Ezekiel 27
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Then the word of the LORD came to me, saying, | SWKCV 1 Neno la Bwana likanijia kusema: |
| BSB 2 “Now you, son of man, take up a lament for Tyre. | SWKCV 2 “Mwanadamu, fanya maombolezo kwa ajili ya Tiro. |
| BSB 3 Tell Tyre, who dwells at the gateway to the sea, merchant of the peoples on many coasts, that this is what the Lord GOD says: You have said, O Tyre, ‘I am perfect in beauty.’ | SWKCV 3 Umwambie Tiro, ulioko kwenye lango la bahari, ufanyao biashara na mataifa mengi ya pwani, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ee Tiro, wewe umesema, “Mimi ni mkamilifu katika uzuri.” |
| BSB 4 Your borders are in the heart of the seas; your builders perfected your beauty. | SWKCV 4 Mipaka yako ilikuwa katika moyo wa bahari, wajenzi wako walikamilisha uzuri wako. |
| BSB 5 They constructed all your planking with cypress from Senir. They took a cedar from Lebanon to make a mast for you. | SWKCV 5 Walizifanya mbao zako zote kwa misunobari itokayo Seniri; walichukua mierezi kutoka Lebanoni kukutengenezea mlingoti. |
| BSB 6 Of oaks from Bashan they made your oars; of wood from the coasts of Cyprus they made your deck, inlaid with ivory. | SWKCV 6 Walichukua mialoni toka Bashani wakakutengenezea makasia yako; kwa miti ya msanduku kutoka pwani ya Kitimu wakatengeneza sitaha yako na kuipamba kwa pembe za ndovu. |
| BSB 7 Of embroidered fine linen from Egypt they made your sail, which served as your banner. Of blue and purple from the coasts of Elishah they made your awning. | SWKCV 7 Kitani safi kilichotariziwa kutoka Misri kilikuwa tanga lako, nacho kilikuwa bendera yako; chandarua chako kilikuwa cha rangi ya buluu na ya zambarau kutoka visiwa vya Elisha. |
| BSB 8 The men of Sidon and Arvad were your oarsmen. Your men of skill, O Tyre, were there as your captains. | SWKCV 8 Watu kutoka Sidoni na Arvadi walikuwa wapiga makasia yako; watu wako wenye ustadi, ee Tiro, walikuwa ndio mabaharia wako. |
| BSB 9 The elders of Gebal were aboard as shipwrights, repairing your leaks. All the ships of the sea and their sailors came alongside to barter for your merchandise. | SWKCV 9 Wazee wa Gebali pamoja na mafundi stadi walikuwa mafundi wako melini. Meli zote za baharini na mabaharia wao walikuja kwako ili kubadilishana bidhaa zako. |
| BSB 10 Men of Persia, Lydia, and Put served as warriors in your army. They hung their shields and helmets on your walls; they gave you splendor. | SWKCV 10 “ ‘Watu wa Uajemi, Ludi na Putu walikuwa askari katika jeshi lako. Walitundika ngao zao na chapeo zao kwenye kuta zako, wakileta fahari yako. |
| BSB 11 Men of Arvad and Helech manned your walls all around, and the men of Gammad were in your towers. They hung their shields around your walls; they perfected your beauty. | SWKCV 11 Watu wa Arvadi na wa Heleki walikuwa juu ya kuta zako pande zote; watu wa Gamadi walikuwa kwenye minara yako. Walitundika ngao zao kuzizunguka kuta zako; wakaukamilisha uzuri wako. |
| BSB 12 Tarshish was your merchant because of your great wealth of goods; they exchanged silver, iron, tin, and lead for your wares. | SWKCV 12 “ ‘Tarshishi walifanya biashara nawe kwa sababu ya utajiri wako mkubwa wa bidhaa, walibadilisha fedha, chuma, bati na risasi kwa mali zako. |
| BSB 13 Javan, Tubal, and Meshech were your merchants. They exchanged slaves and bronze utensils for your merchandise. | SWKCV 13 “ ‘Uyunani, Tubali na Mesheki, walifanya biashara nawe, walibadilisha watumwa na vyombo vya shaba kwa bidhaa zako. |
| BSB 14 The men of Beth-togarmah exchanged horses, war horses, and mules for your wares. | SWKCV 14 “ ‘Watu wa Beth-Togarma walibadilisha farasi wa mizigo, farasi wa vita na nyumbu kwa mali zako. |
| BSB 15 The men of Dedan were your clients; many coastlands were your market; they paid you with ivory tusks and ebony. | SWKCV 15 “ ‘Watu wa Dedani walifanya biashara nawe, watu wengi wa nchi za pwani walikuwa wachuuzi wako, walikulipa kwa pembe za ndovu na mpingo. |
| BSB 16 Aram was your customer because of your many products; they exchanged turquoise, purple, embroidered work, fine linen, coral, and rubies for your wares. | SWKCV 16 “ ‘Watu wa Aramu walifanya biashara nawe kwa ajili ya wingi wa kazi za mikono yako, wakibadilishana kwa almasi, vitambaa vya rangi ya zambarau, vitambaa vilivyotariziwa, kitani safi, matumbawe na akiki nyekundu. |
| BSB 17 Judah and the land of Israel traded with you; they exchanged wheat from Minnith, cakes and honey, oil and balm for your merchandise. | SWKCV 17 “ ‘Yuda na Israeli walifanya biashara nawe, walibadilishana kwa ngano kutoka Minithi, mtama, asali, mafuta na zeri ya kuponyeshea. |
| BSB 18 Because of your many products and your great wealth of goods, Damascus traded with you wine from Helbon, wool from Zahar, | SWKCV 18 “ ‘Dameski, kwa sababu ya wingi wa kazi za mikono yako na ukuu wa utajiri wa mali, walifanya biashara nawe wakibadilishana mvinyo kutoka Helboni na sufu kutoka Zahari. |
| BSB 19 and casks of wine from Izal for your wares. Wrought iron, cassia, and sweet cane were exchanged for your merchandise. | SWKCV 19 “ ‘Wadani na Wayunani kutoka Uzali, walikuletea mali za biashara, nao wakabadilishana nawe chuma kilichofuliwa, mdalasini na mchaichai. |
| BSB 20 Dedan was your merchant in saddlecloths for riding. | SWKCV 20 “ ‘Dedani alifanya biashara nawe kwa matandiko ya farasi. |
| BSB 21 Arabia and all the princes of Kedar were your customers, trading in lambs, rams, and goats. | SWKCV 21 “ ‘Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wanunuzi wako waliobadilishana bidhaa zako na wana-kondoo, kondoo dume na mbuzi. |
| BSB 22 The merchants of Sheba and Raamah traded with you; for your wares they exchanged gold, the finest of all spices, and precious stones. | SWKCV 22 “ ‘Wafanyabiashara wa Sheba na wa Raama walifanya biashara nawe, wakabadilishana bidhaa zako na aina zote za vikolezi, vito vya thamani na dhahabu. |
| BSB 23 Haran, Canneh, and Eden traded with you, and so did the merchants of Sheba, Asshur, and Chilmad. | SWKCV 23 “ ‘Harani, Kane na Edeni na wafanyabiashara wa Sheba, Ashuru na Kilmadi walifanya biashara nawe. |
| BSB 24 In your marketplace they traded with you fine garments of blue, embroidered work, and multicolored rugs with cords tightly twisted and knotted. | SWKCV 24 Kwenye soko lako, walifanya biashara nawe kwa mavazi mazuri, vitambaa vya buluu, nguo za kutariziwa na mazulia ya rangi mbalimbali yenye kamba zilizosokotwa na kuwekwa mafundo imara. |
| BSB 25 The ships of Tarshish carried your merchandise. And you were filled with heavy cargo in the heart of the sea. | SWKCV 25 “ ‘Merikebu za Tarshishi ndizo zinazokusafirishia bidhaa zako. Umejazwa shehena kubwa katika moyo wa bahari. |
| BSB 26 Your oarsmen have brought you onto the high seas, but the east wind will shatter you in the heart of the sea. | SWKCV 26 Wapiga makasia wako wanakupeleka mpaka kwenye maji makavu. Lakini upepo wa mashariki umekuvunja vipande vipande katika moyo wa bahari. |
| BSB 27 Your wealth, wares, and merchandise, your sailors, captains, and shipwrights, your merchants and all the warriors within you, with all the other people on board, will sink into the heart of the sea on the day of your downfall. | SWKCV 27 Utajiri wako, bidhaa zako na mali zako, mabaharia wako, manahodha wako, mafundi wako wa meli, wafanyabiashara wako na askari wako wote, na kila mmoja aliyeko melini atazama kwenye moyo wa bahari siku ile ya kuvunjika kwa meli yako. |
| BSB 28 The countryside will shake when your sailors cry out. | SWKCV 28 Nchi za pwani zitatetemeka wakati mabaharia wako watakapopiga kelele. |
| BSB 29 All who handle the oars will abandon their ships. The sailors and all the captains of the sea will stand on the shore. | SWKCV 29 Wote wapigao makasia wataacha meli zao, mabaharia wote na wanamaji wote watasimama pwani. |
| BSB 30 They will raise their voices for you and cry out bitterly. They will throw dust on their heads and roll in ashes. | SWKCV 30 Watapaza sauti zao na kulia sana kwa ajili yako; watajitupia mavumbi juu ya vichwa vyao na kujivingirisha kwenye majivu. |
| BSB 31 They will shave their heads for you and wrap themselves in sackcloth. They will weep over you with anguish of soul and bitter mourning. | SWKCV 31 Watanyoa nywele zao kwa ajili yako, nao watavaa nguo za magunia. Watakulilia kwa uchungu wa moyo na kwa maombolezo makuu. |
| BSB 32 As they wail and mourn over you, they will take up a lament for you: ‘Who was ever like Tyre, silenced in the middle of the sea? | SWKCV 32 Watakapokuwa wanalia na kuomboleza juu yako, watafanya maombolezo kukuhusu wakisema: “Ni nani aliyepata kuangamizwa kama Tiro, katika moyo wa bahari?” |
| BSB 33 When your wares went out to sea, you satisfied many nations. You enriched the kings of the earth with your abundant wealth and merchandise. | SWKCV 33 Wakati bidhaa zako zilipotoka baharini, ulitosheleza mataifa mengi; kwa wingi wa utajiri wako na bidhaa zako ulitajirisha wafalme wa dunia. |
| BSB 34 Now you are shattered by the seas in the depths of the waters; your merchandise and the people among you have gone down with you. | SWKCV 34 Sasa umevunjavunjwa na bahari, katika vilindi vya maji, bidhaa zako na kundi lako lote vimezama pamoja nawe. |
| BSB 35 All the people of the coastlands are appalled over you. Their kings shudder with fear; their faces are contorted. | SWKCV 35 Wote waishio katika nchi za pwani wanakustaajabia; wafalme wao wanatetemeka kwa hofu kuu, nazo nyuso zao zimekunjamana kwa woga. |
| BSB 36 Those who trade among the nations hiss at you; you have come to a horrible end and will be no more.’” | SWKCV 36 Wafanyabiashara miongoni mwa mataifa wanakucheka; umefikia mwisho wa kutisha nawe hutakuwepo tena.’” |
Questions about Ezekiel 27? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.