Jeremiah 30
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 This is the word that came to Jeremiah from the LORD: | SWKCV 1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana: |
| BSB 2 “This is what the LORD, the God of Israel, says: ‘Write in a book all the words that I have spoken to you. | SWKCV 2 “Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Israeli: ‘Andika katika kitabu maneno yote niliyonena na wewe. |
| BSB 3 For behold, the days are coming, declares the LORD, when I will restore from captivity My people Israel and Judah, declares the LORD. I will restore them to the land that I gave to their fathers, and they will possess it.’” | SWKCV 3 Siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘nitakapowaleta watu wangu Israeli na Yuda kutoka uhamishoni, na kuwarudisha katika nchi niliyowapa baba zao ili kuimiliki,’ asema Bwana.” |
| BSB 4 These are the words that the LORD spoke concerning Israel and Judah. | SWKCV 4 Haya ndiyo maneno Bwana aliyoyanena kuhusu Israeli na Yuda: |
| BSB 5 Yes, this is what the LORD says: “A cry of panic is heard—a cry of terror, not of peace. | SWKCV 5 “Hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Vilio vya woga vinasikika: hofu kuu, wala si amani. |
| BSB 6 Ask now, and see: Can a male give birth? Why then do I see every man with his hands on his stomach like a woman in labor and every face turned pale? | SWKCV 6 Ulizeni na mkaone: Je, mwanaume aweza kuzaa watoto? Kwa nini basi ninaona kila mwanaume mwenye nguvu ameweka mikono yake tumboni kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa, kila uso ukigeuka rangi kabisa? |
| BSB 7 How awful that day will be! None will be like it! It is the time of Jacob’s distress, but he will be saved out of it. | SWKCV 7 Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha! Hakutakuwa na nyingine mfano wake. Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo, lakini ataokolewa kutoka hiyo. |
| BSB 8 On that day, declares the LORD of Hosts, I will break the yoke off their necks and tear off their bonds, and no longer will strangers enslave them. | SWKCV 8 “ ‘Katika siku ile,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nitaivunja nira kutoka shingoni mwao na kuvipasua vifungo vyao; wageni hawatawafanya tena watumwa. |
| BSB 9 Instead, they will serve the LORD their God and David their king, whom I will raise up for them. | SWKCV 9 Badala yake, watamtumikia Bwana, Mungu wao na Daudi mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao. |
| BSB 10 As for you, O Jacob My servant, do not be afraid, declares the LORD, and do not be dismayed, O Israel. For I will surely save you out of a distant place, your descendants from the land of their captivity! Jacob will return to quiet and ease, with no one to make him afraid. | SWKCV 10 “ ‘Hivyo usiogope, ee Yakobo mtumishi wangu, usifadhaike, ee Israeli,’ asema Bwana. ‘Hakika, nitakuokoa kutoka mbali, wazao wako kutoka nchi ya uhamisho wao. Yakobo atakuwa tena na amani na usalama, wala hakuna atakayemtia hofu. |
| BSB 11 For I am with you to save you, declares the LORD. Though I will completely destroy all the nations to which I have scattered you, I will not completely destroy you. Yet I will discipline you justly, and will by no means leave you unpunished.” | SWKCV 11 Mimi niko pamoja nawe, nami nitakuokoa,’ asema Bwana. ‘Ingawa nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambamo miongoni mwao nimewatawanya, sitawaangamiza ninyi kabisa. Nitawaadhibu, lakini kwa haki. Sitawaacha kabisa bila adhabu.’ |
| BSB 12 For this is what the LORD says: “Your injury is incurable; your wound is grievous. | SWKCV 12 “Hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Kidonda chako hakina dawa, jeraha lako haliponyeki. |
| BSB 13 There is no one to plead your cause, no remedy for your sores, no recovery for you. | SWKCV 13 Hakuna yeyote wa kukutetea shauri lako, hakuna dawa ya kidonda chako, wewe hutapona. |
| BSB 14 All your lovers have forgotten you; they no longer seek you, for I have struck you as an enemy would, with the discipline of someone cruel, because of your great iniquity and your numerous sins. | SWKCV 14 Wale walioungana nawe wote wamekusahau, hawajali chochote kukuhusu wewe. Nimekupiga kama vile adui angelifanya, na kukuadhibu kama vile mtu mkatili angelifanya, kwa sababu hatia yako ni kubwa mno na dhambi zako ni nyingi sana. |
| BSB 15 Why do you cry out over your wound? Your pain has no cure! Because of your great iniquity and your numerous sins I have done these things to you. | SWKCV 15 Kwa nini unalia kwa ajili ya jeraha lako, yale maumivu yako yasiyoponyeka? Kwa sababu ya uovu wako mkubwa na dhambi zako nyingi nimekufanyia mambo haya. |
| BSB 16 Nevertheless, all who devour you will be devoured, and all your adversaries—every one of them—will go off into exile. Those who plundered you will be plundered, and all who raided you will be raided. | SWKCV 16 “ ‘Lakini watu wote wakuangamizao wataangamizwa; adui zako wote watakwenda uhamishoni. Wale wote wakutekao nyara watatekwa nyara; wote wakufanyao mateka nitawafanya mateka. |
| BSB 17 But I will restore your health and heal your wounds, declares the LORD, because they call you an outcast, Zion, for whom no one cares.” | SWKCV 17 Lakini nitakurudishia afya yako na kuyaponya majeraha yako,’ asema Bwana, ‘kwa sababu umeitwa mwenye kutupwa, Sayuni ambaye hakuna yeyote anayekujali.’ |
| BSB 18 This is what the LORD says: “I will restore the fortunes of Jacob’s tents and have compassion on his dwellings. And the city will be rebuilt on her own ruins, and the palace will stand in its rightful place. | SWKCV 18 “Hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo, na kuhurumia maskani yake. Mji utajengwa tena juu ya magofu yake, nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi. |
| BSB 19 Thanksgiving will proceed from them, a sound of celebration. I will multiply them, and they will not be decreased; I will honor them, and they will not be belittled. | SWKCV 19 Nyimbo za kushukuru zitatoka kwao na sauti ya furaha. Nitaiongeza idadi yao wala hawatapungua, nitawapa heshima na hawatadharauliwa. |
| BSB 20 Their children will be as in days of old, and their congregation will be established before Me; and I will punish all their oppressors. | SWKCV 20 Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa siku za zamani, nayo jumuiya yao itaimarishwa mbele yangu; nitawaadhibu wale wote wawaoneao. |
| BSB 21 Their leader will be one of their own, and their ruler will arise from their midst. And I will bring him near, and he will approach Me, for who would dare on his own to approach Me?” declares the LORD. | SWKCV 21 Mmoja wao atakuwa kiongozi wao; mtawala wao atainuka miongoni mwao. Nitamleta karibu nami, naye atanikaribia mimi, kwa maana ni nani yule atakayejitolea kuwa karibu nami?’ asema Bwana. |
| BSB 22 “And you will be My people, and I will be your God.” | SWKCV 22 ‘Kwa hiyo ninyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.’” |
| BSB 23 Behold, the storm of the LORD has gone out with fury, a whirlwind swirling down upon the heads of the wicked. | SWKCV 23 Tazama, tufani ya Bwana italipuka kwa ghadhabu, upepo wa kisulisuli uendao kasi utashuka juu ya vichwa vya waovu. |
| BSB 24 The fierce anger of the LORD will not turn back until He has fully accomplished the purposes of His heart. In the days to come you will understand this. | SWKCV 24 Hasira kali ya Bwana haitarudi nyuma mpaka atakapotimiza makusudi yote ya moyo wake. Siku zijazo mtayaelewa haya. |
Questions about Jeremiah 30? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.