Exodus 37
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Bezalel went on to construct the ark of acacia wood, two and a half cubits long, a cubit and a half wide, and a cubit and a half high. | SWKCV 1 Bezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu. |
| BSB 2 He overlaid it with pure gold, both inside and out, and made a gold molding around it. | SWKCV 2 Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu. |
| BSB 3 And he cast four gold rings for its four feet, two rings on one side and two on the other. | SWKCV 3 Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. |
| BSB 4 Then he made poles of acacia wood and overlaid them with gold. | SWKCV 4 Kisha akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. |
| BSB 5 He inserted the poles into the rings on the sides of the ark in order to carry it. | SWKCV 5 Akaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. |
| BSB 6 He constructed a mercy seat of pure gold, two and a half cubits long and a cubit and a half wide. | SWKCV 6 Akatengeneza kifuniko cha upatanisho kwa dhahabu safi: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. |
| BSB 7 He made two cherubim of hammered gold at the ends of the mercy seat, | SWKCV 7 Kisha akatengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. |
| BSB 8 one cherub on one end and one on the other, all made from one piece of gold. | SWKCV 8 Akatengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; akawatengeneza kuwa kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. |
| BSB 9 And the cherubim had wings that spread upward, overshadowing the mercy seat. The cherubim faced each other, looking toward the mercy seat. | SWKCV 9 Makerubi hao walikuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, wakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao walielekeana, wakitazama hicho kifuniko. |
| BSB 10 He also made the table of acacia wood two cubits long, a cubit wide, and a cubit and a half high. | SWKCV 10 Akatengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili, upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu. |
| BSB 11 He overlaid it with pure gold and made a gold molding around it. | SWKCV 11 Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. |
| BSB 12 And he made a rim around it a handbreadth wide and put a gold molding on the rim. | SWKCV 12 Pia akatengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne, na kuufanyia ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote. |
| BSB 13 He cast four gold rings for the table and fastened them to the four corners at its four legs. | SWKCV 13 Akasubu pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na kuzifungia kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. |
| BSB 14 The rings were placed close to the rim, to serve as holders for the poles used to carry the table. | SWKCV 14 Pete hizo ziliwekwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko iliyotumika kuibebea hiyo meza. |
| BSB 15 He made the poles of acacia wood for carrying the table and overlaid them with gold. | SWKCV 15 Mipiko hiyo ya kubebea meza ilitengenezwa kwa mti wa mshita, na ilikuwa imefunikwa kwa dhahabu. |
| BSB 16 He also made the utensils for the table out of pure gold: its plates and dishes, as well as its bowls and pitchers for pouring drink offerings. | SWKCV 16 Vyombo vyote vya mezani vilitengenezwa kwa dhahabu safi: yaani sahani zake, masinia, na bakuli na bilauri zake kwa ajili ya kumiminia sadaka za vinywaji. |
| BSB 17 Then he made the lampstand out of pure hammered gold, all of one piece: its base and shaft, its cups, and its buds and petals. | SWKCV 17 Akatengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vilivyofanana na ua, matovu na maua vilikuwa kitu kimoja. |
| BSB 18 Six branches extended from the sides, three on one side and three on the other. | SWKCV 18 Matawi sita yalitokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. |
| BSB 19 There were three cups shaped like almond blossoms on the first branch, each with buds and petals, three on the next branch, and the same for all six branches that extended from the lampstand. | SWKCV 19 Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vilikuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yaliyotokeza kwenye kile kinara cha taa. |
| BSB 20 And on the lampstand were four cups shaped like almond blossoms with buds and petals. | SWKCV 20 Juu ya kinara chenyewe kulikuwepo na vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. |
| BSB 21 A bud was under the first pair of branches that extended from the lampstand, a bud under the second pair, and a bud under the third pair. | SWKCV 21 Tovu moja lilikuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani, matawi sita kwa jumla. |
| BSB 22 The buds and branches were all of one piece with the lampstand, hammered out of pure gold. | SWKCV 22 Matovu na matawi yote yalikuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakiwa yamefuliwa kwa dhahabu safi. |
| BSB 23 He also made its seven lamps, its wick trimmers, and trays of pure gold. | SWKCV 23 Akatengeneza taa zake saba, na pia mikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote kwa dhahabu safi. |
| BSB 24 He made the lampstand and all its utensils from a talent of pure gold. | SWKCV 24 Akatengeneza kinara hicho cha taa pamoja na vifaa vyake vyote kutumia talanta moja ya dhahabu safi. |
| BSB 25 He made the altar of incense out of acacia wood. It was square, a cubit long, a cubit wide, and two cubits high. Its horns were of one piece. | SWKCV 25 Akatengeneza madhabahu ya kufukizia uvumba kwa mbao za mshita. Ilikuwa ya mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zilikuwa kitu kimoja nayo. |
| BSB 26 And he overlaid with pure gold the top and all the sides and horns. Then he made a molding of gold around it. | SWKCV 26 Akafunika hayo madhabahu juu na pande zote na pia zile pembe zake kwa dhahabu safi, na akayafanyizia ukingo wa dhahabu kuizunguka. |
| BSB 27 He made two gold rings below the molding on opposite sides to hold the poles used to carry it. | SWKCV 27 Akatengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, zikiwa mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko iliyotumika kuyabebea madhabahu. |
| BSB 28 And he made the poles of acacia wood and overlaid them with gold. | SWKCV 28 Akatengeneza mipiko kwa miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu. |
| BSB 29 He also made the sacred anointing oil and the pure, fragrant incense, the work of a perfumer. | SWKCV 29 Pia akatengeneza mafuta matakatifu ya upako, na uvumba safi wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. |
Questions about Exodus 37? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.