Acts 13
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now in the church at Antioch there were prophets and teachers: Barnabas, Simeon called Niger, Lucius of Cyrene, Manaen (who had been brought up with Herod the tetrarch), and Saul. | SWKCV 1 Katika kanisa huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu, yaani: Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli. |
| BSB 2 While they were worshiping the Lord and fasting, the Holy Spirit said, “Set apart for Me Barnabas and Saul for the work to which I have called them.” | SWKCV 2 Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, “Nitengeeni Sauli na Barnaba kwa kazi ile maalum niliyowaitia.” |
| BSB 3 And after they had fasted and prayed, they laid their hands on them and sent them off. | SWKCV 3 Ndipo baada ya kufunga na kuomba, wakawawekea mikono yao na wakawatuma waende zao. |
| BSB 4 So Barnabas and Saul, sent forth by the Holy Spirit, went down to Seleucia and sailed from there to Cyprus. | SWKCV 4 Hivyo, wakiwa wametumwa na Roho Mtakatifu, wakashuka kwenda Seleukia na kutoka huko wakasafiri baharini mpaka kisiwa cha Kipro. |
| BSB 5 When they arrived at Salamis, they proclaimed the word of God in the Jewish synagogues. And John was with them as their helper. | SWKCV 5 Walipowasili katika mji wa Salami, wakahubiri neno la Mungu katika sinagogi la Wayahudi. Pia walikuwa na Yohana Marko kuwa msaidizi wao. |
| BSB 6 They traveled through the whole island as far as Paphos, where they found a Jewish sorcerer and false prophet named Bar-Jesus, | SWKCV 6 Walipokwisha kupita katika nchi zote hizo wakafika Pafo, ambapo walikutana na Myahudi mmoja mchawi aliyekuwa nabii wa uongo, jina lake Bar-Yesu. |
| BSB 7 an attendant of the proconsul, Sergius Paulus. The proconsul, a man of intelligence, summoned Barnabas and Saul because he wanted to hear the word of God. | SWKCV 7 Mtu huyu alikuwa pamoja na Sergio Paulo, mtu mwenye hekima aliyekuwa msaidizi wa mwakilishi wa mtawala wa kile kisiwa. Sergio Paulo akawaita Sauli na Barnaba akitaka kusikia neno la Mungu. |
| BSB 8 But Elymas the sorcerer (for that is what his name means) opposed them and tried to turn the proconsul from the faith. | SWKCV 8 Lakini Elima yule mchawi (hii ndiyo maana ya jina lake), aliwapinga Barnaba na Sauli na kujaribu kumpotosha yule mkuu wa kile kisiwa aiache imani. |
| BSB 9 Then Saul, who was also called Paul, filled with the Holy Spirit, looked directly at Elymas | SWKCV 9 Ndipo Sauli, ambaye pia aliitwa Paulo, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, akamkazia macho Elima huyo mchawi, |
| BSB 10 and said, “O child of the devil and enemy of all righteousness, you are full of all kinds of deceit and trickery! Will you never stop perverting the straight ways of the Lord? | SWKCV 10 akamwambia, “Ewe mwana wa ibilisi, wewe ni adui wa kila kilicho haki! Umejaa kila aina ya udanganyifu na ulaghai. Je, hutaacha kuzipotosha njia za Bwana zilizonyooka? |
| BSB 11 Now look, the hand of the Lord is against you, and for a time you will be blind and unable to see the light of the sun.” Immediately mist and darkness came over him, and he groped about, seeking someone to lead him by the hand. | SWKCV 11 Nawe sasa sikiliza, mkono wa Bwana u dhidi yako. Utakuwa kipofu, wala hutaona jua kwa muda.” Mara ukungu na giza vikamfunika, naye akaenda huku na huko akitafuta mtu wa kumshika mkono ili amwonyeshe njia. |
| BSB 12 When the proconsul saw what had happened, he believed, for he was astonished at the teaching about the Lord. | SWKCV 12 Yule mkuu wa kile kisiwa alipoona yaliyotukia, akaamini kwa sababu alistaajabishwa na mafundisho kuhusu Bwana. |
| BSB 13 After setting sail from Paphos, Paul and his companions came to Perga in Pamphylia, where John left them to return to Jerusalem. | SWKCV 13 Kisha Paulo na wenzake wakasafiri toka Pafo wakafika Perga huko Pamfilia. Lakini, Yohana Marko akawaacha huko, akarejea Yerusalemu. |
| BSB 14 And from Perga, they traveled inland to Pisidian Antioch, where they entered the synagogue on the Sabbath and sat down. | SWKCV 14 Kutoka Perga wakaendelea hadi Antiokia ya Pisidia. Siku ya Sabato wakaingia ndani ya sinagogi, wakaketi. |
| BSB 15 After the reading from the Law and the Prophets, the synagogue leaders sent word to them: “Brothers, if you have a word of encouragement for the people, please speak.” | SWKCV 15 Baada ya Sheria ya Mose na Kitabu cha Manabii kusomwa, viongozi wa sinagogi wakawatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mna neno la kuwafariji watu hawa, tafadhali lisemeni.” |
| BSB 16 Paul stood up, motioned with his hand, and began to speak: “Men of Israel and you Gentiles who fear God, listen to me! | SWKCV 16 Paulo akasimama, akawapungia mkono na kusema: “Enyi wanaume wa Israeli na ninyi nyote mnaomcha Mungu. |
| BSB 17 The God of the people of Israel chose our fathers. He made them into a great people during their stay in Egypt, and with an uplifted arm He led them out of that land. | SWKCV 17 Mungu wa watu hawa wa Israeli aliwachagua baba zetu, akawafanya kustawi walipokuwa huko Misri, kwa uwezo mwingi akawaongoza na kuwatoa katika nchi ile. |
| BSB 18 He endured their conduct for about forty years in the wilderness. | SWKCV 18 Kwa muda wa miaka arobaini alivumilia matendo yao walipokuwa jangwani. |
| BSB 19 And having vanquished seven nations in Canaan, He gave their land to His people as an inheritance. | SWKCV 19 Naye baada ya kuyaangamiza mataifa saba waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, akawapa Waisraeli nchi yao iwe urithi wao. |
| BSB 20 All this took about 450 years. After this, God gave them judges until the time of Samuel the prophet. | SWKCV 20 Haya yote yalichukua kama muda wa miaka 450. “Baada ya haya, Mungu akawapa waamuzi mpaka wakati wa nabii Samweli. |
| BSB 21 Then the people asked for a king, and God gave them Saul son of Kish, from the tribe of Benjamin, who ruled forty years. | SWKCV 21 Ndipo watu wakaomba wapewe mfalme, naye Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi wa kabila la Benyamini, aliyetawala kwa miaka arobaini. |
| BSB 22 After removing Saul, He raised up David as their king and testified about him: ‘I have found David son of Jesse a man after My own heart; he will carry out My will in its entirety.’ | SWKCV 22 Baada ya kumwondoa Sauli katika ufalme, akawainulia Daudi kuwa mfalme wao. Mungu pia alimshuhudia, akisema, ‘Nimemwona Daudi mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayetimiza mapenzi yangu yote.’ |
| BSB 23 From the descendants of this man, God has brought to Israel the Savior Jesus, as He promised. | SWKCV 23 “Kutoka uzao wa mtu huyu, Mungu amewaletea Israeli Mwokozi Yesu, kama alivyoahidi. |
| BSB 24 Before the arrival of Jesus, John preached a baptism of repentance to all the people of Israel. | SWKCV 24 Kabla ya kuja kwa Yesu, Yohana alihubiri toba na ubatizo kwa watu wote wa Israeli. |
| BSB 25 As John was completing his course, he said, ‘Who do you suppose I am? I am not that One. But there is One coming after me whose sandals I am not worthy to untie.’ | SWKCV 25 Yohana alipokuwa anakamilisha kazi yake, alisema: ‘Ninyi mnadhani mimi ni nani? Mimi si yeye. La hasha, lakini yeye yuaja baada yangu, ambaye mimi sistahili kufungua kamba za viatu vya miguu yake.’ |
| BSB 26 Brothers, children of Abraham, and you Gentiles who fear God, it is to us that this message of salvation has been sent. | SWKCV 26 “Ndugu zangu, wana wa Abrahamu, nanyi watu wa Mataifa mnaomcha Mungu, ujumbe huu wa wokovu umeletwa kwetu. |
| BSB 27 The people of Jerusalem and their rulers did not recognize Jesus, yet in condemning Him they fulfilled the words of the prophets that are read every Sabbath. | SWKCV 27 Kwa sababu wakaao Yerusalemu na viongozi wao hawakumtambua wala kuelewa maneno ya manabii yasomwayo kila Sabato, bali waliyatimiza maneno hayo kwa kumhukumu yeye. |
| BSB 28 And though they found no ground for a death sentence, they asked Pilate to have Him executed. | SWKCV 28 Ijapokuwa hawakupata sababu yoyote ya kumhukumu kifo, walimwomba Pilato aamuru auawe. |
| BSB 29 When they had carried out all that was written about Him, they took Him down from the tree and laid Him in a tomb. | SWKCV 29 Walipokwisha kufanya yale yote yaliyoandikwa kumhusu, walimshusha kutoka msalabani na kumzika kaburini. |
| BSB 30 But God raised Him from the dead, | SWKCV 30 Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. |
| BSB 31 and for many days He was seen by those who had accompanied Him from Galilee to Jerusalem. They are now His witnesses to our people. | SWKCV 31 Naye kwa siku nyingi akawatokea wale waliokuwa pamoja naye kuanzia Galilaya hadi Yerusalemu. Nao sasa wamekuwa mashahidi wake kwa watu wetu. |
| BSB 32 And now we proclaim to you the good news: What God promised our fathers | SWKCV 32 “Nasi tunawaletea habari njema, kwamba yale Mungu aliyowaahidi baba zetu |
| BSB 33 He has fulfilled for us, their children, by raising up Jesus. As it is written in the second Psalm: ‘You are My Son; today I have become Your Father.’ | SWKCV 33 sasa ameyatimiza kwetu sisi watoto wao, kwa kumfufua Yesu, kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili: “ ‘Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa.’ |
| BSB 34 In fact, God raised Him from the dead, never to see decay. As He has said: ‘I will give you the holy and sure blessings promised to David.’ | SWKCV 34 Kwa kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu asioze kamwe, alitamka maneno haya: “ ‘Nitakupa wewe baraka takatifu zilizo za hakika nilizomwahidi Daudi.’ |
| BSB 35 So also, He says in another Psalm: ‘You will not let Your Holy One see decay.’ | SWKCV 35 Kama ilivyosemwa mahali pengine katika Zaburi, “ ‘Hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu.’ |
| BSB 36 For when David had served God’s purpose in his own generation, he fell asleep. His body was buried with his fathers and saw decay. | SWKCV 36 “Kwa maana Daudi akiisha kulitumikia kusudi la Mungu katika kizazi chake, alilala; akazikwa pamoja na baba zake na mwili wake ukaoza. |
| BSB 37 But the One whom God raised from the dead did not see decay. | SWKCV 37 Lakini yule ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu hakuona uharibifu. |
| BSB 38 Therefore let it be known to you, brothers, that through Jesus the forgiveness of sins is proclaimed to you. | SWKCV 38 “Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. |
| BSB 39 Through Him everyone who believes is justified from everything from which you could not be justified by the law of Moses. | SWKCV 39 Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Mose. |
| BSB 40 Watch out, then, that what was spoken by the prophets does not happen to you: | SWKCV 40 Kwa hiyo jihadharini ili yale waliyosema manabii yasiwapate: |
| BSB 41 ‘Look, you scoffers, wonder and perish! For I am doing a work in your days that you would never believe, even if someone told you.’” | SWKCV 41 “ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka, mkastaajabu, mkaangamie, kwa maana nitatenda jambo wakati wenu ambalo hamtasadiki, hata kama mtu akiwaambia.’” |
| BSB 42 As Paul and Barnabas were leaving the synagogue, the people urged them to continue this message on the next Sabbath. | SWKCV 42 Paulo na Barnaba walipokuwa wakitoka nje ya sinagogi, watu wakawaomba wazungumze tena mambo hayo Sabato iliyofuata. |
| BSB 43 After the synagogue was dismissed, many of the Jews and devout converts to Judaism followed Paul and Barnabas, who spoke to them and urged them to continue in the grace of God. | SWKCV 43 Baada ya kusanyiko la Sinagogi kutawanyika, wengi wa Wayahudi na waongofu wa dini ya Kiyahudi wakawafuata Paulo na Barnaba, wakazungumza nao na kuwahimiza wadumu katika neema ya Mungu. |
| BSB 44 On the following Sabbath, nearly the whole city gathered to hear the word of the Lord. | SWKCV 44 Sabato iliyofuata, karibu watu wote wa mji walikuja kusikiliza neno la Bwana. |
| BSB 45 But when the Jews saw the crowds, they were filled with jealousy, and they blasphemously contradicted what Paul was saying. | SWKCV 45 Lakini Wayahudi walipoona ule umati mkubwa wa watu walijawa na wivu, wakayakanusha maneno Paulo aliyokuwa akisema. |
| BSB 46 Then Paul and Barnabas answered them boldly: “It was necessary to speak the word of God to you first. But since you reject it and do not consider yourselves worthy of eternal life, we now turn to the Gentiles. | SWKCV 46 Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa. |
| BSB 47 For this is what the Lord has commanded us: ‘I have made you a light for the Gentiles, to bring salvation to the ends of the earth.’” | SWKCV 47 Kwa maana hili ndilo Bwana alilotuamuru: “ ‘Nimewafanya ninyi kuwa nuru kwa watu wa Mataifa, ili mpate kuuleta wokovu hadi miisho ya dunia.’” |
| BSB 48 When the Gentiles heard this, they rejoiced and glorified the word of the Lord, and all who were appointed for eternal life believed. | SWKCV 48 Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. |
| BSB 49 And the word of the Lord spread throughout that region. | SWKCV 49 Neno la Bwana likaenea katika eneo lile lote. |
| BSB 50 The Jews, however, incited the religious women of prominence and the leading men of the city. They stirred up persecution against Paul and Barnabas and drove them out of their district. | SWKCV 50 Lakini Wayahudi wakawachochea wanawake wenye kumcha Mungu, wenye vyeo pamoja na watu maarufu katika mji, wakachochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na kuwafukuza kutoka eneo hilo. |
| BSB 51 So they shook the dust off their feet in protest against them and went to Iconium. | SWKCV 51 Hivyo Paulo na Barnaba wakakungʼuta mavumbi ya miguu yao ili kuwapinga, nao wakaenda Ikonio. |
| BSB 52 And the disciples were filled with joy and with the Holy Spirit. | SWKCV 52 Wanafunzi wakajawa na furaha na Roho Mtakatifu. |
Questions about Acts 13? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.