Acts 14
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 At Iconium, Paul and Barnabas went as usual into the Jewish synagogue, where they spoke so well that a great number of Jews and Greeks believed. | SWKCV 1 Huko Ikonio Paulo na Barnaba waliingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi kama ilivyokuwa desturi yao. Huko wakahubiri kwa uwezo mkubwa kiasi kwamba Wayahudi pamoja na watu wa Mataifa wakaamini. |
| BSB 2 But the unbelieving Jews stirred up the Gentiles and poisoned their minds against the brothers. | SWKCV 2 Lakini wale Wayahudi waliokataa kuamini, wakawachochea watu wa Mataifa, wakatia chuki ndani ya mioyo yao dhidi ya wale walioamini. |
| BSB 3 So Paul and Barnabas spent considerable time there, speaking boldly for the Lord, who affirmed the message of His grace by enabling them to perform signs and wonders. | SWKCV 3 Hivyo Paulo na Barnaba wakakaa huko kwa muda wa kutosha wakihubiri kwa ujasiri juu ya Bwana, ambaye alithibitisha ujumbe wa neema yake kwa kuwawezesha kufanya ishara na miujiza. |
| BSB 4 The people of the city were divided. Some sided with the Jews, and others with the apostles. | SWKCV 4 Lakini watu wa mji ule waligawanyika, wengine wakakubaliana na Wayahudi na wengine na mitume. |
| BSB 5 But when the Gentiles and Jews, together with their rulers, set out to mistreat and stone them, | SWKCV 5 Watu wa Mataifa na Wayahudi wakajiunga na baadhi ya viongozi, wakafanya mpango wa kuwatendea mitume mabaya na kuwapiga mawe. |
| BSB 6 they found out about it and fled to the Lycaonian cities of Lystra and Derbe and to the surrounding region, | SWKCV 6 Lakini mitume walipopata habari hizi wakakimbilia Listra na Derbe, miji ya Likaonia na sehemu zilizopakana nayo. |
| BSB 7 where they continued to preach the gospel. | SWKCV 7 Huko wakaendelea kuhubiri habari njema. |
| BSB 8 In Lystra there sat a man crippled in his feet, who was lame from birth and had never walked. | SWKCV 8 Katika mji wa Listra, alikuwako kiwete, ambaye alikuwa amelemaa tangu kuzaliwa na hakuwa ametembea kamwe. |
| BSB 9 This man was listening to the words of Paul, who looked intently at him and saw that he had faith to be healed. | SWKCV 9 Alimsikiliza Paulo alipokuwa akihubiri. Paulo alipomtazama akaona ana imani ya kuponywa. |
| BSB 10 In a loud voice Paul called out, “Stand up on your feet!” And the man jumped up and began to walk. | SWKCV 10 Paulo akapaza sauti, “Simama kwa miguu yako!” Mara yule mtu akasimama upesi akaanza kutembea! |
| BSB 11 When the crowds saw what Paul had done, they lifted up their voices in the Lycaonian language: “The gods have come down to us in human form!” | SWKCV 11 Ule umati wa watu ulipoona yaliyokuwa yamefanywa na Paulo, wakapiga kelele kwa lugha yao ya Kilikaonia wakasema, “Miungu imetushukia katika umbo la binadamu!” |
| BSB 12 Barnabas they called Zeus, and Paul they called Hermes, because he was the chief speaker. | SWKCV 12 Wakamwita Barnaba Zeu na Paulo wakamwita Herme kwa kuwa ndiye alikuwa msemaji mkuu. |
| BSB 13 The priest of Zeus, whose temple was just outside the city, brought bulls and wreaths to the city gates, hoping to offer a sacrifice along with the crowds. | SWKCV 13 Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje kidogo tu ya mji, akaleta mafahali na mashada ya maua penye lango la mji kwa sababu yeye na ule umati wa watu walitaka kuwatolea dhabihu. |
| BSB 14 But when the apostles Barnabas and Paul found out about this, they tore their clothes and rushed into the crowd, shouting, | SWKCV 14 Lakini mitume Paulo na Barnaba waliposikia haya, wakararua nguo zao, wakawaendea wale watu kwa haraka, wakawapigia kelele, wakisema, |
| BSB 15 “Men, why are you doing this? We too are only men, human like you. We are bringing you good news that you should turn from these worthless things to the living God, who made heaven and earth and sea and everything in them. | SWKCV 15 “Enyi watu, kwa nini mnafanya mambo haya? Sisi ni wanadamu tu kama ninyi! Tunawaletea habari njema, tukiwaambia kwamba mgeuke mtoke katika mambo haya yasiyofaa, mmwelekee Mungu aliye hai, aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo. |
| BSB 16 In past generations, He let all nations go their own way. | SWKCV 16 Zamani aliwaachia mataifa waishi walivyotaka. |
| BSB 17 Yet He has not left Himself without testimony to His goodness: He gives you rain from heaven and fruitful seasons, filling your hearts with food and gladness.” | SWKCV 17 Lakini hakuacha kuwaonyesha watu uwepo wake: Ameonyesha wema kwa kuwanyeshea mvua toka mbinguni na kuwapa mazao kwa majira yake, naye amewapa chakula tele na kuijaza mioyo yenu na furaha.” |
| BSB 18 Even with these words, Paul and Barnabas could hardly stop the crowds from sacrificing to them. | SWKCV 18 Hata kwa maneno haya yote, ilikuwa vigumu kuuzuia ule umati wa watu kuwatolea dhabihu. |
| BSB 19 Then some Jews arrived from Antioch and Iconium and won over the crowds. They stoned Paul and dragged him outside the city, presuming he was dead. | SWKCV 19 Ndipo wakaja baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio wakawashawishi wale watu, wakampiga Paulo kwa mawe, wakamburuta hadi nje ya mji, wakidhani amekufa. |
| BSB 20 But after the disciples had gathered around him, he got up and went back into the city. And the next day he left with Barnabas for Derbe. | SWKCV 20 Lakini baada ya wanafunzi kukusanyika akainuka na kurudi mjini. Kesho yake yeye na Barnaba wakaondoka kwenda Derbe. |
| BSB 21 They preached the gospel to that city and made many disciples. Then they returned to Lystra, Iconium, and Antioch, | SWKCV 21 Wakahubiri habari njema katika mji huo na kupata wanafunzi wengi. Kisha wakarudi Listra, Ikonio na Antiokia, |
| BSB 22 strengthening the souls of the disciples and encouraging them to continue in the faith. “We must endure many hardships to enter the kingdom of God,” they said. | SWKCV 22 wakiwaimarisha wanafunzi na kuwatia moyo waendelee kudumu katika imani. Wakawaonya wakisema, “Imetupasa kuingia katika Ufalme wa Mungu kwa kupitia katika taabu nyingi.” |
| BSB 23 Paul and Barnabas appointed elders for them in each church, praying and fasting as they entrusted them to the Lord, in whom they had believed. | SWKCV 23 Nao baada ya kuwateua wazee katika kila kanisa, kwa kufunga na kuomba wakawakabidhi kwa Bwana waliyemwamini. |
| BSB 24 After passing through Pisidia, they came to Pamphylia. | SWKCV 24 Kisha wakapitia Pisidia wakafika Pamfilia. |
| BSB 25 And when they had spoken the word in Perga, they went down to Attalia. | SWKCV 25 Baada ya kuhubiri neno la Mungu huko Perga, wakateremkia Atalia. |
| BSB 26 From Attalia they sailed to Antioch, where they had been commended to the grace of God for the work they had just completed. | SWKCV 26 Kutoka Atalia wakasafiri baharini wakarudi Antiokia, ambako walikuwa wamesifiwa kwa ajili ya neema ya Mungu kutokana na ile huduma waliyokuwa wameikamilisha. |
| BSB 27 When they arrived, they gathered the church together and reported all that God had done through them, and how He had opened the door of faith to the Gentiles. | SWKCV 27 Walipowasili Antiokia wakaliita kanisa pamoja na kutoa taarifa ya yale yote Mungu aliyokuwa ametenda kupitia kwao na jinsi alivyokuwa amefungua mlango wa imani kwa ajili ya watu wa Mataifa. |
| BSB 28 And they spent a long time there with the disciples. | SWKCV 28 Nao wakakaa huko pamoja na wanafunzi kwa muda mrefu. |
Questions about Acts 14? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.