2 Corinthians 6
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 As God’s fellow workers, then, we urge you not to receive God’s grace in vain. | SWKCV 1 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. |
| BSB 2 For He says: “In the time of favor I heard you, and in the day of salvation I helped you.” Behold, now is the time of favor; now is the day of salvation! | SWKCV 2 Kwa maana asema: “Wakati wangu uliokubalika nilikusikia, siku ya wokovu nilikusaidia.” Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa. |
| BSB 3 We put no obstacle in anyone’s way, so that no one can discredit our ministry. | SWKCV 3 Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama. |
| BSB 4 Rather, as servants of God we commend ourselves in every way: in great endurance; in troubles, hardships, and calamities; | SWKCV 4 Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida; |
| BSB 5 in beatings, imprisonments, and riots; in labor, sleepless nights, and hunger; | SWKCV 5 katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga; |
| BSB 6 in purity, knowledge, patience, and kindness; in the Holy Spirit and in sincere love; | SWKCV 6 katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, na katika utu wema; katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli; |
| BSB 7 in truthful speech and in the power of God; with the weapons of righteousness in the right hand and in the left; | SWKCV 7 katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; |
| BSB 8 through glory and dishonor, slander and praise; viewed as imposters, yet genuine; | SWKCV 8 katika utukufu na katika kudharauliwa; katika sifa mbaya na katika sifa nzuri; tukiwa kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli; |
| BSB 9 unknown, yet well-known; dying, and yet we live on; punished, yet not killed; | SWKCV 9 tukiwa maarufu, lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana; tukiwa kama wanaokufa, lakini tunaishi; tukipigwa, lakini hatuuawi; |
| BSB 10 sorrowful, yet always rejoicing; poor, yet making many rich; having nothing, and yet possessing everything. | SWKCV 10 tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote. |
| BSB 11 We have spoken freely to you, Corinthians. Our hearts are open wide. | SWKCV 11 Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa. |
| BSB 12 It is not our affection, but yours, that is restrained. | SWKCV 12 Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu kwetu. |
| BSB 13 As a fair exchange—I speak as to my children—open wide your hearts also. | SWKCV 13 Sasa nasema, kama na watoto wangu: Ninyi pia ifungueni mioyo yenu kabisa. |
| BSB 14 Do not be unequally yoked with unbelievers. For what partnership can righteousness have with wickedness? Or what fellowship does light have with darkness? | SWKCV 14 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? |
| BSB 15 What harmony is there between Christ and Belial? Or what does a believer have in common with an unbeliever? | SWKCV 15 Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? |
| BSB 16 What agreement can exist between the temple of God and idols? For we are the temple of the living God. As God has said: “I will dwell with them and walk among them, and I will be their God, and they will be My people.” | SWKCV 16 Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.” |
| BSB 17 “Therefore come out from among them and be separate, says the Lord. Touch no unclean thing, and I will receive you.” | SWKCV 17 “Kwa hiyo tokeni miongoni mwao, mkatengwe nao, asema Bwana. Msiguse kitu chochote kilicho najisi, nami nitawakaribisha.” |
| BSB 18 And: “I will be a Father to you, and you will be My sons and daughters, says the Lord Almighty.” | SWKCV 18 “Mimi nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu, asema Bwana Mwenyezi.” |
Questions about 2 Corinthians 6? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.