Luke 7

Berean Standard Bible tier 2Kiswahili Contemporary Version tier 3
BSB

1 When Jesus had concluded His discourse in the hearing of the people, He went to Capernaum.

SWKCV

1 Baada ya Yesu kumaliza kusema haya yote watu wakiwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu.

BSB

2 There a highly valued servant of a centurion was sick and about to die.

SWKCV

2 Mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu kufa.

BSB

3 When the centurion heard about Jesus, he sent some Jewish elders to ask Him to come and heal his servant.

SWKCV

3 Jemadari huyo aliposikia habari za Yesu, aliwatuma wazee wa Kiyahudi kwake, wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo jemadari.

BSB

4 They came to Jesus and pleaded with Him earnestly, “This man is worthy to have You grant this,

SWKCV

4 Wale wazee walipofika kwa Yesu, wakamsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, “Mtu huyu anastahili wewe umfanyie jambo hili,

BSB

5 for he loves our nation and has built our synagogue.”

SWKCV

5 kwa sababu analipenda taifa letu tena ametujengea sinagogi.”

BSB

6 So Jesus went with them. But when He was not far from the house, the centurion sent friends with the message: “Lord, do not trouble Yourself, for I am not worthy to have You come under my roof.

SWKCV

6 Hivyo Yesu akaongozana nao, lakini alipokuwa hayuko mbali na nyumbani, yule jemadari akatuma rafiki zake kumwambia Yesu, “Bwana, usijisumbue, kwani mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu.

BSB

7 That is why I did not consider myself worthy to come to You. But just say the word, and my servant will be healed.

SWKCV

7 Ndiyo maana sikujiona hata ninastahili kuja kwako wewe. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona.

BSB

8 For I myself am a man under authority, with soldiers under me. I tell one to go, and he goes, and another to come, and he comes. I tell my servant to do something, and he does it.”

SWKCV

8 Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.”

BSB

9 When Jesus heard this, He marveled at the centurion. Turning to the crowd following Him, He said, “I tell you, not even in Israel have I found such great faith.”

SWKCV

9 Yesu aliposikia maneno haya, alishangazwa naye sana. Akaugeukia ule umati wa watu uliokuwa unamfuata, akawaambia, “Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli.”

BSB

10 And when the messengers returned to the house, they found the servant in good health.

SWKCV

10 Nao wale watu waliokuwa wametumwa kwa Yesu waliporudi nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona.

BSB

11 Soon afterward, Jesus went to a town called Nain. His disciples went with Him, accompanied by a large crowd.

SWKCV

11 Baadaye kidogo, Yesu alikwenda katika mji mmoja ulioitwa Naini. Nao wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu walikwenda pamoja naye.

BSB

12 As He approached the town gate, He saw a dead man being carried out, the only son of his mother, and she was a widow. And a large crowd from the town was with her.

SWKCV

12 Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mwanamke.

BSB

13 When the Lord saw her, He had compassion on her and said, “Do not weep.”

SWKCV

13 Bwana Yesu alipomwona yule mjane, moyo wake ulimhurumia, akamwambia, “Usilie.”

BSB

14 Then He went up and touched the coffin, and those carrying it stood still. “Young man,” He said, “I tell you, get up!”

SWKCV

14 Kisha akasogea mbele akaligusa lile jeneza na wale waliokuwa wamelibeba wakasimama kimya. Akasema, “Kijana, nakuambia inuka.”

BSB

15 And the dead man sat up and began to speak! Then Jesus gave him back to his mother.

SWKCV

15 Yule aliyekuwa amekufa akaketi akaanza kuongea, naye Yesu akamkabidhi kwa mama yake.

BSB

16 A sense of awe swept over all of them, and they glorified God. “A great prophet has appeared among us!” they said. “God has visited His people!”

SWKCV

16 Watu wote wakajawa na hofu ya Mungu, nao wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea miongoni mwetu, Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”

BSB

17 And the news about Jesus spread throughout Judea and all the surrounding region.

SWKCV

17 Habari hizi za mambo aliyoyafanya Yesu zikaenea Uyahudi wote na sehemu zote za jirani.

BSB

18 Then John’s disciples informed him about all these things.

SWKCV

18 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji wakamweleza Yohana mambo haya yote. Hivyo Yohana akawaita wanafunzi wake wawili

BSB

19 So John called two of his disciples and sent them to ask the Lord, “Are You the One who was to come, or should we look for someone else?”

SWKCV

19 na kuwatuma kwa Bwana ili kumuuliza, “Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?”

BSB

20 When the men came to Jesus, they said, “John the Baptist sent us to ask, ‘Are You the One who was to come, or should we look for someone else?’”

SWKCV

20 Wale watu walipofika kwa Yesu wakamwambia, “Yohana Mbatizaji ametutuma tukuulize, ‘Wewe ndiye yule aliyekuwa aje, au tumngojee mwingine?’”

BSB

21 At that very hour Jesus healed many people of their diseases, afflictions, and evil spirits, and He gave sight to many who were blind.

SWKCV

21 Wakati huo huo, Yesu aliwaponya wengi waliokuwa na magonjwa, maradhi na pepo wachafu, na pia akawafungua vipofu wengi macho wakapata kuona.

BSB

22 So He replied, “Go back and report to John what you have seen and heard: The blind receive sight, the lame walk, the lepers are cleansed, the deaf hear, the dead are raised, and the good news is preached to the poor.

SWKCV

22 Hivyo akawajibu wale wajumbe, “Rudini mkamwambie Yohana yote mnayoyaona na kuyasikia: Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa habari njema.

BSB

23 Blessed is the one who does not fall away on account of Me.”

SWKCV

23 Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”

BSB

24 After John’s messengers had left, Jesus began to speak to the crowds about John: “What did you go out into the wilderness to see? A reed swaying in the wind?

SWKCV

24 Wajumbe wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kusema na makutano kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mlipokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo?

BSB

25 Otherwise, what did you go out to see? A man dressed in fine clothes? Look, those who wear elegant clothing and live in luxury are found in palaces.

SWKCV

25 Kama sivyo, mlikwenda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha, watu wanaovaa mavazi ya kifahari na kuishi maisha ya anasa wako katika majumba ya kifalme.

BSB

26 What then did you go out to see? A prophet? Yes, I tell you, and more than a prophet.

SWKCV

26 Lakini mlikwenda kuona nini? Mlikwenda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii.

BSB

27 This is the one about whom it is written: ‘Behold, I will send My messenger ahead of You, who will prepare Your way before You.’

SWKCV

27 Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa: “ ‘Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, atakayetengeneza njia mbele yako.’

BSB

28 I tell you, among those born of women there is no one greater than John, yet even the least in the kingdom of God is greater than he.”

SWKCV

28 Nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hakuna aliye mkuu kuliko Yohana. Lakini yeye aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana.”

BSB

29 All the people who heard this, even the tax collectors, acknowledged God’s justice. For they had received the baptism of John.

SWKCV

29 (Watu wote hata watoza ushuru waliposikia maneno ya Yesu, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yohana.

BSB

30 But the Pharisees and experts in the law rejected God’s purpose for themselves, because they had not been baptized by John.

SWKCV

30 Lakini Mafarisayo na wataalamu wa sheria walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokubali kubatizwa na Yohana.)

BSB

31 “To what, then, can I compare the men of this generation? What are they like?

SWKCV

31 Yesu akawauliza, “Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Wanafanana na nini?

BSB

32 They are like children sitting in the marketplace and calling out to one another: ‘We played the flute for you, and you did not dance; we sang a dirge, and you did not weep.’

SWKCV

32 Wao ni kama watoto waliokaa sokoni wakiitana wao kwa wao, wakisema: “ ‘Tuliwapigia filimbi, lakini hamkucheza; tuliwaimbia nyimbo za maombolezo, lakini hamkulia.’

BSB

33 For John the Baptist came neither eating bread nor drinking wine, and you say, ‘He has a demon!’

SWKCV

33 Kwa maana Yohana Mbatizaji alikuja, alikuwa hali mkate wala hanywi divai, nanyi mkasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’

BSB

34 The Son of Man came eating and drinking, and you say, ‘Look at this glutton and drunkard, a friend of tax collectors and sinners!’

SWKCV

34 Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nanyi mnasema: ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.”’

BSB

35 But wisdom is vindicated by all her children.”

SWKCV

35 Nayo hekima huthibitishwa kuwa kweli na watoto wake wote.”

BSB

36 Then one of the Pharisees invited Jesus to eat with him, and He entered the Pharisee’s house and reclined at the table.

SWKCV

36 Basi Farisayo mmoja alimwalika Yesu nyumbani kwake kwa chakula. Hivyo Yesu akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kukaa katika nafasi yake mezani.

BSB

37 When a sinful woman from that town learned that Jesus was dining there, she brought an alabaster jar of perfume.

SWKCV

37 Naye mwanamke mmoja kwenye ule mji, ambaye alikuwa mwenye dhambi, alipojua kwamba Yesu alikuwa akila chakula nyumbani kwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marhamu yenye manukato.

BSB

38 As she stood behind Him at His feet weeping, she began to wet His feet with her tears and wipe them with her hair. Then she kissed His feet and anointed them with the perfume.

SWKCV

38 Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Yesu akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.

BSB

39 When the Pharisee who had invited Jesus saw this, he said to himself, “If this man were a prophet, He would know who this is and what kind of woman is touching Him—for she is a sinner!”

SWKCV

39 Yule Farisayo aliyemwalika Yesu alipoona yanayotendeka, akawaza moyoni mwake, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua kwamba ni nani anayemgusa, na kwamba yeye ni mwanamke wa namna gani, na ya kuwa huyu mwanamke ni mwenye dhambi.”

BSB

40 But Jesus answered him, “Simon, I have something to tell you.” “Tell me, Teacher,” he said.

SWKCV

40 Yesu akanena akamwambia, “Simoni, nina jambo la kukuambia.” Simoni akajibu, “Mwalimu, sema.”

BSB

41 “Two men were debtors to a certain moneylender. One owed him five hundred denarii, and the other fifty.

SWKCV

41 “Palikuwa na mtu mmoja aliyewakopesha watu wawili fedha: Mmoja alidaiwa dinari 500 na mwingine dinari hamsini.

BSB

42 When they were unable to repay him, he forgave both of them. Which one, then, will love him more?”

SWKCV

42 Wote wawili walipokuwa hawawezi kulipa, aliyafuta madeni yao wote wawili. Sasa ni yupi kati yao atakayempenda yule aliyewasamehe zaidi?”

BSB

43 “I suppose the one who was forgiven more,” Simon replied. “You have judged correctly,” Jesus said.

SWKCV

43 Simoni akajibu, “Nadhani ni yule aliyesamehewa deni kubwa zaidi.” Naye Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.”

BSB

44 And turning toward the woman, He said to Simon, “Do you see this woman? When I entered your house, you did not give Me water for My feet, but she wet My feet with her tears and wiped them with her hair.

SWKCV

44 Kisha akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, “Je, unamwona mwanamke huyu? Nilipoingia nyumbani mwako, hukunipa maji ya kunawa miguu yangu, lakini huyu ameninawisha miguu kwa machozi yake, na kunifuta kwa nywele zake.

BSB

45 You did not greet Me with a kiss, but she has not stopped kissing My feet since I arrived.

SWKCV

45 Hukunisalimu kwa busu, lakini huyu mwanamke hajaacha kuibusu miguu yangu tangu nilipoingia.

BSB

46 You did not anoint My head with oil, but she has anointed My feet with perfume.

SWKCV

46 Hukunipaka mafuta kichwani mwangu, lakini yeye ameipaka miguu yangu manukato.

BSB

47 Therefore I tell you, her many sins have been forgiven, for she has loved much. But he who has been forgiven little loves little.”

SWKCV

47 Kwa hiyo, nakuambia, dhambi zake zilizokuwa nyingi zimesamehewa, kwani ameonyesha upendo mwingi. Lakini yule aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo.”

BSB

48 Then Jesus said to her, “Your sins are forgiven.”

SWKCV

48 Kisha akamwambia yule mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.”

BSB

49 But those at the table began to say to themselves, “Who is this who even forgives sins?”

SWKCV

49 Lakini wale waliokuwa wameketi pamoja naye chakulani wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani ambaye hata anasamehe dhambi?”

BSB

50 And Jesus told the woman, “Your faith has saved you; go in peace.”

SWKCV

50 Yesu akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”

Questions about Luke 7? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.