Luke 6
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 One Sabbath Jesus was passing through the grainfields, and His disciples began to pick the heads of grain, rub them in their hands, and eat them. | SWKCV 1 Ikawa siku moja ya Sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya nafaka, nao wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya nafaka, wakayafikicha kwa mikono yao na kula punje zake. |
| BSB 2 But some of the Pharisees asked, “Why are you doing what is unlawful on the Sabbath?” | SWKCV 2 Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnafanya mambo yasiyo halali kufanywa siku ya Sabato?” |
| BSB 3 Jesus replied, “Have you not read what David did when he and his companions were hungry? | SWKCV 3 Yesu akawajibu, “Je, ninyi hamjasoma kamwe alivyofanya Daudi wakati yeye na wenzake walikuwa na njaa? |
| BSB 4 He entered the house of God, took the consecrated bread and gave it to his companions, and ate what is lawful only for the priests to eat.” | SWKCV 4 Aliingia ndani ya nyumba ya Mungu, akaichukua na kuila ile mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ni halali kuliwa na makuhani peke yao. Naye pia akawapa wenzake.” |
| BSB 5 Then Jesus declared, “The Son of Man is Lord of the Sabbath.” | SWKCV 5 Yesu akawaambia, “Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.” |
| BSB 6 On another Sabbath Jesus entered the synagogue and was teaching, and a man was there whose right hand was withered. | SWKCV 6 Ikawa siku nyingine ya Sabato, Yesu aliingia ndani ya sinagogi na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. |
| BSB 7 Looking for a reason to accuse Jesus, the scribes and Pharisees were watching Him closely to see if He would heal on the Sabbath. | SWKCV 7 Mafarisayo na walimu wa sheria walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Yesu. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato. |
| BSB 8 But Jesus knew their thoughts and said to the man with the withered hand, “Get up and stand among us.” So he got up and stood there. | SWKCV 8 Lakini Yesu alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, “Inuka usimame mbele ya watu wote.” Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote. |
| BSB 9 Then Jesus said to them, “I ask you, which is lawful on the Sabbath: to do good or to do evil, to save life or to destroy it?” | SWKCV 9 Ndipo Yesu akawaambia wale walimu wa sheria na Mafarisayo, “Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?” |
| BSB 10 And after looking around at all of them, He said to the man, “Stretch out your hand.” He did so, and it was restored. | SWKCV 10 Akawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule aliyepooza mkono, “Nyoosha mkono wako!” Akaunyoosha na mkono wake ukaponywa kabisa. |
| BSB 11 But the scribes and Pharisees were filled with rage and began to discuss with one another what they might do to Jesus. | SWKCV 11 Wale wakuu wakakasirika sana, wakashauriana wao kwa wao ni nini watakachomtendea Yesu. |
| BSB 12 In those days Jesus went out to the mountain to pray, and He spent the night in prayer to God. | SWKCV 12 Ikawa katika siku hizo Yesu alikwenda mlimani kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu. |
| BSB 13 When daylight came, He called His disciples to Him and chose twelve of them, whom He also designated as apostles: | SWKCV 13 Kulipopambazuka, akawaita wanafunzi wake, naye akachagua kumi na wawili, ambao pia aliwaita mitume: |
| BSB 14 Simon, whom He named Peter, and his brother Andrew; James and John; Philip and Bartholomew; | SWKCV 14 Simoni aliyemwita Petro, Andrea nduguye, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, |
| BSB 15 Matthew and Thomas; James son of Alphaeus and Simon called the Zealot; | SWKCV 15 Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni aliyeitwa Zelote, |
| BSB 16 Judas son of James, and Judas Iscariot, who became a traitor. | SWKCV 16 Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda Iskariote ambaye alikuwa msaliti. |
| BSB 17 Then Jesus came down with them and stood on a level place. A large crowd of His disciples was there, along with a great number of people from all over Judea, Jerusalem, and the seacoast of Tyre and Sidon. | SWKCV 17 Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Uyahudi, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. |
| BSB 18 They had come to hear Him and to be healed of their diseases, and those troubled by unclean spirits were healed. | SWKCV 18 Walikuwa wamekuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Wale waliokuwa wakiteswa na pepo wachafu akawaponya. |
| BSB 19 The entire crowd was trying to touch Him, because power was coming from Him and healing them all. | SWKCV 19 Watu wote walikuwa wanajitahidi kumgusa kwa sababu nguvu zilikuwa zikimtoka na kuwaponya wote. |
| BSB 20 Looking up at His disciples, Jesus said: “Blessed are you who are poor, for yours is the kingdom of God. | SWKCV 20 Akawatazama wanafunzi wake, akasema: “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa sababu Ufalme wa Mungu ni wenu. |
| BSB 21 Blessed are you who hunger now, for you will be filled. Blessed are you who weep now, for you will laugh. | SWKCV 21 Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, kwa sababu mtacheka. |
| BSB 22 Blessed are you when people hate you, and when they exclude you and insult you and reject your name as evil because of the Son of Man. | SWKCV 22 Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu. |
| BSB 23 Rejoice in that day and leap for joy, because great is your reward in heaven. For their fathers treated the prophets in the same way. | SWKCV 23 “Furahini na kurukaruka kwa shangwe, kwa sababu thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo baba zao walivyowatenda manabii. |
| BSB 24 But woe to you who are rich, for you have already received your comfort. | SWKCV 24 “Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri, kwa sababu mmekwisha kupokea faraja yenu. |
| BSB 25 Woe to you who are well fed now, for you will hunger. Woe to you who laugh now, for you will mourn and weep. | SWKCV 25 Ole wenu ninyi mlioshiba sasa, maana mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, maana mtaomboleza na kulia. |
| BSB 26 Woe to you when all men speak well of you, for their fathers treated the false prophets in the same way. | SWKCV 26 Ole wenu watu watakapowasifu, kwani ndivyo baba zao walivyowasifu manabii wa uongo. |
| BSB 27 But to those of you who will listen, I say: Love your enemies, do good to those who hate you, | SWKCV 27 “Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. |
| BSB 28 bless those who curse you, pray for those who mistreat you. | SWKCV 28 Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya. |
| BSB 29 If someone strikes you on one cheek, turn to him the other also. And if someone takes your cloak, do not withhold your tunic as well. | SWKCV 29 Kama mtu akikupiga shavu moja, mgeuzie na la pili pia. Mtu akikunyangʼanya koti lako, usimzuie kuchukua joho pia. |
| BSB 30 Give to everyone who asks you, and if anyone takes what is yours, do not demand it back. | SWKCV 30 Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie. |
| BSB 31 Do to others as you would have them do to you. | SWKCV 31 Watendeeni wengine kama ambavyo mngetaka wawatendee ninyi. |
| BSB 32 If you love those who love you, what credit is that to you? Even sinners love those who love them. | SWKCV 32 “Kama mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwapenda wale wawapendao. |
| BSB 33 If you do good to those who do good to you, what credit is that to you? Even sinners do the same. | SWKCV 33 Tena mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea ninyi mema, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ hufanya vivyo hivyo. |
| BSB 34 And if you lend to those from whom you expect repayment, what credit is that to you? Even sinners lend to sinners, expecting to be repaid in full. | SWKCV 34 Tena mnapowakopesha wale tu mnaotegemea wawalipe, mwapata sifa gani? Hata ‘wenye dhambi’ huwakopesha ‘wenye dhambi’ wenzao wakitarajia kulipwa mali yao yote. |
| BSB 35 But love your enemies, do good to them, and lend to them, expecting nothing in return. Then your reward will be great, and you will be sons of the Most High; for He is kind to the ungrateful and wicked. | SWKCV 35 Lakini wapendeni adui zenu, watendeeni mema, wakopesheni bila kutegemea kurudishiwa mlichokopesha. Ndipo thawabu yenu itakapokuwa kubwa, nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu Sana, kwa sababu yeye ni mwema kwa watu wasio na shukrani na kwa wale waovu. |
| BSB 36 Be merciful, just as your Father is merciful. | SWKCV 36 Kuweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma. |
| BSB 37 Do not judge, and you will not be judged. Do not condemn, and you will not be condemned. Forgive, and you will be forgiven. | SWKCV 37 “Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa. Msilaumu, nanyi hamtalaumiwa. Sameheni, nanyi mtasamehewa. |
| BSB 38 Give, and it will be given to you. A good measure, pressed down, shaken together, and running over will be poured into your lap. For with the measure you use, it will be measured back to you.” | SWKCV 38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa. Kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa.” |
| BSB 39 Jesus also told them a parable: “Can a blind man lead a blind man? Will they not both fall into a pit? | SWKCV 39 Pia akawapa mfano akasema, “Je, kipofu aweza kumwongoza kipofu? Je, wote wawili hawatatumbukia shimoni? |
| BSB 40 A disciple is not above his teacher, but everyone who is fully trained will be like his teacher. | SWKCV 40 Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake, ila yule aliyehitimu aweza kuwa kama mwalimu wake. |
| BSB 41 Why do you look at the speck in your brother’s eye but fail to notice the beam in your own eye? | SWKCV 41 “Mbona unatazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, wala huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe? |
| BSB 42 How can you say, ‘Brother, let me take the speck out of your eye,’ while you yourself fail to see the beam in your own eye? You hypocrite! First take the beam out of your own eye, and then you will see clearly to remove the speck from your brother’s eye. | SWKCV 42 Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako. |
| BSB 43 No good tree bears bad fruit, nor does a bad tree bear good fruit. | SWKCV 43 “Hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri. |
| BSB 44 For each tree is known by its own fruit. Indeed, figs are not gathered from thornbushes, nor grapes from brambles. | SWKCV 44 Kila mti hujulikana kwa matunda yake. Kwa maana watu hawachumi tini kwenye miiba, wala zabibu kwenye michongoma. |
| BSB 45 The good man brings good things out of the good treasure of his heart, and the evil man brings evil things out of the evil treasure of his heart. For out of the overflow of the heart the mouth speaks. | SWKCV 45 Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka kwenye hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka kwenye hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake. |
| BSB 46 Why do you call Me ‘Lord, Lord,’ but do not do what I say? | SWKCV 46 “Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? |
| BSB 47 I will show you what he is like who comes to Me and hears My words and acts on them: | SWKCV 47 Nitawaonyesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. |
| BSB 48 He is like a man building a house, who dug down deep and laid his foundation on the rock. When the flood came, the torrent crashed against that house but could not shake it, because it was well built. | SWKCV 48 Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, maji ya ghafula yaliipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. |
| BSB 49 But the one who hears My words and does not act on them is like a man who built his house on ground without a foundation. The torrent crashed against that house, and immediately it fell—and great was its destruction!” | SWKCV 49 Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.” |
Questions about Luke 6? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.