Mark 12
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then Jesus began to speak to them in parables: “A man planted a vineyard. He put a wall around it, dug a wine vat, and built a watchtower. Then he rented it out to some tenants and went away on a journey. | SWKCV 1 Yesu akaanza kusema nao kwa mifano, akawaambia: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akachimba shimo ndani yake kwa ajili ya shinikizo la kusindika divai, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha shamba hilo la mizabibu kwa wakulima fulani, kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. |
| BSB 2 At harvest time, he sent a servant to the tenants to collect his share of the fruit of the vineyard. | SWKCV 2 Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba akamtuma mtumishi wake kwa hao wapangaji ili kuchukua sehemu yake ya mavuno ya shamba la mizabibu kutoka kwa hao wapangaji. |
| BSB 3 But they seized the servant, beat him, and sent him away empty-handed. | SWKCV 3 Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. |
| BSB 4 Then he sent them another servant, and they struck him over the head and treated him shamefully. | SWKCV 4 Kisha yule mwenye shamba akamtuma mtumishi mwingine kwao; nao wale wakulima wakampiga kichwani na kumfanyia mambo ya aibu. |
| BSB 5 He sent still another, and this one they killed. He sent many others; some they beat and others they killed. | SWKCV 5 Kisha akamtuma mtumishi mwingine, naye huyo wakamuua. Akawatuma wengine wengi; baadhi yao wakawapiga, na wengine wakawaua. |
| BSB 6 Finally, having one beloved son, he sent him to them. ‘They will respect my son,’ he said. | SWKCV 6 “Mwenye shamba alikuwa bado na mmoja wa kumtuma, mwanawe aliyempenda. Hatimaye akamtuma akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’ |
| BSB 7 But the tenants said to one another, ‘This is the heir. Come, let us kill him, and the inheritance will be ours.’ | SWKCV 7 “Lakini wale wapangaji wakasemezana pamoja, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumuue, nao urithi utakuwa wetu.’ |
| BSB 8 So they seized the son, killed him, and threw him out of the vineyard. | SWKCV 8 Hivyo wakamchukua na kumuua, wakamtupa nje ya lile shamba la mizabibu. |
| BSB 9 What then will the owner of the vineyard do? He will come and kill those tenants and give the vineyard to others. | SWKCV 9 “Sasa basi yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja na kuwaua hao wapangaji, kisha atawapa wapangaji wengine hilo shamba la mizabibu. |
| BSB 10 Have you never read this Scripture: ‘The stone the builders rejected has become the cornerstone. | SWKCV 10 Je, hamjasoma Andiko hili: “ ‘Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni; |
| BSB 11 This is from the Lord, and it is marvelous in our eyes’?” | SWKCV 11 Bwana ndiye alitenda jambo hili, nalo ni ajabu machoni petu’?” |
| BSB 12 At this, the leaders sought to arrest Jesus, for they knew that He had spoken this parable against them. But fearing the crowd, they left Him and went away. | SWKCV 12 Walipotambua kuwa amesema mfano huo kwa ajili yao, wakataka kumkamata, lakini wakaogopa ule umati wa watu. Wakamwacha, wakaondoka, wakaenda zao. |
| BSB 13 Later, they sent some of the Pharisees and Herodians to catch Jesus in His words. | SWKCV 13 Baadaye wakawatuma baadhi ya Mafarisayo na Maherode ili kwenda kumtega Yesu katika yale anayosema. |
| BSB 14 “Teacher,” they said, “we know that You are honest and seek favor from no one. Indeed, You are impartial and teach the way of God in accordance with the truth. Is it lawful to pay taxes to Caesar or not? Should we pay them or not?” | SWKCV 14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwadilifu. Wewe huyumbishwi na wanadamu, kwa kuwa huna upendeleo. Lakini wewe huifundisha njia ya Mungu katika kweli. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la? |
| BSB 15 But Jesus saw through their hypocrisy and said, “Why are you testing Me? Bring Me a denarius to inspect.” | SWKCV 15 Je, tulipe kodi au tusilipe?” Lakini Yesu alijua unafiki wao. Akawauliza “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni hiyo dinari niione.” |
| BSB 16 So they brought it, and He asked them, “Whose image is this? And whose inscription?” “Caesar’s,” they answered. | SWKCV 16 Wakamletea hiyo sarafu. Naye akawauliza, “Sura hii ni ya nani? Na maandishi haya ni ya nani?” Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” |
| BSB 17 Then Jesus told them, “Give to Caesar what is Caesar’s, and to God what is God’s.” And they marveled at Him. | SWKCV 17 Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.” Nao wakamstaajabia sana. |
| BSB 18 Then the Sadducees, who say there is no resurrection, came to Jesus and questioned Him: | SWKCV 18 Kisha Masadukayo, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu, wakamjia Yesu, |
| BSB 19 “Teacher, Moses wrote for us that if a man’s brother dies and leaves a wife but no children, the man is to marry his brother’s widow and raise up offspring for him. | SWKCV 19 wakasema, “Mwalimu, Mose alituandikia kuwa kama ndugu wa mtu akifa na kumwacha mkewe bila mtoto, basi huyo mtu inampasa amwoe huyo mjane ili amzalie ndugu yake watoto. |
| BSB 20 Now there were seven brothers. The first one married and died, leaving no children. | SWKCV 20 Basi palikuwepo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa mke, naye akafa pasipo kuwa na mtoto yeyote. |
| BSB 21 Then the second one married the widow, but he also died and left no children. And the third did likewise. | SWKCV 21 Wa pili akamwoa yule mjane, lakini naye akafa bila kuacha mtoto yeyote. Ikawa vivyo hivyo kwa yule wa tatu. |
| BSB 22 In this way, none of the seven left any children. And last of all, the woman died. | SWKCV 22 Hakuna hata mmojawapo wa hao ndugu wote saba aliyeacha mtoto. Hatimaye yule mwanamke naye akafa. |
| BSB 23 In the resurrection, then, whose wife will she be? For all seven were married to her.” | SWKCV 23 Kwa hiyo wakati wa ufufuo, yeye atakuwa mke wa nani, maana aliolewa na ndugu wote saba?” |
| BSB 24 Jesus said to them, “Aren’t you mistaken, because you do not know the Scriptures or the power of God? | SWKCV 24 Yesu akawajibu, “Je, hampotoki kwa sababu hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu? |
| BSB 25 When the dead rise, they will neither marry nor be given in marriage. Instead, they will be like the angels in heaven. | SWKCV 25 Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa, bali watakuwa kama malaika wa mbinguni. |
| BSB 26 But concerning the dead rising, have you not read about the burning bush in the Book of Moses, how God told him, ‘I am the God of Abraham, the God of Isaac, and the God of Jacob’? | SWKCV 26 Basi kuhusu wafu kufufuliwa, je hamjasoma katika Kitabu cha Mose jinsi Mungu alivyosema na Mose kutoka kile kichaka akisema, ‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaki, na Mungu wa Yakobo?’ |
| BSB 27 He is not the God of the dead, but of the living. You are badly mistaken!” | SWKCV 27 Yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.” |
| BSB 28 Now one of the scribes had come up and heard their debate. Noticing how well Jesus had answered them, he asked Him, “Which commandment is the most important of all?” | SWKCV 28 Mwalimu mmoja wa sheria akaja, akawasikia wakijadiliana. Akiona kwamba Yesu amewajibu vyema, naye akamuuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?” |
| BSB 29 Jesus replied, “This is the most important: ‘Hear, O Israel, the Lord our God, the Lord is One. | SWKCV 29 Yesu akajibu, “Amri iliyo kuu ndiyo hii: ‘Sikia ee Israeli. Bwana Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja. |
| BSB 30 Love the Lord your God with all your heart and with all your soul and with all your mind and with all your strength.’ | SWKCV 30 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.’ |
| BSB 31 The second is this: ‘Love your neighbor as yourself.’ No other commandment is greater than these.” | SWKCV 31 Ya pili ndiyo hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.” |
| BSB 32 “Right, Teacher,” the scribe replied. “You have stated correctly that God is One and there is no other but Him, | SWKCV 32 Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, umejibu vyema kwamba Mungu ni mmoja, wala hakuna mwingine ila yeye. |
| BSB 33 and to love Him with all your heart and with all your understanding and with all your strength, and to love your neighbor as yourself. This is more important than all burnt offerings and sacrifices.” | SWKCV 33 Kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu zote.” |
| BSB 34 When Jesus saw that the man had answered wisely, He said, “You are not far from the kingdom of God.” And no one dared to question Him any further. | SWKCV 34 Yesu alipoona kwamba amejibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumuuliza maswali tena. |
| BSB 35 While Jesus was teaching in the temple courts, He asked, “How can the scribes say that the Christ is the Son of David? | SWKCV 35 Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, akauliza, “Imekuwaje walimu wa sheria wanasema kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi? |
| BSB 36 Speaking by the Holy Spirit, David himself declared: ‘The Lord said to my Lord, “Sit at My right hand until I put Your enemies under Your feet.”’ | SWKCV 36 Kwa maana Daudi mwenyewe, akinena kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, alisema: “ ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: “Keti mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.”’ |
| BSB 37 David himself calls Him ‘Lord.’ So how can He be David’s son?” And the large crowd listened to Him with delight. | SWKCV 37 Kwa hiyo Daudi mwenyewe anamwita ‘Bwana.’ Awezaje basi yeye kuwa mwanawe?” Ule umati wote wa watu wakamsikiliza kwa furaha. |
| BSB 38 In His teaching Jesus also said, “Watch out for the scribes. They like to walk around in long robes, to receive greetings in the marketplaces, | SWKCV 38 Alipokuwa akifundisha, Yesu alisema, “Jihadharini na walimu wa sheria. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. |
| BSB 39 and to have the chief seats in the synagogues and the places of honor at banquets. | SWKCV 39 Pia wao hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kupewa nafasi za heshima katika karamu. |
| BSB 40 They defraud widows of their houses, and for a show make lengthy prayers. These men will receive greater condemnation.” | SWKCV 40 Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.” |
| BSB 41 As Jesus was sitting opposite the treasury, He watched the crowd putting money into it. And many rich people put in large amounts. | SWKCV 41 Kisha Yesu akaketi mkabala na sehemu ambapo sadaka zilikuwa zinawekwa na kuangalia umati wa watu wakiweka fedha zao kwenye sanduku la hazina ya Hekalu. Matajiri wengi wakaweka kiasi kikubwa cha fedha. |
| BSB 42 Then one poor widow came and put in two small copper coins, which amounted to a small fraction of a denarius. | SWKCV 42 Lakini mjane mmoja maskini akaja na kuweka sarafu mbili ndogo za shaba zenye thamani ya senti mbili. |
| BSB 43 Jesus called His disciples to Him and said, “Truly I tell you, this poor widow has put more than all the others into the treasury. | SWKCV 43 Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Amin, nawaambia, huyu mjane maskini ameweka katika sanduku la hazina zaidi ya watu wengine wote. |
| BSB 44 For they all contributed out of their surplus, but she out of her poverty has put in all she had to live on.” | SWKCV 44 Wengine wote wametoa kutokana na ziada ya mali zao. Lakini huyu mjane ametoa kutokana na umaskini wake, akaweka kila kitu alichokuwa nacho, hata kile alichohitaji ili kuishi.” |
Questions about Mark 12? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.