Genesis 46
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 So Israel set out with all that he had, and when he came to Beersheba, he offered sacrifices to the God of his father Isaac. | SWKCV 1 Hivyo Israeli akaondoka na vyote vilivyokuwa mali yake, naye alipofika Beer-Sheba, akamtolea dhabihu Mungu wa Isaki baba yake. |
| BSB 2 And that night God spoke to Israel in a vision: “Jacob, Jacob!” He said. “Here I am,” replied Jacob. | SWKCV 2 Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, “Yakobo! Yakobo!” Akajibu, “Mimi hapa.” |
| BSB 3 “I am God,” He said, “the God of your father. Do not be afraid to go down to Egypt, for I will make you into a great nation there. | SWKCV 3 Mungu akamwambia, “Mimi ndimi Mungu wa baba yako, usiogope kushuka Misri, kwa maana huko nitakufanya taifa kubwa. |
| BSB 4 I will go down with you to Egypt, and I will surely bring you back. And Joseph’s own hands will close your eyes.” | SWKCV 4 Nitashuka Misri pamoja nawe, nami hakika nitakurudisha tena Kanaani. Mikono ya Yosefu mwenyewe ndiyo itakayofunga macho yako.” |
| BSB 5 Then Jacob departed from Beersheba, and the sons of Israel took their father Jacob in the wagons Pharaoh had sent to carry him, along with their children and wives. | SWKCV 5 Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha. |
| BSB 6 They also took the livestock and possessions they had acquired in the land of Canaan, and Jacob and all his offspring went to Egypt. | SWKCV 6 Wakachukua pia mifugo yao na mali walizokuwa wamezipata Kanaani, Yakobo na uzao wake wote wakashuka Misri. |
| BSB 7 Jacob took with him to Egypt his sons and grandsons, and his daughters and granddaughters—all his offspring. | SWKCV 7 Akawachukua wanawe na binti zake, wajukuu wake wa kiume na wa kike, yaani uzao wake wote mpaka Misri. |
| BSB 8 Now these are the names of the sons of Israel (Jacob and his descendants) who went to Egypt: Reuben, Jacob’s firstborn. | SWKCV 8 Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli (Yakobo na wazao wake), waliokwenda Misri: Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Yakobo. |
| BSB 9 The sons of Reuben: Hanoch, Pallu, Hezron, and Carmi. | SWKCV 9 Wana wa Reubeni ni: Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. |
| BSB 10 The sons of Simeon: Jemuel, Jamin, Ohad, Jachin, Zohar, and Shaul the son of a Canaanite woman. | SWKCV 10 Wana wa Simeoni ni: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. |
| BSB 11 The sons of Levi: Gershon, Kohath, and Merari. | SWKCV 11 Wana wa Lawi ni: Gershoni, Kohathi na Merari. |
| BSB 12 The sons of Judah: Er, Onan, Shelah, Perez, and Zerah; but Er and Onan died in the land of Canaan. The sons of Perez: Hezron and Hamul. | SWKCV 12 Wana wa Yuda ni: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera (lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi ni: Hesroni na Hamuli. |
| BSB 13 The sons of Issachar: Tola, Puvah, Job, and Shimron. | SWKCV 13 Wana wa Isakari ni: Tola, Puva, Yashubu na Shimroni. |
| BSB 14 The sons of Zebulun: Sered, Elon, and Jahleel. | SWKCV 14 Wana wa Zabuloni ni: Seredi, Eloni na Yaleeli. |
| BSB 15 These are the sons of Leah born to Jacob in Paddan-aram, in addition to his daughter Dinah. The total number of sons and daughters was thirty-three. | SWKCV 15 Hawa ndio wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan-Aramu pamoja na binti yake Dina. Jumla ya wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu. |
| BSB 16 The sons of Gad: Ziphion, Haggi, Shuni, Ezbon, Eri, Arodi, and Areli. | SWKCV 16 Wana wa Gadi ni: Sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli. |
| BSB 17 The children of Asher: Imnah, Ishvah, Ishvi, Beriah, and their sister Serah. The sons of Beriah: Heber and Malchiel. | SWKCV 17 Wana wa Asheri ni: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera. Wana wa Beria ni: Heberi na Malkieli. |
| BSB 18 These are the sons of Jacob born to Zilpah—whom Laban gave to his daughter Leah—sixteen in all. | SWKCV 18 Hawa ndio watoto Zilpa aliomzalia Yakobo, ambao Labani alimpa binti yake Lea; jumla yao walikuwa kumi na sita. |
| BSB 19 The sons of Jacob’s wife Rachel: Joseph and Benjamin. | SWKCV 19 Wana wa Raheli mke wa Yakobo ni: Yosefu na Benyamini. |
| BSB 20 Manasseh and Ephraim were born to Joseph in the land of Egypt by Asenath daughter of Potiphera, priest of On. | SWKCV 20 Huko Misri, Asenathi binti wa Potifera, aliyekuwa kuhani wa mji wa Oni, alimzalia Yosefu wana wawili, Manase na Efraimu. |
| BSB 21 The sons of Benjamin: Bela, Becher, Ashbel, Gera, Naaman, Ehi, Rosh, Muppim, Huppim, and Ard. | SWKCV 21 Wana wa Benyamini ni: Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu na Ardi. |
| BSB 22 These are the sons of Rachel born to Jacob—fourteen in all. | SWKCV 22 Hawa ndio wana wa Raheli aliomzalia Yakobo; jumla yao ni kumi na wanne. |
| BSB 23 The son of Dan: Hushim. | SWKCV 23 Mwana wa Dani ni: Hushimu. |
| BSB 24 The sons of Naphtali: Jahzeel, Guni, Jezer, and Shillem. | SWKCV 24 Wana wa Naftali ni: Yaseeli, Guni, Yeseri na Shilemu. |
| BSB 25 These are the sons of Jacob born to Bilhah, whom Laban gave to his daughter Rachel—seven in all. | SWKCV 25 Hawa walikuwa wana wa Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alikuwa amempa Raheli binti yake; jumla yao walikuwa saba. |
| BSB 26 All those belonging to Jacob who came to Egypt—his direct descendants, besides the wives of Jacob’s sons—numbered sixty-six persons. | SWKCV 26 Wote waliokwenda Misri pamoja na Yakobo, waliokuwa wazao wake hasa pasipo kuhesabu wakwe zake, walikuwa watu sitini na sita. |
| BSB 27 And with the two sons who had been born to Joseph in Egypt, the members of Jacob’s family who went to Egypt were seventy in all. | SWKCV 27 Pamoja na wana wawili waliozaliwa na Yosefu huko Misri, jumla yote ya jamaa ya Yakobo, waliokwenda Misri, walikuwa sabini. |
| BSB 28 Now Jacob had sent Judah ahead of him to Joseph to get directions to Goshen. When Jacob’s family arrived in the land of Goshen, | SWKCV 28 Basi Yakobo akamtanguliza Yuda aende kwa Yosefu ili amwelekeze njia ya Gosheni. Walipofika nchi ya Gosheni, |
| BSB 29 Joseph prepared his chariot and went there to meet his father Israel. Joseph presented himself to him, embraced him, and wept profusely. | SWKCV 29 gari kubwa zuri la Yosefu liliandaliwa, naye akaenda Gosheni kumlaki baba yake Israeli. Mara Yosefu alipofika mbele yake, alimkumbatia baba yake, akalia kwa muda mrefu. |
| BSB 30 Then Israel said to Joseph, “Finally I can die, now that I have seen your face and know that you are still alive!” | SWKCV 30 Israeli akamwambia Yosefu, “Sasa niko tayari kufa, kwa kuwa nimejionea mwenyewe kwamba bado uko hai.” |
| BSB 31 Joseph said to his brothers and to his father’s household, “I will go up and inform Pharaoh: ‘My brothers and my father’s household from the land of Canaan have come to me. | SWKCV 31 Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake na watu wa nyumbani mwa baba yake, “Nitapanda kwa Farao na kumwambia, ‘Ndugu zangu na watu wa nyumbani mwa baba yangu, waliokuwa wakiishi katika nchi ya Kanaani, wamekuja kwangu. |
| BSB 32 The men are shepherds; they raise livestock, and they have brought their flocks and herds and all that they own.’ | SWKCV 32 Watu hao ni wachunga mifugo, huchunga mifugo, wamekuja na makundi ya kondoo, mbuzi na ngʼombe pamoja na kila kitu walicho nacho.’ |
| BSB 33 When Pharaoh summons you and asks, ‘What is your occupation?’ | SWKCV 33 Farao atakapowaita na kuwaulizeni, ‘Kazi yenu ni nini?’ |
| BSB 34 you are to say, ‘Your servants have raised livestock ever since our youth—both we and our fathers.’ Then you will be allowed to settle in the land of Goshen, since all shepherds are detestable to the Egyptians.” | SWKCV 34 Mjibuni, ‘Watumwa wako wamekuwa wachunga mifugo tangu ujana wetu mpaka sasa, kama baba zetu walivyofanya.’ Ndipo mtakaporuhusiwa kukaa katika nchi ya Gosheni, kwa kuwa wachunga mifugo wote ni chukizo kwa Wamisri.” |
Questions about Genesis 46? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.