1 Chronicles 11
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then all Israel came together to David at Hebron and said, “Here we are, your own flesh and blood. | SWKCV 1 Israeli yote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni wakamwambia, “Sisi ni nyama yako na damu yako. |
| BSB 2 Even in times past, while Saul was king, you were the one who led Israel out and brought them back. And the LORD your God said, ‘You will shepherd My people Israel, and you will be ruler over them.’” | SWKCV 2 Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Bwana Mungu wako alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’” |
| BSB 3 So all the elders of Israel came to the king at Hebron, where David made a covenant with them before the LORD. And they anointed him king over Israel, according to the word of the LORD through Samuel. | SWKCV 3 Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Bwana, nao wakamtia Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na Bwana alivyoahidi kupitia kwa Samweli. |
| BSB 4 Then David and all the Israelites marched to Jerusalem (that is, Jebus), where the Jebusites inhabited the land. | SWKCV 4 Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo |
| BSB 5 The people of Jebus said to David, “You will never get in here.” Nevertheless, David captured the fortress of Zion (that is, the City of David). | SWKCV 5 wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi. |
| BSB 6 Now David had said, “Whoever is the first to strike down a Jebusite will become chief commander.” And Joab son of Zeruiah went up first, and he became the chief. | SWKCV 6 Daudi alikuwa amesema, “Yeyote aongozaye mashambulizi dhidi ya Wayebusi, atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu. |
| BSB 7 So David took up residence in the fortress; that is why it was called the City of David. | SWKCV 7 Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi. |
| BSB 8 He built up the city around it, from the supporting terraces to the surrounding wall, while Joab restored the rest of the city. | SWKCV 8 Akajenga mji pande zote, kuanzia kwenye mito hadi kwenye ukuta kuzunguka, wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu. |
| BSB 9 And David became greater and greater, for the LORD of Hosts was with him. | SWKCV 9 Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote alikuwa pamoja naye. |
| BSB 10 Now these were the chiefs of David’s mighty men, who, together with all Israel, bolstered and strengthened his kingdom, according to the word of the LORD concerning Israel. | SWKCV 10 Hawa ndio waliokuwa wakuu wa mashujaa wa Daudi: wao pamoja na Israeli wote wakauimarisha ufalme wake ili kuenea katika nchi yote, kama Bwana alivyoahidi. |
| BSB 11 This is the list of David’s mighty men: Jashobeam son of Hachmoni was chief of the officers; he wielded his spear against three hundred men, whom he killed at one time. | SWKCV 11 Hii ndio orodha ya mashujaa wa Daudi: Yashobeamu, Mhakmoni, alikuwa mkuu wa maafisa; yeye aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua katika pambano moja. |
| BSB 12 Next in command was Eleazar son of Dodo the Ahohite, one of the three mighty men. | SWKCV 12 Aliyefuata alikuwa Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu. |
| BSB 13 He was with David at Pas-dammim when the Philistines gathered there for battle. At a place with a field full of barley, the troops fled from the Philistines. | SWKCV 13 Huyo alikuwa pamoja na Daudi huko Pas-Damimu, wakati Wafilisti walikusanyika huko kwa ajili ya vita. Huko ambapo kulikuwa na shamba lililokuwa limejaa shayiri, vikosi vya Israeli vikawakimbia Wafilisti. |
| BSB 14 But Eleazar and David stationed themselves in the middle of the field and defended it. They struck down the Philistines, and the LORD brought about a great victory. | SWKCV 14 Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa. |
| BSB 15 Three of the thirty chief men went down to David, to the rock at the cave of Adullam, while a company of Philistines was encamped in the Valley of Rephaim. | SWKCV 15 Wakuu watatu miongoni mwa wale thelathini, walimwendea Daudi katika mwamba huko kwenye pango la Adulamu, wakati kikundi cha Wafilisti kilikuwa kimepiga kambi katika Bonde la Warefai. |
| BSB 16 At that time David was in the stronghold, and the garrison of the Philistines was at Bethlehem. | SWKCV 16 Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome, na kambi ya Wafilisti ilikuwa huko Bethlehemu. |
| BSB 17 David longed for water and said, “Oh, that someone would get me a drink of water from the well near the gate of Bethlehem!” | SWKCV 17 Daudi akatamani maji, akasema, “Laiti mtu angenipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilichoko karibu na lango la Bethlehemu!” |
| BSB 18 So the Three broke through the Philistine camp, drew water from the well at the gate of Bethlehem, and brought it back to David. But he refused to drink it; instead, he poured it out to the LORD, | SWKCV 18 Kwa hivyo wale watatu, wakapita katikati ya safu za Wafilisti, wakachota maji kutoka kwa kisima kilicho karibu na lango la Bethlehemu, wakamletea Daudi. Lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake, aliyamimina mbele za Bwana. |
| BSB 19 saying, “Far be it from me, my God, to do this! How can I drink the blood of these men who risked their lives?” Because they had brought it at the risk of their lives, David refused to drink it. Such were the exploits of the three mighty men. | SWKCV 19 Akasema, “Mungu apishie mbali kwamba nifanye hivi! Je kweli, niinywe damu ya watu hawa waliohatarisha maisha yao?” Kwa sababu walihatarisha maisha yao kuyaleta yale maji, Daudi hakukubali kuyanywa. Huo ndio uliokuwa ujasiri wa wale mashujaa watatu. |
| BSB 20 Now Abishai, the brother of Joab, was chief of the Three, and he wielded his spear against three hundred men, killed them, and won a name along with the Three. | SWKCV 20 Abishai, ndugu yake Yoabu ndiye alikuwa kiongozi wa hao Watatu. Aliinua mkuki wake dhidi ya watu 300, ambao aliwaua, kwa hiyo naye akawa na sifa kama hao Watatu. |
| BSB 21 He was doubly honored above the Three, and he became their commander, even though he was not included among the Three. | SWKCV 21 Alitunukiwa heshima maradufu ya wale Watatu, akawa jemadari wao, ingawa hakuhesabiwa miongoni mwao. |
| BSB 22 And Benaiah son of Jehoiada was a man of valor from Kabzeel, a man of many exploits. He struck down two champions of Moab, and on a snowy day he went down into a pit and killed a lion. | SWKCV 22 Benaya, mwana wa Yehoyada alikuwa mpiganaji hodari kutoka Kabseeli ambaye alifanya mambo makubwa ya ujasiri. Aliwaua mashujaa wawili waliokuwa hodari kuliko wote wa Moabu. Pia alishuka shimoni kulipokuwa na theluji na kumuua simba. |
| BSB 23 He also struck down an Egyptian, a huge man five cubits tall. Although the Egyptian had a spear like a weaver’s beam in his hand, Benaiah went against him with a club, snatched the spear from his hand, and killed the Egyptian with his own spear. | SWKCV 23 Alimuua Mmisri aliyekuwa na urefu kama dhiraa tano. Ingawa Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi mwake, Benaya alimwendea na rungu. Akamnyangʼanya Mmisri mkuki wake na kumuua nao. |
| BSB 24 These were the exploits of Benaiah son of Jehoiada, who won a name along with the three mighty men. | SWKCV 24 Haya yalikuwa mambo ya ushujaa ya Benaya mwana wa Yehoyada; naye pia alikuwa maarufu kama wale mashujaa watatu. |
| BSB 25 He was most honored among the Thirty, but he did not become one of the Three. And David appointed him over his guard. | SWKCV 25 Yeye aliheshimiwa zaidi ya wale Thelathini, lakini hakujumuishwa miongoni mwa wale Watatu: Daudi akamweka kuwa kiongozi wa walinzi wake. |
| BSB 26 Now these were the mighty men: Asahel the brother of Joab, Elhanan son of Dodo of Bethlehem, | SWKCV 26 Wale watu mashujaa walikuwa: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu, |
| BSB 27 Shammoth the Harorite, Helez the Pelonite, | SWKCV 27 Shamothi Mharori, Helesi Mpeloni, |
| BSB 28 Ira son of Ikkesh the Tekoite, Abiezer the Anathothite, | SWKCV 28 Ira mwana wa Ikeshi kutoka Tekoa, Abiezeri kutoka Anathothi, |
| BSB 29 Sibbecai the Hushathite, Ilai the Ahohite, | SWKCV 29 Sibekai Mhushathi, Ilai Mwahohi, |
| BSB 30 Maharai the Netophathite, Heled son of Baanah the Netophathite, | SWKCV 30 Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana, Mnetofathi, |
| BSB 31 Ithai son of Ribai from Gibeah of the Benjamites, Benaiah the Pirathonite, | SWKCV 31 Itai mwana wa Ribai kutoka Gibea ya Benyamini, Benaya Mpirathoni, |
| BSB 32 Hurai from the brooks of Gaash, Abiel the Arbathite, | SWKCV 32 Hurai kutoka mabonde ya Gaashi, Abieli Mwaribathi, |
| BSB 33 Azmaveth the Baharumite, Eliahba the Shaalbonite, | SWKCV 33 Azmawethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni, |
| BSB 34 the sons of Hashem the Gizonite, Jonathan son of Shagee the Hararite, | SWKCV 34 wana wa Hashemu Mgiloni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari, |
| BSB 35 Ahiam son of Sachar the Hararite, Eliphal son of Ur, | SWKCV 35 Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifale mwana wa Uru, |
| BSB 36 Hepher the Mecherathite, Ahijah the Pelonite, | SWKCV 36 Heferi Mmekerathi, Ahiya Mpeloni, |
| BSB 37 Hezro the Carmelite, Naarai son of Ezbai, | SWKCV 37 Hezro Mkarmeli, Naarai mwana wa Ezbai, |
| BSB 38 Joel the brother of Nathan, Mibhar son of Hagri, | SWKCV 38 Yoeli nduguye Nathani, Mibhari mwana wa Hagri, |
| BSB 39 Zelek the Ammonite, Naharai the Beerothite, the armor-bearer of Joab son of Zeruiah, | SWKCV 39 Seleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya, |
| BSB 40 Ira the Ithrite, Gareb the Ithrite, | SWKCV 40 Ira Mwithiri, Garebu Mwithiri, |
| BSB 41 Uriah the Hittite, Zabad son of Ahlai, | SWKCV 41 Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Alai, |
| BSB 42 Adina son of Shiza the Reubenite, chief of the Reubenites, and the thirty with him, | SWKCV 42 Adina mwana wa Shiza Mreubeni, ambaye alikuwa mkuu wa Wareubeni, akiwa pamoja na watu thelathini, |
| BSB 43 Hanan son of Maacah, Joshaphat the Mithnite, | SWKCV 43 Hanani mwana wa Maaka, Yoshafati Mmithni, |
| BSB 44 Uzzia the Ashterathite, Shama and Jeiel the sons of Hotham the Aroerite, | SWKCV 44 Uzia Mwashterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Mwaroeri, |
| BSB 45 Jediael son of Shimri and his brother Joha the Tizite, | SWKCV 45 Yediaeli mwana wa Shimri, nduguye Yoha Mtizi, |
| BSB 46 Eliel the Mahavite, Jeribai and Joshaviah, the sons of Elnaam, Ithmah the Moabite, | SWKCV 46 Elieli Mmahawi, Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, Ithma Mmoabu, |
| BSB 47 Eliel, Obed, and Jaasiel the Mezobaite. | SWKCV 47 Elieli, na Obedi na Yaasieli Mmesobai. |
Questions about 1 Chronicles 11? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.