Song of Solomon 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 I have come to my garden, my sister, my bride; I have gathered my myrrh with my spice. I have eaten my honeycomb with my honey; I have drunk my wine with my milk. Eat, O friends, and drink; drink freely, O beloved. | SWKCV 1 Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni, enyi marafiki, mnywe; kunyweni ya kutosha, ee wapenzi. |
| BSB 2 I sleep, but my heart is awake. A sound! My beloved is knocking: “Open to me, my sister, my darling, my dove, my flawless one. My head is drenched with dew, my hair with the dampness of the night.” | SWKCV 2 Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho. Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha: “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, asiye na hitilafu. Kichwa changu kimeloa umande, na nywele zangu manyunyu ya usiku.” |
| BSB 3 I have taken off my robe—must I put it back on? I have washed my feet—must I soil them again? | SWKCV 3 Nimevua joho langu: je, ni lazima nivae tena? Nimenawa miguu yangu: je, ni lazima niichafue tena? |
| BSB 4 My beloved put his hand to the latch; my heart pounded for him. | SWKCV 4 Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo; moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake. |
| BSB 5 I rose up to open for my beloved. My hands dripped with myrrh, my fingers with flowing myrrh on the handles of the bolt. | SWKCV 5 Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu, mikono yangu ikidondosha manemane, vidole vyangu vikitiririka manemane, penye vipini vya komeo. |
| BSB 6 I opened for my beloved, but he had turned and gone. My heart sank at his departure. I sought him but did not find him. I called, but he did not answer. | SWKCV 6 Nilimfungulia mpenzi wangu, lakini mpenzi wangu alishaondoka; alikuwa amekwenda zake. Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake. Nilimtafuta lakini sikumpata. Nilimwita lakini hakunijibu. |
| BSB 7 I encountered the watchmen on their rounds of the city. They beat me and bruised me; they took away my cloak, those guardians of the walls. | SWKCV 7 Walinzi walinikuta walipokuwa wakifanya zamu za ulinzi mjini. Walinipiga, wakanijeruhi, wakaninyangʼanya joho langu, hao walinzi wa kuta! |
| BSB 8 O daughters of Jerusalem, I adjure you, if you find my beloved, tell him I am sick with love. | SWKCV 8 Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza: kama mkimpata mpenzi wangu, mtamwambia nini? Mwambieni ninazimia kwa mapenzi. |
| BSB 9 How is your beloved better than others, O most beautiful among women? How is your beloved better than another, that you charge us so? | SWKCV 9 Je, mpendwa wako ni bora kuliko wengine namna gani, wewe uliye mzuri kupita wanawake wote? Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani, hata unatuagiza hivyo? |
| BSB 10 My beloved is dazzling and ruddy, outstanding among ten thousand. | SWKCV 10 Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu, wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu. |
| BSB 11 His head is purest gold; his hair is wavy and black as a raven. | SWKCV 11 Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote, nywele zake ni za mawimbi na ni nyeusi kama kunguru. |
| BSB 12 His eyes are like doves beside the streams of water, bathed in milk and mounted like jewels. | SWKCV 12 Macho yake ni kama ya hua kandokando ya vijito vya maji, aliyeogeshwa kwenye maziwa, yaliyopangwa kama vito vya thamani. |
| BSB 13 His cheeks are like beds of spice, towers of perfume. His lips are like lilies, dripping with flowing myrrh. | SWKCV 13 Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezo yakitoa manukato. Midomo yake ni kama yungiyungi inayodondosha manemane. |
| BSB 14 His arms are rods of gold set with beryl. His body is polished ivory bedecked with sapphires. | SWKCV 14 Mikono yake ni fimbo za dhahabu iliyopambwa kwa krisolitho. Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyongʼarishwa iliyopambwa na yakuti samawi. |
| BSB 15 His legs are pillars of marble set on bases of pure gold. His appearance is like Lebanon, as majestic as the cedars. | SWKCV 15 Miguu yake ni nguzo za marmar zilizosimikwa katika vitako vya dhahabu safi. Sura yake ni kama Lebanoni, bora kama miti yake ya mierezi. |
| BSB 16 His mouth is most sweet; he is altogether lovely. This is my beloved, and this is my friend, O daughters of Jerusalem. | SWKCV 16 Kinywa chake chenyewe ni utamu, kwa ujumla yeye ni wa kupendeza. Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu, ee binti za Yerusalemu. |
Questions about Song of Solomon 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.