Romans 16
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 I commend to you our sister Phoebe, a servant of the church in Cenchrea. | SWKCV 1 Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea. |
| BSB 2 Welcome her in the Lord in a manner worthy of the saints, and assist her with anything she may need from you. For she has been a great help to many people, including me. | SWKCV 2 Naomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao. |
| BSB 3 Greet Prisca and Aquila, my fellow workers in Christ Jesus, | SWKCV 3 Wasalimuni Prisila na Akila, watumishi wenzangu katika Kristo Yesu. |
| BSB 4 who have risked their lives for me. Not only I but all the churches of the Gentiles are grateful to them. | SWKCV 4 Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu; wala si mimi tu ninayewashukuru bali pia makanisa yote ya watu wa Mataifa. |
| BSB 5 Greet also the church that meets at their house. Greet my beloved Epenetus, who was the first convert to Christ in the province of Asia. | SWKCV 5 Lisalimuni pia kanisa linalokutana nyumbani mwao. Msalimuni rafiki yangu mpendwa Epaineto, aliyekuwa mtu wa kwanza kumwamini Kristo huko Asia. |
| BSB 6 Greet Mary, who has worked very hard for you. | SWKCV 6 Msalimuni Maria, aliyefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu. |
| BSB 7 Greet Andronicus and Junia, my fellow countrymen and fellow prisoners. They are outstanding among the apostles, and they were in Christ before I was. | SWKCV 7 Wasalimuni Androniko na Yunia, jamaa zangu ambao wamekuwa gerezani pamoja nami. Wao ni maarufu miongoni mwa mitume, nao walikuwa katika Kristo kabla yangu. |
| BSB 8 Greet Ampliatus, my beloved in the Lord. | SWKCV 8 Msalimuni Ampliato, yeye nimpendaye katika Bwana. |
| BSB 9 Greet Urbanus, our fellow worker in Christ, and my beloved Stachys. | SWKCV 9 Msalimuni Urbano, mtendakazi mwenzetu katika Kristo, pamoja na rafiki yangu mpendwa Stakisi. |
| BSB 10 Greet Apelles, who is approved in Christ. Greet those who belong to the household of Aristobulus. | SWKCV 10 Msalimuni Apele aliyejaribiwa na akaithibitisha imani yake katika Kristo. Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Aristobulo. |
| BSB 11 Greet Herodion, my fellow countryman. Greet those from the household of Narcissus who are in the Lord. | SWKCV 11 Msalimuni ndugu yangu Herodioni. Wasalimuni wote walio nyumbani mwa Narkisi walio katika Bwana. |
| BSB 12 Greet Tryphena and Tryphosa, women who have worked hard in the Lord. Greet my beloved Persis, who has worked very hard in the Lord. | SWKCV 12 Wasalimuni Trifaina na Trifosa, wale wanawake wanaofanya kazi kwa bidii katika Bwana. Msalimuni rafiki yangu mpendwa Persisi, mwanamke mwingine aliyefanya kazi kwa bidii katika Bwana. |
| BSB 13 Greet Rufus, chosen in the Lord, and his mother, who has been a mother to me as well. | SWKCV 13 Msalimuni Rufo, mteule katika Bwana, pamoja na mama yake, ambaye amekuwa mama kwangu pia. |
| BSB 14 Greet Asyncritus, Phlegon, Hermes, Patrobas, Hermas, and the brothers with them. | SWKCV 14 Wasalimuni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao. |
| BSB 15 Greet Philologus and Julia, Nereus and his sister, and Olympas and all the saints with them. | SWKCV 15 Wasalimuni Filologo, Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa na watakatifu wote walio pamoja nao. |
| BSB 16 Greet one another with a holy kiss. All the churches of Christ send you greetings. | SWKCV 16 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yanawasalimu. |
| BSB 17 Now I urge you, brothers, to watch out for those who create divisions and obstacles that are contrary to the teaching you have learned. Turn away from them. | SWKCV 17 Ndugu zangu, nawasihi mjihadhari na kujiepusha na wale watu waletao matengano na kuweka vikwazo mbele yenu dhidi ya mafundisho mliyojifunza. |
| BSB 18 For such people are not serving our Lord Christ, but their own appetites. By smooth talk and flattery they deceive the hearts of the naive. | SWKCV 18 Kwa maana watu kama hao hawamtumikii Bwana Kristo, bali wanatumikia tamaa zao wenyewe. Kwa kutumia maneno laini na ya kubembeleza, hupotosha mioyo ya watu wajinga. |
| BSB 19 Everyone has heard about your obedience, so I rejoice over you. But I want you to be wise about what is good and innocent about what is evil. | SWKCV 19 Kila mtu amesikia juu ya utii wenu, nami nimejawa na furaha tele kwa ajili yenu. Lakini nataka mwe na hekima katika mambo mema na bila hatia katika mambo maovu. |
| BSB 20 The God of peace will soon crush Satan under your feet. The grace of our Lord Jesus Christ be with you. | SWKCV 20 Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu iwe nanyi. Amen. |
| BSB 21 Timothy, my fellow worker, sends you greetings, as do Lucius, Jason, and Sosipater, my fellow countrymen. | SWKCV 21 Timotheo, mtendakazi mwenzangu anawasalimu. Vivyo hivyo Lukio, Yasoni, na Sosipatro, ndugu zangu. |
| BSB 22 I, Tertius, who wrote down this letter, greet you in the Lord. | SWKCV 22 Mimi, Tertio, niliye mwandishi wa waraka huu, nawasalimu katika Bwana. |
| BSB 23 Gaius, who has hosted me and all the church, sends you greetings. Erastus, the city treasurer, sends you greetings, as does our brother Quartus. | SWKCV 23 Gayo, ambaye ni mwenyeji wangu na wa kanisa lote, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto ndugu yetu pia wanawasalimu. [ |
| BSB | SWKCV 24 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amen.] |
| BSB 25 Now to Him who is able to strengthen you by my gospel and by the proclamation of Jesus Christ, according to the revelation of the mystery concealed for ages past | SWKCV 25 Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale. |
| BSB 26 but now revealed and made known through the writings of the prophets by the command of the eternal God, in order to lead all nations to the obedience that comes from faith— | SWKCV 26 Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii |
| BSB 27 to the only wise God be glory forever through Jesus Christ! Amen. | SWKCV 27 Mungu aliye pekee, mwenye hekima, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo utukufu ni wake milele na milele! Amen. |
Questions about Romans 16? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.