Acts 5
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Now a man named Ananias, together with his wife Sapphira, also sold a piece of property. | SWKCV 1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania pamoja na mkewe Safira waliuza kiwanja. |
| BSB 2 With his wife’s full knowledge, he kept back some of the proceeds for himself, but brought a portion and laid it at the apostles’ feet. | SWKCV 2 Huku mkewe akijua kikamilifu, Anania alificha sehemu ya fedha alizopata, akaleta kiasi kilichobaki na kukiweka miguuni pa mitume. |
| BSB 3 Then Peter said, “Ananias, how is it that Satan has filled your heart to lie to the Holy Spirit and withhold some of the proceeds from the land? | SWKCV 3 Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja? |
| BSB 4 Did it not belong to you before it was sold? And after it was sold, was it not at your disposal? How could you conceive such a deed in your heart? You have not lied to men, but to God!” | SWKCV 4 Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.” |
| BSB 5 On hearing these words, Ananias fell down and died. And great fear came over all who heard what had happened. | SWKCV 5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia. |
| BSB 6 Then the young men stepped forward, wrapped up his body, and carried him out and buried him. | SWKCV 6 Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika. |
| BSB 7 About three hours later his wife also came in, unaware of what had happened. | SWKCV 7 Saa tatu baadaye mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia. |
| BSB 8 “Tell me,” said Peter, “is this the price you and your husband got for the land?” “Yes,” she answered, “that is the price.” | SWKCV 8 Petro akamuuliza, “Niambie, je, mliuza kiwanja kwa thamani hii?” Akajibu, “Ndiyo, tuliuza kwa thamani hiyo.” |
| BSB 9 “How could you agree to test the Spirit of the Lord?” Peter replied. “Look, the feet of the men who buried your husband are at the door, and they will carry you out also.” | SWKCV 9 Ndipo Petro akamwambia, “Imekuwaje mkakubaliana kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama! Nyayo za vijana waliomzika mumeo ziko mlangoni, wewe nawe watakuchukua nje.” |
| BSB 10 At that instant she fell down at his feet and died. Then the young men came in and, finding her dead, carried her out and buried her beside her husband. | SWKCV 10 Saa ile ile akaanguka chini miguuni mwake na kufa. Nao wale vijana wakaingia, wakamkuta amekufa, wakamchukua wakamzika kando ya mumewe. |
| BSB 11 And great fear came over the whole church and all who heard about these events. | SWKCV 11 Hofu kuu ikalipata kanisa lote pamoja na watu wote waliosikia juu ya matukio haya. |
| BSB 12 The apostles performed many signs and wonders among the people, and with one accord the believers gathered together in Solomon’s Colonnade. | SWKCV 12 Mitume wakafanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Walioamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Solomoni. |
| BSB 13 Although the people regarded them highly, no one else dared to join them. | SWKCV 13 Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kuambatana nao ijapokuwa waliheshimiwa sana na watu. |
| BSB 14 Yet more and more believers were brought to the Lord—large numbers of both men and women. | SWKCV 14 Hata hivyo, waliomwamini Bwana wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake. |
| BSB 15 As a result, people brought the sick into the streets and laid them on cots and mats, so that at least Peter’s shadow might fall on some of them as he passed by. | SWKCV 15 Hata wakawa wanawaleta wagonjwa na kuwalaza kwenye magodoro na kwenye vitanda barabarani ili yamkini Petro akipita kivuli chake kiwaguse baadhi yao. |
| BSB 16 Crowds also gathered from the towns around Jerusalem, bringing the sick and those tormented by unclean spirits, and all of them were healed. | SWKCV 16 Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa. |
| BSB 17 Then the high priest and all his associates, who belonged to the party of the Sadducees, were filled with jealousy. They went out | SWKCV 17 Kisha kuhani mkuu na wenzake wote waliokuwa pamoja naye, waliokuwa wa kundi la Masadukayo, wakajawa na wivu. |
| BSB 18 and arrested the apostles and put them in the public jail. | SWKCV 18 Wakawakamata mitume na kuwatia gerezani. |
| BSB 19 But during the night an angel of the Lord opened the doors of the jail and brought them out, saying, | SWKCV 19 Lakini wakati wa usiku, malaika wa Bwana akaja, akafungua milango ya gereza na akawatoa nje. Akawaambia, |
| BSB 20 “Go, stand in the temple courts and tell the people the full message of this new life.” | SWKCV 20 “Nendeni, mkasimame Hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu mpya.” |
| BSB 21 At daybreak the apostles entered the temple courts as they had been told and began to teach the people. When the high priest and his associates arrived, they convened the Sanhedrin—the full assembly of the elders of Israel—and sent to the jail for the apostles. | SWKCV 21 Waliposikia haya wakaenda Hekaluni alfajiri wakaendelea kufundisha watu. Kuhani mkuu na wale waliokuwa pamoja nao walipowasili, alikusanya baraza na wazee wote wa Israeli wakatuma wale mitume waletwe kutoka gerezani. |
| BSB 22 But on arriving at the jail, the officers did not find them there. So they returned with the report: | SWKCV 22 Lakini wale walinzi wa Hekalu walipokwenda gerezani hawakuwakuta mitume mle. Kwa hiyo wakarudi na kutoa habari. |
| BSB 23 “We found the jail securely locked, with the guards posted at the doors; but when we opened them, we found no one inside.” | SWKCV 23 Wakasema, “Tumekuta milango ya gereza imefungwa sawasawa na askari wa gereza wamesimama nje ya mlango, lakini tulipofungua milango hakuwepo mtu yeyote ndani.” |
| BSB 24 When the captain of the temple guard and the chief priests heard this account, they were perplexed as to what was happening. | SWKCV 24 Basi mkuu wa walinzi wa Hekalu na viongozi wa makuhani waliposikia haya, wakafadhaika na kushangaa sana kwa ajili yao kwamba jambo hili litakuwaje. |
| BSB 25 Then someone came in and announced, “Look, the men you put in jail are standing in the temple courts teaching the people!” | SWKCV 25 Ndipo mtu mmoja akaja akawaambia, “Tazameni watu mliowatia gerezani wako Hekaluni wakiwafundisha watu.” |
| BSB 26 At that point, the captain went with the officers and brought the apostles—but not by force, for fear the people would stone them. | SWKCV 26 Ndipo yule mkuu wa walinzi wa Hekalu wakaenda pamoja na askari wakawaleta wale mitume, lakini bila ghasia kwa sababu waliogopa kupigwa mawe na watu. |
| BSB 27 They brought them in and made them stand before the Sanhedrin, where the high priest interrogated them. | SWKCV 27 Wakiisha kuwaleta mitume wakawaamuru kusimama mbele ya baraza ili kuhani mkuu awahoji. |
| BSB 28 “We gave you strict orders not to teach in this name,” he said. “Yet you have filled Jerusalem with your teaching and are determined to make us responsible for this man’s blood.” | SWKCV 28 “Tuliwaonya kwa nguvu msifundishe kwa jina hili, lakini ninyi mmeijaza Yerusalemu yote mafundisho yenu na tena mmekusudia kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.” |
| BSB 29 But Peter and the other apostles replied, “We must obey God rather than men. | SWKCV 29 Petro na wale mitume wengine wakajibu, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. |
| BSB 30 The God of our fathers raised up Jesus, whom you had killed by hanging Him on a tree. | SWKCV 30 Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu kutoka kwa wafu, ambaye ninyi mlimuua kwa kumtundika kwenye msalaba. |
| BSB 31 God exalted Him to His right hand as Prince and Savior, in order to grant repentance and forgiveness of sins to Israel. | SWKCV 31 Mungu alimtukuza, akamweka mkono wake wa kuume kuwa Kiongozi na Mwokozi ili awape Israeli toba na msamaha wa dhambi. |
| BSB 32 We are witnesses of these things, and so is the Holy Spirit, whom God has given to those who obey Him.” | SWKCV 32 Nasi tu mashahidi wa mambo haya, vivyo hivyo na Roho Mtakatifu ambaye Mungu amewapa wale wanaomtii.” |
| BSB 33 When the Council members heard this, they were enraged, and they resolved to put the apostles to death. | SWKCV 33 Wale wajumbe wa baraza la wazee waliposikia haya, walijawa na ghadhabu, wakataka kuwaua mitume. |
| BSB 34 But a Pharisee named Gamaliel, a teacher of the law who was honored by all the people, stood up in the Sanhedrin and ordered that the men be put outside for a short time. | SWKCV 34 Lakini Farisayo mmoja, jina lake Gamalieli, aliyekuwa mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote, akasimama mbele ya baraza akaamuru mitume watolewe nje kwa muda. |
| BSB 35 “Men of Israel,” he said, “consider carefully what you are about to do to these men. | SWKCV 35 Ndipo alipowaambia wajumbe wa baraza, “Enyi watu wa Israeli, fikirini kwa uangalifu mnayotaka kuwatendea watu hawa. |
| BSB 36 Some time ago Theudas rose up, claiming to be somebody, and about four hundred men joined him. He was killed, all his followers were dispersed, and it all came to nothing. | SWKCV 36 Kwa maana wakati uliopita, aliinuka mtu mmoja jina lake Theuda, alijidai kuwa yeye ni mtu maarufu, akapata wafuasi wapatao 400 walioambatana naye. Lakini aliuawa, na wafuasi wake wote wakatawanyika, wakawa si kitu. |
| BSB 37 After him, Judas the Galilean appeared in the days of the census and drew away people after him. He too perished, and all his followers were scattered. | SWKCV 37 Baada yake, alitokea Yuda Mgalilaya wakati wa kuorodhesha watu, naye akaongoza kundi la watu kuasi. Yeye pia aliuawa, nao wafuasi wake wakatawanyika. |
| BSB 38 So in the present case I advise you: Leave these men alone. Let them go! For if their purpose or endeavor is of human origin, it will fail. | SWKCV 38 Kwa hiyo, kwa habari ya jambo hili nawashauri, jiepusheni na watu hawa. Waacheni waende zao! Kwa maana kama kusudi lao na shughuli yao imetokana na mwanadamu, haitafanikiwa. |
| BSB 39 But if it is from God, you will not be able to stop them. You may even find yourselves fighting against God.” | SWKCV 39 Lakini ikiwa imetoka kwa Mungu, hamtaweza kuwazuia watu hawa. Badala yake mtajikuta mnapigana na Mungu.” |
| BSB 40 At this, they yielded to Gamaliel. They called the apostles in and had them flogged. Then they ordered them not to speak in the name of Jesus, and released them. | SWKCV 40 Wakapokea ushauri wa Gamalieli. Wakawaita mitume ndani, wakaamuru wachapwe mijeledi, kisha wakawaagiza wasinene tena kwa jina la Yesu, wakawaachia waende zao. |
| BSB 41 The apostles left the Sanhedrin, rejoicing that they had been counted worthy of suffering disgrace for the Name. | SWKCV 41 Nao mitume wakatoka nje ya baraza, wakiwa wamejaa furaha kwa sababu wamehesabiwa kustahili kupata aibu kwa ajili ya jina la Yesu. |
| BSB 42 Every day, in the temple courts and from house to house, they did not stop teaching and proclaiming the good news that Jesus is the Christ. | SWKCV 42 Kila siku, Hekaluni na nyumba kwa nyumba, hawakuacha kufundisha na kuhubiri habari njema kwamba Yesu ndiye Kristo. |
Questions about Acts 5? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.