1 Chronicles 10
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now the Philistines fought against Israel, and the men of Israel fled before them, and many fell slain on Mount Gilboa. | SWKCV 1 Basi Wafilisti wakapigana na Israeli. Waisraeli wakawakimbia, na wengi wakauawa katika mlima Gilboa. |
| BSB 2 The Philistines followed hard after Saul and his sons, and they killed Saul’s sons Jonathan, Abinadab, and Malchishua. | SWKCV 2 Wafilisti wakawafuatia kwa bidii Sauli na wanawe, wakawaua Yonathani, Abinadabu na Malki-Shua. |
| BSB 3 When the battle intensified against Saul, the archers overtook him and wounded him. | SWKCV 3 Mapigano yakawa makali kumzunguka Sauli na wakati wapiga mishale walipompata, wakamjeruhi. |
| BSB 4 Then Saul said to his armor-bearer, “Draw your sword and run me through with it, or these uncircumcised men will come and torture me!” But his armor-bearer was terrified and refused to do it. So Saul took his own sword and fell on it. | SWKCV 4 Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Futa upanga wako unichome nao, la sivyo hawa watu wasiotahiriwa watakuja na kunidhalilisha.” Lakini mbeba silaha wake akaogopa sana wala hakuweza kufanya hivyo. Kwa hiyo Sauli akachukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia. |
| BSB 5 When his armor-bearer saw that Saul was dead, he too fell on his own sword and died. | SWKCV 5 Mbeba silaha wake alipoona kwamba Sauli amekufa, naye pia akauangukia upanga wake akafa. |
| BSB 6 So Saul died together with his three sons and all his house. | SWKCV 6 Kwa hiyo Sauli na wanawe watatu wakafa, pamoja na nyumba yake yote. |
| BSB 7 When all the Israelites in the valley saw that the army had fled and that Saul and his sons had died, they abandoned their cities and ran away. So the Philistines came and occupied their cities. | SWKCV 7 Waisraeli wote waliokuwa bondeni walipoona kwamba jeshi limekimbia na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliacha miji yao wakakimbia. Nao Wafilisti wakaja na kukaa humo. |
| BSB 8 The next day, when the Philistines came to strip the dead, they found Saul and his sons fallen on Mount Gilboa. | SWKCV 8 Kesho yake Wafilisti walipokuja kuwavua maiti silaha, walimkuta Sauli na wanawe wameanguka katika Mlima Gilboa. |
| BSB 9 They stripped Saul, cut off his head, took his armor, and sent messengers throughout the land of the Philistines to proclaim the news in the temple of their idols and among their people. | SWKCV 9 Wakamvua mavazi, wakachukua kichwa chake pamoja na silaha zake, wakawatuma wajumbe katika nchi yote ya Wafilisti kutangaza habari hizi miongoni mwa sanamu zao na watu wao. |
| BSB 10 They put his armor in the temple of their gods and hung his head in the temple of Dagon. | SWKCV 10 Waliweka silaha zake katika hekalu la miungu yao, wakatundika kichwa chake katika hekalu la Dagoni. |
| BSB 11 When all the people of Jabesh-gilead heard about everything the Philistines had done to Saul, | SWKCV 11 Wakazi wote wa Yabeshi-Gileadi waliposikia yote Wafilisti waliyomtendea Sauli, |
| BSB 12 all their men of valor set out and retrieved the bodies of Saul and his sons and brought them to Jabesh. And they buried their bones under the oak in Jabesh and fasted seven days. | SWKCV 12 mashujaa wao wote wakaondoka, wakautwaa mwili wa Sauli na miili ya wanawe, wakaileta Yabeshi. Wakaizika mifupa yao chini ya mti mkubwa huko Yabeshi, nao wakafunga kwa siku saba. |
| BSB 13 So Saul died for his unfaithfulness to the LORD, because he did not keep the word of the LORD and even consulted a medium for guidance, | SWKCV 13 Sauli alikufa kwa sababu hakuwa mwaminifu kwa Bwana. Hakulishika neno la Bwana, hata akataka shauri kwa mwaguzi kwa ajili ya uongozi, |
| BSB 14 and he failed to inquire of the LORD. So the LORD put him to death and turned the kingdom over to David son of Jesse. | SWKCV 14 hakumuuliza Bwana. Kwa hiyo Bwana alimuua, na ufalme akampa Daudi mwana wa Yese. |
Questions about 1 Chronicles 10? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.