutupa mbali, ewe mtu mwenye nguvu. |
| BSB 18 roll you into a ball, and sling you into a wide land. There you will die, and there your glorious chariots will remain—a disgrace to the house of your master. | SWKCV 18 Atakuvingirisha uwe kama mpira na kukutupa katika nchi kubwa. Huko ndiko utakakofia, na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia, wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako! |
| BSB 19 I will remove you from office, and you will be ousted from your position. | SWKCV 19 Nitakuondoa kutoka kazi yako, nawe utaondoshwa kutoka nafasi yako. |
| BSB 20 On that day I will summon My servant, Eliakim son of Hilkiah. | SWKCV 20 “Katika siku ile, nitamwita mtumishi wangu, Eliakimu mwana wa Hilkia. |
| BSB 21 I will clothe him with your robe and tie your sash around him. I will put your authority in his hand, and he will be a father to the dwellers of Jerusalem and to the house of Judah. | SWKCV 21 Nitamvika joho lako, nami nitamfunga mshipi wako kiunoni mwake, na kumkabidhi mamlaka yako. Yeye atakuwa baba kwa wale wanaoishi Yerusalemu na kwa nyumba ya Yuda. |
| BSB 22 I will place on his shoulder the key to the house of David. What he opens no one can shut, and what he shuts no one can open. | SWKCV 22 Nitaweka mabegani mwake ufunguo wa nyumba ya Daudi. Kile afunguacho hakuna awezaye kufunga, na kile afungacho hakuna awezaye kufungua. |
| BSB 23 I will drive him like a peg into a firm place, and he will be a throne of glory for the house of his father. | SWKCV 23 Nitamgongomea kama kigingi kilicho mahali palipo imara, naye atakuwa kiti cha enzi cha heshima kwa ajili ya nyumba ya baba yake. |
| BSB 24 So they will hang on him all the glory of his father’s house: the descendants and the offshoots—all the lesser vessels, from bowls to every kind of jar. | SWKCV 24 Utukufu wote wa jamaa yake utakuwa juu yake: Watoto wa jamaa hiyo na machipukizi yake, vyombo vyake vyote vidogo, tangu bakuli hadi magudulia yote.” |
| BSB 25 In that day, declares the LORD of Hosts, the peg driven into a firm place will give way; it will be sheared off and fall, and the load upon it will be cut down.” Indeed, the LORD has spoken. | SWKCV 25 Bwana Mwenye Nguvu Zote asema, “Katika siku ile, kigingi kilichogongomewa mahali imara kitaachia njia. Kitakatwa, nacho kitaanguka na mzigo ulioningʼinia juu yake utaanguka chini.” Bwana amesema. |
Questions about Isaiah 22? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.