Luke 8
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Soon afterward, Jesus traveled from one town and village to another, preaching and proclaiming the good news of the kingdom of God. The Twelve were with Him, | SWKCV 1 Baada ya haya Yesu alikwenda, akawa anazunguka katika miji na vijiji akihubiri habari njema za Ufalme wa Mungu. Wale wanafunzi wake kumi na wawili walikuwa pamoja naye, |
| BSB 2 as well as some women who had been healed of evil spirits and infirmities: Mary called Magdalene, from whom seven demons had gone out, | SWKCV 2 pia baadhi ya wanawake waliokuwa wametolewa pepo wachafu na kuponywa magonjwa. Miongoni mwao alikuwepo Maria Magdalene, aliyetolewa pepo wachafu saba; |
| BSB 3 Joanna the wife of Herod’s household manager Chuza, Susanna, and many others. These women were ministering to them out of their own means. | SWKCV 3 Yoana mkewe Kuza, msimamizi wa nyumba ya watu wa nyumbani mwa Herode; Susana; na wengine wengi waliokuwa wakimhudumia kwa mali zao. |
| BSB 4 While a large crowd was gathering and people were coming to Jesus from town after town, He told them this parable: | SWKCV 4 Umati mkubwa wa watu ulipokuwa ukija kwa Yesu kutoka kila mji, akawaambia mfano huu: |
| BSB 5 “A farmer went out to sow his seed. And as he was sowing, some seed fell along the path, where it was trampled, and the birds of the air devoured it. | SWKCV 5 “Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia; zikakanyagwa, nao ndege wa angani wakazila. |
| BSB 6 Some fell on rocky ground, and when it came up, the seedlings withered because they had no moisture. | SWKCV 6 Mbegu nyingine zilianguka penye miamba, nazo zilipoota, hiyo mimea ikakauka kwa kukosa unyevu. |
| BSB 7 Other seed fell among thorns, which grew up with it and choked the seedlings. | SWKCV 7 Nazo mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo ile miiba ikakua pamoja nazo, na kuisonga hiyo mimea. |
| BSB 8 Still other seed fell on good soil, where it sprang up and produced a crop—a hundredfold.” As Jesus said this, He called out, “He who has ears to hear, let him hear.” | SWKCV 8 Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri. Zikaota na kuzaa mara mia moja zaidi ya mbegu alizopanda.” Baada ya kusema haya, Yesu akapaza sauti, akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.” |
| BSB 9 Then His disciples asked Him what this parable meant. | SWKCV 9 Wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo. |
| BSB 10 He replied, “The knowledge of the mysteries of the kingdom of God has been given to you, but to others I speak in parables, so that, ‘though seeing, they may not see; though hearing, they may not understand.’ | SWKCV 10 Naye akasema, “Ninyi mmepewa kufahamu siri za Ufalme wa Mungu, lakini kwa wengine nazungumza kwa mifano, ili, “ ‘ingawa wanatazama, wasione; ingawa wanasikiliza, wasielewe.’ |
| BSB 11 Now this is the meaning of the parable: The seed is the word of God. | SWKCV 11 “Maana ya mfano huu ni hii: Mbegu ni neno la Mungu. |
| BSB 12 The seeds along the path are those who hear, but the devil comes and takes away the word from their hearts, so that they may not believe and be saved. | SWKCV 12 Zile zilizoanguka kando ya njia ni wale ambao husikia neno, naye ibilisi anakuja na kuliondoa neno kutoka mioyoni mwao, ili wasije wakaamini na kuokoka. |
| BSB 13 The seeds on rocky ground are those who hear the word and receive it with joy, but they have no root. They believe for a season, but in the time of testing, they fall away. | SWKCV 13 Zile mbegu zilizoanguka kwenye mwamba ni wale ambao hulipokea neno kwa furaha wanapolisikia, lakini hawana mizizi. Wanaamini kwa muda mfupi, lakini wakati wa kujaribiwa huiacha imani. |
| BSB 14 The seeds that fell among the thorns are those who hear, but as they go on their way, they are choked by the worries, riches, and pleasures of this life, and their fruit does not mature. | SWKCV 14 Zile mbegu zilizoanguka kwenye miiba ni mfano wa wale wanaosikia, lakini wanapoendelea husongwa na masumbufu ya maisha haya, utajiri na anasa, nao hawakui. |
| BSB 15 But the seeds on good soil are those with a noble and good heart, who hear the word, cling to it, and by persevering produce a crop. | SWKCV 15 Lakini zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo mzuri ni mfano wa wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mnyofu wa utiifu, nao kwa kuvumilia kwingi huzaa matunda. |
| BSB 16 No one lights a lamp and covers it with a jar or puts it under a bed. Instead, he sets it on a stand, so those who enter can see the light. | SWKCV 16 “Hakuna mtu awashaye taa na kuificha ndani ya gudulia au kuiweka mvunguni mwa kitanda. Badala yake, huiweka juu ya kinara, ili wale waingiao ndani waone mwanga. |
| BSB 17 For there is nothing hidden that will not be disclosed, and nothing concealed that will not be made known and brought to light. | SWKCV 17 Kwa maana hakuna jambo lolote lililofichika ambalo halitafichuliwa, wala lolote lililositirika ambalo halitajulikana na kuwekwa wazi. |
| BSB 18 Pay attention, therefore, to how you listen. Whoever has will be given more, but whoever does not have, even what he thinks he has will be taken away from him.” | SWKCV 18 Kwa hiyo, kuweni waangalifu mnavyosikia. Kwa maana yeyote aliye na kitu atapewa zaidi. Lakini yule asiye na kitu, hata kile anachodhani anacho atanyangʼanywa.” |
| BSB 19 Then Jesus’ mother and brothers came to see Him, but they were unable to reach Him because of the crowd. | SWKCV 19 Wakati mmoja mama yake Yesu na ndugu zake walikuja kumwona, lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. |
| BSB 20 He was told, “Your mother and brothers are standing outside, wanting to see You.” | SWKCV 20 Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.” |
| BSB 21 But He replied, “My mother and brothers are those who hear the word of God and carry it out.” | SWKCV 21 Yesu akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulifanya.” |
| BSB 22 One day Jesus said to His disciples, “Let us cross to the other side of the lake.” So He got into a boat with them and set out. | SWKCV 22 Siku moja Yesu alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, “Tuvukeni twende mpaka ngʼambo ya ziwa.” Nao wakaondoka. |
| BSB 23 As they sailed, He fell asleep, and a windstorm came down on the lake, so that the boat was being swamped, and they were in great danger. | SWKCV 23 Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa. |
| BSB 24 The disciples went and woke Him, saying, “Master, Master, we are perishing!” Then Jesus got up and rebuked the wind and the raging waters, and they subsided, and all was calm. | SWKCV 24 Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, “Bwana, Bwana, tunaangamia!” Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari. |
| BSB 25 “Where is your faith?” He asked. Frightened and amazed, they asked one another, “Who is this? He commands even the winds and the water, and they obey Him!” | SWKCV 25 Akawauliza wanafunzi wake, “Imani yenu iko wapi?” Kwa woga na mshangao wakaulizana, “Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?” |
| BSB 26 Then they sailed to the region of the Gerasenes, across the lake from Galilee. | SWKCV 26 Basi wakafika katika nchi ya Wagerasi, ambayo iko upande wa pili wa ziwa kutoka Galilaya. |
| BSB 27 When Jesus stepped ashore, He was met by a demon-possessed man from the town. For a long time this man had not worn clothing or lived in a house, but he stayed in the tombs. | SWKCV 27 Yesu aliposhuka kutoka mashua na kukanyaga ufuoni, alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye kwa muda mrefu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini. |
| BSB 28 When the man saw Jesus, he cried out and fell down before Him, shouting in a loud voice, “What do You want with me, Jesus, Son of the Most High God? I beg You not to torture me!” | SWKCV 28 Alipomwona Yesu, alipiga kelele, akajitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kuu, “Una nini nami, Yesu, Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana? Nakuomba, usinitese!” |
| BSB 29 For Jesus had commanded the unclean spirit to come out of the man. Many times it had seized him, and though he was bound with chains and shackles, he had broken the chains and been driven by the demon into solitary places. | SWKCV 29 Wakati huo Yesu alikuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke huyo mtu. Mara nyingi huyo pepo mchafu alimpagaa, na hata alipofungwa kwa minyororo mikono na miguu na kuwekwa chini ya ulinzi, alikata hiyo minyororo na kupelekwa na huyo pepo mchafu kwenda nyikani. |
| BSB 30 “What is your name?” Jesus asked. “Legion,” he replied, because many demons had gone into him. | SWKCV 30 Yesu akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Legioni,” kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno. |
| BSB 31 And the demons kept begging Jesus not to order them to go into the Abyss. | SWKCV 31 Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda katika Shimo. |
| BSB 32 There on the hillside a large herd of pigs was feeding. So the demons begged Jesus to let them enter the pigs, and He gave them permission. | SWKCV 32 Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Yesu awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu. |
| BSB 33 Then the demons came out of the man and went into the pigs, and the herd rushed down the steep bank into the lake and was drowned. | SWKCV 33 Wale pepo wachafu walipomtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremkia gengeni kwa kasi, likatumbukia ziwani na kuzama. |
| BSB 34 When those tending the pigs saw what had happened, they ran off and reported this in the town and countryside. | SWKCV 34 Wale watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe walipoona yaliyotukia, wakakimbia, wakaeneza habari hizi mjini na mashambani. |
| BSB 35 So the people went out to see what had happened. They came to Jesus and found the man whom the demons had left, sitting at Jesus’ feet, clothed and in his right mind; and they were afraid. | SWKCV 35 Nao watu wakatoka kwenda kujionea wenyewe yaliyotukia. Walipofika hapo alipokuwa Yesu, wakamkuta yule mtu aliyetokwa na pepo wachafu amekaa karibu na Yesu, akiwa amevaa nguo na mwenye akili timamu! Wakaogopa. |
| BSB 36 Meanwhile, those who had seen it reported how the demon-possessed man had been healed. | SWKCV 36 Wale walioyaona mambo hayo wakawaeleza watu wengine jinsi yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu alivyoponywa. |
| BSB 37 Then all the people of the region of the Gerasenes asked Jesus to depart from them, because great fear had taken hold of them. So He got into the boat and started back. | SWKCV 37 Ndipo watu wote wa nchi ile ya Wagerasi wakamwomba Yesu aondoke kwao, kwa sababu walikuwa wamejawa na hofu. Basi akaingia katika mashua, akaondoka zake. |
| BSB 38 The man whom the demons had left begged to go with Jesus. But He sent him away, saying, | SWKCV 38 Yule mtu aliyetokwa na pepo wachafu akamsihi Yesu afuatane naye, lakini Yesu akamuaga, akamwambia: |
| BSB 39 “Return home and describe how much God has done for you.” So the man went away and proclaimed all over the town how much Jesus had done for him. | SWKCV 39 “Rudi nyumbani ukawaeleze mambo makuu Mungu aliyokutendea.” Kwa hiyo yule mtu akaenda, akatangaza katika mji wote mambo makuu ambayo Yesu alimtendea. |
| BSB 40 When Jesus returned, the crowd welcomed Him, for they had all been waiting for Him. | SWKCV 40 Basi Yesu aliporudi, umati mkubwa wa watu ukampokea kwa furaha, kwani walikuwa wakimngojea. |
| BSB 41 Just then a synagogue leader named Jairus came and fell at Jesus’ feet. He begged Him to come to his house, | SWKCV 41 Kisha mtu mmoja, jina lake Yairo, aliyekuwa kiongozi wa sinagogi, akaja na kuanguka miguuni mwa Yesu, akimwomba afike nyumbani kwake, |
| BSB 42 because his only daughter, who was about twelve, was dying. As Jesus went with him, the crowds pressed around Him, | SWKCV 42 kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa. Yesu alipokuwa akienda, umati wa watu ukamsonga sana. |
| BSB 43 including a woman who had suffered from bleeding for twelve years. She had spent all her money on physicians, but no one was able to heal her. | SWKCV 43 Katika umati huo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu, wala hakuna yeyote aliyeweza kumponya. |
| BSB 44 She came up behind Jesus and touched the fringe of His cloak, and immediately her bleeding stopped. | SWKCV 44 Huyo mwanamke akaja kwa nyuma ya Yesu na kugusa upindo wa vazi lake. Mara kutokwa damu kwake kukakoma. |
| BSB 45 “Who touched Me?” Jesus asked. But they all denied it. “Master,” said Peter, “the people are crowding and pressing against You.” | SWKCV 45 Yesu akauliza, “Ni nani aliyenigusa?” Watu wote walipokana, Petro akasema, “Bwana, huu umati wa watu unakusonga na kukusukuma kila upande.” |
| BSB 46 But Jesus declared, “Someone touched Me, for I know that power has gone out from Me.” | SWKCV 46 Lakini Yesu akasema, “Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka.” |
| BSB 47 Then the woman, seeing that she could not escape notice, came trembling and fell down before Him. In the presence of all the people, she explained why she had touched Him and how she had immediately been healed. | SWKCV 47 Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Yesu. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara. |
| BSB 48 “Daughter,” said Jesus, “your faith has healed you. Go in peace.” | SWKCV 48 Basi Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.” |
| BSB 49 While He was still speaking, someone arrived from the house of the synagogue leader. “Your daughter is dead,” he told Jairus. “Do not bother the Teacher anymore.” | SWKCV 49 Yesu alipokuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani kwa Yairo, yule kiongozi wa sinagogi, kumwambia, “Binti yako amekwisha kufa. Usiendelee kumsumbua Mwalimu.” |
| BSB 50 But Jesus overheard them and said to Jairus, “Do not be afraid; just believe, and she will be healed.” | SWKCV 50 Yesu aliposikia jambo hili, akamwambia Yairo, “Usiogope. Amini tu, naye binti yako atapona.” |
| BSB 51 When He entered the house, He did not allow anyone to go in with Him except Peter, John, James, and the child’s father and mother. | SWKCV 51 Walipofika nyumbani kwa Yairo, hakumruhusu mtu yeyote aingie ndani naye isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, pamoja na baba na mama wa yule binti. |
| BSB 52 Meanwhile, everyone was weeping and mourning for her. But Jesus said, “Stop weeping; she is not dead but asleep.” | SWKCV 52 Wakati ule ule watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili ya huyo binti. Yesu akawaambia, “Acheni kulia. Huyu binti hajafa, ila amelala.” |
| BSB 53 And they laughed at Him, knowing that she was dead. | SWKCV 53 Wao wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekwisha kufa. |
| BSB 54 But Jesus took her by the hand and called out, “Child, get up!” | SWKCV 54 Yesu akamshika yule binti mkono na kuita, “Binti, amka!” |
| BSB 55 Her spirit returned, and at once she got up. And He directed that she be given something to eat. | SWKCV 55 Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara moja. Akaamuru apewe kitu cha kula. |
| BSB 56 Her parents were astounded, but Jesus ordered them not to tell anyone what had happened. | SWKCV 56 Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote juu ya yale yaliyotukia. |
Questions about Luke 8? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.