1 Samuel 24
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 After Saul had returned from pursuing the Philistines, he was told, “David is in the wilderness of En-gedi.” | SWKCV 1 Baada ya Sauli kurudi kuwafuatia Wafilisti, akaambiwa kwamba, “Daudi yuko katika Jangwa la En-Gedi.” |
| BSB 2 So Saul took three thousand chosen men from all Israel and went to look for David and his men in the region of the Rocks of the Wild Goats. | SWKCV 2 Basi Sauli akachukua watu hodari 3,000 kutoka Israeli yote kwenda kumsaka Daudi na watu wake karibu na Majabali ya Mbuzi-Mwitu. |
| BSB 3 Soon Saul came to the sheepfolds along the road, where there was a cave, and he went in to relieve himself. And David and his men were hiding in the recesses of the cave. | SWKCV 3 Akaja mpaka kwenye mazizi ya kondoo kando ya njia, hapo palikuwa na pango, na Sauli akaingia ndani kujipumzisha. Daudi na watu wake walikuwa wamo mle pangoni kwa ndani zaidi. |
| BSB 4 So David’s men said to him, “This is the day about which the LORD said to you, ‘Behold, I will deliver your enemy into your hand, that you may do with him as you wish.’” Then David crept up and stealthily cut off a corner of Saul’s robe. | SWKCV 4 Watu wa Daudi wakasema, “Hii ndiyo siku aliyonena Bwana akikuambia, ‘Nitamtia adui yako mikononi mwako ili wewe umtendee utakavyo.’” Basi Daudi akanyemelea bila kuonekana na kukata upindo wa joho la Sauli. |
| BSB 5 Afterward, David’s conscience was stricken because he had cut off the corner of Saul’s robe. | SWKCV 5 Baada ya hilo, dhamiri ya Daudi ikataabika kwa kukata upindo wa joho la Sauli. |
| BSB 6 So he said to his men, “The LORD forbid that I should do such a thing to my master, the LORD’s anointed. May I never lift my hand against him, since he is the LORD’s anointed.” | SWKCV 6 Akawaambia watu wake, “Bwana na apishie mbali nisije nikafanya jambo kama hilo kwa bwana wangu, yeye ambaye ni mpakwa mafuta wa Bwana, au kuinua mkono wangu dhidi yake; kwani yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana.” |
| BSB 7 With these words David restrained his men, and he did not let them rise up against Saul. Then Saul left the cave and went on his way. | SWKCV 7 Kwa maneno haya Daudi akawaonya watu wake na hakuwaruhusu wamshambulie Sauli. Naye Sauli akaondoka pangoni na kwenda zake. |
| BSB 8 After that, David got up, went out of the cave, and called out to Saul, “My lord the king!” When Saul looked behind him, David bowed facedown in reverence | SWKCV 8 Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kusujudu uso wake mpaka nchi. |
| BSB 9 and said to Saul, “Why do you listen to the words of men who say, ‘Look, David intends to harm you’? | SWKCV 9 Akamwambia Sauli, “Kwa nini unasikiliza wakati watu wanapokuambia, ‘Daudi amenuia kukudhuru’? |
| BSB 10 Behold, this day you have seen with your own eyes that the LORD delivered you into my hand in the cave. I was told to kill you, but I spared you and said, ‘I will not lift my hand against my lord, since he is the LORD’s anointed.’ | SWKCV 10 Leo umeona kwa macho yako mwenyewe jinsi Bwana alivyokutia mikononi mwangu huko pangoni. Watu wengine walisisitiza nikuue, lakini nilikuacha, nikisema, ‘Sitainua mkono wangu dhidi ya bwana wangu, kwa sababu yeye ni mpakwa mafuta wa Bwana.’ |
| BSB 11 See, my father, look at the corner of your robe in my hand. For I cut it off, but I did not kill you. Know and see that there is no evil or rebellion in my hands. I have not sinned against you, even though you are hunting me down to take my life. | SWKCV 11 Tazama, baba yangu, ona kipande hiki cha joho lako mkononi mwangu! Nilikata upindo wa joho lako lakini sikukuua. Basi ujue na kutambua kuwa sina hatia ya kutenda mabaya wala ya kuasi. Wewe sijakukosea, lakini wewe unaniwinda mimi ili kuuondoa uhai wangu. |
| BSB 12 May the LORD judge between you and me, and may the LORD take vengeance on you, but my hand will never be against you. | SWKCV 12 Bwana na ahukumu kati yangu na wewe. Naye Bwana alipize mabaya unayonitendea, lakini mkono wangu hautakugusa. |
| BSB 13 As the old proverb says, ‘Wickedness proceeds from the wicked.’ But my hand will never be against you. | SWKCV 13 Kama msemo wa kale usemavyo, ‘Kutoka kwa watenda maovu hutoka matendo maovu,’ kwa hiyo mkono wangu hautakugusa wewe. |
| BSB 14 Against whom has the king of Israel come out? Whom are you pursuing? A dead dog? A flea? | SWKCV 14 “Je, mfalme wa Israeli ametoka dhidi ya nani? Ni nani unayemfuatia? Je, ni mbwa mfu? Ni kiroboto? |
| BSB 15 May the LORD be our judge and decide between you and me. May He take notice and plead my case and deliver me from your hand.” | SWKCV 15 Bwana na awe mwamuzi wetu, yeye na aamue kati yetu. Yeye na anitetee shauri langu; anihesabie haki kwa kuniokoa mkononi mwako.” |
| BSB 16 When David had finished saying these things, Saul called back, “Is that your voice, David my son?” Then Saul wept aloud | SWKCV 16 Daudi alipomaliza kusema haya, Sauli akamuuliza, “Je, hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?” Ndipo Sauli akalia kwa sauti kuu, akisema, |
| BSB 17 and said to David, “You are more righteous than I, for you have rewarded me with good, though I have rewarded you with evil. | SWKCV 17 “Wewe ni mwenye haki kuliko mimi; umenitendea mema, lakini mimi nimekutendea mabaya. |
| BSB 18 And you have declared this day how you have treated me well, for when the LORD delivered me into your hand, you did not kill me. | SWKCV 18 Sasa umeniambia juu ya mema uliyonitendea. Bwana alinitia mikononi mwako, lakini wewe hukuniua. |
| BSB 19 When a man finds his enemy, does he let him go away unharmed? May the LORD reward you with good for what you have done for me this day. | SWKCV 19 Je, mtu ampatapo adui yake, humwacha aende zake bila kumdhuru? Bwana na akulipe mema kwa jinsi ulivyonitenda leo. |
| BSB 20 Now I know for sure that you will be king and that the kingdom of Israel will be established in your hands. | SWKCV 20 Ninajua kwamba hakika utakuwa mfalme na ya kwamba ufalme wa Israeli utakuwa imara mikononi mwako. |
| BSB 21 So now, swear to me by the LORD that you will not cut off my descendants or wipe out my name from my father’s house.” | SWKCV 21 Sasa niapie kwa Bwana kwamba hutakatilia mbali uzao wangu wala kulifuta jina langu kutoka jamaa ya baba yangu.” |
| BSB 22 So David gave his oath to Saul. Then Saul returned home, but David and his men went up to the stronghold. | SWKCV 22 Basi Daudi akamwapia Sauli. Kisha Sauli akarudi zake nyumbani, lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni. |
Questions about 1 Samuel 24? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.