2 Corinthians 13
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 This is the third time I am coming to you. “Every matter must be established by the testimony of two or three witnesses.” | SWKCV 1 Hii ndiyo mara ya tatu mimi kuja kwenu. “Shtaka lolote lazima lithibitishwe na mashahidi wawili au watatu.” |
| BSB 2 I already warned you the second time I was with you. So now in my absence I warn those who sinned earlier and everyone else: If I return, I will not spare anyone, | SWKCV 2 Nimekwisha kuwaonya nilipokuwa pamoja nanyi mara ya pili. Sasa narudia wakati sipo, kwamba nikija tena sitawahurumia wale waliokuwa wametenda dhambi hapo awali na wengine wote, |
| BSB 3 since you are demanding proof that Christ is speaking through me. He is not weak in dealing with you but is powerful among you. | SWKCV 3 kwa kuwa mnadai uthibitisho kwamba Kristo anazungumza kwa kunitumia mimi. Yeye si dhaifu katika kushughulika nanyi, bali ana nguvu kati yenu. |
| BSB 4 For He was indeed crucified in weakness, yet He lives by God’s power. For we are also weak in Him, yet by God’s power we will live with Him concerning you. | SWKCV 4 Kwa kuwa alisulubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Vivyo hivyo, sisi tu dhaifu kupitia kwake, lakini katika kuwashughulikia ninyi tutaishi pamoja naye kwa nguvu za Mungu. |
| BSB 5 Examine yourselves to see whether you are in the faith; test yourselves. Do you not realize that Jesus Christ is in you—unless you fail the test? | SWKCV 5 Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi katika imani. Jipimeni wenyewe. Je, hamtambui ya kuwa Yesu Kristo yumo ndani yenu? Kama sivyo, basi, mmeshindwa kufikia kipimo hicho! |
| BSB 6 And I hope you will realize that we have not failed the test. | SWKCV 6 Natumaini mtaona kuwa sisi hatukushindwa. |
| BSB 7 Now we pray to God that you will not do anything wrong—not that we will appear to have stood the test, but that you will do what is right, even if we appear to have failed. | SWKCV 7 Lakini tunamwomba Mungu msije mkatenda kosa lolote, si ili sisi tuonekane kuwa tumeshinda hilo jaribio, bali ili ninyi mtende lililo haki, hata kama tutaonekana kuwa tumeshindwa. |
| BSB 8 For we cannot do anything against the truth, but only for the truth. | SWKCV 8 Kwa maana hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, bali kuithibitisha kweli tu. |
| BSB 9 In fact, we rejoice when we are weak but you are strong, and our prayer is for your perfection. | SWKCV 9 Tunafurahi wakati wowote sisi tunapokuwa dhaifu, lakini ninyi mkawa na nguvu. Nayo maombi yetu ni kwamba mpate kuwa wakamilifu. |
| BSB 10 This is why I write these things while absent, so that when I am present I will not need to be severe in my use of the authority that the Lord gave me for building you up, not for tearing you down. | SWKCV 10 Hii ndiyo sababu nawaandikia mambo haya wakati sipo, ili nikija nisiwe mkali katika kutumia mamlaka yangu, mamlaka Bwana aliyonipa ya kuwajenga ninyi wala si ya kuwabomoa. |
| BSB 11 Finally, brothers, rejoice! Aim for perfect harmony, encourage one another, be of one mind, live in peace. And the God of love and peace will be with you. | SWKCV 11 Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, mkafarijike, kuweni wa nia moja, kaeni kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. |
| BSB 12 Greet one another with a holy kiss. | SWKCV 12 Salimianeni ninyi kwa ninyi kwa busu takatifu. |
| BSB 13 All the saints send you greetings. | SWKCV 13 Watakatifu wote wanawasalimu. |
| BSB 14 The grace of the Lord Jesus Christ, and the love of God, and the fellowship of the Holy Spirit be with all of you. | SWKCV 14 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote. Amen. |
Questions about 2 Corinthians 13? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.