Song of Solomon 3
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 On my bed at night I sought the one I love; I sought him, but did not find him. | SWKCV 1 Usiku kucha kwenye kitanda changu nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata. |
| BSB 2 I will arise now and go about the city, through the streets and squares. I will seek the one I love. So I sought him but did not find him. | SWKCV 2 Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, katika barabara zake na viwanja; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata. |
| BSB 3 I encountered the watchmen on their rounds of the city: “Have you seen the one I love?” | SWKCV 3 Walinzi walinikuta walipokuwa wakizunguka mji. Nikawauliza, “Je, mmemwona yule moyo wangu umpendaye?” |
| BSB 4 I had just passed them when I found the one I love. I held him and would not let go until I had brought him to my mother’s house, to the chamber of the one who conceived me. | SWKCV 4 Kitambo kidogo tu baada ya kuwapita nilimpata yule moyo wangu umpendaye. Nilimshika na sikumwachia aende mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu, katika chumba cha yule aliyenichukua mimba. |
| BSB 5 O daughters of Jerusalem, I adjure you by the gazelles and does of the field: Do not arouse or awaken love until the time is right. | SWKCV 5 Binti za Yerusalemu, ninawaagiza kwa paa na kwa ayala wa shambani: Msichochee wala kuamsha mapenzi hata yatakapotaka yenyewe. |
| BSB 6 Who is this coming up from the wilderness like a column of smoke, scented with myrrh and frankincense from all the spices of the merchant? | SWKCV 6 Ni nani huyu anayekuja kutoka jangwani kama nguzo ya moshi, anayenukia manemane na uvumba iliyotengenezwa kwa vikolezo vyote vya mfanyabiashara? |
| BSB 7 Behold, it is Solomon’s carriage, escorted by sixty of the mightiest men of Israel. | SWKCV 7 Tazama! Ni gari la Solomoni lisindikizwalo na mashujaa sitini, walio wakuu sana wa Israeli, |
| BSB 8 All are skilled with the sword, experienced in warfare. Each has his sword at his side prepared for the terror of the night. | SWKCV 8 wote wamevaa panga, wote wazoefu katika vita, kila mmoja na upanga wake pajani, wamejiandaa kwa ajili ya hofu za usiku. |
| BSB 9 King Solomon has made his carriage out of the timber of Lebanon. | SWKCV 9 Mfalme Solomoni alijitengenezea gari; alilitengeneza kwa mbao kutoka Lebanoni. |
| BSB 10 He has made its posts of silver, its base of gold, its seat of purple fabric. Its interior is inlaid with love by the daughters of Jerusalem. | SWKCV 10 Nguzo zake alizitengeneza kwa fedha, kitako chake kwa dhahabu. Kiti chake kilipambwa kwa zambarau, gari lake likanakshiwa njumu kwa upendo na binti za Yerusalemu. |
| BSB 11 Come out, O daughters of Zion, and gaze at King Solomon, wearing the crown with which his mother crowned him on the day of his wedding—the day of his heart’s rejoicing. | SWKCV 11 Tokeni nje, ninyi binti za Sayuni, mkamtazame Mfalme Solomoni akiwa amevaa taji, taji ambalo mama yake alimvika siku ya arusi yake, siku ambayo moyo wake ulishangilia. |
Questions about Song of Solomon 3? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.