Jeremiah 48
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Concerning Moab, this is what the LORD of Hosts, the God of Israel, says: “Woe to Nebo, for it will be devastated. Kiriathaim will be captured and disgraced; the fortress will be shattered and dismantled. | SWKCV 1 Kuhusu Moabu: Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Ole wake Nebo, kwa maana utaharibiwa. Kiriathaimu utaaibishwa na kutekwa; Misgabu itaaibishwa na kuvunjavunjwa. |
| BSB 2 There is no longer praise for Moab; in Heshbon they devise evil against her: ‘Come, let us cut her off from nationhood.’ You too, O people of Madmen, will be silenced; the sword will pursue you. | SWKCV 2 Moabu haitasifiwa tena; huko Heshboni watu watafanya shauri baya la anguko lake: ‘Njooni na tuangamize taifa lile.’ Wewe nawe, ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia. |
| BSB 3 A voice cries out from Horonaim: ‘Devastation and great destruction!’ | SWKCV 3 Sikiliza kilio kutoka Horonaimu, kilio cha maangamizi makuu na uharibifu. |
| BSB 4 Moab will be shattered; her little ones will cry out. | SWKCV 4 Moabu utavunjwa, wadogo wake watapiga kelele. |
| BSB 5 For on the ascent to Luhith they weep bitterly as they go, and on the descent to Horonaim cries of distress resound over the destruction: | SWKCV 5 Wanapanda kwenda njia ya kuelekea Luhithi, wakilia kwa uchungu wanapotembea, kwenye njia inayoshuka kwenda Horonaimu, kilio cha uchungu kwa ajili ya uharibifu kinasikika. |
| BSB 6 ‘Flee! Run for your lives! Become like a juniper in the desert.’ | SWKCV 6 Kimbieni! Okoeni maisha yenu, kuweni kama kichaka jangwani. |
| BSB 7 Because you trust in your works and treasures, you too will be captured, and Chemosh will go into exile with his priests and officials. | SWKCV 7 Kwa kuwa mmetumainia matendo yenu na mali zenu, ninyi pia mtachukuliwa mateka, naye Kemoshi atakwenda uhamishoni, pamoja na makuhani wake na maafisa wake. |
| BSB 8 The destroyer will move against every city, and not one town will escape. The valley will also be ruined, and the high plain will be destroyed, as the LORD has said. | SWKCV 8 Mharabu atakuja dhidi ya kila mji, wala hakuna mji utakaookoka. Bonde litaangamizwa na uwanda utaharibiwa, kwa sababu Bwana amesema. |
| BSB 9 Put salt on Moab, for she will be laid waste; her cities will become desolate, with no one to dwell in them. | SWKCV 9 Wekeni chumvi kwa ajili ya Moabu, kwa kuwa ataangamizwa; miji yake itakuwa ukiwa, pasipo kuwa na mtu atakayeishi ndani yake. |
| BSB 10 Cursed is the one who is remiss in doing the work of the LORD, and cursed is he who withholds his sword from bloodshed. | SWKCV 10 “Alaaniwe yeye afanyaye kazi ya Bwana kwa hila! Alaaniwe yeye auzuiaye upanga wake usimwage damu! |
| BSB 11 Moab has been at ease from youth, settled like wine on its dregs; he has not been poured from vessel to vessel or gone into exile. So his flavor has remained the same, and his aroma is unchanged. | SWKCV 11 “Moabu amestarehe tangu ujana wake, kama divai iliyoachwa kwenye machujo yake, haikumiminwa kutoka chombo kimoja hadi kingine, hajaenda uhamishoni. Kwa hiyo ana ladha ile ile kama aliyokuwa nayo, nayo harufu yake haijabadilika. |
| BSB 12 Therefore behold, the days are coming, declares the LORD, when I will send to him wanderers, who will pour him out. They will empty his vessels and shatter his jars. | SWKCV 12 Lakini siku zinakuja,” asema Bwana, “nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia, nao watamimina; wataacha magudulia yake yakiwa matupu na kuvunja mitungi yake. |
| BSB 13 Then Moab will be ashamed of Chemosh, just as the house of Israel was ashamed when they trusted in Bethel. | SWKCV 13 Kisha Moabu atamwonea aibu mungu wao Kemoshi, kama vile nyumba ya Israeli walivyoona aibu walipotegemea mungu wa Betheli. |
| BSB 14 How can you say, ‘We are warriors, mighty men ready for battle’? | SWKCV 14 “Mwawezaje kusema, ‘Sisi ni mashujaa, watu jasiri katika vita’? |
| BSB 15 Moab has been destroyed and its towns have been invaded; the best of its young men have gone down in the slaughter, declares the King, whose name is the LORD of Hosts. | SWKCV 15 Moabu ataangamizwa na miji yake itavamiwa, vijana wake waume walio bora sana watachinjwa,” asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote. |
| BSB 16 Moab’s calamity is at hand, and his affliction is rushing swiftly. | SWKCV 16 “Kuanguka kwa Moabu kumekaribia, janga kubwa litamjia kwa haraka. |
| BSB 17 Mourn for him, all you who surround him, everyone who knows his name; tell how the mighty scepter is shattered—the glorious staff! | SWKCV 17 Ombolezeni kwa ajili yake, ninyi nyote mnaomzunguka, ninyi nyote mnaojua sifa zake, semeni, ‘Tazama jinsi ilivyovunjika fimbo ya kifalme yenye nguvu, tazama jinsi ilivyovunjika fimbo iliyotukuka!’ |
| BSB 18 Come down from your glory; sit on parched ground, O daughter dwelling in Dibon, for the destroyer of Moab has come against you; he has destroyed your fortresses. | SWKCV 18 “Shuka kutoka fahari yako na uketi katika ardhi iliyokauka, enyi wenyeji wa Binti wa Diboni, kwa maana yeye aangamizaye Moabu atakuja dhidi yako, na kuangamiza miji yako iliyozungushiwa maboma. |
| BSB 19 Stand by the road and watch, O dweller of Aroer! Ask the man fleeing or the woman escaping, ‘What has happened?’ | SWKCV 19 Simama kando ya barabara na utazame, wewe unayeishi Aroeri. Muulize mwanaume anayekimbia na mwanamke anayetoroka, waulize, ‘Kumetokea nini?’ |
| BSB 20 Moab is put to shame, for it has been shattered. Wail and cry out! Declare by the Arnon that Moab is destroyed. | SWKCV 20 Moabu amefedheheshwa, kwa kuwa amevunjavunjwa. Lieni kwa huzuni na kupiga kelele! Tangazeni kando ya Arnoni kwamba Moabu ameangamizwa. |
| BSB 21 Judgment has come upon the high plain—upon Holon, Jahzah, and Mephaath, | SWKCV 21 Hukumu imefika kwenye uwanda wa juu: katika Holoni, Yahasa na Mefaathi, |
| BSB 22 upon Dibon, Nebo, and Beth-diblathaim, | SWKCV 22 katika Diboni, Nebo na Beth-Diblathaimu, |
| BSB 23 upon Kiriathaim, Beth-gamul, and Beth-meon, | SWKCV 23 katika Kiriathaimu, Beth-Gamuli na Beth-Meoni, |
| BSB 24 upon Kerioth, Bozrah, and all the towns of Moab, those far and near. | SWKCV 24 katika Keriothi na Bosra; kwa miji yote ya Moabu, iliyoko mbali na karibu. |
| BSB 25 The horn of Moab has been cut off, and his arm is broken,” declares the LORD. | SWKCV 25 Pembe ya Moabu imekatwa, mkono wake umevunjwa,” asema Bwana. |
| BSB 26 “Make him drunk, because he has magnified himself against the LORD; so Moab will wallow in his own vomit, and he will also become a laughingstock. | SWKCV 26 “Mlevye, kwa kuwa amemdharau Bwana. Moabu na agaegae katika matapishi yake, yeye na awe kitu cha dhihaka. |
| BSB 27 Was not Israel your object of ridicule? Was he ever found among thieves? For whenever you speak of him you shake your head. | SWKCV 27 Je, Israeli hakuwa kitu chako cha kudhihakiwa? Je, alikamatwa miongoni mwa wezi, kiasi cha kutikisa kichwa chako kwa dharau kila mara unapozungumza juu yake? |
| BSB 28 Abandon the towns and settle among the rocks, O dwellers of Moab! Be like a dove that nests at the mouth of a cave. | SWKCV 28 Ondokeni kwenye miji yenu, mkaishi katikati ya miamba, enyi mnaoishi Moabu. Kuweni kama huwa ambaye hutengeneza kiota chake kwenye mdomo wa pango. |
| BSB 29 We have heard of Moab’s pomposity, his exceeding pride and conceit, his proud arrogance and haughtiness of heart. | SWKCV 29 “Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu: kutakabari kwake kwa kiburi na majivuno, kiburi chake na ufidhuli wake, na kujivuna kwa moyo wake. |
| BSB 30 I know his insolence,” declares the LORD, “but it is futile. His boasting is as empty as his deeds. | SWKCV 30 Ninaujua ujeuri wake, lakini ni bure,” asema Bwana, “nako kujisifu kwake hakumsaidii chochote. |
| BSB 31 Therefore I will wail for Moab; I will cry out for all of Moab; I will moan for the men of Kir-heres. | SWKCV 31 Kwa hiyo namlilia Moabu, kwa ajili ya Moabu yote ninalia, ninaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. |
| BSB 32 I will weep for you, O vine of Sibmah, more than I weep for Jazer. Your tendrils have extended to the sea; they reach even to Jazer. The destroyer has descended on your summer fruit and grape harvest. | SWKCV 32 Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, enyi mizabibu ya Sibma. Matawi yako yameenea hadi baharini; yamefika hadi bahari ya Yazeri. Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva na mizabibu yako iliyoiva. |
| BSB 33 Joy and gladness are removed from the orchard and from the fields of Moab. I have stopped the flow of wine from the presses; no one treads them with shouts of joy; their shouts are not for joy. | SWKCV 33 Shangwe na furaha vimetoweka kutoka bustani na mashamba ya Moabu. Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo; hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe. Ingawa kuna kelele, sio kelele za shangwe. |
| BSB 34 There is a cry from Heshbon to Elealeh; they raise their voices to Jahaz, from Zoar to Horonaim and Eglath-shelishiyah; for even the waters of Nimrim have dried up. | SWKCV 34 “Sauti ya kilio chao inapanda kutoka Heshboni hadi Eleale na Yahazi, kutoka Soari hadi Horonaimu na Eglath-Shelishiya, kwa kuwa hata maji ya Nimrimu yamekauka. |
| BSB 35 In Moab, declares the LORD, I will bring an end to those who make offerings on the high places and burn incense to their gods. | SWKCV 35 Nitakomesha wale wote katika Moabu watoao sadaka mahali pa juu, na kufukiza uvumba kwa miungu yao,” asema Bwana. |
| BSB 36 Therefore My heart laments like a flute for Moab; it laments like a flute for the men of Kir-heres, because the wealth they acquired has perished. | SWKCV 36 “Kwa hiyo moyo wangu unaomboleza kwa ajili ya Moabu kama filimbi; unaomboleza kama filimbi kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. Utajiri waliojipatia umetoweka. |
| BSB 37 For every head is shaved and every beard is clipped; on every hand is a gash, and around every waist is sackcloth. | SWKCV 37 Kila kichwa kimenyolewa na kila mwenye ndevu zimekatwa; kila mkono umekatwa na kila kiuno kimefunikwa kwa nguo ya gunia. |
| BSB 38 On all the rooftops of Moab and in the public squares, everyone is mourning; for I have shattered Moab like an unwanted jar,” declares the LORD. | SWKCV 38 Juu ya mapaa yote katika Moabu na katika viwanja hakuna kitu chochote isipokuwa maombolezo, kwa kuwa nimemvunja Moabu kama gudulia ambalo hakuna mtu yeyote anayelitaka,” asema Bwana. |
| BSB 39 “How shattered it is! How they wail! How Moab has turned his back in shame! Moab has become an object of ridicule and horror to all those around him.” | SWKCV 39 “Tazama jinsi alivyovunjikavunjika! Jinsi wanavyolia kwa huzuni! Tazama jinsi Moabu anavyogeuka kwa aibu! Moabu amekuwa kitu cha kudhihakiwa, kitu cha kutisha kwa wale wote wanaomzunguka.” |
| BSB 40 For this is what the LORD says: “Behold, an eagle swoops down and spreads his wings against Moab. | SWKCV 40 Hili ndilo asemalo Bwana: “Tazama! Tai anashuka chini, akitanda mabawa yake juu ya Moabu. |
| BSB 41 Kirioth has been taken, and the strongholds seized. In that day the heart of Moab’s warriors will be like the heart of a woman in labor. | SWKCV 41 Miji itatekwa na ngome zake zitatwaliwa. Katika siku hiyo, mioyo ya mashujaa wa Moabu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika utungu wa kuzaa. |
| BSB 42 Moab will be destroyed as a nation because he vaunted himself against the LORD. | SWKCV 42 Moabu ataangamizwa kama taifa kwa sababu amemdharau Bwana. |
| BSB 43 Terror and pit and snare await you, O dweller of Moab,” declares the LORD. | SWKCV 43 Hofu kuu, shimo na mtego vinawangojea, enyi watu wa Moabu,” asema Bwana. |
| BSB 44 “Whoever flees the panic will fall into the pit, and whoever climbs from the pit will be caught in the snare. For I will bring upon Moab the year of their punishment,” declares the LORD. | SWKCV 44 “Yeyote atakayeikimbia hiyo hofu kuu ataanguka ndani ya shimo, yeyote atakayepanda kutoka shimoni, atanaswa katika mtego, kwa sababu nitaletea Moabu mwaka wa adhabu yake,” asema Bwana. |
| BSB 45 “Those who flee will stand helpless in Heshbon’s shadow, because fire has gone forth from Heshbon and a flame from within Sihon. It devours the foreheads of Moab and the skulls of the sons of tumult. | SWKCV 45 “Katika kivuli cha Heshboni, wakimbizi wamesimama pasipo msaada, kwa kuwa moto umezimika huko Heshboni, mwali wa moto kutoka katikati ya Sihoni; unaunguza vipaji vya nyuso za Moabu, mafuvu yao wenye kujivuna kwa kelele. |
| BSB 46 Woe to you, O Moab! The people of Chemosh have perished; for your sons have been taken into exile and your daughters have gone into captivity. | SWKCV 46 Ole wako, ee Moabu! Watu wa Kemoshi wameangamizwa; wana wako wamepelekwa uhamishoni na binti zako wamechukuliwa mateka. |
| BSB 47 Yet in the latter days I will restore Moab from captivity,” declares the LORD. Here ends the judgment on Moab. | SWKCV 47 “Lakini nitarudisha mateka wa Moabu, katika siku zijazo,” asema Bwana. Huu ndio mwisho wa hukumu juu ya Moabu. |
Questions about Jeremiah 48? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.