Matthew 21
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 As they approached Jerusalem and came to Bethphage on the Mount of Olives, Jesus sent out two disciples, | SWKCV 1 Walipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Yesu akawatuma wanafunzi wake wawili, |
| BSB 2 saying to them, “Go into the village ahead of you, and at once you will find a donkey tied there, with her colt beside her. Untie them and bring them to Me. | SWKCV 2 akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. |
| BSB 3 If anyone questions you, tell him that the Lord needs them, and he will send them right away.” | SWKCV 3 Kama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.” |
| BSB 4 This took place to fulfill what was spoken through the prophet: | SWKCV 4 Haya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema: |
| BSB 5 “Say to the Daughter of Zion, ‘See, your King comes to you, gentle and riding on a donkey, on a colt, the foal of a donkey.’” | SWKCV 5 “Mwambieni Binti Sayuni, ‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mnyenyekevu, naye amepanda punda, juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’” |
| BSB 6 So the disciples went and did as Jesus had directed them. | SWKCV 6 Wale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Yesu alivyokuwa amewaagiza. |
| BSB 7 They brought the donkey and the colt and laid their cloaks on them, and Jesus sat on them. | SWKCV 7 Wakamleta yule punda na mwana-punda, nao wakatandika mavazi yao juu ya hao punda, naye Yesu akaketi juu yake. |
| BSB 8 A massive crowd spread their cloaks on the road, while others cut branches from the trees and spread them on the road. | SWKCV 8 Umati mkubwa wa watu ukatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakakata matawi kutoka kwenye miti, wakayatandaza barabarani. |
| BSB 9 The crowds that went ahead of Him and those that followed were shouting: “Hosanna to the Son of David!” “Blessed is He who comes in the name of the Lord!” “Hosanna in the highest!” | SWKCV 9 Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema, “Hosana, Mwana wa Daudi!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Hosana juu mbinguni!” |
| BSB 10 When Jesus had entered Jerusalem, the whole city was stirred and asked, “Who is this?” | SWKCV 10 Yesu alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakauliza, “Huyu ni nani?” |
| BSB 11 The crowds replied, “This is Jesus, the prophet from Nazareth in Galilee.” | SWKCV 11 Ule umati wa watu ukajibu, “Huyu ni Yesu, yule nabii kutoka Nazareti katika Galilaya.” |
| BSB 12 Then Jesus entered the temple courts and drove out all who were buying and selling there. He overturned the tables of the money changers and the seats of those selling doves. | SWKCV 12 Yesu akaingia katika eneo la Hekalu na kuwafukuza wote waliokuwa wakinunua na kuuza vitu Hekaluni. Akazipindua meza za wale waliokuwa wakibadilisha fedha, na pia viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. |
| BSB 13 And He declared to them, “It is written: ‘My house will be called a house of prayer.’ But you are making it ‘a den of robbers.’” | SWKCV 13 Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyangʼanyi.” |
| BSB 14 The blind and the lame came to Him at the temple, and He healed them. | SWKCV 14 Vipofu na vilema wakamwendea kule Hekaluni, naye akawaponya. |
| BSB 15 But the chief priests and scribes were indignant when they saw the wonders He performed and the children shouting in the temple courts, “Hosanna to the Son of David!” | SWKCV 15 Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika. |
| BSB 16 “Do You hear what these children are saying?” they asked. “Yes,” Jesus answered. “Have you never read: ‘From the mouths of children and infants You have ordained praise’?” | SWKCV 16 Wakamuuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa’?” |
| BSB 17 Then He left them and went out of the city to Bethany, where He spent the night. | SWKCV 17 Akawaacha, akatoka nje ya mji, akaenda hadi Bethania, akalala huko. |
| BSB 18 In the morning, as Jesus was returning to the city, He was hungry. | SWKCV 18 Asubuhi na mapema, Yesu alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa. |
| BSB 19 Seeing a fig tree by the road, He went up to it but found nothing on it except leaves. “May you never bear fruit again!” He said. And immediately the tree withered. | SWKCV 19 Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka. |
| BSB 20 When the disciples saw this, they marveled and asked, “How did the fig tree wither so quickly?” | SWKCV 20 Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, “Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?” |
| BSB 21 “Truly I tell you,” Jesus replied, “if you have faith and do not doubt, not only will you do what was done to the fig tree, but even if you say to this mountain, ‘Be lifted up and thrown into the sea,’ it will happen. | SWKCV 21 Yesu akawajibu, “Amin, nawaambia, kama mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ngʼoka, ukatupwe baharini,’ litafanyika. |
| BSB 22 If you believe, you will receive whatever you ask for in prayer.” | SWKCV 22 Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.” |
| BSB 23 When Jesus returned to the temple courts and began to teach, the chief priests and elders of the people came up to Him. “By what authority are You doing these things?” they asked. “And who gave You this authority?” | SWKCV 23 Yesu alipoingia Hekaluni, viongozi wa makuhani na wazee wa watu wakamjia alipokuwa anafundisha na kusema, “Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Na ni nani aliyekupa mamlaka hayo?” |
| BSB 24 “I will also ask you one question,” Jesus replied, “and if you answer Me, I will tell you by what authority I am doing these things. | SWKCV 24 Yesu akawajibu, “Nami nitawauliza swali moja. Kama mkinijibu, nami nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. |
| BSB 25 What was the source of John’s baptism? Was it from heaven or from men?” They deliberated among themselves and said, “If we say, ‘From heaven,’ He will ask, ‘Why then did you not believe him?’ | SWKCV 25 Ubatizo wa Yohana, ulitoka wapi? Je, ulitoka mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wao kwa wao na kusema, “Tukisema ulitoka mbinguni atatuuliza, ‘Mbona basi hamkumwamini?’ |
| BSB 26 But if we say, ‘From men,’ we are afraid of the people, for they all regard John as a prophet.” | SWKCV 26 Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii.” |
| BSB 27 So they answered, “We do not know.” And Jesus replied, “Neither will I tell you by what authority I am doing these things. | SWKCV 27 Kwa hiyo wakamjibu Yesu, “Sisi hatujui.” Naye akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani ninatenda mambo haya.” |
| BSB 28 But what do you think? There was a man who had two sons. He went to the first one and said, ‘Son, go and work today in the vineyard.’ | SWKCV 28 “Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na wana wawili. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ |
| BSB 29 ‘I will not,’ he replied. But later he changed his mind and went. | SWKCV 29 “Yule mwanawe akamjibu ‘Mimi sitakwenda.’ Baadaye akabadili mawazo yake akaenda. |
| BSB 30 Then the man went to the second son and told him the same thing. ‘I will, sir,’ he said. But he did not go. | SWKCV 30 “Kisha yule baba akamwendea yule mwanawe mwingine akamwambia vilevile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda, bwana,’ lakini hakwenda. |
| BSB 31 Which of the two did the will of his father?” “The first,” they answered. Jesus said to them, “Truly I tell you, the tax collectors and prostitutes are entering the kingdom of God before you. | SWKCV 31 “Ni yupi kati yao hao wawili aliyetimiza kile alichotaka baba yake?” Wakamjibu, “Ni yule wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu. |
| BSB 32 For John came to you in the way of righteousness, and you did not believe him, but the tax collectors and prostitutes did. And even after you saw this, you did not repent and believe him. | SWKCV 32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki. |
| BSB 33 Listen to another parable: There was a landowner who planted a vineyard. He put a wall around it, dug a winepress in it, and built a tower. Then he rented it out to some tenants and went away on a journey. | SWKCV 33 “Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo ndani yake na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri kwenda nchi nyingine. |
| BSB 34 When the harvest time drew near, he sent his servants to the tenants to collect his share of the fruit. | SWKCV 34 Wakati wa mavuno ulipokaribia, akawatuma watumishi wake kwa hao wapangaji ili kukusanya matunda yake. |
| BSB 35 But the tenants seized his servants. They beat one, killed another, and stoned a third. | SWKCV 35 “Wale wapangaji wakawakamata wale watumishi, wakampiga mmoja, wakamuua mwingine, na yule wa tatu wakampiga mawe. |
| BSB 36 Again, he sent other servants, more than the first group. But the tenants did the same to them. | SWKCV 36 Kisha akawatuma kwao watumishi wengine, wengi kuliko wale wa kwanza, nao wale wapangaji wakawatendea vilevile. |
| BSB 37 Finally, he sent his son to them. ‘They will respect my son,’ he said. | SWKCV 37 Mwisho wa yote, akamtuma mwanawe kwao, akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’ |
| BSB 38 But when the tenants saw the son, they said to one another, ‘This is the heir. Come, let us kill him and take his inheritance.’ | SWKCV 38 “Lakini wale wapangaji walipomwona mwanawe, wakasemezana wao kwa wao, ‘Huyu ndiye mrithi. Njooni tumuue, ili tuchukue urithi wake.’ |
| BSB 39 So they seized him and threw him out of the vineyard and killed him. | SWKCV 39 Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu, wakamuua. |
| BSB 40 Therefore, when the owner of the vineyard returns, what will he do to those tenants?” | SWKCV 40 “Kwa hiyo, huyo mwenye shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanyia nini hao wakulima?” |
| BSB 41 “He will bring those wretches to a wretched end,” they replied, “and will rent out the vineyard to other tenants who will give him his share of the fruit at harvest time.” | SWKCV 41 Wakamjibu, “Kwa huzuni kuu atawaangamiza kabisa hao wadhalimu na kulipangisha shamba lake la mizabibu kwa wakulima wengine ambao watampatia fungu lake la matunda wakati wa mavuno.” |
| BSB 42 Jesus said to them, “Have you never read in the Scriptures: ‘The stone the builders rejected has become the cornerstone. This is from the Lord, and it is marvelous in our eyes’? | SWKCV 42 Yesu akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko kwamba: “ ‘Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni. Bwana ndiye alitenda jambo hili, nalo ni la ajabu machoni petu’? |
| BSB 43 Therefore I tell you that the kingdom of God will be taken away from you and given to a people who will produce its fruit. | SWKCV 43 “Kwa hiyo ninawaambia, Ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu na kupewa watu wengine wawezao kuzaa matunda yake. |
| BSB 44 He who falls on this stone will be broken to pieces, but he on whom it falls will be crushed.” | SWKCV 44 Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.” |
| BSB 45 When the chief priests and Pharisees heard His parables, they knew that Jesus was speaking about them. | SWKCV 45 Viongozi wa Makuhani na Mafarisayo waliposikia mifano ya Yesu, walitambua kuwa alikuwa akiwasema wao. |
| BSB 46 Although they wanted to arrest Him, they were afraid of the crowds, because the people regarded Him as a prophet. | SWKCV 46 Wakatafuta njia ya kumkamata, lakini wakaogopa umati wa watu, kwa kuwa watu walimwona Yesu kuwa ni nabii. |
Questions about Matthew 21? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.