Genesis 2
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Thus the heavens and the earth were completed in all their vast array. | SWKCV 1 Kwa hiyo mbingu na dunia zikakamilika, pamoja na vyote vilivyomo. |
| BSB 2 And by the seventh day God had finished the work He had been doing; so on that day He rested from all His work. | SWKCV 2 Katika siku ya saba Mungu alikuwa amekamilisha kazi aliyokuwa akiifanya, hivyo siku ya saba akapumzika kutoka kazi zake zote. |
| BSB 3 Then God blessed the seventh day and sanctified it, because on that day He rested from all the work of creation that He had accomplished. | SWKCV 3 Mungu akaibariki siku ya saba akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya. |
| BSB 4 This is the account of the heavens and the earth when they were created, in the day that the LORD God made them. | SWKCV 4 Haya ndiyo maelezo ya mbingu na dunia wakati zilipoumbwa. Bwana Mungu alipoziumba mbingu na dunia, |
| BSB 5 Now no shrub of the field had yet appeared on the earth, nor had any plant of the field sprouted, for the LORD God had not yet sent rain upon the earth, and there was no man to cultivate the ground. | SWKCV 5 hapakuwepo na mche wa shambani uliokuwa umejitokeza ardhini, wala hapakuwepo na mmea wa shamba uliokuwa umeota, kwa kuwa Bwana Mungu alikuwa hajanyeshea mvua juu ya nchi, na hapakuwepo mtu wa kuilima ardhi, |
| BSB 6 But springs welled up from the earth and watered the whole surface of the ground. | SWKCV 6 lakini umande ulitokeza kutoka ardhini na kunyesha uso wote wa nchi: |
| BSB 7 Then the LORD God formed man from the dust of the ground and breathed the breath of life into his nostrils, and the man became a living being. | SWKCV 7 Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai. |
| BSB 8 And the LORD God planted a garden in Eden, in the east, where He placed the man He had formed. | SWKCV 8 Basi Bwana Mungu alikuwa ameotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, huko akamweka huyo mtu aliyemuumba. |
| BSB 9 Out of the ground the LORD God gave growth to every tree that is pleasing to the eye and good for food. And in the middle of the garden were the tree of life and the tree of the knowledge of good and evil. | SWKCV 9 Bwana Mungu akafanya aina zote za miti ziote kutoka ardhini, miti yenye kupendeza macho na mizuri kwa chakula. Katikati ya bustani ulikuwepo mti wa uzima na mti wa kujua mema na mabaya. |
| BSB 10 Now a river flowed out of Eden to water the garden, and from there it branched into four headwaters: | SWKCV 10 Mto wa kunyeshea bustani ulitiririka toka Edeni, kuanzia hapa ukagawanyika kuwa mito minne. |
| BSB 11 The name of the first river is the Pishon; it winds through the whole land of Havilah, where there is gold. | SWKCV 11 Mto wa kwanza uliitwa Pishoni, nao huzunguka nchi yote ya Havila ambako kuna dhahabu. |
| BSB 12 And the gold of that land is pure, and bdellium and onyx are found there. | SWKCV 12 (Dhahabu ya nchi hiyo ni nzuri, bedola na vito shohamu pia hupatikana huko.) |
| BSB 13 The name of the second river is the Gihon; it winds through the whole land of Cush. | SWKCV 13 Jina la mto wa pili ni Gihoni, ambao huzunguka nchi yote ya Kushi. |
| BSB 14 The name of the third river is the Tigris; it runs along the east side of Assyria. And the fourth river is the Euphrates. | SWKCV 14 Jina la mto wa tatu ni Tigrisi, unaopita mashariki ya Ashuru. Mto wa nne ni Frati. |
| BSB 15 Then the LORD God took the man and placed him in the Garden of Eden to cultivate and keep it. | SWKCV 15 Bwana Mungu akamchukua huyo mtu, akamweka kwenye Bustani ya Edeni ailime na kuitunza. |
| BSB 16 And the LORD God commanded him, “You may eat freely from every tree of the garden, | SWKCV 16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akamwambia, “Uko huru kula matunda ya mti wowote katika bustani, |
| BSB 17 but you must not eat from the tree of the knowledge of good and evil; for in the day that you eat of it, you will surely die.” | SWKCV 17 lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa.” |
| BSB 18 The LORD God also said, “It is not good for the man to be alone. I will make for him a suitable helper.” | SWKCV 18 Bwana Mungu akasema, “Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa.” |
| BSB 19 And out of the ground the LORD God formed every beast of the field and every bird of the air, and He brought them to the man to see what he would name each one. And whatever the man called each living creature, that was its name. | SWKCV 19 Basi Bwana Mungu alikuwa amefanyiza kutoka ardhi wanyama wote wa porini na ndege wote wa angani. Akawaleta kwa huyu mtu aone atawaitaje, nalo jina lolote alilokiita kila kiumbe hai, likawa ndilo jina lake. |
| BSB 20 The man gave names to all the livestock, to the birds of the air, and to every beast of the field. But for Adam no suitable helper was found. | SWKCV 20 Hivyo Adamu akawapa majina wanyama wote wa kufugwa, ndege wa angani, na wanyama wote wa porini. Lakini kwa Adamu hakupatikana msaidizi wa kumfaa. |
| BSB 21 So the LORD God caused the man to fall into a deep sleep, and while he slept, He took one of the man’s ribs and closed up the area with flesh. | SWKCV 21 Hivyo Bwana Mungu akamfanya Adamu kulala usingizi mzito, naye alipokuwa amelala akachukua moja ya mbavu zake, akapafunika mahali pale kwa nyama. |
| BSB 22 And from the rib that the LORD God had taken from the man, He made a woman and brought her to him. | SWKCV 22 Kisha Bwana Mungu akamfanya mwanamke kutoka kwenye ule ubavu aliouchukua kutoka kwa huyo mwanaume, akamleta huyo mwanamke kwa huyo mwanaume. |
| BSB 23 And the man said: “This is now bone of my bones and flesh of my flesh; she shall be called ‘woman,’ for out of man she was taken.” | SWKCV 23 Huyo mwanaume akasema, “Huyu sasa ni mfupa wa mifupa yangu na nyama ya nyama yangu, ataitwa ‘mwanamke,’ kwa kuwa alitolewa katika mwanaume.” |
| BSB 24 For this reason a man will leave his father and mother and be united to his wife, and they will become one flesh. | SWKCV 24 Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. |
| BSB 25 And the man and his wife were both naked, and they were not ashamed. | SWKCV 25 Adamu na mkewe wote wawili walikuwa uchi, wala hawakuona aibu. |
Questions about Genesis 2? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.