John 13
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 It was now just before the Passover Feast, and Jesus knew that His hour had come to leave this world and return to the Father. Having loved His own who were in the world, He loved them to the very end. | SWKCV 1 Ilikuwa mara tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka. Yesu alijua ya kuwa wakati wake wa kuondoka ulimwenguni ili kurudi kwa Baba umewadia. Alikuwa amewapenda watu wake waliokuwa ulimwenguni, naam, aliwapenda hadi kipimo cha mwisho. |
| BSB 2 The evening meal was underway, and the devil had already put into the heart of Judas, the son of Simon Iscariot, to betray Jesus. | SWKCV 2 Wakati alipokuwa akila chakula cha jioni na wanafunzi wake, ibilisi alikuwa amekwisha kutia ndani ya moyo wa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni, wazo la kumsaliti Yesu. |
| BSB 3 Jesus knew that the Father had delivered all things into His hands, and that He had come from God and was returning to God. | SWKCV 3 Yesu akijua ya kwamba Baba ameweka vitu vyote chini ya mamlaka yake na kwamba yeye alitoka kwa Mungu na alikuwa anarudi kwa Mungu, |
| BSB 4 So He got up from the supper, laid aside His outer garments, and wrapped a towel around His waist. | SWKCV 4 hivyo aliondoka chakulani, akavua vazi lake la nje, akajifunga kitambaa kiunoni. |
| BSB 5 After that, He poured water into a basin and began to wash the disciples’ feet and dry them with the towel that was around Him. | SWKCV 5 Kisha akamimina maji kwenye sinia na kuanza kuwanawisha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa kile kitambaa alichokuwa amejifunga kiunoni. |
| BSB 6 He came to Simon Peter, who asked Him, “Lord, are You going to wash my feet?” | SWKCV 6 Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, je, wewe utaninawisha mimi miguu?” |
| BSB 7 Jesus replied, “You do not realize now what I am doing, but later you will understand.” | SWKCV 7 Yesu akamjibu, “Hivi sasa hutambui lile ninalofanya, lakini baadaye utaelewa.” |
| BSB 8 “Never shall You wash my feet!” Peter told Him. Jesus answered, “Unless I wash you, you have no part with Me.” | SWKCV 8 Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.” Yesu akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.” |
| BSB 9 “Then, Lord,” Simon Peter replied, “not only my feet, but my hands and my head as well!” | SWKCV 9 Ndipo Simoni Petro akajibu, “Usininawishe miguu peke yake, Bwana, bali pamoja na mikono na kichwa pia!” |
| BSB 10 Jesus told him, “Whoever has already bathed needs only to wash his feet, and he will be completely clean. And you are clean, though not all of you.” | SWKCV 10 Yesu akamjibu, “Mtu aliyekwisha kuoga anahitaji kunawa miguu tu, kwani mwili wake wote ni safi. Ninyi ni safi, ingawa si kila mmoja wenu.” |
| BSB 11 For He knew who would betray Him. That is why He said, “Not all of you are clean.” | SWKCV 11 Kwa kuwa yeye alijua ni nani ambaye angemsaliti, ndiyo sababu akasema si kila mmoja aliyekuwa safi. |
| BSB 12 When Jesus had washed their feet and put on His outer garments, He reclined with them again and asked, “Do you know what I have done for you? | SWKCV 12 Alipomaliza kuwanawisha miguu yao, alivaa tena mavazi yake, akarudi alikokuwa ameketi, akawauliza, “Je, mmeelewa nililowafanyia? |
| BSB 13 You call Me Teacher and Lord, and rightly so, because I am. | SWKCV 13 Ninyi mnaniita mimi ‘Mwalimu’ na ‘Bwana,’ hii ni sawa, maana ndivyo nilivyo. |
| BSB 14 So if I, your Lord and Teacher, have washed your feet, you also should wash one another’s feet. | SWKCV 14 Kwa hiyo, ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu, pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi. |
| BSB 15 I have set you an example so that you should do as I have done for you. | SWKCV 15 Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi. |
| BSB 16 Truly, truly, I tell you, no servant is greater than his master, nor is a messenger greater than the one who sent him. | SWKCV 16 Amin, amin nawaambia, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala aliyetumwa si mkuu kuliko yule aliyemtuma. |
| BSB 17 If you know these things, you will be blessed if you do them. | SWKCV 17 Sasa kwa kuwa mmejua mambo haya, heri yenu ninyi kama mkiyatenda. |
| BSB 18 I am not speaking about all of you; I know whom I have chosen. But this is to fulfill the Scripture: ‘The one who shares My bread has lifted up his heel against Me.’ | SWKCV 18 “Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni ili Andiko lipate kutimia, kwamba, ‘Yeye aliyekula chakula changu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.’ |
| BSB 19 I am telling you now before it happens, so that when it comes to pass, you will believe that I am He. | SWKCV 19 “Ninawaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa Mimi ndiye. |
| BSB 20 Truly, truly, I tell you, whoever receives the one I send receives Me, and whoever receives Me receives the One who sent Me.” | SWKCV 20 Amin, amin nawaambia, yeyote anayempokea yule niliyemtuma anipokea mimi, naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenituma mimi.” |
| BSB 21 After Jesus had said this, He became troubled in spirit and testified, “Truly, truly, I tell you, one of you will betray Me.” | SWKCV 21 Baada ya kusema haya, Yesu alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.” |
| BSB 22 The disciples looked at one another, perplexed as to which of them He meant. | SWKCV 22 Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. |
| BSB 23 One of His disciples, the one whom Jesus loved, was reclining at His side. | SWKCV 23 Mmoja wa wanafunzi wake ambaye Yesu alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Yesu. |
| BSB 24 So Simon Peter motioned to him to ask Jesus which one He was talking about. | SWKCV 24 Simoni Petro akampungia mkono yule mwanafunzi, akamwambia, “Muulize anamaanisha nani.” |
| BSB 25 Leaning back against Jesus, he asked, “Lord, who is it?” | SWKCV 25 Yule mwanafunzi akamwegemea Yesu, akamuuliza, “Bwana, tuambie, ni nani?” |
| BSB 26 Jesus answered, “It is the one to whom I give this morsel after I have dipped it.” Then He dipped the morsel and gave it to Judas son of Simon Iscariot. | SWKCV 26 Yesu akajibu, “Ni yule nitakayempa hiki kipande cha mkate baada ya kukichovya kwenye bakuli.” Hivyo baada ya kukichovya kile kipande cha mkate, akampa Yuda Iskariote, mwana wa Simoni. |
| BSB 27 And when Judas had taken the morsel, Satan entered into him. Then Jesus said to Judas, “What you are about to do, do quickly.” | SWKCV 27 Mara tu baada ya kukipokea kile kipande cha mkate, Shetani akamwingia. Yesu akamwambia Yuda, “Lile unalotaka kulitenda litende haraka.” |
| BSB 28 But no one at the table knew why Jesus had said this to him. | SWKCV 28 Hakuna hata mmoja wa wale waliokuwa wameketi naye mezani aliyeelewa kwa nini Yesu alimwambia hivyo. |
| BSB 29 Since Judas kept the money bag, some thought that Jesus was telling him to buy what was needed for the feast, or to give something to the poor. | SWKCV 29 Kwa kuwa Yuda alikuwa mtunza fedha, wengine walifikiri Yesu alikuwa amemwambia akanunue vitu vilivyohitajika kwa ajili ya Sikukuu, au kuwapa maskini chochote. |
| BSB 30 As soon as he had received the morsel, Judas went out into the night. | SWKCV 30 Mara tu baada ya kupokea ule mkate, Yuda akatoka nje. Wakati huo ulikuwa ni usiku. |
| BSB 31 When Judas had gone out, Jesus said, “Now the Son of Man is glorified, and God is glorified in Him. | SWKCV 31 Baada ya Yuda kutoka nje, Yesu akasema, “Sasa Mwana wa Adamu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. |
| BSB 32 If God is glorified in Him, God will also glorify the Son in Himself—and will glorify Him at once. | SWKCV 32 Ikiwa Mungu ametukuzwa ndani ya Mwana, Mungu atamtukuza Mwana ndani yake mwenyewe naye atamtukuza mara. |
| BSB 33 Little children, I am with you only a little while longer. You will look for Me, and as I said to the Jews, so now I say to you: ‘Where I am going, you cannot come.’ | SWKCV 33 “Watoto wangu, mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama vile nilivyowaambia Wayahudi, vivyo hivyo sasa nawaambia na ninyi. Niendako, ninyi hamwezi kuja. |
| BSB 34 A new commandment I give you: Love one another. As I have loved you, so you also must love one another. | SWKCV 34 “Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. |
| BSB 35 By this everyone will know that you are My disciples, if you love one another.” | SWKCV 35 Kama mkipendana ninyi kwa ninyi, kwa njia hii, watu wote watajua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu.” |
| BSB 36 “Lord, where are You going?” Simon Peter asked. Jesus answered, “Where I am going, you cannot follow Me now, but you will follow later.” | SWKCV 36 Simoni Petro akamuuliza, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akamjibu, “Ninakokwenda huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.” |
| BSB 37 “Lord,” said Peter, “why can’t I follow You now? I will lay down my life for You.” | SWKCV 37 Petro akamuuliza tena, “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Mimi niko tayari kuutoa uhai wangu kwa ajili yako.” |
| BSB 38 “Will you lay down your life for Me?” Jesus replied. “Truly, truly, I tell you, before the rooster crows, you will deny Me three times. | SWKCV 38 Yesu akamjibu, “Je, ni kweli uko tayari kuutoa uhai wako kwa ajili yangu? Amin, amin nakuambia, kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.” |
Questions about John 13? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.