2 Corinthians 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 For we know that if the earthly tent we live in is dismantled, we have a building from God, an eternal house in heaven, not built by human hands. | SWKCV 1 Kwa maana twajua kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu. |
| BSB 2 For in this tent we groan, longing to be clothed with our heavenly dwelling, | SWKCV 2 Katika hema hii twalia kwa uchungu, tukitamani kuvikwa makao yetu ya mbinguni, |
| BSB 3 because when we are clothed, we will not be found naked. | SWKCV 3 kwa kuwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tena kuwa uchi. |
| BSB 4 For while we are in this tent, we groan under our burdens, because we do not wish to be unclothed but clothed, so that our mortality may be swallowed up by life. | SWKCV 4 Kwa kuwa tukiwa bado katika hema hii twalia kwa uchungu na kulemewa, kwa sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili kwamba kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima. |
| BSB 5 And it is God who has prepared us for this very purpose and has given us the Spirit as a pledge of what is to come. | SWKCV 5 Basi Mungu ndiye alitufanya kwa ajili ya jambo lilo hilo naye ametupa Roho Mtakatifu kuwa amana, akituhakikishia ahadi ya kile kijacho. |
| BSB 6 Therefore we are always confident, although we know that while we are at home in the body, we are away from the Lord. | SWKCV 6 Kwa hiyo siku zote tunalo tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana, |
| BSB 7 For we walk by faith, not by sight. | SWKCV 7 kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. |
| BSB 8 We are confident, then, and would prefer to be away from the body and at home with the Lord. | SWKCV 8 Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana. |
| BSB 9 So we aspire to please Him, whether we are at home in this body or away from it. | SWKCV 9 Kwa hiyo, kama tuko katika mwili huu au tuko mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana. |
| BSB 10 For we must all appear before the judgment seat of Christ, that each one may receive his due for the things done in the body, whether good or bad. | SWKCV 10 Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mmoja apate kulipwa kwa ajili ya yale ambayo yametendwa katika mwili wake, yakiwa mema au mabaya. |
| BSB 11 Therefore, since we know what it means to fear the Lord, we try to persuade men. What we are is clear to God, and I hope it is clear to your conscience as well. | SWKCV 11 Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Bwana, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia. |
| BSB 12 We are not commending ourselves to you again. Instead, we are giving you an occasion to be proud of us, so that you can answer those who take pride in appearances rather than in the heart. | SWKCV 12 Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu ya mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni. |
| BSB 13 If we are out of our mind, it is for God; if we are of sound mind, it is for you. | SWKCV 13 Kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu; kama tuna akili timamu, ni kwa ajili yenu. |
| BSB 14 For Christ’s love compels us, because we are convinced that One died for all, therefore all died. | SWKCV 14 Kwa kuwa upendo wa Kristo unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. |
| BSB 15 And He died for all, that those who live should no longer live for themselves, but for Him who died for them and was raised again. | SWKCV 15 Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili kwamba wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao. |
| BSB 16 So from now on we regard no one according to the flesh. Although we once regarded Christ in this way, we do so no longer. | SWKCV 16 Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu yeyote kwa mtazamo wa kibinadamu. Ingawa wakati fulani tulimwangalia Kristo kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena hivyo. |
| BSB 17 Therefore if anyone is in Christ, he is a new creation. The old has passed away. Behold, the new has come! | SWKCV 17 Kwa hiyo kama mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama, yamekuwa mapya. |
| BSB 18 All this is from God, who reconciled us to Himself through Christ and gave us the ministry of reconciliation: | SWKCV 18 Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kwa njia ya Yesu Kristo na kutupata sisi huduma ya upatanisho: |
| BSB 19 that God was reconciling the world to Himself in Christ, not counting men’s trespasses against them. And He has committed to us the message of reconciliation. | SWKCV 19 Kwamba Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. |
| BSB 20 Therefore we are ambassadors for Christ, as though God were making His appeal through us. We implore you on behalf of Christ: Be reconciled to God. | SWKCV 20 Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Kristo, mpatanishwe na Mungu. |
| BSB 21 God made Him who knew no sin to be sin on our behalf, so that in Him we might become the righteousness of God. | SWKCV 21 Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kwake yeye. |
Questions about 2 Corinthians 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.