Hosea 6
| Berean Standard Bible tier 2 | Kiswahili Contemporary Version tier 3 |
|---|---|
| BSB 1 Come, let us return to the LORD. For He has torn us to pieces, but He will heal us; He has wounded us, but He will bind up our wounds. | SWKCV 1 “Njooni, tumrudie Bwana. Ameturarua vipande vipande lakini atatuponya; ametujeruhi lakini atatufunga majeraha yetu. |
| BSB 2 After two days He will revive us; on the third day He will raise us up, that we may live in His presence. | SWKCV 2 Baada ya siku mbili atatufufua; katika siku ya tatu atatuinua, ili tuweze kuishi mbele zake. |
| BSB 3 So let us know—let us press on to know the LORD. As surely as the sun rises, He will appear; He will come to us like the rain, like the spring showers that water the earth. | SWKCV 3 Tumkubali Bwana, tukaze kumkubali yeye. Kutokea kwake ni hakika kama vile kuchomoza kwa jua; atatujia kama mvua za masika, kama vile mvua za vuli ziinyweshavyo nchi.” |
| BSB 4 What shall I do with you, O Ephraim? What shall I do with you, O Judah? For your loyalty is like a morning mist, like the early dew that vanishes. | SWKCV 4 “Nifanye nini nawe, Efraimu? Nifanye nini nawe, Yuda? Upendo wako ni kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao. |
| BSB 5 Therefore I have hewn them by the prophets; I have slain them by the words of My mouth, and My judgments go forth like lightning. | SWKCV 5 Kwa hiyo ninawakata ninyi vipande vipande kwa kutumia manabii wangu; nimewaua ninyi kwa maneno ya kinywa changu, hukumu zangu zinawaka kama umeme juu yenu. |
| BSB 6 For I desire mercy, not sacrifice, and the knowledge of God rather than burnt offerings. | SWKCV 6 Kwa maana nataka rehema, wala si dhabihu, kumkubali Mungu zaidi kuliko sadaka za kuteketezwa. |
| BSB 7 But they, like Adam, have transgressed the covenant; there they were unfaithful to Me. | SWKCV 7 Wamevunja Agano kama Adamu: huko hawakuwa waaminifu kwangu. |
| BSB 8 Gilead is a city of evildoers, tracked with footprints of blood. | SWKCV 8 Gileadi ni mji wenye watu waovu, umetiwa madoa kwa nyayo za damu. |
| BSB 9 Like raiders who lie in ambush, so does a band of priests; they murder on the way to Shechem; surely they have committed atrocities. | SWKCV 9 Kama wanyangʼanyi wamviziavyo mtu, ndivyo magenge ya makuhani wafanyavyo; wanaulia watu kwenye njia iendayo Shekemu, wakifanya uhalifu wa aibu. |
| BSB 10 In the house of Israel I have seen a horrible thing: Ephraim practices prostitution there, and Israel is defiled. | SWKCV 10 Nimeona jambo la kutisha katika nyumba ya Israeli. Huko Efraimu amejitolea kwa ukahaba na Israeli amenajisika. |
| BSB 11 Also for you, O Judah, a harvest is appointed, when I restore My people from captivity. | SWKCV 11 “Pia kwa ajili yako, Yuda, mavuno yameamriwa. “Wakati wowote ningerejesha neema ya watu wangu, |
Questions about Hosea 6? Ask — answers come only from the text, with every claim marked.