Genesis 41
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 After two full years had passed, Pharaoh had a dream: He was standing beside the Nile, | SWKCV 1 Baada ya miaka miwili kamili kupita, Farao aliota ndoto: Tazama alikuwa amesimama kando ya Mto Naili, |
| BSB 2 when seven cows, sleek and well-fed, came up from the river and began to graze among the reeds. | SWKCV 2 wakati ngʼombe saba, wazuri na wanono, walitokea mtoni wakajilisha kwenye matete. |
| BSB 3 After them, seven other cows, sickly and thin, came up from the Nile and stood beside the well-fed cows on the bank of the river. | SWKCV 3 Baada yao ngʼombe wengine saba, wabaya na waliokonda, wakatokea mtoni Naili wakasimama kando ya wale wanono ukingoni mwa mto. |
| BSB 4 And the cows that were sickly and thin devoured the seven sleek, well-fed cows. Then Pharaoh woke up, | SWKCV 4 Wale ngʼombe wabaya na waliokonda wakawala wale saba wazuri na wanono. Kisha Farao akaamka. |
| BSB 5 but he fell back asleep and dreamed a second time: Seven heads of grain, plump and ripe, came up on one stalk. | SWKCV 5 Farao akaingia usingizini tena akaota ndoto ya pili: Akaona masuke saba ya nafaka, yenye afya na mazuri, yanakua katika bua moja. |
| BSB 6 After them, seven other heads of grain sprouted, thin and scorched by the east wind. | SWKCV 6 Baadaye, masuke mengine saba yakachipua, yakiwa membamba yaliyonyaushwa na upepo wa mashariki. |
| BSB 7 And the thin heads of grain swallowed up the seven plump, ripe ones. Then Pharaoh awoke and realized it was a dream. | SWKCV 7 Masuke yale membamba yakameza yale masuke saba yenye afya na yaliyojaa. Basi Farao akaamka kutoka usingizini, kumbe ilikuwa ndoto. |
| BSB 8 In the morning his spirit was troubled, so he summoned all the magicians and wise men of Egypt. Pharaoh told them his dreams, but no one could interpret them for him. | SWKCV 8 Asubuhi yake, alifadhaika akilini, hivyo akawaita waaguzi wote pamoja na watu wenye busara wa Misri. Walipokuja, Farao akawaeleza ndoto zake, lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kumfasiria. |
| BSB 9 Then the chief cupbearer said to Pharaoh, “Today I recall my failures. | SWKCV 9 Ndipo mnyweshaji mkuu alipomwambia Farao, “Leo nimekumbushwa kuhusu kosa langu. |
| BSB 10 Pharaoh was once angry with his servants, and he put me and the chief baker in the custody of the captain of the guard. | SWKCV 10 Wakati fulani Farao aliwakasirikia watumishi wake, akanifunga mimi na mwokaji mkuu katika nyumba ya mkuu wa ulinzi. |
| BSB 11 One night both the chief baker and I had dreams, and each dream had its own meaning. | SWKCV 11 Kila mmoja wetu aliota ndoto katika usiku mmoja na kila ndoto ilikuwa na maana yake tofauti. |
| BSB 12 Now a young Hebrew was there with us, a servant of the captain of the guard. We told him our dreams and he interpreted them for us individually. | SWKCV 12 Basi kijana wa Kiebrania aliyekuwa pamoja nasi huko, alikuwa mtumishi wa mkuu wa kikosi cha ulinzi. Tulimweleza ndoto zetu, naye akatufasiria, akitupa kila mtu tafsiri ya ndoto yake. |
| BSB 13 And it happened to us just as he had interpreted: I was restored to my position, and the other man was hanged.” | SWKCV 13 Nayo mambo yakawa sawa kabisa na jinsi alivyotufasiria ndoto zetu: Mimi nilirudishwa kazini mwangu na huyo mtu mwingine akaangikwa.” |
| BSB 14 So Pharaoh sent for Joseph, who was quickly brought out of the dungeon. After he had shaved and changed his clothes, he went in before Pharaoh. | SWKCV 14 Basi, Farao akatuma Yosefu aitwe, naye akatolewa kifungoni haraka. Baada ya kunyoa na kubadilisha nguo zake akaenda mbele ya Farao. |
| BSB 15 Pharaoh said to Joseph, “I had a dream, and no one can interpret it. But I have heard it said of you that when you hear a dream you can interpret it.” | SWKCV 15 Farao akamwambia Yosefu, “Nimeota ndoto, wala hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuifasiri. Lakini nimesikia ikisemwa kwa habari yako kwamba unapoelezwa ndoto waweza kuifasiri.” |
| BSB 16 “I myself cannot do it,” Joseph replied, “but God will give Pharaoh a sound answer.” | SWKCV 16 Yosefu akamjibu Farao, “Siwezi kuifasiri, lakini Mungu atampa Farao jibu analolihitaji.” |
| BSB 17 Then Pharaoh said to Joseph: “In my dream I was standing on the bank of the Nile, | SWKCV 17 Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Katika ndoto yangu nilikuwa nimesimama ukingoni mwa Mto Naili, |
| BSB 18 when seven cows, well-fed and sleek, came up from the river and began to graze among the reeds. | SWKCV 18 nikawaona ngʼombe saba, wazuri na wanono, wakijitokeza kutoka mtoni wakaja kujilisha kwenye matete. |
| BSB 19 After them, seven other cows—sickly, ugly, and thin—came up. I have never seen such ugly cows in all the land of Egypt! | SWKCV 19 Baada ya hao, ngʼombe wengine saba wadhaifu wakatokea, wabaya sana na waliokonda. Kamwe sikuwahi kuona ngʼombe wabaya jinsi hiyo katika nchi yote ya Misri. |
| BSB 20 Then the thin, ugly cows devoured the seven well-fed cows that were there first. | SWKCV 20 Hao ngʼombe waliokonda na wabaya sana wakawala wale ngʼombe saba walionona waliojitokeza kwanza. |
| BSB 21 When they had devoured them, however, no one could tell that they had done so; their appearance was as ugly as it had been before. Then I awoke. | SWKCV 21 Lakini hata baada ya kuwala, hakuna mtu ambaye angeweza kusema kwamba wamekula, bado walionekana wabaya kama mwanzoni. Kisha nikaamka kutoka usingizini. |
| BSB 22 In my dream I also saw seven heads of grain, plump and ripe, growing on a single stalk. | SWKCV 22 “Pia katika ndoto zangu niliona masuke saba ya nafaka, yamejaa na mazuri, yanakua katika bua moja. |
| BSB 23 After them, seven other heads of grain sprouted—withered, thin, and scorched by the east wind. | SWKCV 23 Baada ya hayo masuke mengine saba yakachipua, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki. |
| BSB 24 And the thin heads of grain swallowed the seven plump ones. I told this dream to the magicians, but no one could explain it to me.” | SWKCV 24 Yale masuke membamba ya nafaka yakayameza yale masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka. Nimewaeleza waaguzi, wala hakuna yeyote aliyeweza kunifasiria.” |
| BSB 25 At this, Joseph said to Pharaoh, “The dreams of Pharaoh are one and the same. God has revealed to Pharaoh what He is about to do. | SWKCV 25 Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni ndoto iyo hiyo moja. Mungu amemfunulia Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. |
| BSB 26 The seven good cows are seven years, and the seven ripe heads of grain are seven years. The dreams have the same meaning. | SWKCV 26 Ngʼombe saba wazuri ni miaka saba, nayo masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka ni miaka saba, ni ndoto iyo hiyo moja. |
| BSB 27 Moreover, the seven thin, ugly cows that came up after them are seven years, and so are the seven worthless heads of grain scorched by the east wind—they are seven years of famine. | SWKCV 27 Ngʼombe saba waliokonda na wabaya wale waliojitokeza baadaye ni miaka saba, vivyo hivyo masuke saba ya ngano yaliyodhoofika na kukaushwa na upepo wa mashariki, ni miaka saba ya njaa. |
| BSB 28 It is just as I said to Pharaoh: God has shown Pharaoh what He is about to do. | SWKCV 28 “Ni kama vile nilivyomwambia Farao: Mungu amemwonyesha Farao jambo analokusudia kufanya karibuni. |
| BSB 29 Behold, seven years of great abundance are coming throughout the land of Egypt, | SWKCV 29 Miaka saba ya neema inakuja katika nchi yote ya Misri, |
| BSB 30 but seven years of famine will follow them. Then all the abundance in the land of Egypt will be forgotten, and the famine will devastate the land. | SWKCV 30 lakini itafuata miaka saba ya njaa. Ndipo neema yote ya Misri itasahaulika na njaa itaikumba nchi. |
| BSB 31 The abundance in the land will not be remembered, since the famine that follows it will be so severe. | SWKCV 31 “Neema iliyokuwa katika nchi haitakumbukwa, kwa sababu njaa itakayofuata itakuwa kali mno. |
| BSB 32 Moreover, because the dream was given to Pharaoh in two versions, the matter has been decreed by God, and He will carry it out shortly. | SWKCV 32 Sababu ya ndoto kumjia Farao kwa namna mbili ni kwamba jambo hilo Mungu ameshaamua kwa hakika, naye Mungu atalifanya karibuni. |
| BSB 33 Now, therefore, Pharaoh should look for a discerning and wise man and set him over the land of Egypt. | SWKCV 33 “Basi sasa Farao na atafute mtu mwenye akili na hekima ili amweke kuwa msimamizi wa nchi ya Misri. |
| BSB 34 Let Pharaoh take action and appoint commissioners over the land to take a fifth of the harvest of Egypt during the seven years of abundance. | SWKCV 34 Farao na aweke wenye amri nchini kote wakusanye sehemu ya tano ya mavuno ya Misri katika miaka hii saba ya neema. |
| BSB 35 Under the authority of Pharaoh, let them collect all the excess food from these good years, that they may come and lay up the grain to be preserved as food in the cities. | SWKCV 35 Wakusanye chakula chote katika miaka hii saba ya neema inayokuja na kuhifadhi nafaka chini ya mamlaka ya Farao, iwe akiba ya chakula katika miji. |
| BSB 36 This food will be a reserve for the land during the seven years of famine to come upon the land of Egypt. Then the country will not perish in the famine.” | SWKCV 36 Chakula hiki kitakuwa akiba ya tahadhari kwa ajili ya nchi, ili kitumike katika ile miaka saba ya njaa itakayokuja Misri, ili nchi isiharibiwe na njaa.” |
| BSB 37 This proposal pleased Pharaoh and all his officials. | SWKCV 37 Mpango huu ulionekana mzuri kwa Farao na kwa maafisa wake wote. |
| BSB 38 So Pharaoh asked them, “Can we find anyone like this man, in whom the Spirit of God abides?” | SWKCV 38 Hivyo Farao akawauliza, “Je tunaweza kumpata yeyote kama mtu huyu, ambaye Roho wa Mungu yumo ndani yake?” |
| BSB 39 Then Pharaoh said to Joseph, “Since God has made all this known to you, there is no one as discerning and wise as you. | SWKCV 39 Ndipo Farao akamwambia Yosefu, “Maadamu Mungu amekufunulia yote haya, hakuna mwingine yeyote mwenye akili na hekima kama wewe. |
| BSB 40 You shall be in charge of my house, and all my people are to obey your commands. Only with regard to the throne will I be greater than you.” | SWKCV 40 Wewe utakuwa msimamizi wa jumba langu la kifalme, na watu wangu wote watatii amri zako. Ni kuhusu kiti cha ufalme tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.” |
| BSB 41 Pharaoh also told Joseph, “I hereby place you over all the land of Egypt.” | SWKCV 41 Kwa hiyo Farao akamwambia Yosefu, “Sasa nakuweka uwe msimamizi wa nchi yote ya Misri.” |
| BSB 42 Then Pharaoh removed the signet ring from his finger, put it on Joseph’s finger, clothed him in garments of fine linen, and placed a gold chain around his neck. | SWKCV 42 Ndipo Farao akaivua pete yake ya muhuri kutoka kidoleni mwake na kuivalisha katika kidole cha Yosefu. Akamvika majoho mazuri ya kitani safi na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. |
| BSB 43 He had Joseph ride in his second chariot, with men calling out before him, “Bow the knee!” So he placed him over all the land of Egypt. | SWKCV 43 Akampandisha katika gari lake la farasi kama msaidizi wake, watu wakatangulia wakishangilia, wakisema, “Fungueni njia!” Ndivyo Farao alivyomweka Yosefu kuwa msimamizi wa nchi yote ya Misri. |
| BSB 44 And Pharaoh declared to Joseph, “I am Pharaoh, but without your permission, no one in all the land of Egypt shall lift his hand or foot.” | SWKCV 44 Kisha Farao akamwambia Yosefu, “Mimi ni Farao, lakini pasipo neno lako, hakuna mtu mwenye ruhusa kuinua mkono au mguu katika nchi yote ya Misri.” |
| BSB 45 Pharaoh gave Joseph the name Zaphenath-paneah, and he gave him Asenath daughter of Potiphera, priest of On, to be his wife. And Joseph took charge of all the land of Egypt. | SWKCV 45 Farao akamwita Yosefu Safenath-Panea, pia akampa Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, kuwa mke wake. Ndipo Yosefu akaitembelea nchi yote ya Misri. |
| BSB 46 Now Joseph was thirty years old when he entered the service of Pharaoh king of Egypt. And Joseph left Pharaoh’s presence and traveled throughout the land of Egypt. | SWKCV 46 Yosefu alikuwa na miaka thelathini alipoingia katika utumishi wa Farao mfalme wa Misri. Naye Yosefu akatoka mbele ya Farao akasafiri katika nchi yote ya Misri. |
| BSB 47 During the seven years of abundance, the land brought forth bountifully. | SWKCV 47 Katika ile miaka saba ya neema nchi ilizaa mazao kwa wingi sana. |
| BSB 48 During those seven years, Joseph collected all the excess food in the land of Egypt and stored it in the cities. In every city he laid up the food from the fields around it. | SWKCV 48 Yosefu akakusanya chakula chote kilichozalishwa katika ile miaka saba ya neema nchini Misri, akakihifadhi katika ghala za miji. Katika kila mji kulihifadhiwa chakula kilichozalishwa katika mashamba yaliyouzunguka mji huo. |
| BSB 49 So Joseph stored up grain in such abundance, like the sand of the sea, that he stopped keeping track of it; for it was beyond measure. | SWKCV 49 Yosefu alihifadhi nafaka nyingi, mfano wa mchanga wa bahari, ilikuwa nyingi mno kiasi kwamba walishindwa kuweka kumbukumbu kwa sababu akiba ilizidi sana kupita kipimo. |
| BSB 50 Before the years of famine arrived, two sons were born to Joseph by Asenath daughter of Potiphera, priest of On. | SWKCV 50 Kabla ya miaka ya njaa kuanza, Asenathi binti Potifera, kuhani wa mji wa Oni, alikuwa amemzalia Yosefu wana wawili wa kiume. |
| BSB 51 Joseph named the firstborn Manasseh, saying, “God has made me forget all my hardship and all my father’s household.” | SWKCV 51 Yosefu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenifanya nisahau taabu zangu zote pamoja na jamaa yote ya nyumba ya baba yangu.” |
| BSB 52 And the second son he named Ephraim, saying, “God has made me fruitful in the land of my affliction.” | SWKCV 52 Mwana wa pili akamwita Efraimu, akisema, “Ni kwa sababu Mungu amenistawisha katika nchi ya mateso yangu.” |
| BSB 53 When the seven years of abundance in the land of Egypt came to an end, | SWKCV 53 Ile miaka saba ya neema huko Misri ikaisha, |
| BSB 54 the seven years of famine began, just as Joseph had said. And although there was famine in every country, there was food throughout the land of Egypt. | SWKCV 54 nayo miaka ile saba ya njaa ikaanza, sawasawa na alivyosema Yosefu. Kulikuwa na njaa katika nchi nyingine zote, bali katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula. |
| BSB 55 When extreme hunger came to all the land of Egypt and the people cried out to Pharaoh for food, he told all the Egyptians, “Go to Joseph and do whatever he tells you.” | SWKCV 55 Wakati nchi yote ya Misri ilipopatwa na njaa, watu wakamlilia Farao ili awape chakula. Ndipo Farao alipowaagiza Wamisri wote, akisema, “Nendeni kwa Yosefu, nanyi mfanye anachowaambia.” |
| BSB 56 When the famine had spread over all the land, Joseph opened up all the storehouses and sold grain to the Egyptians; for the famine was severe in the land of Egypt. | SWKCV 56 Wakati njaa ilipokuwa imeenea katika nchi yote, Yosefu akafungua ghala za vyakula na kuwauzia Wamisri nafaka, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno katika nchi yote ya Misri. |
| BSB 57 And every nation came to Joseph in Egypt to buy grain, because the famine was severe over all the earth. | SWKCV 57 Pia nchi nyingine zote zilikuja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yosefu, kwa sababu njaa ilikuwa kali mno duniani kote. |
Questions about Genesis 41? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.